PAKA BADO KALALA JIKONI HAPA NESHNO KWANI SI TAIFA STARS WALA CAMEROUN ALIYEPATA BAO.
MASHAMBULIZI NI YA ZAMU, ILA WACHEZAJI WA STARS WANAKUWA NA KIGUGUMIZI WANAPOINGIA KWENYE 18 YA ADUI. TAYARI STARS WAMESHAPATA KONA MBILI AMBAZO ZOTE HAZIJAZAA MATUNDA.
HIVI SASA NI DAKIKA YA 75 NA DAN MRUANDA KAANGUSHWA NDANI YA 18 KWA MAKUSUDI, LAKINI REFA KAPETA. SI MAKELELE HAYO...PENATI... PENATI!!!!. LAKINI WAPI
LAKINI GEMU TUNAWACHEZEA NUSU UWANJA NA DAN MRUANDA KAWAKOSAKOSA TENA SASA HIVI. DAH!
KILA MTU ANA RAHA HIVI SASA NA WENGINE WANATANIA KWAMBA HATA WAKITUFUNGA HAINA NOMA. KUMBE NI BINADAMU KAMA SISI NA PIA WANAFUNGIKA KABISA.
DAN MRUANDA KAANGUKA CHINI NA ANATOLEWA NJE KWA MACHELA. KOCHA MSAIDIZI WA CAMEROUN THOMAS NKONO AMEANZA KUMZONGA KIBENDERA.
ABDI KASSIM 'BABI' AMENGIA KUCHUKA NAFASI YA NIZAR KHALFANI AMBAYE RIGOBERT SONG ALIMPANIA KUTWA NZIMA LEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2008

    Tutawafunga dk ya 87 kwa goli la Abdi Kassim! Mchawi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2008

    Huyo Mrwanda mbona alikua anarukaruka tu naona unampa fagio saaana,sijaona alichofanya zaidi ya hutunyima raha tu leo,binafsi nimevutiwa na Shadrack Nsajigwa "Fuso".Huyu anaahitaji vitu vidogo tu ili akamilike.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...