Home
Unlabelled
ze comedy production
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wanaleta mzaha kwenye jambo kuu la Taifa? Hii itasaidia jamii? wanao husika inabidi wawajibishwe
ReplyDeletewanatumia staili gani? ile ya zecomedy au nyingine kama zi-comedi na nyingine zilizopendekezwa na wadau humundani?
ReplyDeleteHuku ni kuwadhalilisha ze-comedy.Hawa ni watu maarufu hawahitaji mechi hizi kujirusha.Waacheni waitathmini mechi hii kwenye ze comedy.Hapa walitakiwa akina Dr liki na wataalamu wengine tupate hoja za msingi kuhusiana na kandanda letu.
ReplyDeletekAMA ndio wamebailisha jina na kujiita ze comedi productions wamwchemka. Biashara inahitaji jina rahisi kutamkika ikiwezekana na kila mtu.
ReplyDeleteNawashauri watafute jina jingine fupi na la kawaida. Waachane na jina la ze comedy au mengine yoyote yanayofanana na hilo. hii ni kwa sababu kama EATV wataanzisha ze comedy nyingine na hawa akina masanja waendelee kujiita ze comedi au hata jin alinalofanana na hilo hawatapeleka ujumbe wa tofauti na hicho kikundi kipya.
Majina yapo mengi la muhimu wao wasisambaratike. watafute hata watu wawapendekezee kisha hilo jina walitangaze kwa nguvu watanyanyuka na hiyo ya EATV itakufa kifo cha mende. Kwani washabiki watafuata hilo jipya na kuachana na Ze comedy.
Wajuzi w abiashara za matangazo wawasaidie kububi jin arahisi kutamkika litalowapambanua na ze comedy ya EATV. La muhimu wasisambaratike na wengine kurudi EATV.
waswahili kwa kumeza mambo, mara wataalamu wawepo. jamani kila kitu na mida yake, kuna wakati wa Dr.Liki, kuna wakati wa ze comedi, kuna wakati wa hata wanawake kutathimini.acheni kukremu, kama lengo l;a TBC ni kufurahisha raia kupiTIA ZE comedi no problemu.wataalamu wameongea weee, nilezeni nani huwa anachukua na kuyafanyia kazi ??
ReplyDeleteMbona watu wabishi kukubali.hata mtoto mdogo anaweza kujua kwamba wamechemka kuwaweka hao hapo.kila mtu ana sehemu yao mambo ya wanamichezo waacheni wana michezo.kwa vile ze comedy wanpendwa haimaanisha huwatumie kila sehemu.wamechanganya fani kubalini yaishe.
ReplyDeleteMichuzi habari za weekend.Huyu Mkurugenzi au msimamizi wa matangazo wa TBC1 aliyeruhusu hao watu kukaa kwenye lunginga wakati wa mechi ni nani?Ningekuwa 'bosi wake ningemfuta kazi au ningempa written warning.Ze comedy hawakuwa mahala pake.TBC walichezea hela zetu za kodi.
ReplyDeleteKuna kituo kingine cha TV kilikuwa kimewaalika(Na mara nyingi huwa wanawaalika 'watu wa mpira') JUMA MGUNDA NA SANIFU LAZARO.Ambao mpira ,walitoa maelezo kutusaidia kutokana na uzoefu wao wa nyuma.Mama Mhaville na timu yako mko juu sana na kituo chenu cha Television.Keep it up
mi naona wajiite ZE-KOMEDI.hapo watakuwa hawaingiliani na ze comedy maana zitakuwa na spelling tofauti halafu wasijaribu kabisa kutengana ndio watakuwa wamejiua wote moja kwa moja.jaribu kuangalia wanamuziki au makundi mengine ya sanaa walojitenga ameishia wapi.nawakilisha
ReplyDeletenilikasirika sana, nilitaka kuwasikia wataalam kama Charles Boniface, Dr liki etc wakitueleza mwelekeo wa mchezo, matokeo yake ikawa utani kwenye suala muhimu la kitaifa. Everything has its time....nilichukia sana nika switch to ITV
ReplyDeleteNAWALAUMU SANA TBC1, MMEANZA KUCHEMSHA
Mimi ni mtaalamu wa analysis:
ReplyDeleteKwanza angalia tofauti ya mida ILIYOTUMIKA KUTUMA HAYA MAONI, UTAGUNDU NI WATU WALIOKAA SEHEMU MOJA WAKAYATUMA NDANI YA MUDA MFUPI. PILI MWELEKEO WOTE NI MMOJA NA
ila nawahakikishieni ninyi ni waajiriw atu na hamna lolote hata maamuzi hakuna, na isitoshe najua mishahara yenu hapo! endeleeni na TV yenu zulumishi, ila hawa vijana kipaji kipo na nakuhakikshia wajiite zikomedi zekomed productions hata wajiite wajinga bado hamuwezi kufuta kipaji, hawa hawawezekaniki na wameteka jiji na nchi! Ukifikia mpaka onesho linakatishwa kisa watazamaji wamepagawa na upenzi unadhani unaweza kufuta upenzi huu kwa kuwekea hati miliki staili ya kutembea, upuuzi! njooni muwekee na style yangu ya kupiga mswaki! Mawazo ya kimasikini sana!
MWISHO KABISA NATOA PONGEZI KWA TBC, mi si mtazama TV ila kwa hao vijana LAZIMA TUWE PAMOJA TBC. Nbiashara kwaio sishangai ugomvi na ubishi! ZE KOMEDI HATA MFUNGIWE NCHI NZIMA MNABAKI KUWA KUNDI LA KIPEKEE NA HAIJAWAHI KUTOKEA! SAFI SANAAAAAA!
Nilisha tabiri kupitia blogu hii hii kwamba kitendo cha Ze Comedy ya zamani kuondoka EATV bila ya ustaarabu na shukrani kitawagharimu sana.Wasubiri watakiona ninacho kisema.Huu ndiyo mwanzo wa mwisho wa kikundi hicho.Kwanini?Kwanza,hivi sasa EATV watakuwa wanakisuka upya kikundi kipya cha ZeComedy ambacho amini usiamini hawa kina Mesenja ni ChaMtoto!.Pili,katika hatua ya kukomoana,lazima atakoea PDG mmoja atakaye mchoropoa mmoja wa wasanii nyota wa kikundi hicho cha Zee Komedi ambaye akikosekana huyo kikundi hicho kitapoteza kabisa ladha ya usanii ya kikundi hicho na hata kupoteza mwelekeo.Atachomolewa msanii mmoja au wawili kwa Pesa Mbaya sana amabayo hawawezi kuitema!Na wakiondoka hao kikundi kimekufa!Unabisha?Wewe subiri.Kila mtu mjanja na mjuaji katika nchi hii.Wewe ukijiona una pesa wenzako wana Mapesa baba!Au Revoiur Zee Komedi!Hiyo ndiyo Shombo ya Pesa!Kharaha!Huli Ukashiba.
ReplyDeleteTBC isiwe kituko na kufanya mahala pa kuwakilisha mambo binafsi ya mtu na mtu tulisha oona vita vimefanyika kwenye vyombo vya kutunga sheria na kutafsiri sheria na ukweli na haki ukadhihiri sasa bado tu watu wanaendelea zaidi mpaka wanaingiliana kwenye sehemu zao za biashara ! .Sawa kama bado kuna upande mmoja unaendeleza libeneke basi kaa chini na ujipange vizuri kinachofanyika sasa ni vita za kitoto ! kabisa tunaona mifano mingi sana nje kwenye TV Production companies actor anatoka kutengeneza movies/drama/series! Na hakimaliza hapo na kwenda kwenye company ingine huwa aendelei na jina lake la kuigiza ila linabaki la asili basi na huwezi sikia Rambo kamaliza urambo wake na kwenda kwingine na kujiita Rombo ! itakuwa ni ujinga .Mfano hata hapo ITV kulikuwa na Drama inaitwa jahazi na kikundi kinaitwa Kaole lkn walipotoka na kwenda TVT wakaanza na majina ya kuigiza mapya kabisaa !! na wamendelea mpaka leo na hatukusikia kokoro yoyote sasa leo ni vioja vitupu ! Ze Comedy natumai lilikuwa ni jina la kipindi sina hakika kama ni jina la kikundi na Production ilikuwa ni ya EATV ! na kama wamemeliza mkataba na kwenda kwingine kwa ajili ya masilahi basi huyo anayewasimamia awe ni mtu amkini basi ! tafuta majina mapya ! tafuta jina la kipindi ! sababu jina la Ze Comedy sio Hirizi ya kufanyia kazi ! je isingelikuwa EATV kuanzisha Ze Comedy msingelijulikana ? Mlijaribu kuteka hisia za watanzania na wakawakubali na mkawa ndio mnaangaliwa kwa wingi na watu wa rika lote kwa wingi kupita kipindi chochote ! sasa naona mkajisahau kabisa na sasa sawa mnatafuta maslahi zaidi sawa ! basi msijiaibishe kwa kuleta malumbano yasio na msingi zaidi ya kijiporomosha kiusanii ! msidanganywe kuwa wadanganyika hawataoona kuwa mnafanya upuuzi kwa kugombania jina ! anaye washauri hivyo nadhani ni kwa maslahi yake binafsi na anawafanya nyinyi ndio wajinga ! mwaweza poteza umaarufu ndugu zetu ! kaeni chini na mtoke na kitu cha maana .TBC tulitegemea kuna watu ambao ni watauluma kwa kazi zao za TV Production pamoja na Adminstration sasa mwaleta kitu cha ajabu na kuishushia heshima. TBC ! hau ni chombo cha maslahi binafsi kimekuwa sasa ? tunawaomba sisi wadanganyika wenye hiyo TV msituaibishe kwa upuuzi huu ! na tunajaribu kuliona kuwa ni la kiutawala zaidi sababu hapa kwetu tumezoea kuona wana taaluma huwa hawasikilizwi na wakubwa zao wa kazi na hupelekea mara zote kuleta matatizo mbeleni ! acheni hii tabia mbadilike ki ukweli kweli kama tulivyotegemea na si kufanya mambo ambayo si mazuri.Tunawapenda sana nyote TBC ni ya kwetu na waigizaji hao ni wadogo zetu na kaka zetu.Mungu ibariki Afrika ! Mungu ibariki Tanzania.(usiibane michuzi wakilisha !)
ReplyDeleteMzushi !