nahodha wa simba saleh londa akipokea kombe la ushindi wa pili
mgeni rasmi wa mpambano wa yanga na simba washington dc richard kasesela (kati) akiwa na waandaaji na makombe ya wahindi
hatario langoni pa simba
refa manyoto ndimbo akiwa na manahodha wa yanga na simbaWashington DC, Marekani
TIMU inayoundwa na washabiki wa Yanga wanaoishi mjini Washington DC na vitongoji vyake jana iliwachapa wenzao wa Simba kwa mabao 5-2 katika mchezo mkali uliochezwa kwenye uwanja wa Meadowbrook, kilomita mbili na nusu nje ya Washington.
Ikicheza kwa staili ya Maximo ya kudhibiti mashambulizi na kupeleka mipira hatari langoni mwa wapinzani, Yanga jana iliwazidi wapinzani wao katika kila idara uwanjani tofauti na mwaka jana zilipotoka sare ya 3-3 katika mchezo uliovunjika kunako dakika za majeruhi baada ya mwamuzi kuipa Yanga penalti.
Yanga ilianza kutikisa nyavu za Simba kunako dakika ya 19 kupitia kwa Seif Ndosa kabla ya Ernest Fotachwi, mzaliwa wa Cameroon, kuongeza bao la pili kwenye dakika ya 45 na kusababisha benchi la ufundi lililoongozwa na kocha Robert Sabuni, kuzozana bila maelewano wakati wa mapumziko.
Dakika kumi baada ya kipindi cha pili kuanza, mshambualiaji hatari wa Yanga, Innocent Geofrey, nusura afunge alipobaki na kipa wa Simba, Saleh Londa aliyekuwa mchezaji bora wa mechi ya jana kutokana na kuiokoa Simba na adhabu ya magoli.
Simba ilisawazisha kunako dakika ya 63 kupitia kwa Shabani, lakini mvua ya magoli ilibadilika kwenye dakika ya 78 wakati beki Aristotle Maruma alipopachika bao la tatu kabla ya Hussein Ibrahim kuongeza la nne na tano kwenye dakika za 80 na 85.
Mwamuzi wa mchezo huo, Kassim Khamis ambaye alionekana kunogewa na mvua ya magoli aliachia dakika za majeruhi kupitiliza na kuisaidia Simba kupata bao la pili kupitia kwa Vincent Ndusilo aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Tobby Nkai, mzaliwa wa Sierra Leone.
Mgeni rasmi wa pambano hilo, Richard Kasesela ‘Bibo’ ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), alikabidhi kombe la ushindi kwa nahodha wa Yanga, golikipa Diddy Ruba, ambaye baada ya sherehe kubwa alimkabidhi mzee wa timu, Profesa Nicholls Boas.
Timu zote jana zilitumia wachezaji wa kulipwa ambapo Yanga ilikuwa nao wanne kutoka Kenya, Uganda na Cameroon wakati Simba ilikuwa na watano kutoka Sierra Leone, Nigeria na Liberia. Timu zote zilibadili wachezaji zaidi ya watatu katika dakika 90.
Aidha mechi ya jana itakumbukwa kwa shoo ya jezi iliooneshwa na Simba ambapo ya kupasha msuli moto, ilibadili jezi na kuvaa zenye nembo ya Manchester United. Simba wote walivalia bukta nyeupe na soksi nyekundu.
Hata hivyo hali kwa watani zao wa Jangwani haikuwa hivyo kutokana na suala la jezi kuwaumiza vichwa ambapo kwa wakati mmoja wachezaji watatu walivalia jezi zenye namba kumi mgongoni na karibu kila mchezaji alikuwa na bukta na soksi mchanganyiko.
Baada ya hafla ya kula nyama za kuchoma uwanjani hapo, uongozi wa Watanzania mjini Washington ulitangaza kwamba mechi hiyo itarudiwa tena Julai 4, kwenye siku ya uhuru wa Marekani ili kuipa nafasi Simba kulipa kisasi.


Suala la jezi limekuwa tatizo kubwa sana kwa timu ya Yanga, nafikiri mtakumbuka hata enzi za '80 wao jezi imekuwa anasa, wakati Simba na timu za Zenji hilo siyo tatizo.Sikutegemea kama ule ugonjwa bado upo hata huko USA. Kipa mashuhuri dj Luke, beki mstaarabu Vuvyian walicheza au??? Hongera sana wadau wa DC, salaamu toka Bongo.
ReplyDeleteMdau wa Washington uneiremba habari ya mechi hiyo kwa madaha na ufundi mkubwa kama Benni Kiko wa enzi hizo na ni changamoto kwa Michuzi na waandishi wa Bongo.
ReplyDeleteRudi nyunbani Bingo uwe mwandishi wa michezo kwani kwa sasa magazeti yote ya Bongo hayana waandishi wa spoti wenye uwezo wa kufurahisha wasomaji, maana habari hii nilipo isoma ni kama vile naangalia 'live' pambano hili hapo Washington DC.
Mdau
Rocky
London
safi sana Yanga!!
ReplyDeleteE BWANA NAWAFAGILIA SAAAAANA SIMBA NA YANGA WA WASHINGTON KWA KUDUMISHA UTAMADUNI.
ReplyDeleteSIO HAWA WABONGO WANAOFUNGUA MATAWI YA LIVERPOOL HAPA NYUMBANI.
AU NDIO KAMA MAMBO YA NDOA KWAMBA ALIYE NDANI ANATAKA KUTOKA NA ALIYE NJE ANATAKA KUINGIA .. :))
BIG UP UP UP WANDUGU. HUU NDIO UTANZANIA
Washington DC na uwanja una viraka hivi!noma hiyo.
ReplyDeleteHivi, hiyo picha ya mwisho - huyo mcheza mpira aliyetilia red shati na bukta nyeupe na socks nyekundu - siyo yule mtoto wa shangarai pale moshi jamani - Kama si kosei anaitwa Evans - yaani amekaa kisport ile mbaya - Big up!!!
ReplyDeleteSIO MBAYA BAADAYA KUPIGA BOX KWA SANA WATU MKAJIPONGEZA KWA MICHEZO KWANI NI AINA MOJA WAPO YA KUONDOA UCHOVU NA MSONGO WA MAWAZO HASA KWA NYIE WA UGHAIBUNI.SIE HUKU HOME TZ AKU ,JK BOYS WANATUPA RAHA. "MBONI RAHA"
ReplyDeleteWell, mechi ilikuwa nzuri na nyama choma pia zilipendeza kwa walioziwahi kabla hazijaisha. Timu ndio zilibadili manahodha kama unavyoweza kuona pichani ndio maana Nahodha aliyekwenda kusaidia kuchagua upande wa kuanza (hao waliosimama na refa) sio waliokwenda kupokea makombe kwa timu zote mbili. Nadhani ni jambo linaloeleweka hasa kwa mechi kama hizi ambazo wachezaji wanabadilishwa sana ili kukidhi mahitaji ya mchezo. Kwa hiyo nilitaka kuweka hilo sawa ili wenye wasi wasi juu ya kuwepo kwa manahodha wawili (kabla ya kuanza na baada ya mechi) watambue hilo.
ReplyDeleteAsante
Hii habari ya Simba na Yanga lazima imeandikwa na Matinyi, huyu jamaa anaipenda Simba mno ndiyo maana kashambulia jezi za Yanga baada ya kuona wamefungwa. Lakini tuache utani, jamaa anaandika, ukisoma utafikiri uko uwanjani ungaangalia. Rudi mshikaji uokoe jahazi huku watu hata kumuuliza maswali Maximo kwa Kimombo wanababaika, la usipande bichwa.
ReplyDeletePicha zimetulia. Kwani michuzi ulienda huko? Yaani Matinyi kamwaga habari ki-Majiramajira nawe umeweka picha ki-Mfanyakazi vile. Yaani ni "Combo" ya nguvu.
ReplyDeleteGood Job
HUYO MGENI WA HESHIMA MBONA AMEKENDA UWANJANI AKIWA AMEVAA JEZI YA YANGA SI ATAKUWA ALIKUWA BIASED? AU ALIKUWA AKIIWAKILISHA CCM? NI VIPI UNAPOKWENDA KWENYE WASHINDANI WAWILI UKIWA MGENI RASMI UNAAMUA KUVAA JEZI YA TIMU MOJAWAPO! IWAPO KAMA ALITEULIWA AKIWA NJIANI KWENDA UWANJANI KAMA MTAZAMAJI SIMLAUMU LAKINI KAMA ALIJULISHWA MAPEMA BASI AJIFUNZE KUVAA KULINGANA NA SHUGHULI.
ReplyDeleteMECHI KAMA HII NI TAMU MNO NA INA HARI NA MOYO WA KWELI. MAANA MASHABIKI HUWA HAWAHAMI TIMU BALI WACHEZAJI , SASA HAWA NI MASHABIKI.
ReplyDeletePICHA MLETE WENYEWE.....HABARI MUANDIKE WENYEWE....NA KUCHANGIA PIA MCHANGIE WENYEWE...!!??!! JOOB TRUE TRUE !!!
ReplyDeletenaona Manyoto kapendeza sana lakini hiyo miguu vipi? mkorogo au maana juu na chini rangi tofauti.
ReplyDeletembona kaptura iko kiajabu ya huyo wa chini mwenye nyekundu?au sijui ndio simba
ReplyDeletekweli huyo mchezaji hapo mrefu aliyetilia shati lekundu na kaptula nyeupe huyo nimemind .vipi umeoa kaka????
ReplyDeleteKumbe walivaa Jearsey za Manchester IoI Chapa mabishoo hao kisago tu YANGA ndio Imara popote
ReplyDelete