HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI ZINASEMA ALBINO MMOJA AMEUWAWA KIKATILI KATIKATI YA JUMA HILI NA VIUNGO VYA MWILI WAKE KUCHUKULIWA HUKO BIHARAMULO, MKOA WA KAGERA.
MAREHEMU AMBAYE AMETAMBULIKA KWA JINA LA JOVIN MAJALIWA MWENYE UMRI WA MIAKA 46 NA MKAZI WA KIJIJI CHA NYAKATARA ALIKUWA AMEJIPUMZISHA NYUMBANI KWAKE BAADA YA KAZI KWENYE SHAMBA LAKE KABLA YA KUKUMBWA NA HILO BALAA.

INASEMEKANA MNAMO MAJIRA YA SAA NANE HIVI KUNDI LA WATU WALIOBEBA MAPANGA WALIMVAMIA NA KUMKATA MGUU WAKE WA KULIA NA SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA KUTOKOMEA

MKE WA MAREHEMU, ALIYETAMBULIKA KAMA SARAH JOVIN, NA AMBAYE PIA NI ALBINO, ALIPOSIKIA PURUKUSHANI WAKATI AKIANDAA MAAKULI YA JIKONI ALIPIGA KELELE, AMBAPO WAUAJI HAO WAKAMVAMIA NA YEYE PIA NA KUMJERUHI VIBAYA. JIRANI WALIPOKUJA KUTOA MSAADA MAJAMAA YAKAKIMBIA NA HIZO SEHEMU ZA MWILI WA MAREHEMU, WAKIMWACHA SARAH HOI.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA KAGERA, HENRY SALEWI, AKITHIBISHA TUKIO HILO LA KINYAMA ALISEMA KWAMBA SARAH AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA BIHARAMULO NA KWAMBA HALI YAKE INAENDELEA VYEMA.

KAMANDA SALEWI AMESEMA JUHUDI ZA KUWASAKA WAUAJI HAO ZINAENDELEA INGAWA HADI SASA HAKUNA MTU ALIYETIWA MBARONI KUHUSIANA NA TUKIO HILO LA KINYAMA.

MAREHEMU NA MKEWE WAMEJAALIWA KUPATA WATOTO WATATU WENYE UMRI KATI YA MIAKA 4 NA 15 NA MAJIRANI SASA WANA WASIWASI NA HAO WATOTO, KWANI WAWILI KATI YAO NI ALBINO PIA.
HII NI MARA YA TATU KWA WILAYA YA BIHARAMULO KUKUMBWA NA MKASA WA KUSIKITISHA KAMA HUO. MWAKA JANA MAALBINO WAWILI WALIUWAWA KIKATILI NA SEHEMU ZA VIUNGO VYAO KUCHUKULIWA.

----------------------------------------------------------------------

globu hii ya jamii, kwa niaba ya wadau wote wanaoitakia mema nchi yetu, inatoa rambirambi kwa familia hiyo, na kulaani vitendo hivyo kwa nguvu zote. inaungana pia na juhudi za kutokomeza nuksi iliyolikumba taifa letu ya imani potofu za kishirikina zinazochochea mauaji ya kishirikina.

tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti si tu ya kukomesha tabia hiyo ya kinyama bali pia kuwasaka wahusika wote kutoka kwenye vyanzo vyake ambao wanasadikiwa kuwa ni baadhi ya waganga wa kienyeji wenye nia mbaya na taifa hili.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2008

    Nafikiri la awali ni serikali iifanyie kazi mara moja ripoti ya mwanahabari Vicky Ntetema. Waganga wa kienyeji waliomo ndani ya ripoti yake hiyo ni wauaji sawa na wauaji wenyewe kwani ndio wanaowahimiza wafanye hivyo. Vicky kafanya kitu kikubwa na hakika angestahili tuzo ya taifa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2008

    Inasikitisha sana na inaonekana hakuna juhudi madhubuti zilizochukuliwa na serikali kudhibiti hali hiyo zaidi ya viongozi kusimama na kusema "tunalaani vikali vitendo hivyo" lakini hakuna kinachofuata baada ya hapo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2008

    Kaka Michuzi unganisha hii na ile ya mdau Pius, Ukiweza ipigie Debe na wewe watu wasign tupo wengi na tunaweza kufikisha kama tunakupeleka ukapata visitor milion kwa mwezi mmoja iweje hii 100,000 ishindikane? Kama alivyosema mdau mmoja pale tufanikishe hili kwa kuifanya iwe Blog ya Jamii kweli.
    Ni mtazamo Tuu
    Bi Nsipitwe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2008

    kwa mtazamo wangu nashangaa serikali inasubiri nini kuwatafuta na kuwahukumu wahusika hii ni aibu siyo tu kwa taifa hata kwa muumba.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2008

    NI JANA TU KUNA MDAU ALITOA MADA YA KULAAN MAUAJ YA ALBINO,LEO NIMEPATA HABARI KUNA MTU KAUAWA NIMESHTUKA SANA,YA NI AIBU KULIKO WALIYOIPATA SOUTH AFRICA KUUWA WAGAN,SIS TUNAUWA WENYEJ NA AFRICA IMEKUWA MSTARI WA MBELE KULALAMIKA KUHUSU UBAGUZ WAKAT SIS WENYEWE BADO TUNABAGUANA.NAONA HIZ NI DALIL ZA SIKU YA MWISHO POLEN SANA WAFIWA TUKO PAMOJA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2008

    Kwanza natoa pole sana kwa ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu.Ni jana tu nilisema haya mauaji yapo tusilaumu Al-jazeera,CNN,BBC n.k.Wanablog tunaendelea kulaani hivi vitendo na kuitupia lawama moja moja serikali hasa waziri anayehusika kwa kushindwa kudhibiti hii hali.Kama hali itaendelea itabidi wananchi tufanye maandamano nchi nzima.Wanaharakati wa haki za binadamu mko wapi???

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2008

    It is a shame to all tanzanian's......shame on you........it is gonna get ugly very soon..the government needs to take actions...i am pissed...Now i see why white people calls us animals,i wont blame them considering wat is happening to tanzania....very sad.......

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2008

    Mauaji ya albino ni jambo la kusikitisha, kikatili, na ni ukiukwaji mkubwa wa hahi za binadamu. Wanaofanya mauaji haya si waungwana hata kidogo, hawana hata chembe ya ubindamu hivyo hawa si watu wa kuwavumilia hata kidogo katika jamii ya Watanzania ambayo kwa muda mrefu imeaminika kuwa ni jamii ya wastaarabu. Hizo imani za kishirikina zilipita utu wa binadamu hazistahmilik hata kidogo. Serikali ishirikiane na kila raia mwema kutokomeza kadhia hii katika jamii yetu ambayo imewaweka ndugu zetu albino katika hali ya wasi wasi ndani ya nci yao wenyewe. Ni aibu kubwa kwa Taifa letu kwa mauaji haya ninawasilisha kwa wahusika kuwa wale wote waliokamatwa wachukuliwe hatua kali za kisheria. Mauaji ya albino ni kitendo kisichokubalika kabisa hasa katika jamii yetu ya Kistaarabu ya Tanzania. Ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi inayotambulika kikatiba nchini kwetu na pia katika jamii ya Kimataifa haukubaliki hata kidogo. Natumia fursa hii kuwapa pole wale wote walioathirika na vitendo hivi, wale waliopoteza maisha yao kwa kuuawa kikatili Mwenyezi Mungu awape pumziko la amani. Changamoto kwetu sote tunaoitakia mema Tanzania na kuwajali wenzetu albino Tushiriki kwa hali na mali kulaania vitendo hivi. Wale mliopo huko nyumbani Tanzania muwafichue wale wote wanaochochea mauji haya. Sote pamoja tuifanye Tanzania mahali salama pa kuishi kwa raia wake wote na wageni bila kujali rangi,dini, kabila, jinsi. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE. AMEN

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2008

    Huu ni uzembe wa viongozi wa serikari yaani mimi naona hata wao hawadhamini maisha ya hawa watu.

    polisi mkuu wa mkoa wowote kwanzia sasa tukisikia mauaji hana kazi na atafikishwa mahakamani.

    kwani polisi kazi yao nini??
    au kama hawawezi wapeni ulinzi hawa watu kila sehemu walipo kuwe na dolia

    sio mnakaa tu mahofisini bila kazi na kusubili mishahara

    hawa watu wanahitaji kuishi kama wewe rais wa nchi unavyoitaji kuishi weka ulinzi

    yaani imeniuma kweli ila huu wote ni uzembe wa viongozi hawana wanaloliweza iwe rusha mmeshindwa kuizibiti na mauaji sasa mnafanyanini??? si mjiuzuru kama hamuwezi kazi sio kuuwisha watu kwa uzembe wenu

    hivi mumepewa madalaka jina au mlinde watu??? hao waganga wa kienyeji wako wangapi na seikari kushindwa kuwazibiti???

    watu wenyewe hawakuenda shule wanawashinda vipi??

    sasa kesho kwa mola mtajibu nini kama aliwapa nafasi za uongozi mukasababisha mauaji??

    naomba mpeane majukumu kamanda wa polisi wa mkoa wowote aweke ulizi hawezi ajiuzuru la sivyo yakitokea mauaji yeye ndiye atakekuwa mshitakiwa no moja!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2008

    HALAFU WATANZANIA TUNASEMA TUNA SERIKALI TENA KWA BWE BWE KABISA TUNASEMA NI SERIKALI YA AWAMU YA 4.!!!

    MTU MWENYE AKILI ANGEDHANI SERIKALI YA AWAMU YA NNE INGEKUWA IMEIFUNZA MAMBO MENGI YA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO TOKA SERIKALI YA AWAMU YA 1, 2 NA YA 3..!!!

    BURE KABISA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2008

    KAMA SERIKALI ILIWEZA KUPELEKA WANAJESHI COMORO KWENYE VITA AMBAYO HAUTUSAIDII KITU CHOCHOTE,WANASHINDWA VIPI KUMALIZA HILI TATIZO ?

    SOURCE YA TATIZO LINAJULIKANA KWAMBA NI WAGANGA WA KIENYEJI,WATU WAMEFANYA INVESTIGATION,TATIZO LIKO WAPI ?

    WAPE KAZI WANAJESHI WAKAKAMATE WAGANGA WOTE NCHI NZIMA,WAPATE KIPIGO KIZURI KABISA THEN TUONE KAMA HUU UPUMBAZU UTAENDELEA....

    AMA SERIKALI IWAPE ULINZI,KILA MKUU WA MKOA APATE KUJUA KUNA ALBINO WANGAPI KWENYE MKOA WAKE NA HAKIKISHE HAKUNA HATA MMOJA ANAPATA MATATIZO.

    WATU WAMEKAA TUU MAOFISINI NA VITAMBI VIKUBWA,HAWAFANYI KAZI YOYOTE.

    SIJASIKIA WATU WAKISEMA IWEKWE KAMATI MAALUMU KUWEZA KUMALIZA HILI TATIZO,INAELEKEA FEDHA NI MUHIMU SANA KULIKO MAISHA YA BINADAMU,MAANA INGEKUWA ISSUE YA FEDHA WATU WANGEKUWA WAKALI KAMA NINI.

    ANYWAYS,MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.MAANA HII NI AIBU KUBWA SANA KWA TANZANIA...................

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2008

    Mruzi mingi humpoteza Mbwa
    Wadau tuweke comments sehemu moja ili tupate wingi wa signature, comment yako ndio signature yako
    Fiki wajameno?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2008

    serikali itaingilia vipi hili swala wakati viongozi wake wanajihusisha na ushirikina hata hao polosi wenyewe, na wanapenda ushirikina.

    ReplyDelete
  14. MIE NATAKA KUJUA KWA NINI...HILI WIMBI LIMEIBUKA SASA ALL OF A SUDENLY???AU LILIKUWEPO TANGU ZAMANI??KM LILIKUWEPO KWA NINI...KUPINDI HIKI LIMEKUJA KWA KASI YA JUU??NINI KICHOCHEZI...???TUKISHAJUA HAYO LABDA TUTAJUA JINSI YA KUTATUA....

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 28, 2008

    viongozi wetu wengi ni vitambi tuuuuuuuuuuuuuu vikubwa... Mapimbi kabisa!!! hakuna kabisa leadership skills. Kila sector ya serikali ni watu wenye vitambi tuu.. aibu jamani viongozi wa Tanzania!!!!!!, Issue inaooneka wazi, kwamba tatizo (1)liko kwa waganga wa kienyeji kwa hiyo nikitu gani kinawashinda hawa viongozi mbumbumbu kuwatafuta na kuwathibi hawa waganga! (2)kama anon hapo juu alivo-suggest, viongozi wa mikoa wawatafute ndugu zetu albino na wawape ulinzi mkali! how hard is it!

    K

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...