msanii nguli katika Sanaa za maonyesho Tanzania Bw. Mgunga Mwa Mnyenyelwa 'Tangulia Mwalimu' wa Parapanda Arts Theatre Lab akiwa na mai waifu wake Grace katika hafla ya sherehe ya harusi yao iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Lion Sinza Dar es Salaam, Hafla hiyo ya harusi iliambatana na maonyesho kadhaa ya sanaa yaliyokuwa na ujumbe mzuri kwa Wanadoa hao na wengine waliohudhuria hafla hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2008

    Maharusi mmependeza kweli, nimependa kweli hizo nguo za asili.
    Nawatakia ndoa njema yenye furaha tele.Kaka una kipaji kweli sijui kama unakiendeleza manake ule ujumbe wa 'tangulia Mwalimu' wakati wa msiba wa baba wa Taifa sitakaa niusahau, keep it up your talent Bro.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2008

    Hongera Emmanuel Mnyenyelwa,
    karibu kwenye maisha ya ndoa.
    Classmate wako Mwenge Primary 1983(Moshi,Kilimanjaro).

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2008

    huyu jamaa sitamsahau kwa ule wimbo wa "tangulia mwalimu", mwimbo mzuri sana, tungo kali sana, na ulitungwa kwa muda mfupi sana, hapo ndiyo utajua kweli nani msanii wa kweli na nani mvamiaji. Mwimbo wa masikitiko sana na pia wa kisomi sana, sipo nyumbani lakini mwimbo huo nausikiliza sana hadi leo kwenye"tape" bahati mbaya sina CD.Sijaoa bado, lakini naona 'umetangulia nyota".
    " mvua inye, na jua limweke" na mimi lazima nitaoa siku moja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu unaweza kunirushia natafuta sana huo wimbo nadhan hapa bongo kea kiasi fulani nyimbo zake huyu Bwana huwaga zinakandamizwa hazisikiki kirahisi

      Delete
  4. AnonymousJune 23, 2008

    Duh!!! Jamaa kafanana na wewe michuzi kama kioo cha kujiangalia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2008

    Huyu jamaa hajafanana na michuzi, mi naona kafanana na mzee small wa Cheka na CTN! hahaha, hadi kofia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2008

    sina budi nami nitoe pongezi kwa jinsi maharusi mlivyopendeza hususan kwa vazi la harusi linaloonyesha kuwa nasi tunaweza kuwa na ubunifu na kutengeneza kitu bomba, badala ya kuona kila design ya 'ulaya' ndio usasa. tafadhali litangaze na lipigie debe, tuachane na misuti na migauni ya ulaya. HONGERA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2008

    huyo aliyeoa ni bwana michuzi mwenyewe anarekebisha ndoa yake ya sita hongera mkuu wa mkoa wa tegeta

    ReplyDelete
  8. Mgunga ni mwema saana kwenye sanaa. Naheshimu mengi ktk sanaa yako na utambaji. Nakumbuka saana lile igizo la Mfalme Juha ambalo Parapanda mlilifanya ukiwa na wakali wengine kama Bw Mrisho Mpoto, Ms Mona Mwakalinga na wengine wengi ambao kwa hakika mlikuna wengi kwa ujumbe na utambaji.
    Ni mbaya kuona wahudhuriaji na wathamini wakubwa wa sanaa yenu nzuri na kali ni wataalamu wa sanaa wa ndani na nje ya nchi na watu toka nje ya nchi. Ukweli ni kwamba sanaa halisi ya Kitanzania imewekwa pembeni na hizi "Big-G" za sanaa zilizokosa asili yetu na kutofikia thamani ya kule zitokako ambavyo hutufanya tubaki bila kujulikana tuko wapi.
    Kazi njema katika kila jema utendalo na Sanaa njema Kaka.
    Baraka kwako na familia mpya

    ReplyDelete
  9. Dah!! Nilisahau Kaka Michuzi, kwa wapendao kuona na kusoma mengi kuhusu Mgunga na Parapanda kwa ujumla watembelee http://www.parapanda.org/
    Blessings

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 24, 2008

    Hongera sana bwana Mwamnyenyelwa angalau sasa umetutoa shaka watu wengi kwamba na wewe kumbe wamo ukizingatia kuwa wewe ulikuwa ni mwanafunzi pekee wa kiume pale Zanaki wakati huo , wengi tulikuwa na hofu na mashaka makubwa juu yako ukichanganya na muda uliokaa tangu uhitimu shahada ya kwanza palee Mlimani , anyway mimi nakukumbuka sana kwa igizo lako la njia panda pale Makutupora JKT .

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2008

    Huyu bwana tulikuwa nae pale Mawenzi secondary alikuwa ana talent ya sanaa tangu kule. Alikuwa anapiga ngoma sana nakumbuka alituongoza mawenzi house tukashinda interhouse comps. maigizo na ngoma za asili. Hata NJENJE wanamkubali. MICHUUUUUU

    ReplyDelete
  12. Emannuel Mnyenyelwa hongera sana, Mungu aibariki ndoa yako.

    Hivi ni yule aliyekuwa Makutupora JKT Operation Kambarage. B-Coy? Kama ndiye utamaduni naona uko kwenye damu, kile kikundi cha utamaduni ulichokuwa ukikiendesha pale Makutupora JKT Operatio Kambarage UKIWA NA KIVAZI NA AFANDE MWIBA, MWASHAMBA, AFANDE CHACHA MAPUUZA!!!! NIMEFURAHI SANA.

    FOSI NAMBA AKA....

    ReplyDelete
  13. Nawashukuru sana mliotoa maoni yenu. Nafurahi kusikia zile habari njema za MwengeSM, Mawenzi Sec/School, Zanaki sec na Makutupora kwa afande mwiba!! Na CO Mtu mrefu!!!!!

    Ndimi Mgunga Mwa Mnyenyelwa.Ningali katika harakatio za KIJITAFUTA!! Samahani kwa kimya nilikuwa nimebanwa na masomo ya MA katika Sanaa ambayo karibu namaliza.


    Natumaini kuwa mmeuona pia wimbo wa FUTENI MACHOZI!! katika TV hasa Cahenel 10.

    Mungu wa wafrika awe nanyi!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...