Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi 4,353 milioni.

C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa:-
1. Mheshimiwa Spika, inapendekezwa kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura ya 147 kama ifuatavyo:-

(i) Kupunguza kiwango cha Ushuru wa Bidhaa kwenye mafuta mazito ya HFO kutoka Shilingi 117 kwa lita hadi Shilingi 97 ili kupunguza gharama ya uzalishaji viwandani, na kuongeza uwezo wa ushindani wa bidhaa zetu katika soko;

(ii) Kurekebisha mfumo wa kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye magari kutoka mfumo wa sasa wa kutoza ushuru wa asilimia 10 kwa magari yenye ukubwa wa ingini unaozidi cc2000 na kuwa na viwango viwili vya asilimia 5 na asilimia 10 kama ifuatavyo:

(a) Magari yenye ujazo wa ingini usiozidi cc1000 hayatalipa ushuru wa bidhaa;
(b) Magari yenye ujazo wa injini unoazidi cc1000 lakini hauzidi cc2000 kiwango cha ushuru kitakuwa asilimia 5 ya thamani ya gari;
(c) Magari yenye ujazo wa ingini unaozidi cc2000 kiwango cha ushuru kitakuwa asilimia 10 ya thamani ya gari.


(iii) Kurekebisha kiwango cha ushuru wa bidhaa katika huduma za simu za mkononi kutoka asilimia 7 ya gharama ya matumizi ya huduma, hadi asilimia 10 ya gharama hiyo. Sababu kubwa ya rekebisho hili ni kwenda sanjari na mfumuko wa bei (adjustment for inflation);

(iv) Kurekebisha kwa asilimia 12 viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zinazotozwa ushuru huu kwa viwango maalum (specific rates), isipokuwa zile za mafuta ya petroli. Viwango vya sasa na vile vinavyopendekezwa ni kama ifuatavyo:

(a) Vinywaji baridi kutoka shilingi 48 kwa lita hadi shilingi 54 kwa lita;

(b) Bia inayotengenezwa na nafaka ya hapa nchini na ambayo haijaoteshwa, kutoka shilingi 173 kwa lita hadi shilingi 194 kwa lita;

(c) Bia nyingine zote, kutoka shilingi 294 kwa lita hadi shilingi 329 kwa lita;

(d) Mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, kutoka shilingi 940 kwa lita hadi shilingi 1,053 kwa lita; na

(e) Vinywaji vikali, kutoka shilingi 1,394 kwa lita hadi shilingi 1,561 kwa lita.
(v) Kurekebisha viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye sigara kama ifuatavyo:-
(a) Sigara zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kutoka shilingi 4,775 hadi shilingi 5,348 kwa sigara elfu moja;

(b) Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kutoka shilingi 11,266 hadi shilingi 12,618 kwa sigara elfu moja;

(c) Sigara nyingine zenye sifa tofauti na (a) na (b) kutoka shilingi 20,460 hadi shilingi 22,915 kwa sigara elfu moja;
(d) Tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara (“cut filler’) kutoka Shilingi 10,333 hadi shilingi 11,573 kwa kilo; na
(e) Ushuru wa “Cigar” unabaki asilimia 30.

D. Sheria zinazosimamia Kodi za Magari
2. Mheshimiwa Spika, inapendekezwa kufanya marekebisho yafuatayo katika kodi za magari:-

(i) Kupunguza viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari kama ifuatavyo:-
(a) Kwa magari yenye ujazo wa ingini usiozidi cc500 kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 30,000;

(b) Kwa magari yenye ujazo wa injini unaozidi cc500 lakini hauzidi cc1500 kutoka shilingi 80,000 hadi shilingi 50,000;

(c) Kwa magari yenye ujazo wa injini unaozidi cc1500 lakini hauzidi cc2500 kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 120,000;

(d) Kwa magari yenye ujazo wa injini unaozidi cc2500 lakini hauzidi cc5000 kutoka shilingi 330,000 hadi shilingi 140,000; na

(e) Kwa magari yenye ujazo wa ingini unaozidi cc5000 kutoka shilingi 175,000 hadi shilingi 150,000.

(ii) Kusamehe ada ya mwaka ya leseni za magari kwa matrekta ya kilimo

(iii) Kuongeza viwango vya ada ya usajili wa magari kutoka shilingi 27,000 kwa pikipiki na shilingi 90,000 kwa gari, hadi shilingi 35,000 kwa pikipiki na shilingi 120,000 kwa gari. Ada hii inalipwa mara moja tu na mwenye gari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2008

    Nothing but some kinds of euphenism,the reality will be seen after 2 or 3 months,i guess

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2008

    ADA YA MWAKA LESENI ZA MAGARI,SERIKALI NAIPONGEZA.HASA ZILE GARI ZA CC2500-CC5000.ILIKUWA NI NOMA.MAMA MEGHJI UPOO?CCM OYEEEEE.
    BIA,SIGARA,SIUJUI POMBE KALI NI ANASA TU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2008

    Bajeti ni nzuri na imetengenezwa kitaalaamu kuliko ile bajeti uchwara takataka ya mwaka uliopita.

    Ila serikali inabidi ianze kutengeneza budget inayotoa "incentives" kwa wasomi na watu wa mijini wapende kilimo na kuwekeza kwenye kilimo.

    Kupandisha marupurupu (incentives) ya wafanyakazi wa serikali ili kuwahamasisha wapende kufanya kazi kwa juhudi bila kutoa marupurupu kwa wakulima ili wahamasike kulima na wapende kulima kwa juhudi zaidi sidhani kama kutabadilisha sana uzalishaji katika nchi.Tufikirie namna ya kutoa incentives kwa wakulima kuliko maofisa waaandika makaratasi wa serikali.

    Kwa ufupi bajeti hii mapato yake itategemea zaidi watu wa mijini kuifanikisha.(CITY AND TOWN CONSUMERS OF GOODS ) ambao ndio wenye hela za kunywa pombe,kunywa soda,kuvuta sigara na kuagiza magari mitumba kijapani ili waendeshe kwa mbwembwe wawakoge wakulima vijijini.

    Hii BUDGET ni CITY AND TOWN ORIENTED kwa utegemezi wa mapato.

    Lakini kwa Upande wa matumizi naona inaweza kuwa "Rural Expenditure oriented" kama hizo pesa zilizotolewa nyingi kwa budget za barabara zitatumika kujenga barabara za maeneo ya vijijini na mikoa inayozalisha kwa wingi.Lakini kama sehemu kubwa ya pesa hizo za bajeti zilizoko kwa ajiri ya barabara zitatumika kwa ujenzi wa barabara za mijini na vichochoro na majiji kama Dar es salaam hapo hakutakuwa na maana yoyote utakuwa ni uhuni na upuuzi usiosaidia uchumi kufunguka na kuuamsha.Sijajua mchanganuo wake kwenye eneo hilo la ujenzi wa mabarabara ndio maana nimesema yaweza kuwa rural oriented kama........

    Kwa ujumla bajeti nzuri serikali imejitahidi safari hii.Hongera Raisi Kikwete.Safari hii sikuzomei nakupongeza.Sasa hivi nadhani wataalamu wa bajeti hawajaangusha.Hata wabunge watakaojadili hii budget wana kazi ya ziada maana akili iliyotengeneza hii budget ni kubwa.Yataka mbunge akitaka kuijadili atafute ma-consultants vinginevyo ataishia kutoa pumba tupu bungeni.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2008

    Lets Face it.Hii Bajeti ni SIFURI.nikiwa na maana ya kwamba hakuna lolote jipya kimfumo katika Bajeti hii.Kwa kiasi kikubwa ni MARUDIO YA YALE YALE ya miaka yote iliyopita.Kodi zaidi kwa bidhaa zilezile kama Bia,Sigara,Soda na hata kama Mafuta ya Petroli yanaonekana kama hayakuguswa lakini ukweli ni kwamba Bei ya Mafuta itazidi kupanda juu!Imesemwa kwamba Wigo wa Kodi utapanuliwa zaidi lakini papo hapo imetamkwa kwamba kupanuka kwa wigo huo wa kodi kutategemea kasi ya kukua kwa uchumi(?).Vichocheo katika sekta ya Kilimo havikuwekwa wazi mbali na kutamka kwamba asilimia 6% ya fungu la bajeti katika Kilimo litafidiwa na kile kilichotengwa katika sekta zingine(?) na kuelekezwa katika Kilimo.Bajeti ipo kimya kabisa kuhusu sekta ya viwanda.Ipo kimya kabisa kuhusu suala la kutengeneza Ajira Mpya.Na awali ya yote haikutanabaisha wazi KIWANGO CHA TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA NCHINI NI KIKUBWA KIASI GANI(what could be the current official Unemployment Rate in the country?What measures have been put in place to solve the 'Unemployment Crisis'facing the illtrained and semi skilled Youths in our country in the face of fast growing global Labour Mobility?)Achilia mbali kiwango cha Inflation kilichotajwa,na annual GDP growth rate wanayo ijua wao!Wapi Bajeti au annual economic survey ya 2007/08 imezungumzia kuhusu mpasuko baina ya wenye kipato kikubwa sana na wale wenye kipato cha dola moja kwa siku hapa nchini(the current pattern of income distribution in the country or matters of growing income inequality among various income groups in the country)na athari zake katika uzalishaji na utengamano katika uzalishaji mali hapa nchini?Bajeti au Mapitio ya Hali ya Uchumi(annual economic survey)yasipo zungumzia kuhusu hayo HIYO NI BAJETI GANI?.Leo asubuhi nilikuwa nafuatilia Habari za Kimataifa katika TV Channels mbalimbali ulimwenguni,sikuona hata katika TV Channel moja ambako Habari za Bajeti ya Tanzania zikizungumziwa au kutolewa vidokezo(news highlights) lakini cha ajabu ni kwamba Bajeti zote za wenzetu wa Uganda na Kenya zilizungumziwa na kutolewa comments-vidokezo(?).Hiyo ilikuwa ina ashiria kitu gani?abda watanzania wenzangu watanisaidia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2008

    Bajeti ni maneno yanayoambatana na pesa.Huwezi kuwa na maneno mengi yasiyoambatana na pesa.Visingeainishwa vitu vingi wakati uwezo wa kuvigharimia kipesa haupo.Ukiona kitu hakipo kwenye bajeti ujue uwezo wake kugharimia haupo ndiyo maana kikaachwa kuongelewa.

    Bajeti hii ni ya kimaskini kulingana na uwezo uliopo.Maskini huwa na vipau mbele vichache ndicho kitu bajeti hii imefanya.

    Kuhusu bajeti kutotangazwa na vyombo vya kimataifa hilo ni juu yao vyombo vya habari.Ni uhuru wao wa habari kutangaza au kutotangaza.Sasa kama wameamua watangaze ya kenya au uganda na kuacha ya Tanzania ni uhuru wao.Islaumiwe nchi au wao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2008

    EBWANAAEE HUKO BONGO HAKUNA VINYOZI?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2008

    Dawa ni kuweka permanent tax kwa muda fulani kabla hazija expire. Huu mpango wa kubadili tax bracket kila mwaka hazina maana yoyote sababu huwezi kucontrol impact yake katika economy.

    Ni vizuri kuwa na budget, lakini kubadilisha tax code kila mwaka that is total crazy.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...