
Wazee wanayo nafasi ya kuendelea kukitumikia chama kwa njia ya kutoa ushauri na kukilea chama kisitoke nje ya mstari wa kanuni zake hata baada ya kustaafu, mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewaambia wazee waasisi wa CCM wa Mkoa wa Musoma waliofika Ikulu leo kumtembelea na kumshukuru kwa kufanikisha ziara ya wazee hao kutembelea sehemu mbalimbali za kumbukumbu na historia Tanzania bara na visiwani.
“Nyinyi mnakijua chama vizuri zaidi kuliko vijana, mchango wenu hauwi na maslahi yeyote bali ni mchango wa dhati na mapenzi kwa chama, nyie mnayo nafasi kubwa ya kukisaidia na kukiweka chama kwenye mstari na kurudisha maslahi ya wanachama [WINDOWS-1252?]wake”
Wazee waasisi hao kumi na saba (17), wakiongozwa na mwenyekiti wao mzee Ramadhan Mawazo, wametembelea mikoa ya Arusha na kutembelea sehemu mbalimbali zenye kumbukumbu za Azimio la Arusha, Dar-Es-Salaam ambapo wamemtembelea Mzee Rashid Mfaume Kawawa na kufika hadi Zanzibar ambapo wametembelea kaburi la Hayati Abeid Amaan Karume na majengo ya kihistoria na mji mkongwe, na kesho wanatarajiwa kutembelea Dodoma ambapo watapata fursa ya kutembelea na kuona shughuli zinavyoendeshwa Bungeni.
Katika risala yao kwa Mwenyekiti wa CCM, wazee wamemshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha ziara yao hii na baadaye katika mazungumzo yao wamemuomba awasaidie kuendeleza Saccos yao ambayo ni changa na inakabiliwa na matatizo ya kukopesheka kwa sababu ya umri wao.
“Nyinyi mnakijua chama vizuri zaidi kuliko vijana, mchango wenu hauwi na maslahi yeyote bali ni mchango wa dhati na mapenzi kwa chama, nyie mnayo nafasi kubwa ya kukisaidia na kukiweka chama kwenye mstari na kurudisha maslahi ya wanachama [WINDOWS-1252?]wake”
Wazee waasisi hao kumi na saba (17), wakiongozwa na mwenyekiti wao mzee Ramadhan Mawazo, wametembelea mikoa ya Arusha na kutembelea sehemu mbalimbali zenye kumbukumbu za Azimio la Arusha, Dar-Es-Salaam ambapo wamemtembelea Mzee Rashid Mfaume Kawawa na kufika hadi Zanzibar ambapo wametembelea kaburi la Hayati Abeid Amaan Karume na majengo ya kihistoria na mji mkongwe, na kesho wanatarajiwa kutembelea Dodoma ambapo watapata fursa ya kutembelea na kuona shughuli zinavyoendeshwa Bungeni.
Katika risala yao kwa Mwenyekiti wa CCM, wazee wamemshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha ziara yao hii na baadaye katika mazungumzo yao wamemuomba awasaidie kuendeleza Saccos yao ambayo ni changa na inakabiliwa na matatizo ya kukopesheka kwa sababu ya umri wao.
Duh!! Poleni sana wazee wangu kwa kupishana na pesa kwani waliopo madarakani sasa hivi hata kwenye hiyo CCM tu achilia mbali waliopo serikalini wanamaisha mazuri kuliko viongozi wa wakati wenu. Kwa sasa ninyi mmebaki kuwa wapiga mapambio huku vijana wakifaidi ulimwengu kwa pesa za ufisadi na kuwafariji kwamba wazee ni hazina. Siyo siri siku hizi hata ukiwa mwenyekiti wa kitongoji/mtaa (licha hata ya kuwa mbunge/waziri/mkuu wa wilaya n.k) tu ni dili kwani unaweza kuuza barabara ya mtaa na maisha yako yakawa bomba tofauti na viongozi wa zamani ambao nadhani hapo walikuwa na vyeo katika mkoa au wilaya lakini wanaonekana wamechoka. Wazee wangu nawaonea huruma lakini afadhali ya nyie jua limeshazama lakini mimi kijana hali ndiyo mbaya zaidi kwani mahitaji mengi na pesa sifuri. Wazee mwambieni JK mafisadi wanaiharibu nchi na siyo kumsifia kwa kufadhiliwa kwa safari kwani vijana tunaona kwamba hajachukua hatua za kutosha kuinusuru nchi. Vijisenti vilivyohifadhiwa ulaya nadhani vingetosha kufadhili SACCO za wazee nchi nzima. NARUDIA kusema wazee poleni ila msipomwambia ukweli kiongozi wa nchi kuhusu watendaji wanavyoiharibu nchi nanyi mtakuwa wanafiki na mna lengo la kuangamiza kizazi cha leo, kesho
ReplyDeletekaka ulietuma hii picha na maandiko yaelekea wewe ni mkongo,au kiongozi fulani wa kata huko Nyeri Kenya,yaani hujui Musoma ni wilaya sio mkoa?mkoa ni mara
ReplyDeletejaribu kusoma na kumuuliza michu kabla hujatuma
ni mimi mdau toka visiwa vya LUKUBA
Ndugu,
ReplyDeleteMusoma ni mji na ni wilaya vilevile, sio Mkoa! Musoma iko katika mkoa wa Mara.
Wewe uliyemkosoa mtuma habari nakuunga mkono kwamba musoma ni wilaya na si mkoa.Lakini pia nawewe nataka ujue kwamba sehemu uliyotoa haiitwi LUKUBA bali ni LUKUBHA.Hii si wewe tu ila ni hata akina-MAKOBHA ambao hujiita MAKOBA.Jina linaandikwa linavyotamkwa,na ikiwa umetoka LUKUBHA nadhani hilo eneo sisi wenyeji tunaliita LUKUBHA na SIYO LUKUBA.
ReplyDeleteAsante
I hope one day akija over sea atapata kuongea na Watanzania wenzie waishio nje ya Tanzania.
ReplyDeleteKwani kwa sasa naona kila mwenye different approach ya maendeleo anaonekana mpinzani, something which is real out of control.
Tanzania needs forces from young and adult, people in Tanzania and over sea, however majority yetu tuishio oversea tumekuwa treated like second citizen.
Mdau wa US tawi # 1
Duh...CCM iyo! Imejaa mafisadi wanakuja kutudanganya na wazee hapa. Unajua CCM inanikumbusha kitabu kimoja cha George Orwell kinaitwa 'Animal Farm'. Jamaa(wanyama) walileta mapinduzi vizuri halafu sasa wale viongozi(nguruwe) wakaanza kubadilika. Yani ndo CCM ilivyogeuka. Siku izi hamna cha kuleta maendeleo nchini. Ni kula uwezavyo alafu timka! Nchi imeibiwa mpk basi! Inaudhi sana sema basi tu! Lakini zote hizi zinaanzia kwa Nyerere. Alijifanya mjanja sana na kujiweka katika nafasi ya juu sana nchini ambapo ndo matokeo yake haya. Halafu kuna swali moja linaniumaga sana toka zamani...Kwa nini Rais wa Zanzibar anaitwa Rais na wakati Zanzibar si nchi? Au hiyo ilikuwa ni mojawapo ya danganya toto za Nyerere.
ReplyDeleteIs this really a Viable Economic Entreprise? What could be the Internal Rate of Return? Changamkieni Tenda hiyo,kila Mkoa upeleke Wazee Wake(?),wakakumbushie Historia!Anaye sema Zanzibar siyo nchi akafunue Mabuku ya Umoja wa Mataifa halafu achungulie humo mwaka 1960 hali ilikuwaje?Majuto Mjukuu.
ReplyDeleteKuna mtu anataka kusema Zanzibar ni nchi hapa?...kweli ndo hapo Watanzania tumedanganywa! Zanzibar haitambulika kwenye UN hata kidogo. Ilipopata uhuru...sawa lakini baada ya Muungano sio nchi tena! Nchi ni Tanzania!
ReplyDeletehii ni point ya nje lakini hata ukiwauliza wana-spoti wa znz...timu yao ya mpira haiwezi kucheza kwenye mashindano ya kimataifa kama African Cup of Nations au World Cup. Haitambuliki na FIFA au tuseme sio member wa FIFA na kwa nini?sababu sio nchi!!Kuita rais wa znz rais ni upotofu wa mawazo tu!Namuunga mkono huyo anon wa june 24 9:42. Zamani znz ilikuwa 'constitutional monarchy' na baada ya muungano ikasizi! mfano wa constitutional monarchy ni Monaco! Sasa kama bongo tungekuwa wajanja tungeigeuza znz kuwa the Monaco of Africa. Tunapunguza taxes, legalize gambling, nk...sema ndo ivyo tena!
ZENJI HATA HAIELEWEKI ATA HUU MUUNGANO NAO SIJUI NDO NINI??yan ukisoma history ndipo utajua yan kuna vitu vingi vya msingi havikutiliwa maana yan ni km ubabe-ubabe ivi,,aya tena mana hata sioni maana ya kuwa na rais wa zenji,,,labda angekua makamu wa rais/waziri mkuu,,,ila izi siasa jaman??
ReplyDeletemaskini wazee hawa,,,wala hawatasaidiwa lolote,,km vimeshindikana vya iliyokua Jumuiya ya afrika mashariki,,,!!!yan ivi ndo vituko aswaaa iyo pesa wanayolipwa nimechoka kbs
Bwana we...ishu za zenji si ndogo na ni very interesting. Na kuielewa vizuri inabidi ucheki historia kidogo. Zenji ilikuwa inatawaliwa ki-sultani! Waingereza wakaingia na kuitawala mpk dec 1963. lakini kuitawala yenyewe haikuwa kama koloni la uingereza...wenyewe wanaita 'protectorate' yani eneo linalojitawala binafsi huku likipewa ulinzi na nchi kubwa zaidi. (an autonomous territory that is "protected" by a stronger state). Sasa wakachukua uhuru dec 63 kurudishwa kwa ma-sultani. Jan 26 1964 mapinduzi...kina Karume wakazama ndani! Sasa ukumbuke wakati huo vita vya baridi vilikuwa vikiendelea duniani. Wakati huo mambo ya Cuba ndo yameiva...bay of pigs na kadhalika. Zenji ingekuwa strategic territory (samahani kwa kiingereza hapo) kwa pande zote mbili yani marekani na urusi! yani kama Urusi ingewahi zenji, marekani ingezama bongo. Pia waarabu nao wametoka kupinduliwa wangeweza kuvamia maana ni ma-sultani kutoka Oman hao! Sasa mzee Karume akaona janja hana ikabidi amwombe Nyerere waungane...tofauti kati ya muungano huu na ile 'kutawaliwa' na uingereza ni kwamba sasa ivi nchi mbili zimeungana na kuwa moja. Ivyo zanzibar sio nchi tena wala Tanganyika sio nchi tena! Na ivyo bwana huyu jamaa wa juu is right. Zanzibar haiwezi kuwa na rais maana si nchi. Wanatakiwa wabadilishe iyo title na kuwa na waziri mkuu tu au kama wakitaki waanzishe u-chief huko iwe mambo ya kurithiana tu...hehehe! Masahihisho napokea kwa furaha wadau!
ReplyDelete