Natanguliza salaam zangu za dhati kwako Mh Mbunge, wilaya ya Mwanga.

Kumekuwa na tatizo la wanakijiji wa Mamba-Ugweno kuumwa na mbwa anayedhaniwa kuwa na kichaa cha mbwa. Habari nilizonazo ni kwamba mpaka hivi leo kuna watu wasiopungua watano(5) na mifugo kadhaa kushambuliwa na mbwa huyo.

Lakusikitisha ni kwamba mpaka hivi sasa uongozi wa wilaya (Hospitali) haijaweza kuwapatia chanjo wale walioathirika, pamoja na kuwa wamefika hospitali ya Usangi na kuambiwa ya kuwa hakuna chanjo hiyo. Aidha hakujawa na hatua yeyote ya kudhibiti ugonjwa huo. Ni wazi kwamba afya za wakazi wa Mamba na vijiji vingine vya jirani ipo hatarini huku hakuna hatua za haraka zilizochukuliwa.

Tafadhali nakuomba uliangalie jambo hili kwa makini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuna uwajibikaji katika wilaya yetu kutuko ngazi ya kijiji mpaka mkoa. Wananchi wanastahili kupewa huduma muhimu kama za chanjo ya kichaa cha mbwa ambayo bila hilo afya zao ziko mashakani sana.

Wapo wanakijiji walioweza kutafuta chanjo hiyo kwenye maduka ya dawa kwa gharama zao wenyewe, lakini wapo pia ambao hawana uwezo wa kununua chanjo hiyo. Ni vipi wananchi waone umuhimu wa kununua chanjo hiyo hali kwamba uongozi wa hospitali ukiwa hauoni hilo? Je jambo hilo si la dharura?

Natumai suala hili litakugusa na kulishughulikia haraka iwezekanavyo.

Mwisho, Kwa wale waliotumia gharama zao kununua chanjo hiyo, gharama zao zitarudishwa na uongozi wa hospitali ambao haukuwa makini kwa hilo? Nini tamko lako juu ya suala hili kwa uongozi wote wa Wilaya yetu?

Ahsante,

Ombeni Msangi
Mwanakijiji cha Mamba-Ugweno.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2008

    Wapare bwana ndio oja mmeona ya kuleta huku!!! Kweli wapare ni wapare tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2008

    sasa mbunge mpaka aje kwa michuzi si mbwa atakuwa ameishamaliza watu wote kijijini.mpigie simu kama kweli kuna tatizo.

    ReplyDelete
  3. Hatua sahihi ilikuwa ni kuwasiliana na uongozi wa Afya wa Wilaya au Mkoa.

    Nimewasiliana na wahusika wanaoshughulikia masuala haya Wizara ya Afya, wakaniambia wana taarifa.
    Natumai tatizo hili litashughulikiwa.

    Mdau
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2008

    Ndugu Ombeni Msangi, namna-ani avae! Haya kweli ni mambo ya kupeleka kwa mbunge. Kwa hiyo mbunge afanye nini, aje kusaidia kufukuza mbwa mwenye kichaa?

    Suala la kwanza kuzuia kusambaa kwa huo ugonjwa hata wewe unaweza kumthibiti huyo mbwa hapo kwenu Mamba.
    La pili, afya ya wagonjwa ni muhimu na si lazima dawa zitoke serkalini ndiyo afya yao iwe bora. Kama ulivyoweza kulileta hili suala hapa kwa Michuzi, ungeweza kulipeleka vile vile kwa wahisani kadhaa kusaidia upatikanaji wa dawa kuokoa maisha.

    Wa-Pare kwa kesi na ubishi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2008

    EEEEhhh ndio za wapare hizo. Tunaziita MBURI. Ukiishi kule ni burudani tosha. Wanajifanya wajanjaaaaaa kumbe maneno tu na makesi yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

    Utawaona tu eti anataka uiongozi uwajibike kutoka ngazi ya kijiji hadi mkoa wakt amesshasema mbwa kauma wanakijiji na kamuandkia mbunge sasa hapo mkoa ufanyeje.

    Halfu si ajabu kapigiwa simu na mwenzake huko kijijini. Unamsikia eti anataka waliojitibu walipwe fidia na wasipolipwa watakwenda mahakamani.

    Kila la kheri wapare wangu. Inaelekea kampeni za ubunge zilishaanza hivyo unamtafutia kasoro mbnge kwa vile mbwa ameuma watu.

    hahahahahhaaaaa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 16, 2008

    huyo mbwa si muueni.manake mbunge wenu huenda hataiona meseji hii kwenye globu(kama huwa anaingia huku).au manbo ya kipare ya kununua kesi?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2008

    Wewe Mpare Ray wa dc tumekupata vizuri na hiyo stori

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2008

    Wewe Faustine, hao jamaaa wanaelewa nini kilitokea huko kijijini. Sasa unaposema uongozi wa wilaya uarifiwe wakati wana taarifa hizo bila ya kuchukua hatua zozote unafikri hiyo ni sahihi? Na kama kweli wewe ni daktari, unasemaje kwa wale ambao hawana uwezo wa kununua chanjo hiyo? Inamaana wasubiri kufa wakati serikali ya wilaya inauwezo wa kuchukua hatua za kiutendaji jushughulikia suala hilo?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2008

    Ombeni mwanakijiji gani hali kwamba upo hapa Meryland! Au umeambiwa kwa simu kutoka huko, mimi thithemi.
    Ok, lakini kwa suala kama hilo hongera kwaniwahusika washughulikiwe kwani hawawezi kucheza na uhai wa watu babake.
    Big up! Watanzania lazima tubadilke na kuwa na desturi za uwajibikaji.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2008

    jamani acheni swala la kuumwa na mbwa mi nilishaumwa duu nilikoma hii uduma inapatikana bure chakusikitisha niliambiwa nikanunue dawa nikaelekezwa na duka la kununua nikienda duka lingine linaniambia hizi dawa tumekatazwa kuuza kwani huduma inapatikana bure serikalini ikabidi niende kwenye hilo duka alilonielekeza nikakuta sindano moja ni elfu 30,000 nilichokaaaaaaaa. sasa kwa mtu asiye na uwezo sianakufa na mbwa walioningata walikuwa hawajawahi kupata chanjo.
    dada cheusi
    Arusha.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 17, 2008

    we kama kweli mpare tafuta vijana wawili wape kazi ya kumzimisha huyo mbwa mwisho wa mchezo acha kelele tu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 18, 2008

    Oya Ray uwanakijiji umeanza lini wewe blazaa! Unapata wapi mida ya kudeliver?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...