Pole sana kwa pilikapilika za kuhabarisha walimwengu.Nimejitokeza leo kuunga mkono wazo lako la kuwa na Bongo Reds Club hapa nyumbani Tanzania.
Binafsi mimi ni mpenzi mzuri wa Liverpool ingawa si MNAZI sana kama wanavyoweza kuwa watu wengine.Kuonesha kuunga mkono harakati zako hizo,nimeamua kutoa kamchango kangu ili kuzidi kukusukuma (motivation) na kukuonesha kuwa kuwa kuna watu tuko bega kwa bega nawe (siyo nyuma yako) kwenye juhudi zako hizi (YU WILI NEVA WOKU ALONI),kamchango kangu ni wazo la logo ya kile tunachotizamia kukianzisha.
Tafadhali iweke mtandaoni ili na wadau wengine waione na kutoa mawazo yao,nakaribisha maoni,kukosolewa nakurekebishwa.
Naomba kuwasilisha mkuu!
Mdau,
eddyjunior.


Mimi ni manchester lakini nimsifu tu jamaa logo yake sii kitoto nzuri mnooooo mpaka nimeona wivu
ReplyDeletemdogo wake Will UK
Jamani bwawa la maini nawaonea wivu,nembo nzuri sana iko bomba ,Jamani wadau naomba kuuliza mimi na uwezo wakutoa majengo ambayo yalikuwa kwajili ya kufungua shule lakini hatukufungua tena kuna vitanda na magodoro double decker yani kama shule mnavyojua vipya havijatumika uwezo wakuchukua wanafunzi 150, hAYO Majengo sasa hivi hatutumii na eneo ukubwa wa acre 120 ,huko Arusha mimi binfasi nimpenzi wa mpira na nimecheza ,Nilishawahi kusema na mpango wakufungua chuo cha mpira sio kuhusu kuingiza hela ni swala la kuendeleza mpira Tanzania sasa naomba kuuliza wadau Mnadhani mfano tukaanzanisha chuo cha mpira nadhani nikitu ambacho hakijawahi kutokea Tanzania ,
ReplyDeleteNaomba wadau ushauri wenu!tutaanzisha Pia website ambayo itakuwa na documentary na kila kitu kuhusu hicho chuo!location Arusha 10km from town,Ingekuwa Dar es salaam ni Rahisi ila Arusha nadhani ni ngumu kidogo.
Au wadau mnataka tufungue chuo kiwe cha fans of Man utd,Liverpool,Chelsea na Arsenal ,maana ndio zinazo washabiki wengi
William Uk(United for Life)
WAZO LA KUWA NA NEMBO YETU SISI WANA BWAWA LA MAINI (LIVERPOOL) TAWI LA TANZANIA NI ZURI ILA MIMI SIAFIKIANI NA NEMBO ALIYOITOA HUYO MDAU AJIITAYE EDDY JUNIOR KWANI HIYO KAITOA KWA WANA BWANA LA MAINI WENZETU WA DUBAI KAMA TULIVYOSOMA KWA MAELEKEZO YA BW. MISUPU ALIPOSEMA TUBOFYE SEHEMU FULANI !!!! KWANINI TUSIBUNI YA KWETU WENYEWE IKIWA NI PAMOJA NA KUTOPOTEZA ALAMA MUHIMU ZILIZOKO KWENYE NEMBO ORIGINAL ?!?!?!?!?!?**&!&!*!&!*!(*!(!()????
ReplyDeleteNAWASILISHA WADAU
RAYMOND MREMA
KINGSTON - JAMAICA
Eddy ni mzuri wa graphics... sio, mzuri, ni Mzuri Sana... nadhani kwa Tanzania ni mmoja wa ma top kwenye Graphics, Flash na "Web design and Development".
ReplyDeleteYuko kwenye contacts zangu na nikipata project ya maana huku (UK) nitawasiliana naye.
Nashukuru kuna WaTanzania wanaotumia vyema teknolojia kwa kiwango sawa na watu wa nchi zilizoendelea.
Safi
Mdau, UK.
naomba mshabiki,yoyote wa liverpool anielimishe kwanini uwanja wa liverpool unaitwa 'THE KOP'.
ReplyDeleteKwakua umekubari kulekebishwa hiyo bendela ya Tanzania Inabidi uiangalie tena mwelekeo wa MSTARI,(MICHIRIZI)
ReplyDeleteKwa kumsaidia mdau hapo juu . ni kuwa uwanja wa Liverpool hauitwi "THE KOP" unaitwa ANFIELD ila mashabiki wa Liverpool kwa jina la utani ndio huitwa KOPs.
ReplyDeletemdau Paka la Jikoni-UK
I would have thought the Bongopools would have had their own flag to match Liverpool's. As a devout supporter of my local team in Musoma and as a Tanzanian, I feel dragged into Liverpool sentiments by the logo. Please get something less generalising...
ReplyDeletepaka la jikoni,you got it wrong,ANFIELD,huitwa 'the kop'.the kop ni sehemu south africa ambapo wazulu enzi zile,waliwapiga askari wa kingereza na kuwachinja vibaya sana,uwanja huitwa hivyo wakimaanisha 'machinjioni'
ReplyDeleteWilliam uk kama huko serious na hiloswala la chuo cha soka ni wazo zuri lakini kama ni show off unajaribu kufurahisha nafsi yako sawa pia. Ushauri wangu kama kweli hipo available wasiliana na ubalozi wako hapo U.K ipeleke wazo lako wizara ya michezo kuna hela pale na wewe pia utapata hela kwa mchango wako wa majengo na viwanja.haya kila la kheri kama kweli kama show off to hell with ur idea lol.
ReplyDeleteA short poem from heart:
ReplyDeleteewe Mswahili hadhi yako iko wapi?
Hadhi yako iko wapi?
Bendera ya taifa langu tukufu mbona umeirahisisha kwa kiwango cha uchochoro?Hadhi yako iko wapi?Thamani ya nishani ya uhuru wa taifa langu mpendwa ni sawa na kilabu cha mpira ya nchi ngeni???
Hadhi yako iko wapi?na kweli ujinga wetu mpaka siku ya kiama...
Hadhi yako iko wapi?
Wewe unayejiita Raymond Mrema wa Jamaica,nyie ndiyo watu tunaowapinga katika jamii kila siku,mimi ningekuwa kiongozi wa nchi ya Tz ningeagiza watu wa aina yako watupwe gerezani,maana hutoi maoni yenye kujenga badala yake wewe unaponda tuuu!Mzee vipi?Ndumu?Maana Jamaica ndiyo sigara hiyo.
ReplyDeleteMtu kajipinda kutumia muda wake,ubunifu wake na resource zake kufanya kitu kama hiki,badala ya kumpa ushauri afanyeje kuboresha (kama kweli inahitaji kuboreshwa) au kama haifai kabisa utupe wewe wazo lako,wewe unashupalia kuponda tuuu,jamani wabongo lini mtakuwa na mawazo yaliyofuguka????Eti kakopi!Kakopi nini?Wewe huoni tofauti kati ya yetu na yao?Kwanza sisi wote ni wapenzi wa Liverpool hivyo yapasa tuwe na mfanano mmoja (i.e uniformity),tena ukiangalia vizuri yetu inaonekana kufanana zaidi na ya Liverpool kuliko hiyo ya jamaa wa Dubai!
Mimi nampa big up sana huyu mdau Eddyjunior,kwakweli sikuwahi kudhania kuwa tuna wabongo wenye kuweza kucheza na teknolojia kwa kiasi kikubwa namna hii,jamaa anastahili pongezi,misupu wasiliana naye kama vipi akupe ridhaa yake ututupie contact zake tumpe kazi,kijana/mtu mzima/mzee huyu kwakweli nitampongeza kwa kumpa kazi maana nina kazi nyingi sana za aina hii ambazo nitajisikia faraja sana zikifanywa na Mtanzania mwenzangu huko nyumbani.
Kwa msaada tu,kuna mdau hapo juu kazungumzia michirizi kukaa upande usio sawa,tafadhali angalia kwa umakini mdau,haiitaji jicho la ubunifu sana kugundua kuwa jamaa yuko sahihi maana bendera imegeuziwa upande wa kushoto,kwa maana ya kwamba ingegeuziwa kule alikoiweka ya Liverpool ingeonekana sawia kama jinsi ambavyo mdau huyu alivyokariri.Msikariri jama,fungueni fikra,kweli Mkapa alikuwa na ukweli aliposema wabongo ni wavivu wa kufikiri.
LOGO KALI SANAAAAAAA,atakayekasirika avimbe na apasuke,ukweli ndiyo huooooooooo!Nawasilishaaaaaaaaa...
Mdau,
K.M
Boston,MA.
safi saanaaa babake... LIVERPOOL-TANZANIA oyee..
ReplyDeleteKUHUSU THE "KOP"
'KOP' SIO JINA LA UWANJA WALA JINA LA UTANI LA UWANJA, 'KOP' NI JINA LA MOJA YA STANDS(sehemu ya kukalia-sijui kiswahili chake).. sehemu hiyo ya kukalia ni maarufu sana kwasababu inatoa makelele sana, na mashabiki wa liverpool wooote wenye makelele hukaa huko...
KWANINI SEHEMU HIYO INAITWA 'KOP'?
INAITWA 'THE KOP' KWASABABU KUNA BAADHI YA VIWANJA VYENYE SEHEMU YA KUKALIA NDEFU SANA... SASA SEHEMU HIZI ZIMEBATIZWA JINA LA "KOP" KUTOKANA NA UREFU WAKE UNAFANANA NA MLIMA MMOJA AFRIKA YA KUSINI, MLIMA AMBAO NDIO ULIKUWA UWANJA WA VITA VYA (SPION KOP)...
KAMA UNAONA NAKUPIGA FIKSI, INGIA GOOGLE NA SEARCH (THE KOP)..UTAPATA STORY KAMILI
MDAU # 1 WA LIVERPOOL
HALAFU KUHUSU LOGO, NI KALI SANA HUWEZI AMINI... LAKINI UNGEWEKA BENDERA YA TANZANIA KULIA, NA HIYO NYINGINE KUSHOTO... halafu hiyo bendera ungeichekecha kidogo, maana inafanana na bendera ya CHINA...
ReplyDeleteSAFI SANA LAKINI
MDAU #1 LIVERPOOL
YETU KWELI YAMETUSHINDA SIMBA,YANGA, TUKUYU STAR SASA TUNAANZA KUJIPENDEKEZA KWA WENZETU .YEBOO! TUACHE UJINGA TUBOLESHE KWETU KWANZA
ReplyDeleteLogo ni nzuri sana, ila napenda kuuliza maswali, hiyo bendera nyekundu inawakilisha nini, hizo nyota tano ni ishara ya nini, kama ni makombe ya champions league tukishinda lingine mwakani itakuaje? tutabadilisha nembo?
ReplyDeleteKwa kweli hiyo ndio kasoro pekee niliyoiona kwenye hii nembo yako, vinginevyo nimeipenda.
Hongera sana kwa kuja na concept hii ya nembo, lakini naomba uibadilishe hiyo bendera nyekundu uweke nyingine ama kitu kingine kuwakilisha Liverpool FC.
Mdau Toronto
UPUUZI UTUMWA MTUPU! HAMUONI AIBU??
ReplyDeleteAIBU SANA AHSANTE June 13, 2008 12:43 AM, Mtoa Maoni: Anonymous kwa kufumbua watu macho
naomba niwafamishe kuwa hamna ruksa ya ktumia bendera ya taifa la tanzania kwenye nembo yenu. sheria za nchi zinakataka kutumia nenmbo na bendera ya nchi kwenye vitu kama hivi. Mbali na sheria zetu mikataba ya kimataifa inayohusu sheria za milki ubunifu pia inazuia kitendo kama hiki cha kutumia viashiria vya nchi kama bendra au mihuri ya serikali au hata alama/ nembo ya manispaa.
ReplyDeleteWakati mnafanya hivyo kumbukeni hili.
bendera ya nchi inatumika na viongozi wa serikali kwa shughuli za serikali.
Kuna mdau hapo juu anony 12 june 11:23 kasema idea yangu ni ku show off naomba kuuliza kuna haja gani ya mimi ku show off wakati hamna mtu anayenijua itakuwa na faida gani!Any way it was an idea so you have the right to raise your opinion, All i can say is wait and see .Ushauri wako wa wizara ya michezo ni mzuri thanx
ReplyDeleteWilliam Uk(united for life)
I am appauled with this despicable act of belittling our national flag. Michuzi, you better design another loggo as to some of us patriotic Tanzanians, this is a big, very big insult.
ReplyDeleteThe Kop at Anfield dates back to 1905-06. At the end of that season which saw Liverpool lift the second of their league championships the directors at the club decided to reward the loyalty of the fans by building a new brick and cinder banking at the Walton Breck road end of the ground. It was christened as the Spion Kop by Ernest Jones in memory of the many scousers who died in battle over a hill in South Africa by the same name during the Boer War.
ReplyDeleteNaona hapa utapata kidogo idea ya the Kop...
Pamoja na kupendeza kwa nembo hiyo haipendezi kuweka bendera ya Tanzania ndani yake. Ukiweka bendera ya Tanzania katika kushabikia timu ya nje ni kama unatujumuisha sisi tulio Simba na Yanga bila ridhaa yetu. Ingekuwa bendera ya taifa inaonekana katika nembo ya klabu iliyopo nchini hapo inaeleweka, walau inajivunia taifa lake. Kwa hivi itakuwa kama tunajivunia kutawaliwa.
ReplyDelete