
Kaka Michuzi,
Tafadhali naomba tumpe hongera Mtanzania mwenzetu huyu aliyekula nondoz yake ya Ph.D kutoka katika chuo mashuhuri cha Havard nchini Marekani. Nondo hiyo haikuja pekee yake, bali iliambatanishwa na tuzo ya 'Havard 'Haber' Award', ambayo hutolewa kwa kazi ambazo zimetoa mchango mkubwa kabisa katika field ya 'Biological Science'.
Kwakeli hazina kama hizi ndizo zinazomulika mwenge wa Tanzania duniani.Hongera Dr. Nzovu Ulenga. - Mdau


Hongera zake, lakini Bongo MAFISADI wameshamuandalia mshahara wa vijisenti laki tatu kwa mwezi na PhD yake ya Havard...mambo hayo.....
ReplyDeleteHongera zako. The best University in the world.(Chuo alichosoma Obama na marehemu baba yake n.k.) Wazungu huyo hawamuachi arudi Africa, labda akatae mwenyewe. Ni mfano mzuri.
ReplyDeleteMsitake kutusumbua na vijielimu vyenu vya mitaani phd ya madafu au ya nini maana mnaona rahisi sana kupata phd hamna mjinga hapa........
ReplyDeleteAje bongo kufanyaje? Muache afanye kazi huku kwanza akishazichanga za kutosha aje kufungua hospital yake bongo.hongera sana sana sana sana sana.
ReplyDeleteI salute you brother !! i take my hat off to you !! Umefanya mambo ambayo wengi tumeshindwa kufanya. Sikujui lakini HONGERA SANA.
ReplyDeleteNice work Dude...!and is not easy...!
ReplyDeleteBut too expensive,hopeful return of investment will realized at the end in Tanzania.
Dave
Hongera Doctor! Mojawapo ya wazalendo waliopita Harvard University ni:
ReplyDelete1. Daudi Ballali
2. Andrew Chenge - Mzee wa Vijisenti
3. Fredrick Sumaye
Hao wote wametoa mchango mkubwa sana kwenye nchi yetu :)
hongera kaka! much respect. Tunahitaji watu kama wewe kama hamsini kila mwaka. Piga research majuu, bongo there is no support to scientists. I would advise such achievers to be mentors to young aspiring Tanzanian scientists who would like to achieve the same or similar feat. Hongera Nzovu!
ReplyDeleteMuta, Botswana
Hongera sana kaka kwa kazi kupata PHD na tuzo hilo. Haya ndio mambo ya maendeleo.
ReplyDeleteWewe Anony wa Tarehe June 19, 2008 4:12 AM, acha wivu, majungu na ushamba usiokuwa na maana. Mchango wako kwenye mada hii hauna nafasi kwenye jamii yetu ya kisasa.
HONGERA SANA KAKA SUCH AN ACHIEVEMENT CONGRATULATIONS.WE NEED PEOPLE LIKE YOU HAPA TANZANIA
ReplyDeleteMAANON WOTE NIMEYAZIMIA NANENO YENU KWA UJUMLA KWELI WABONGO WANA MAPHD TANGU TUMBONI MWA MAMAM ZAO HIZI WAZUNGU WANAZATUZUZUA NAZO TUWE NA MAJIVUNO NA MASIFA YA VICHWA MAJI YANATULETEA HASARA SANA. UNAKUTA NA MAPHDS HAYO NDIO KWANZA TUNAKUWA OMBA OMBA WA VIFAA NA SIO TEKINOLOGIA, MPAKA LEO TANZANIA HATUWEZI KUTENGENEZA KA CD ROM TUU SIJUI HAPA MAREHEMU FOE SASA HIVI COLLEGE OF EGINEERING WANAFANYA NINI, WAMEIKALIA POLITIC KUGAWANA MADARAKA NA KUTUPUNGUZIA WAANDISI HALISI VIJANA WANAHAMIA BCOM NCHI INAZIDI KUDIDIMIA KITAALUMA TEGEMEZI. ONA SASA VIJANA WANAITUMIKIA DUNIA NJE YA TANZANIA WAKIRUDU NYUMBANI WANASHINDIWA BAGAAMOYO WAZE HAWATAKI KUWAPISHA. MPAKA SASA TUME TENGENZA PHD ZAIDI YA 100 YA VIJANA WENYE UMRI USIOZID 35 TUNATAKA KURUDI NYUMBANI KUIFANYA TANZANIA NAMBER MOJA DUNIANI. VIJANA WAMECHOKA KUNYONYWA ELIMU YAO UGHAIBUNI WANATAKA KURUDI NYUMBANI, SASA WAZEE HAPO FOE NINATUBU NA MIYAMILA PLUS NYAORO.COM WENZAKO MTUPISHE TUNATAKA NJIA.
ReplyDeleteNchi hizi zilizoendelea wana matatizo.wakiongelea nchi za dunia ya tatu wanasema ni maskini sana cha ajabu ukienda mtoto wa kutoka nchi maskini kusoma vyuo vyao vikuu wanakulipisha ada kubwa kuliko ada wanayotoza watoto wa matajiri unaosoma nao chuo kimoja.
ReplyDeleteKama wangekuwa na huruma wangeanza angalau kusema mtu akienda kusoma kwao walau alipe ada inayolingana na raia wan chi au hata pungufu.Lakini kudai ada zaidi kwa maskini ni uharamia.
Na huyo mtoto wa maskini ambaye kajilipia kusoma au kagharimiwa na kufadhiliwa na kodi za wanachi maskini wan chi yake wakimwona ana akili wanampora na kutaka abaki nchini kwao. Yaani wanapora hela za ada za maskini,halafu pia wanapora na mtoto mwenyewe ambaye maskini ndio tegemeo lake ili ajikwamue kama nchi.
Wazungu wanapenda sana kuchukua hela toka dunia ya tatu ndiyo maana hata ukienda kuomba visa wanataka ulete Benki statement wajue una shilingi ngapi za kwenda nazo kupeleka kwenye nchi zao.Mtoto wa maskini hata awe na akili kama Mungu uwezekano wake wa kwenda kwa wazungu kusoma chuo kikuu haupo maana hatakuwa na ka-benki statement kenye pesa za kumdhibitishia balozi.Mavyuo yao ni vitega uchumi nyonyaji tu vya kuchota hela kwa nchi maskini tu.
Hongera Dr. Dr. Nzovu. Wnegine waliopita Havard ni Abrahaman Kinana, Daudi Balali, Andrew Chenge, Fred Sumaye, Obama Snr & Jnr. Ukiangalia utaona ni mchanganyiko maalumu, wapo wa kuigwa, wapo wa kusahaulika na wapo wa kunyongwa, Sijui wewe utafuata route gani?
ReplyDeleteMdau Tumaini, kumbe nilikuwa sahihi nilivyokuuliza kama wazee wa pale chini mlimalizana. Kwa kusoma zile "pepa" na maoni yako, napenda kuamini bado itakuchukua muda hao kina Mwamila, Nyaoro, Mayo, Lema , Msambichaka, "owen" n.k kukuachia. Lakini songa mbele, sisi tunaoamini, imeandikwa, mlango mmoja ukifungwa mengine 12 imefunguliwa, bisha na utafunguliwa.
Mdau Kiwoso
ANON 10:13UPOFU UMESHATUTOKA ILA SIO WOTE NAOMBA TUUNGANE TUWAKOMBOE HAWA WADAU WENZETU EMAIL ME PLS AT TGEOFREY@GMAIL.COM
ReplyDeletekaka jamani hongera kwanza , pili nina maswahili machache hapa nataka kujua :unamiaka mingapi, umeoa, unatafuta mke, au mpenzi, maana natamani mwanamme wakitanzania tena mimi na wewe tunaweza kujenga maisha haswaaaa.naomba namba yako ya simu kaka.
ReplyDeletenatanguliza shukrani
Mimi navoona hajaoa maana kidole cha pete ya ndoa kitupu! na hakionyeshi dalili pete ilikuwepo ikavuliwa maana hamna hata alama.
ReplyDeletembona pumba humu ndani,its one of the best univ in the world but it is NOT the best univ,the number one univ is oxford,then cambridge then havard then stanford..anon 2!
ReplyDeleteJamani mnatuharibia jina la shule yetu, haiitwi Havard bali ni Harvard. Kwa hiyo kuanzia hivi sasa andikeni hivyo na si vinginevyo. Ni mimi Alumni wa Harvard Law School & Princeton University. XXXL
ReplyDeleteHongera kaka, ni hatua kubwa umepiga na kama ukirudi nyumbani na kuisaidia jamii katika ulojifunza utakuwa nu mchango mkubwa sana kwa taifa. je unaweza kuwusiliana nami kunieleza namna ya kujiunga na Harvard Uni? Ninataka kuanza kujindaa ili kijana wangu asome chuoni hapo atakapokuwa...if u don't mind contact me i will be glad...thanks...
ReplyDeletemysmylove@gmail.com
Vyuo mashuhuri kama hivyo kama vinakutaka watakulipia kila kitu, ninamaanisha scholarships na stipend. Waliopita hapo pia ni wachumi wa Tanzania mashuhuri kama Delphin Rwegasira (PhD, 1974) na Justinian Rweyemamu (PhD, 1970). Hamna masuala ya gharama. Hongera bosi!
ReplyDeleteWewe anon wa June 19, 2008 1:18 PM unayeulizia kama kaoa nk nk na kwamba mtajenga maisha mazuri, je na wewe umesoma ama mdaka magoli tu? Hakuna mwanaume anayetaka mwanamke la saba B so kama shule kwako ni kitendawili utategemea vipi kupata kijana aliyesoma? Utashangaa kila siku unattract wabeba maboksi tu maana you are what you attract hahaha.
ReplyDeletehawa ni wadaka magoli,wanaosubiri wanaume waliotoka ulaya.(namjibu anon 8:41)...kwanza hayo yamepitwa na wakati,siku hizi mwanamke kujishugulisha.sasa bibie,wewe anza kujishugulisha sio unakaa unasubiria watu warudi ni digree zao,haifai ivo
ReplyDeletesasa wewe anon 6:32 unachekesha anko.umetoa email yako,sasa unataka akwambie nini,unataka information si ukaigoogle harvard univ uwatumie email wao ndio wao wakujibu
kwa taarifa yenu fupi,hii harvard uni huingii ivi ivi ni top ten,kama akili sio A++ basi wewe ni sorry!bye bye! ukibahatisha kuingia,mambo kule sio pwerere..kila mtu ana akili mwalimu kaongea nusu,anamaliziwa sentensi utajishangaa baada ya siku 2 unadisco
Hongera sana Dr.Ulenga, ninakumbuka ulivyokuwa unatutesa darsani pale Ilboru, yani ilikuwa kivumbi!!!!
ReplyDeleteAnony unayebisha Harvard siyo ya kwanza Duniani, angalia ranks za vyuo Duniani. Usiropoke tu.
ReplyDeleteHavard university ni chuo kikuu cha kwanza duniani kwa ubora kwa vipimo vya 2007.kikifuatiwa na OXFORD,Cambridge,Yale.
ReplyDeleteKatika vyuo 10 bora duniani 7 ni vya marekani vitatu vya uingereza .
Vyuo hivi hivi bora huchukua watoto wenye akili sana Pesa za kifisadi tu hazina nafasi.Kama mwanao akili hana lakini pesa unazo hawezi kanyaga kwenye hivyo vyuo ataishia vyuo vikuu vya India na vya Tanzania na vile vyuo visivyotambuliwa vya marekani na kuishia kubeba mabox na kuwa raia wa daraja la tatu marekani.
kumsahihisha anon wa mwisho...yani huyu wa juu yangu tu! Mbona watu kama Bush walienda Harvard kama hizo university unazodai kubwa zinachukua ma-vichwa tu? Pia wanaangalia jina bwana...sio vichwa tu! They are also institutions...na majina makubwa yasomapo hapo ndipo wawezavyo kuvutia wengi. Kwa iyo usidhani ni akili tu! Hujakosea sana ila statement yako imehitaji marekebisho kidogo!
ReplyDeleteNadhani huwezi kumaindi!
Unajua, kuangalia majina ilikuwa zamani ndiyo maaana watu kama bush waliiingia kwa sababu ya majina ya familia zao. Sasa hivi mtindo huo umekwisha ni merit tu.
ReplyDeletekwa hiyo na Sumaye nae ni kichwa hadi akapata Harvard au? msitake nicheke, shule US ni biashara tu, ukiwa na hela unasoma.
ReplyDeleteProgram aliyofanya Sumaye ni maalum kwa wazee walikwisha tumikia nchi zao. Yeye hakupitia kwenye admission ya kawaida, alipata upendeleo kidogo.
ReplyDeleteTunasikia University of Dar(UD)ni ktk vyuo bora Duniani. Je ni cha ngapi ktk hiyo rank ya Dunia? kwa anayefahamu. Maana vichwa vya nchi yetu ndiyo vipo pale. Shime wadau tufahamisheni.
ReplyDeleteKusema kweli UD haipo kwenye ranking nilizoangalia za top 400. Lkn sio maana kuwa haina vichwa hapo. Zile ranking zinaangalia vitu vingi ambavyo UD haitaweza kuwa navyo kwa mfano Nobel Prize winners, ratio ya wanafunzi to lecturers, research, nk! Kwa iyo hapo tusahau kuiona UD kwenye ranking. University kama Harvard zinatumia millions of US Dollars kwenye research a year...we UD kufikia hapo labda waache ufisadi. Pili kutokana na story za wanafunzi wa hapo inaelekea hao ma-professor wa hapo mazee wamepinda. Maana anaweza kufelisha mtu bila hata ya reason! Kukupa mfano tu...katika list hiyo university za Africa zilizopo huko kwenye iyo top 400 hazizidi tano!
ReplyDeletenimefarijika kusikia kwamba kuna vijana zaidi ya 100 umri chini ya miaka 35 wana shahada za PhD.
ReplyDeletevijana msisubiri wazee wawapishe. infact, bado wazee hao wanahitajika kwani ujuzi haupotei.
katika safari zangu nimewahi kukutana na lecturer ana miaka 90. yeye hata kutumia LCD projector hajui, anatumia slide projector!! ujuzi wake unahitajika kwahiyo bado anadunda.
sasa nyinyi vijana wenye elimu zenu ombeni kazi CHUO KIKUU DODOMA. mkifika huko mfanye "vitu vyenu" ili pawe ushindani kati UDSM vs UDOM.
Chuo chetu cha UDSM hakiwezi kuwepo kwenye ranking hiyo. We fikiria chuo kama harvard budget yake kwa mwaka ni sawa na budget ya Tanzania. sasa utalinganisha na UDSM ambao hawapati hata 5% ya bajeti ya TZ?
ReplyDelete