Ile mechi ya marudiano kati ya Simba na Yanga za Washington DC iliyokua ifanyike julai 4, 2008 mjini hapa sasa imehamishiwa Columbus Ohio(uwanja wa Amani, Zanzibar).
Waandaaji wa oldskool party of the century ndio watakao gharimia timu hizo kwa lengo la kutoa burudani ya mpira wa miguu kwa wapenzi na mashabiki hao vijana wa zamani wanosemekana kufurika kwa wingi kutoka kila pembe ya dunia.
uongozi wa Simba na Yanga uliokutana jana ulikubaliana kuhamishia mechi hio Columbus Ohio itakayochezwa siku ya jumamosi july 5.Rashid Mkakile (Bamchawi) alipendekeza ichezwe mechi nyingine ya marudiano Washington Dc wakati wa labor day weekend ambayo hufanyika party kubwa inayo wakutanyisha Watanzania vijana wa sasa na zamani.
uongozi wa Simba na Yanga umesema mechi hii ya Columbus ipo wazi kwa mtu yeyote kucheza,mpira ni kama kuendesha baiskeli,kinachohitajika ni pumzi kama uwezo upo njoo na vifaa.
Yanga imesema inataka kuipa Simba kipigo kingine kitakatifu,huu ni mwaka wetu kulipiza kisasi,Kwa upambe wa mahasimu hao wa msimbazi bado moto unafuka hawajui mchawi ni nani,kipigo walichopata kwa Yanga bado ni ndoto
uongozi wa Simba umemfungia kipa wao Saleh Londa kwa muda usiojulika kwa tuhuma za kuuza mechi,inasemekana alionekana nyumbani kwa Dj Luke(Gulamali) asubuhi siku hiyo kabla ya mechi na aliwapeleka wachezaji wa Simba nyumbani kwa Boas ambae aliisha kua mchezaji wa Yanga miaka ya sabini.
Yeye mwenyewe Londa amekana amesema habari hizo si za kweli mimi ni Simba damu,kufunwa ilikua bahati mbaya lakini kama uongozi unaona nimehujumu timu,mimi sina la kusema.
kwa upande wa Yanga,bado wanawatambia wenzao wana sema hata tukiamshwa usiku wa manane,kumfunga Simba kwao ni kama kumsukuma mlevi na wamewaomba washabiki wawe watulivu.
wakati huo huo habari ambazo wenyewe wamekataa kuthibitisha ama kukanusha, refa wa mpambano huo anaweza kuwa mkuu wa wilaya ya tegeta mh. nanihii ambaye redio mbao zinasema ameonekana kwenye shirika la ndege la emirates akiwa na ulimi unaoashiria ana safari ya nje ya nchi.
alipoulizwa kama habari hizo ni za kweli mh. nanihii alionesha kushangazwa kwa jinsi habari zinavyovyuja haraka kiasi kile, na kuishia kusema kwamba lisemwalo huenda lipo. hata hivyo alikubali kupokea mwaliko wa kuhudhuria oldskool bash ila alikataa kusema kama atahudhuria ama la.
Columbus Ohio tunakuja kuwapa Simba kisago kingine.
Visit my website at www.thedjlukeonline.com
Visit my website at www.thedjlukeonline.com




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...