Hakuna ubishi kwamba kipindi cha PowerBreakfast kinachorushwa na radio ya Clouds FM ni mojawapo ya vipindi vya radio vyenye wapenzi na wasikilizaji wengi nchini Tanzania.


Hivyo basi haishangazi kwamba hivi karibuni watangazaji wawili wa kipindi hicho waliokuwa wamezoeleka,Masoud Kipanya (KP) na Fina Mango, walipopotea hewani maswali mengi yaliibuka.Wako wapi KP na Fina?Maoni na e-mails zikarushwa kwetu tukiombwa kuwatafuta na kujua nini kimetokea na kama wapo likizo tu au inakuwaje?
globu dada ya www.bongocelebrity.com inakupa yaliyomsibu KP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2008

    YAANI HUYU JAMAA AMEJIELEZA VIZURI KWENYE BONGO CELEBRITY NA NATAKA NIKWAMBIE KP HAKUNA KATUNI NAPENDA KAMA YAKO ILA KUANZIA LEO HII NIMEKUSHUSHA THAMANI KABISA NA SENTENSI ULOTIFUA NAYO MWISHONI KUHUSU SABABU YA WEWE KUTAFUTA KAZI NYINGINE WEWE NI MTU MZIMA UNA HESHIMA ZAKO BWANA (CELEBRITY)SASA UNAPOTAMKA KITU KUWA MAKINI SANA SENTENSI CHAFU KABISA UMETOA KWANGU HAINA MAELEZO ZAIDI KUISAFISHA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2008

    BC kama mlivyoamua kwamba mnasubiri kusikia upande wa pili wa shilingi yaani kutoka kwa mwajiri,huo ni uamuzi sahihi kabisa. Wadau makini ni lazima tuyapime maelezo ya pande zote mbili kabla ya kutoa lawama kwa upande husika. Siwaelewi walioanza moja kwa moja kumwaga lawama na kuponda ili hali hawajui ukweli uko wapi. Kwa hiyo BC,tuleteeni haraka sana maelezo ya mabosi wake ili tuyapime na kutoa maoni. Hatahivyo katika hali ya kibinadamu tunapaswa kwanza kumpa pole bwana KP kwa yaliyomsibu kwa sababu kuu mbili bila kujali ni upande upi una makosa.
    1.Kufukuzwa kazi, kimsingi sio rekodi nzuri katika maisha ya utumishi.Ni rekodi ambayo yaweza kuleta tabu hata katika upatikanaji wa ajira nyingine.Hivyo hiyo ni taarifa ya kusikitisha.
    2. Hatua hiyo ni wazi kuwa imeathiri kipato cha bwana KP.Sasa hili nalo ni la kumpa pole maana linaweza kuathiri uendeshaji wa maisha ya siku kwa siku kwake na familia yake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2008

    Habari hii hakika imenipa picha nzuri sana.Nimegundua kwamba Capitalists wote wanatabia zinazofanana awe Mzungu au awe Mswahili au yeyote.
    Kutokana na maelezo ya KP kwamba aliamua(waliamua) kugoma,kwa mujibu wa ufahamu wangu kugoma kazi kwa namna yeyote ile ni kosa kwa mujibu wa Capitalist policy,ila inakubalika kisheria kutegemeana na mazingira ya mgomo wenyewe
    Kugomea kazi kwa sababu ya ubovu wa vifaa au hujuma katika sehemu ya kazi si jambo la busara kwani nadhani kuna namna nyingine mbadala ambazo zingeweza kutumika ili kuleta usuluhishi.Hatua ya kugoma kazi huwa ni ya mwisho kabisa endapo hatua nyingine zitashindikana,ikifanyika awali inaonekana kama ni hujuma,kitu ambacho ni kosa kisheria.
    Hivyo kwa mtazamo wangu bwana KP hapo kidogo mliyumba,maana imewachukua muda mfupi sana kufikia uamuzi wa kugoma kazi.
    Uamuzi wa muajiri kusitisha mkataba katika mazingira hayo inakua ni vigumu kwa upande mwingine kudai haki haikutendeka endapo mwajiri atathibitisha kwamba wahusika hawakufuata taratibu zote hadi kufikia hatua ya kufanya mgomo,na hapo ndipo Capitalist wapotake advantage.
    Binafsi nimefurahishwa na maelezo ya KP,ameonesha ukomavu na uvumilivu,pia wote kwa mujibu wa maelezo ya KP yaonesha ni kwa kiasi gani wanatilia maanani umakini katika kazi kwani kutowajibika ipasavyo kwa watu wa technical ndiko hasa imekua chanzo cha wao kutokuwapo Clouds kwaa sasa,kwa kuwajibika na aibu iliyowapa Studio nzima.
    Ila yaonesha ana siri ndani ya nafsi yake ila ni maadili ya kazi ndiyo yanayokua kizuizi chake.
    Kila la kheri Brother KP,bado unabakia kama mtu aliyebalikiwa vipaji lukuki,na katika Dunia ya sasa upo hatua moja mbele
    gEoRGe

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2008

    KP.KUWA MAKINI NA COMMENT ZETU WENGINE WAMEJIPANGA KUKU DISCOURAGE ILA ME NAKUAMINIA WE WACHUJE TUU SI UNAJUA SIKU HIZI UNAWEZA KUWA WORD YA VICHAA UKAWEZA KU ACESS INTERNET,WENGINE NI ROHO YA WIVU MLISOMA WOTE AFU UMEWAPIGA GAPE,WENGINE WAMETUMWA NA KINA NANIHIII WAANDIKE.
    AKILI,VIPAJI NDO VITAKUTOA MWANA.HAWA WADANGANYIKA WASIKUUMIZE KICHWA WAZURI SANA KWENYE KUONGEA.EPA,RICHMOND...WAMESEMA WEE SO NI KATABIA FLANI HIVI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2008

    LOH! POLE SANA KP, ILA USIJALI WALA USIOGOPE KWANI MAISHA NI MAPAMBANO, PAMBANA. PEACE & LOVE FOREVER!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2008

    Masoud mdogo wangu kwa kweli hata mimi niliwapendeni sana kipindi niko hapo nyumbani..hila kama yametokea yametokea tuu!!wewe bwana kaza buti kwenye kazi zako na mungu atakuongoza!!masoud Mungu kamwe huwa halali!!anaona kila kitu..nakutakia kila la kheri na Mungu akubariki sana..endeleza libeneke la katuni please..kwa wingi,na pia kemea kwa katuni uchawi bungeni..asante sana,dada akupendae norway

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2008

    KP ulikuwa umetoa maelezo mazuri sana,nadhani umeandikiwa,manake LUGHA katika sentensi ya mwisho juu ya sababu ya kukufanya wewe utafute kazi, kama alivyodai anony Saidi wa kwanza hapo juu ni VERY UNPROFESSIONAL.
    Bloggers wengi wanafahamu hili swali huwa linaulizwa mara nyingi kwenye 'intavyuu'Kwamba-"Kwanini unatafuta Kazi sehemu nyingine??"Kipanya ukijibu kama ulivyojibu uta-'feli' ndugu yangu.Tafuta watu wakusaidie au ingia kwenye search engines utafute "Interview Tips".
    Michuzi:Ondoa hii topic,haijengi!
    Merci.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2008

    Nimekuwa nikiamini kuwa KP ni kichwa, na hii nimeidhirisha kwa mara nyingine tena kwa hii interview ya BC.

    Maelezo yake yamejitosheleza na yasio kuwa na kuelemea upande mmoja. Ur smart bro, keep it up.

    u have a bright future ahead of you, stick to ur guns.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2008

    Kuwasilisha mapungufu yanayozorostesha utendaji kazi katika idara yako kwa wahusika ndilo jukumu lako. Kama hali inaendelea na unaona 'reputation' yako inaharibika kwa mapungufu hayo' njia sahihi ni kuacha kazi. Kugomea kazi eti kwa ajili ya kuboresha huduma, sio sahihi. Kampuni ina mwenyewe, inawezekana vipi wewe uwe na uchungu kuliko mwenye mali? Angalia sasa umemchomea mwenzako mpaka kapewa barua ya onyo, si unaweza ukasababisha amwange unga wake? Napenda kazi zako za katuni, napenda unavyojituma n.k, lakini katika hili mh!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2008

    Masoud! kugoma kazi ni kosa la kisheria japo mlikuwa mna haki..Gross Insubordination, failing to report an accident or damage to co propety, abuse company benefits etc, haya yote yakitokea employer anaweza kukususpend au kukudismis. Najua utawala mzima wa clouds ha Joseph Kusaga hawakupenda kuchukua maamuzi hayo labda tafsiri ya maamuzi yenu haikuleta maana kwao..Fina ni miongoni mwa waanzilishi wa Clouds ikiwa pale nasaco leo hii mnaita water front wewe Masoud ukafatia kwenye chuchuchu na Bonda, sidhani kama wamiliki wanafurahia na i believe ktk private sector waajiri wanaopenda maendeleo ya watu wake hasa wanapowatumikia kwa muda mrefu ni Clouds, Boni Luv ametoka mbali na Joseph leo yupo wp? amepewa bonge la shavu sitaki kumention, Charles Muhamiji vilevile na wengine kibao…Fina leo ana kampuni yake One Plus Communication, wewe Masoud KP Wear pia na wengine kibao…huku sie tulipo tukianzisha kampuni wakati tupo ndani ya ajira basi ujue siku za ajira yako zinahesabika….Masoud na Fina najua maisha yataendelea na kuwa kama ndoto zenu zinavyowatuma…Clouds imetoka mbali na walioanzisha Clouds ni wachache waliobaki na wengi wao waliondoka bado wanakula kuku..Taji,Christina Moshi aka Seven,Terence,Boby,Jimy,Jide, Ray C,ML Chris,Baina Kamkuru…RIP Kiza na Amina…jama yaliwowakuta Masoud na Fina ni ajari katika pirika za maisha…tumshukuru Mungu kwa Yote.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2008

    People u gotta grow up..Kama kakosea kwenye interview mwambieni kistaarabu sio kusema eti kuanzia siku hiyo unamdis-value kutokana na sentence moja tu..WTF? mara ngapi ma-celebrity kibao wakiwemo marais wa mataifa yenye nguvu duniani wanakosea na watu hawasemi eti wamewashusha thamani?nobody is perfect..kama kakosea kuongea mshauri sio kuponda! idiot...

    Masoud mlichofanya ni sahihi kabisa, nakumbuka ile live mliyokuwa mnafanya toka dodoma bungeni ilikuwa kati ya live mbovu sana kuwahi kuiskia hasa siku ile mnaongea na PM pinda nilituma text ya maoni siku hiyo nikadhani mtairekebisha..Hiyo ya balozi wa unyamwezini sikuiskia kwa hiyo siwezi kuitolea maoni.

    Nways, Kama Gerrard kaamua kuwasaliti na kuendelea na kazi achana nae..wewe na Fina ndo mlikuwa roho ya kile kipindi, hata ukiskiliza sasa hivi utagundua kinaboa na ni ngumu kukizoea kipindi mimi siku hizi nasikiliza east africa power breakfast ya East africa radio manake ssebo nae yuko so comedy kama wewe.Nakushauri usitafute kazi ya kuajiriwa, kuna mdau jana aliwashauri mnunue muda kwenye edio yoyote kama anavyofanya john dilinga najua mtatoka tu.

    Na kama tbc wakiwataka msikatae, u got talent zaidi ya hata hao ze comedy...comedy ya mwaka jana sio sawa na mwaka huu lakini power breakfast ya kila mwaka ilikuwa inapanda chat!

    Keep it up Guys...mlango mmoja wa riziki ukifungwa mwingine hufunguka.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2008

    Ni Mimi Gebo Arajiga wa Arusha.

    Swali ninalojiuliza ni kuwa je?huko TBC watakuwa na uhuru wa kuzungumza kama walivyokuwa wakizungumza katika kipindi chao cha Power Breakfast cha Clouds Fm au ndio wanataka kunyamazishwa wewe Kp uhuru wako unaenda kubwana huko TBC

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2008

    Nadhani watu wengine wakuwe na waanze kuwa kama miili yako katika kufikiri na matendo... kama wewe kaka hapo juu David Villa.. yani watu wengine sijui mpo tuu kukosoa tuu wenzenu kumbuka hamna alie kamilika... as long as u get da point that's all that matters na sio lazima kuandika anyways, unaweza kubaki msomaji tu kama wengine, lol
    Go KP, Mungu akutangulie mwaya

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 19, 2008

    Kusema kweli mimi kwa upande wangu nilikuwa nakipenda kipindi cha Power breakfast kwa ajili ya Masudi, Fina na Hando. Lakini kama unavyojua mafiga matatu. Ukiondoa moja tu umeshaharibu. Sasa sikwambii ukiondoa mawili nadhani jibu litakalo patikani ni baya zaidi. Sasa hivi sina tena hamu ya hicho kipindi, maana nadhani hata Hando kuna kitu anamiss katika utangazaji wake. Tunaomba Kusaga afikiri zaidi ili hawa jamaa warudi. Keep it up Fina na Masudi

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 19, 2008

    Anonymous, June 19, 2008 10:45 AM:

    Huyu ndio ametoa ushauri makini!! soma tena na sote tuelewe hata kama tunahaki basi kuna njia nyingi za kutetea hiyo haki..kwenye business hakuna democracy kama kwenye siasa labda enzi zile za ujamaa ambapo siasa hizo zilichangia kufa kwa mashirika mengi. Employment inahitaji nidhamu....

    soma tena blog ya huyu jamaa "Masoud! kugoma kazi ni kosa la kisheria japo mlikuwa mna haki..Gross Insubordination, failing to report an accident or damage to co propety, abuse company benefits etc, haya yote yakitokea employer anaweza kukususpend au kukudismis."

    Tujifunze nasi wengine.. Hata ningekuwa mimi mtu akinigomea namfukuza..akajifunze nidhamu na asije ambukiza wengine..

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2008

    im proud of you kipanya, umetoa maelezo kwa ufasaha sana, hongera kwa kuwa muwazi!! Mungu atakufungualia mlango mwengine, na utaendelea kupeta, au sio kakayangu!! hujamponda mtu, umeeleza kinaga ubaga, big up.

    nana

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 19, 2008

    Anonymous wa June 19, 8:43 AM

    UMENINIFURAHISHA SANA - YOU MADE MY DAY.

    NI KWELI COMMENT NYINGINE HUMU ZINATOKEA MIREMBE!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 19, 2008

    jamani hawa Fina na Masudi wasiwafanye wajinga ni kwamba wamepata mkataba mnono TBC radio na mtawasikia soon.. msiwe vipofuuu hizo ni sababu tu walizipanga.
    mkereketwa..

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 19, 2008

    nawapongeza sana kwa uamuzi wenu, nilisikiliza ile interview nikashangaa,ilikuwa mbaya!mbaya!mlifanya uamuzi wa busara na nataka niwatie moyo kuwa maisha siyo clouds pekee,wako watu wengi wana maisha yao mazuri tu hawafanyi kazi clouds, your still young u have so many opportunities. pia sikujua kama management ya clouds iko kama ya kihindi hakuna security ya kazi. wamegoma madaktari wenye kuokoa maisha ya watu na wakarudishwa kazini sembuse mtangazaji... Achaneni nao hao wapenda cheap labour, maisha popote.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 19, 2008

    Michuzi hii nitakayokupa usifikiri nimetunga,

    Mi ni mfanyakazi wa Clouds Fm na hiki ndicho kisa halisi cha wao kutimuliwa,

    Hawa Jamaa wamekua wakishupalia sana issue zinazohusu wakubwa kwenye kipindi cha PB mpaka kifikia kul;eta uhasama kati ya hao Wakubwa na Mr. Kusaga,

    Nafikiri wote mnafahamu kua Kusaga ni mfanyabiashara mkubwa tu, na sifa ya biashara ni ku-maximise profit (minimise of expenses).

    Nchi hii ni ngumu sana (near to impossible) kufanya biashara kihalali ukafanikiwa hivyo cha maana ni kujiegemeza kwa wakubwa.

    Biashara za Mr. Kusaga zilishaanza kuyumba baada ya wakubwa kumbana mambo flani, na zaidi ni sababu ya Kipindi cha hawa Jamaa.

    Ndio kusema kua walikua wakitafutiwa kosa siku nyingi tu lakin ikashindikana,

    Sababu alizotoa Masoud ni chache tu lakin sisi wafanyakazi wa Clouds Ent. tunazijua nyingi tu sema tu Masoud hajataka kuzitaja.

    Sababu nyingine ni Celebrity ya Masoud over his Boss Mr. Kusaga and tha Whole Management team. Hii haina ushahidi sana lakin pia imechangia kwa kiasi,

    Ni wengi tu tunamjua Kusaga lakin si sana kama Masoud.

    Inafikia hata mahali kama mtu ana issue na Clouds Fm anawafata kina Masoud badala ya Uongozi.

    Naandika haya kwa uchungu nikijua nitamiss kaka yangu Masoud na dada Yangu Fina lakin yote maisha tu,

    Nachowaomba ni mafanikio katika maisha yenu ya mbele kwani "kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi"

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 19, 2008

    mimi naomba muwe watulivu wa kipindi hichi masoud na fina watu wanawapendeni sana tena sana likitokea dili mkapige nianchowashauri kama mtaweza kununua muda kwenye radio yoyote safi mtatoka sana 3hrs zinaawatosha kabisa nawapenda sana MASOUD NA FINA yaliotokea yametokea songeni mbele kwa mbele

    Mi namfahamu GERADY toka yupo mbezi ni mtu wa kung'ata na kupuliza sana sana sana ni mtu wa kubabaikia hali ya watu fulani ili aonekane yupo juu ivi ana proffessional gani achaneni naye kwanza kashapandisha KENCH hana muda hata ivyo mngemtaabisha bure hawezi tena pilika pilika kila saa kukohoa studio.

    KP na FINA nawatakia maisha mema na pilika pilika zenu tupo tutawasaport

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 19, 2008

    Huyu annon wa June 19, 2008 2:30 PM, ambaye ni mfanyakazi wa Clouds ndie amesema ukweli mtupu, manake nilikuwa najiuliza kosa la kutaka kupewa vitendea kazi bora inakuwa issue ya kufukuzwa kazi? Usomi ni pamoja na kutambua kile kilicho nyuma ya unachokiona mbele ya macho yako, namshukuru Mungu huyu mfanyakazi ametufumbua macho. Mimi huwa sina kawaida ya ku-comment humu ila leo nimeona niseme ukweli kuhusu ili suala la biashara za Bongo kutegemea wakubwa wa serikali. Mimi nafanya kazi kwenye Multinational company moja hapa Europe, haina haja ya kuitaja jina kwa sababu zilizo wazi, na mimi nimeweza kuwa kwenye board inayohusika na investments nchi za nje. Kwa kuwemo kwangu kwenye board of investments, niliishawishi kampuni yetu tuangalie uwezekano wa kuwekeza Tanzania nikiwa na lengo moyoni mwangu kwamba tuta-create ajira na kulipa kodi hapo nyumbani na huo ndio uwe mchango wangu kwa watanzania wenzangu na serikali. Tulipoanza follow up ya kufungua branch hapo, wakubwa serikalini wanaohusika na hiyo sekta walituwekea vizingiti ambavyo vilionyesha kwamba tuwape 10 parcent! Ethics za kampuni yetu ni kufanya biashara bila kujihusisha na corruption, tulipokaa kikao cha bodi tena, ikaonekana tuachane na Tanzania na tuangalie uwezekano wa kuwekeza Afrika Kusini. Iliniuma sana, manake huu ni mradi mkubwa sana, unategemea kutoa ajira zaidi ya 3,000 na utazidi kupanuka. Kwa vikwazo vya wachache ikawa ni lost opportunity! Na hapa naona the same big shots wameweza kuwafanya vijana wetu wakapoteza kazi zao. All the best KP and Fina!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 19, 2008

    Tatizo la wabongo ndio liko hapo mtu anapojaribu kuleta emotions kufunika matatizo ya mtu wote humu ndani mnamsifia kp na kukandamiza uongozi kutokana na maelezo ya kipanya hata mimi ntakuwa mwongo nikisema siko upande wake ila maelezo tuliyoyapata ni ya upande mmoja wote tunajua kp anatoa katuni nzuri zenye uwezo lakini pia changes katika kufanikisha jambo ni kitu muhimu sana nyinyi wote humu ndani naona tu mnatumia emotions na mapenzi yenu kwakwe vipi kuhusu sie ambao tumesikiliza mara moja kipindi chake na kuona ujinga tu unaendelea mle ndani? na kutafuta stations zenye mvuto zaidi pia anony wa kwanza kabisa nakubaliana na wewe sababu za huyu kijana kutafuta kazi nyingine ili watoto waende chooni ni sawa tunajua kabisa watoto wanatakiwa wale waende chooni je kulikuwa na ulazima wowote yeye kutumia hiyo sentensi kuna utani wa kipumbavu sana unaendelea ktk hiyo nchi isiyojua nini inataka PUMBAF.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 19, 2008

    we anon uliyezungumzia sheria we ndo bogazi kweli kweli umeagalia upande wa defendant peke yake na si wa plaintiff. plaintiff pia ana mawakili wake acha ushamba endelea kuwasoma wakina winfield na Hadden
    usifikiri wote tumelala.

    masoud dogo mmmh songambele huku ukimtumaini bwana mungu nasema songambele ...........

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 19, 2008

    RUDI SHULE!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 19, 2008

    TATIZO LA KIUFUNDI HALIKUHUSU KP KWANI WEWE NI MUAKILISHI WA CLOUDS WAACHE MAFUNDI WASHUGHULIKIE KWANI TATIZO LA UFUNDI LITA AFFECT CLOUDS SIO KP AU FINA MANGO.KOSA LAKO ULILOLIFANYA KUGOMA NI KUBWA KULIKO HILO TATIZO LA UFUNDI. Na kama wazo lako la kugoma umetoa wewe umemponza mpaka FINA.Kwa ukweli halisi ulichokifanya ni unproffesional na wana haki ya kukufukuza kosa ni lako.
    Ukipata kazi nyingine waache wahusika washughulikie matatizo yao kila mtu ana cheo chake na wajibu wake.
    Mdau mzawa.
    Kosa lako sawa sawa na mchezaji kugoma kuendelea kucheza kisa kuna mtu fulani anafungisha ,hilo swala unamuachia kocha usichukue maamuzi mwenyewe lol

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 19, 2008

    watuwengine humu ndani kujifanya wajuaji sijui maana yake nini.....sasa hiyo sentesi ya mwisho ya kp inatatizo gani? that got nothing to do with profetional,yeyote anaelewa misemo yakiswahili atajua kua anamaanisha anatafuta kazi ili aweze kuendeleza maisha kubwa lamsingi kwake ni kulea wanawe wapate mahitaji......je wewe mjuaji utawapa kitu watoto wako pasipo sourse ya income?ndi mijambazi yenyewe nyinyi

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 19, 2008

    Hao wanaomlaumu Masoud kwa sentensi ya mwisho katika majibu wananishangaza sana, waelewe hapo hakuwa kwenye interview ya kutafuta kazi ambayo ni lazima atumie lugha fasaha. hapo hajatukana, kwani kwenda chooni ni matusi?
    Na huyo anayesema kuna jinsi ya kujibu swali la "kwanini utafuta kazi nyingine?" kwenye interview, mbona amejibu sawa tu? majibu yanaweza kuwa kama yafuatayo; 1. I need to see myself GROW carrierwise (meaning face new challenges), 2. Earn more money (INCOME)ambayo ndiyo watoto wanaitegemea ili wale na waende chooni 3. Geographical relocation i.e. could be moving to another place 4. There could a problem at your current job that the only solution is for you to look for another job 5. Achieveing your goals, may be on your current job you dont see the opportunities for that, etc, etc...

    All in all, kwa kina Masoud na hata management lazima wakubali kila chenye mwanzo kina mwisho, na mwisho wa kimoja ni mwanzo wa kingine, cha msingi ni kupanga mikakati ya kukibali kitu kipya mbele yako. Kila la heri kwa hizo pande zote mbili.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 20, 2008

    Masudi na fina kazi kweenu.

    Punguza ulevi wa sifa maana hii ndo iliwaponza na mkagoma mkifiri hamuwezi kuchukuliwa hatua.wewe wasema hujalewa sifa,inawezekana hujui au unaogopa kusutwa,si rahisi kuliona banzi jichoni mwako

    Ni vizuri watu wamekusifia kwamba mchapa kazi,celebrity nk.Jihadhali saana na sifa hizi maana zaweza kukupoteza zaidi.Haya mambo yakuitwa celebrity yanawaharibuni,hivi kwani kila mtu clouds ni celebrity kwanini na wanani?

    Hivi mfanyakazi wako mmoja hapo dukani kwako angegoma na kufunga duka bila wewe kuwa na taarifa ukakosa mapato na inawezekana bila sababu za msingi ungechekelea tu?

    Kwakuwa umeeleza unachofikiri ndo kilitokea,nakushauri kaa kimya fanya mambo yako usijeibua mambo mengine.

    MSEMA HUCHAGULIWA KUWA DIWANI

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 20, 2008

    Anon June 19, 2008 4:39 PM
    Muajiri anaporevoke mkataba wako ujue amefata taratibu za kisheria na ukimuuliza Masoud atakuwa amelipwa malipo ya kusitishwa mkataba wake "notice of termination" kusema huyo mchangiajia amebase kwa defendant...sheria za kazi zinasema kanuni na sheria za utii kazini hao washikaji hawakumtii muajiri wao...Kama ivyo basi Mwambie MAsoud atafute mwanasheria uone atafikia wp. Mabwege wengi humu wamezowea kudis bila kuangalia tatizo zima...Joseph amewabeba mno kina Masoud na Fina na kwa kulinganisha ajira binafsi wanahitaji kumshukuru...Fina alianza kama mtangaziji msaidizi tena vipindi vya usiku mpaka akawa producer, marketing manager etc...kwa mtizamo wako mshahara wa mtangazaji wa kawaida wa redio unaweza kuwafikisha hao waungwana hapo walipo? hao wametimuliwa wanapo pa kujishikiza je wengine ambao leo tungewaona na baasha zao za kaki wakiranda kutafuta ajira mpya.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 20, 2008

    Hatimae wawakilishi wa CLOUDS wameongea.........


    Anonymous June 19, 2008 2:30 PM,

    Anonymous June 20, 2008 12:37 AM,

    Anonymous June 20, 2008 8:41 AM.


    Tatizo, mbona hawataji majina yao?

    ReplyDelete
  32. please inform, who is Ruge in clouds fm ie his corporate power etc.Did he agree with Kusaga's decision.Kipanya your comment about reason for looking for another job was not decent, please respect your kids

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...