mdau subi wa nukta 77 katuletea hii na kuwaka wadau wa mbeya, moshi na bukoba watafute mbegu hii ili kufanya mabo yawe tambarare kwa muda mfupi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2008

    Mhhh ingekuwa ndizi mshare kubwa hivyo!!duu wachagga ingechanganya sana..uwe na mikungu yako mia moja uishushe pale mahakama ya ndizi ubungo..si mapesa hayo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2008

    ndizi aka e bitoke aka matoke ni asili ya bukoba huko mkoani kagera.those are the real ndizis

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2008

    hii lazima ni GMO. Haiwezi kuwa ndizo kawaida

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2008

    Hakuna kitu kama hicho hiyo ni picture manipulation.Wake up!!!!

    ReplyDelete
  5. duuh! hii inabidi iuzwe kwa chane maana ukinunua mungu lazima uwe na pick up halafu ndizi nyingine zinaoza kabla mkungu haujaisha kuliwa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2008

    fiks hicho picha imetengenezwa hakuna kitu kama hicho labda kama mzee wa ndumba afanye vitu vyake.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2008

    we anonymous wa 7:10pm acha uhaya....

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2008

    duuuh hii ni real ndizi kabisaaaa.tena kama si ya kamachumu basi ni ya karagwe huko kagera.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2008

    Si bure lazima atakuwa yule 'mzee wa vudu' (voodoo) wa bungeni alitupia mambo yake hapo

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2008

    HAPO NI NYUMBANI KWA YULE MHE. ALIYEMWAGA MIUNGAZI BUNGENI KWANI ZINAONEKANA TUNGULI KIBAO CHINI YA HUO MGOMBA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2008

    Hii Ni Hasheem Thabeet wao!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2008

    ebitoke hii ni 'nyoya ya kibanga' we acha tu. utamu kolea

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2008

    Kubeba mkungu wa ndizi wa ukubwa na urefu huo mgomba lazima uwe wa chuma au at the very least uwe na himili ya mnazi au mti kama msonobari. Kwa nini tunadanganyana? Au ndo namna ya kuchemshana akili?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 19, 2008

    Hii Mwanawane inabid Ku-"invent"staili ya kuivuna, maana haiwezakani zote zikakomaa kwa pamoja. Inabidi wataalam wa Materials management watutafutie formulae ya kuivuna. labda tutumie FIFO!! inaweza kulipa.


    Mzee wa Nyantafulamilwa-Isanju!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 19, 2008

    yewomiiii macharari duuu mkungu balaaa wapi huko jamani kuna ndizi ya namna hiii
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2008

    hata wewe sweet wa Arusha natumaini umeona hawa wazungu wanaokuja eti wanatufundisha kupanda migomba! tangia lini wao wakawa na utaharamu? imagine niwao wanaleta magonjwa ili wapate miradi! kwanza kumbuka chuo cha Kilimo Maruku Bukoba , Tangu walipo anza miradi yao siku hizi watu wa maruku wananunua ndizi BKB mjini hao ni wale wenye uwezo! wenzangu na mie wanakula hiyo inaitwa ebijoge! yaani inatesa sana kuona generation ya sasa hawajuhi hata staple food! aibu hiyo yote ni kutaka misaada, mpaka kupanda migomba? kweli hawa watu ni kulaani kabisa, sasa mdudu wao umeingia hata kwenye mihogo jamani tukimbilie wapi? mdudu kwa chakula , kwenye system tutaishia wapi?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 19, 2008

    mbona kuna uhayalisti humu ndani..mara ebitoke..mara real ndizi..nyie vp

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 19, 2008

    NDIZI KAMA HIYO IKIONEKANA MAENEO YA KIBOSHO KIRIMA NI BALAA KUBWA SANA. ISIPOCHINJIWA MBUZI HARAKA HUWA INAONDOKA NA MMOJA WA WANA FAMILIA. NI ALAMA YA BALAA KATIKA KOO/FAMILIA

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 19, 2008

    mbona kuna uhayalisti sana humu ndani...ebitoke ebitoke

    ReplyDelete
  20. ANON 4:26PM MAY 19 NIMEFURAHISHA NA MCHANGO WAKO NAOMBA NAFASI YA KUKUTUNUKIA DOLA 10 ZA MAONGEZI KATIKA SIMU YAKO. HATA KAM HAUKO HAPA TZ NIPE NAMBA YA MWENZAKO ALIYOKO HAPA AFAIDI ZAWADI HIYO

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 20, 2008

    Uhaya lazima uwepo kwani hiyo picha inaonyesha mahali zinapopatikana ndizi. hauwezi ukasema ugogoni au kwingineko. utakufa na kiziba cha roho.

    Nantombe
    Moshi

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 20, 2008

    kutunukiwa dola 10 kwa simu nashukuru sana, ningeomba hii changamoto tuiweke mstali wa mbele hasa kwa sisi wakereketwa! naomba kabisa wadau wanaosema mambo ya uhaya waondoekabisa fikra potovu Tanzania Hakuna ukabira kabisa ukiona mtu anatoa hoja kwa lugha yoyote ina maana ameguswa na anataka mawazo ya wengine! tusitangulize critics, kinachohitajika ni mawazo na kuona swala kama hilo au tatizo lina madhara gani kwa jamii, Mr. Issa jaribu kuelimisha watu tena maana ya hii blog! infact you should block some of the comments kama ni utumbo! au unaonaje?

    ReplyDelete
  23. UKIANGALIA ALILIMIA 99.999999999999999999999999999999999999 YA WATOA MAONI WANAPOINT AMBAZO NI HASI (NEGATIVE). SISI NI WATAALAMU SANA WA KUBOMOANA. SASA HUO NDIO UNAITWA URANGI NYEUSI. PALE UNAPOKUWA MWEUSI HILO NDIO DOA LAKO DAMU YAKO NI YA KICHAWI KUOMBEA MABAYA WENGINE, KUSHANGILIA WENGINE WANAPOANGUKA, HUU NDIO UUCHAWI MKUU HUNA HAJA YA KUSEMA MCHAWI ANA MACHO MEKUNDU.ITACHUKUA HATA MIAKA MIA TANO KUSAFISHA HII TABIA UKU NEEMA YA MNYAZI MUNGU IKIHITAJIAKA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...