INASEMEKANA MNAMO MAJIRA YA SAA NANE HIVI KUNDI LA WATU WALIOBEBA MAPANGA WALIMVAMIA NA KUMKATA MGUU WAKE WA KULIA NA SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA KUTOKOMEA
MKE WA MAREHEMU, ALIYETAMBULIKA KAMA SARAH JOVIN, NA AMBAYE PIA NI ALBINO, ALIPOSIKIA PURUKUSHANI WAKATI AKIANDAA MAAKULI YA JIKONI ALIPIGA KELELE, AMBAPO WAUAJI HAO WAKAMVAMIA NA YEYE PIA NA KUMJERUHI VIBAYA. JIRANI WALIPOKUJA KUTOA MSAADA MAJAMAA YAKAKIMBIA NA HIZO SEHEMU ZA MWILI WA MAREHEMU, WAKIMWACHA SARAH HOI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA KAGERA, HENRY SALEWI, AKITHIBISHA TUKIO HILO LA KINYAMA ALISEMA KWAMBA SARAH AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA BIHARAMULO NA KWAMBA HALI YAKE INAENDELEA VYEMA.
KAMANDA SALEWI AMESEMA JUHUDI ZA KUWASAKA WAUAJI HAO ZINAENDELEA INGAWA HADI SASA HAKUNA MTU ALIYETIWA MBARONI KUHUSIANA NA TUKIO HILO LA KINYAMA.
----------------------------------------------------------------------
globu hii ya jamii, kwa niaba ya wadau wote wanaoitakia mema nchi yetu, inatoa rambirambi kwa familia hiyo, na kulaani vitendo hivyo kwa nguvu zote. inaungana pia na juhudi za kutokomeza nuksi iliyolikumba taifa letu ya imani potofu za kishirikina zinazochochea mauaji ya kishirikina.
tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti si tu ya kukomesha tabia hiyo ya kinyama bali pia kuwasaka wahusika wote kutoka kwenye vyanzo vyake ambao wanasadikiwa kuwa ni baadhi ya waganga wa kienyeji wenye nia mbaya na taifa hili.
Nafikiri la awali ni serikali iifanyie kazi mara moja ripoti ya mwanahabari Vicky Ntetema. Waganga wa kienyeji waliomo ndani ya ripoti yake hiyo ni wauaji sawa na wauaji wenyewe kwani ndio wanaowahimiza wafanye hivyo. Vicky kafanya kitu kikubwa na hakika angestahili tuzo ya taifa.
ReplyDeleteInasikitisha sana na inaonekana hakuna juhudi madhubuti zilizochukuliwa na serikali kudhibiti hali hiyo zaidi ya viongozi kusimama na kusema "tunalaani vikali vitendo hivyo" lakini hakuna kinachofuata baada ya hapo.
ReplyDeleteKaka Michuzi unganisha hii na ile ya mdau Pius, Ukiweza ipigie Debe na wewe watu wasign tupo wengi na tunaweza kufikisha kama tunakupeleka ukapata visitor milion kwa mwezi mmoja iweje hii 100,000 ishindikane? Kama alivyosema mdau mmoja pale tufanikishe hili kwa kuifanya iwe Blog ya Jamii kweli.
ReplyDeleteNi mtazamo Tuu
Bi Nsipitwe.
kwa mtazamo wangu nashangaa serikali inasubiri nini kuwatafuta na kuwahukumu wahusika hii ni aibu siyo tu kwa taifa hata kwa muumba.
ReplyDeleteNI JANA TU KUNA MDAU ALITOA MADA YA KULAAN MAUAJ YA ALBINO,LEO NIMEPATA HABARI KUNA MTU KAUAWA NIMESHTUKA SANA,YA NI AIBU KULIKO WALIYOIPATA SOUTH AFRICA KUUWA WAGAN,SIS TUNAUWA WENYEJ NA AFRICA IMEKUWA MSTARI WA MBELE KULALAMIKA KUHUSU UBAGUZ WAKAT SIS WENYEWE BADO TUNABAGUANA.NAONA HIZ NI DALIL ZA SIKU YA MWISHO POLEN SANA WAFIWA TUKO PAMOJA
ReplyDeleteKwanza natoa pole sana kwa ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu.Ni jana tu nilisema haya mauaji yapo tusilaumu Al-jazeera,CNN,BBC n.k.Wanablog tunaendelea kulaani hivi vitendo na kuitupia lawama moja moja serikali hasa waziri anayehusika kwa kushindwa kudhibiti hii hali.Kama hali itaendelea itabidi wananchi tufanye maandamano nchi nzima.Wanaharakati wa haki za binadamu mko wapi???
ReplyDeleteIt is a shame to all tanzanian's......shame on you........it is gonna get ugly very soon..the government needs to take actions...i am pissed...Now i see why white people calls us animals,i wont blame them considering wat is happening to tanzania....very sad.......
ReplyDeleteMauaji ya albino ni jambo la kusikitisha, kikatili, na ni ukiukwaji mkubwa wa hahi za binadamu. Wanaofanya mauaji haya si waungwana hata kidogo, hawana hata chembe ya ubindamu hivyo hawa si watu wa kuwavumilia hata kidogo katika jamii ya Watanzania ambayo kwa muda mrefu imeaminika kuwa ni jamii ya wastaarabu. Hizo imani za kishirikina zilipita utu wa binadamu hazistahmilik hata kidogo. Serikali ishirikiane na kila raia mwema kutokomeza kadhia hii katika jamii yetu ambayo imewaweka ndugu zetu albino katika hali ya wasi wasi ndani ya nci yao wenyewe. Ni aibu kubwa kwa Taifa letu kwa mauaji haya ninawasilisha kwa wahusika kuwa wale wote waliokamatwa wachukuliwe hatua kali za kisheria. Mauaji ya albino ni kitendo kisichokubalika kabisa hasa katika jamii yetu ya Kistaarabu ya Tanzania. Ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi inayotambulika kikatiba nchini kwetu na pia katika jamii ya Kimataifa haukubaliki hata kidogo. Natumia fursa hii kuwapa pole wale wote walioathirika na vitendo hivi, wale waliopoteza maisha yao kwa kuuawa kikatili Mwenyezi Mungu awape pumziko la amani. Changamoto kwetu sote tunaoitakia mema Tanzania na kuwajali wenzetu albino Tushiriki kwa hali na mali kulaania vitendo hivi. Wale mliopo huko nyumbani Tanzania muwafichue wale wote wanaochochea mauji haya. Sote pamoja tuifanye Tanzania mahali salama pa kuishi kwa raia wake wote na wageni bila kujali rangi,dini, kabila, jinsi. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE. AMEN
ReplyDeleteHuu ni uzembe wa viongozi wa serikari yaani mimi naona hata wao hawadhamini maisha ya hawa watu.
ReplyDeletepolisi mkuu wa mkoa wowote kwanzia sasa tukisikia mauaji hana kazi na atafikishwa mahakamani.
kwani polisi kazi yao nini??
au kama hawawezi wapeni ulinzi hawa watu kila sehemu walipo kuwe na dolia
sio mnakaa tu mahofisini bila kazi na kusubili mishahara
hawa watu wanahitaji kuishi kama wewe rais wa nchi unavyoitaji kuishi weka ulinzi
yaani imeniuma kweli ila huu wote ni uzembe wa viongozi hawana wanaloliweza iwe rusha mmeshindwa kuizibiti na mauaji sasa mnafanyanini??? si mjiuzuru kama hamuwezi kazi sio kuuwisha watu kwa uzembe wenu
hivi mumepewa madalaka jina au mlinde watu??? hao waganga wa kienyeji wako wangapi na seikari kushindwa kuwazibiti???
watu wenyewe hawakuenda shule wanawashinda vipi??
sasa kesho kwa mola mtajibu nini kama aliwapa nafasi za uongozi mukasababisha mauaji??
naomba mpeane majukumu kamanda wa polisi wa mkoa wowote aweke ulizi hawezi ajiuzuru la sivyo yakitokea mauaji yeye ndiye atakekuwa mshitakiwa no moja!!!
HALAFU WATANZANIA TUNASEMA TUNA SERIKALI TENA KWA BWE BWE KABISA TUNASEMA NI SERIKALI YA AWAMU YA 4.!!!
ReplyDeleteMTU MWENYE AKILI ANGEDHANI SERIKALI YA AWAMU YA NNE INGEKUWA IMEIFUNZA MAMBO MENGI YA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO TOKA SERIKALI YA AWAMU YA 1, 2 NA YA 3..!!!
BURE KABISA.
KAMA SERIKALI ILIWEZA KUPELEKA WANAJESHI COMORO KWENYE VITA AMBAYO HAUTUSAIDII KITU CHOCHOTE,WANASHINDWA VIPI KUMALIZA HILI TATIZO ?
ReplyDeleteSOURCE YA TATIZO LINAJULIKANA KWAMBA NI WAGANGA WA KIENYEJI,WATU WAMEFANYA INVESTIGATION,TATIZO LIKO WAPI ?
WAPE KAZI WANAJESHI WAKAKAMATE WAGANGA WOTE NCHI NZIMA,WAPATE KIPIGO KIZURI KABISA THEN TUONE KAMA HUU UPUMBAZU UTAENDELEA....
AMA SERIKALI IWAPE ULINZI,KILA MKUU WA MKOA APATE KUJUA KUNA ALBINO WANGAPI KWENYE MKOA WAKE NA HAKIKISHE HAKUNA HATA MMOJA ANAPATA MATATIZO.
WATU WAMEKAA TUU MAOFISINI NA VITAMBI VIKUBWA,HAWAFANYI KAZI YOYOTE.
SIJASIKIA WATU WAKISEMA IWEKWE KAMATI MAALUMU KUWEZA KUMALIZA HILI TATIZO,INAELEKEA FEDHA NI MUHIMU SANA KULIKO MAISHA YA BINADAMU,MAANA INGEKUWA ISSUE YA FEDHA WATU WANGEKUWA WAKALI KAMA NINI.
ANYWAYS,MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.MAANA HII NI AIBU KUBWA SANA KWA TANZANIA...................
Mruzi mingi humpoteza Mbwa
ReplyDeleteWadau tuweke comments sehemu moja ili tupate wingi wa signature, comment yako ndio signature yako
Fiki wajameno?
serikali itaingilia vipi hili swala wakati viongozi wake wanajihusisha na ushirikina hata hao polosi wenyewe, na wanapenda ushirikina.
ReplyDeleteMIE NATAKA KUJUA KWA NINI...HILI WIMBI LIMEIBUKA SASA ALL OF A SUDENLY???AU LILIKUWEPO TANGU ZAMANI??KM LILIKUWEPO KWA NINI...KUPINDI HIKI LIMEKUJA KWA KASI YA JUU??NINI KICHOCHEZI...???TUKISHAJUA HAYO LABDA TUTAJUA JINSI YA KUTATUA....
ReplyDeleteviongozi wetu wengi ni vitambi tuuuuuuuuuuuuuu vikubwa... Mapimbi kabisa!!! hakuna kabisa leadership skills. Kila sector ya serikali ni watu wenye vitambi tuu.. aibu jamani viongozi wa Tanzania!!!!!!, Issue inaooneka wazi, kwamba tatizo (1)liko kwa waganga wa kienyeji kwa hiyo nikitu gani kinawashinda hawa viongozi mbumbumbu kuwatafuta na kuwathibi hawa waganga! (2)kama anon hapo juu alivo-suggest, viongozi wa mikoa wawatafute ndugu zetu albino na wawape ulinzi mkali! how hard is it!
ReplyDeleteK