wadau wa banda la ofisi ya ukaguzi wa hesabu za serikali ambalo pamoja na mambo mengine, limetoa ripoti ya ukaguzi uliofanyika kuishia juni mwaka jana na kuiweka kwenye cd ili kila anayeitaka aipate katika mfumo wa kopi laini
f

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2008

    ndo wazee wa ufisadi wenyewe hao....kudadadeki!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2008

    Mh, hawa wana mahesabu wetu wamenona hao, cheki nundu hizo!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2008

    Watu kama hawa hawakupaswa kuweka banda sabasaba. It is a waste of tax payers' money.

    Taasisi zinazopaswa kuweka mabanda sabasaba ni zile zinazotoa huduma kwa jamii. Hawa jaaa kazi yao ni ku-audit mahesabu ya serikali. Ukaaji wao sabasaba hauna maana yoyote.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2008

    Hii idara/ofisi bwana inanuka kwa "Rushwa" pia inasaidia rushwa kuongezeka katika idara za serikali Tanzania.
    Wao wanaona raha sana kuonekana sabasaba kujionyesha wakati ukiwaambia waende mikoa ya Rukwa, Songea, Mara, Bukoba, Mtwara au Lindi kukagua ufisadi watakuambia hawana fedha.(wanasema mafungu ya hizo safari hazijatoka wizara ya fedha)
    Wizi unafanywa na maafisa wa serikali kuu na serikali za mitaa mpaka miaka inapita ndo wao wanakuja kukagua vitabu na kazi na mali.Huku wakitumia mbinu za kizamani za ukaguzi, Kwa ufupi wanakuta kila kitu kimesharekebishwa na wakigundua hata hilo kosa kidogo wanapewa nao chao ambacho kwa lugha fupi ni wizi mwingine-"Rushwa".
    Malamiko yangu ni kama ifuatavyo:
    (1).Toka lini umeona wewe ukaguzi wao unafanya watu kwenda mahakamani, kufutwa au kusimamishwa kazi. Sana sana maafisa wengi wa serikali(Accounting officers) wanaowashika/tuhumu huwa wanahamishwa vituo vya kazi, na wao kusema ni makosa madogo madogo yanatakiwa kusahihishwa kutokana na kutoelewa sheria za kihasibu.
    (2).Website yao kwanza hawana chochote zaidi ya taarifa za (NAO) na ripoti ya (CAG) ambayo ndo hiyo wanatumia CD na kutoa copy za bure sabasaba. Nendeni mikoani mkakague wizi kabla haujafunikwa au saidieni kuupunguza basi.
    (3)Elimu ya wafanyakazi wao wengi ni ile ya zamani isiyoendana na muundo wa sasa wa wizi wa kutumia Technologia.Wenye CPA ni wa kuhesabu na wengi wamepanda vyeo kwa mtindo wa kukaa kazini/serikalini muda mrefu.
    (4) Wanaangalia sana wizara au agencies zenye fedha watakazopata "Rushwa" kama Tanroads, NK.Ambazo wizi wao unafanywa na watu walioenda shule tena za nje za uhandisi.
    Wengi wa wafanyakazi hawa kama kweli ni wataalamu jiulize wakiachishwa hapo kazi wanaweza pata kazi kama hiyo au kufanya kazi kwa ufanisi kama wenzao wa Ernest Young au Pricewater?. Ukiwauliza wanasema mshahara haulingani na wamashirika , lakini je mkipewa huo mshahara na kupunguza idadi ya wafanyakazi ilingane na mashirika mengine kam Ernest young mtaweza.
    (5)Wana-majumba ambayo ukijiuliza wameyapataje, hawana jibu,wakati hakuna hata mikopo waliochukua kutoka katika mabenki kama sio "Rushwa wanazopewa"
    Hii ofisi bwana ina malalamiko sana kama zilivyo zote za serikali na wanajifanya "miungu mtu"
    Nendeni mikoani mkagua kwa ufanisi na fanyeni kweli katika ukaguzi wenu sio kutoa CD kwa copy hapo sabasaba. Tuambiane fedha ngapi zimetumika au zitatumika katika nyinyi kukaa hapo sabasaba na zingesaidiaje katika jambo lingine. Najua jibu litakuwa mmpewa na "Donors" ili mjitangaze lakini je sio nyinyi mlionga'ng'ania kujionyesha hapo au kujenga hoja na yeye akakubali.
    Acheni hizo za kizamani fanyeni kweli katika ukaguzi, nchi imeliwa sana mpaka sasa tunachoka tukiona habari zozote.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 07, 2008

    Hii inaudhi sana jamani!!!
    Kama ni uchungu na nchi basi hii idara ndio mbovu kupita zote.
    waone sasa walivyokaa hapo sabasaba na bosi wao aliyekuwa NBAA (Ludovick Utooh)anajifanya kutoa ripoti ndefu katika CD isiyokuwa na Shoka, wala nguvu za kumshika yeyote. Ukiimu-uliza anakuambia sisi kazi yetu ni kutoa ripoti, then bunge linajadili halafu Rais au bunge linaamua nani wa kushugulikiwa au kufukuzwa.
    Yaani hii idara ni ya kutoa "recomendation tu" katika ripoti yake ya "pages 163". sasa kuna kazi gani kuwepo serikalini. Mtaifishwe na kazi zenu wapewa Ernest young au Pricewaters maana hamfanyi lolote.
    Mfano :Kiasi cha fedha za kiwango cha "Shs billion 25,836,825,981.00 za Kitanzania" kwa mwaka huo wa fedha zimetumika isivyoeleweka katika ununuzi wa vifaa, mali au huduma. Unataka kusema mwizi gani serikalini atatumia njia inayoeleweka ili umbane yeye zaidi ya kuajiri mambumbu na mazumbukuku ili aseme walikuwa hawajui walifanyalo.Angalia ripoti inasema eti vifaa vilivyonunuliwa havikuingizwa katika ledgers(Vitabu vinavyotakiwa) hiyo uliona wapi mtu anajua kuandika na kusoma anaacha kuingiza alichonunua kama sio mwajiriwa wa serikali. Fanya hivyo shirika la kigeni kama huna kazi kesho na gereza linakusubiri keshokutwa.
    Mfano mwingine : Ripoti ya ukaguzi wa Tanzania Embassy Washington DC, - USA inasema
    matters leading to qualification
    • Payment made but not supported by quotations
    Shs.32,966,854.74
    • Expenditure not accounted for Shs.85,278,900
    • Splitting Tenders and contracts Shs.58,340,972
    • Procurement of contract works exceeding subaccounting
    officer’s power Shs 65,784,765
    -kwa kifupi wamekula kiasi cha karibu bilioni 3 za kitanzania maafisa wanane waliopo pale DC wakishirikiana kuilani an wageni wanaotoka TZ kila kukicha na bado wapo kazini mpaka leo. Wapi uliona afisa anaidhinisha kiasi cha millioni 58 au kununua mali ya kiasi cha millioni 32 bila kufuata taratibu za ununuzi kama sio serikalini na hakuna atakayemfanya lolote.
    Acheni hata kutoa hiyo REPORT halafu hakuna sehemu inasema amefungwa nani. Kazi ni kusema "procurement rules were not used accordingly due to unqualified staff".

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2008

    mhh, soma ripoti uone mambo kweli.
    wizara zinazoongoza kwa "Maupungufu" kama wanavyoita wao na sio wizi.
    Mimi nauita wizi wa fedha ya umma. wizara zinazoomgoza ni Ya Rais mwenyewe- Ikulu, the ofisi ya Rais, then Bunge, then TPDF.
    Sasa nani amfunge nani au amshike nani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2008

    This is another scum and a gimmick to simple wananchi's, especially those who don’t know the in-s and out-s of Accountancy and Auditing procedures or whereabouts in our money swindling government.
    It’s shame now that the same Government auditing office which failed to tell us what was happening in one of the biggest money laundering ever to be reported in our nation history, that was done by scrumptious BOT officials with collaboration of some MP’s and greedy fake Tanzanian business folks, is now on front form of faking us in its shame publicity at Sabasaba grounds.
    Where was it -all the years to report on money laundering, until a foreign auditing firm with a branch in Tanzania (Ernst Young?) happens to feed us? Funny haaaa!!!. and without shame they were given the report in matter of days and we all saw the fruitful results. I wish Ernst young was to do all the rest auditing if it was not the case of national security.
    I am wishing this office to disappear in my eyes, as the only thing it is doing now is issuing this phony like, long -reports that’s stands to me as policy which does not harm or do anything. You will not let me read your reports anymore; where you are showing at a least 25 billion Tshs went out of the door that stupidly and no one, I mean no one is in the jail, but just your typed stupid duped recommendations.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2008

    Serikalini si kuna OPRAS? I have lost trust on OPRAS because kama kweli OPRAS inapima utendaji wa wafanyakazi serikalini na kuwachukulia hatua watendaji wabovu, basi ofisi nzima ya hawa jamaa wenye matumbo makubwa ilipaswa kwenda na maji na wakaajiriwa watu wenye kujua wanachokifanya.

    Get rid of OPRAS. It is another EPA.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2008

    wabongo tokea tulipoacha kuvaa kaunda suit na kukimbilia bush suit, basi haturejei mpaka pancha. si unaona maafisa walivyojifunga kamba shingoni hata kama joto linafikia digrii 100. Wabongo tutakufa kiofisa!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2008

    hawa ni mafisadi but u have to see their dilemma. Its a choice between dignity and family. Wewe ukikataa kukunja hesabu kibarua kinaota nyasi. ..ukumbuke kuna watu mia watakaoweza kufanya iyo kazi yako bila wasiwasi wa kuzikunja hizo hesabu. Alafu una familia hapo na wazee kijijini wanakutegemea na kazi yako nzuri. Its a choice no one deserves to make. Tatizo si hawa tu...tatizo ni system nzima. Kwa wanasheria wetu...naomba mtu anieleweshe kifungu/ibara ya 7 ya katiba ya tanzania. Tena ngojea niwawekee copy kabisa:

    7.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali,
    vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenye
    kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria
    au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa
    kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya
    Sehemu hii ya Sura hii.
    (2) Masharti ya Sehemu hii ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya
    kisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchini
    haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au
    kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kama
    sheria, au hukumu yoyote, inaambatana na masharti ya
    Sehemu hii ya Sura hii.

    kweli tuko nyuma

    mtoto

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2008

    Anon wa jina la mtoto unachoandika au kuqoute hakipo.
    Unasema ni dignity, hivyo unahalalisha waibe kwa kuwa system nzima ni ya wezi. Basi hakuna maana ya kuwa na idara ya ukaguzi wa mahesabu kama hakuna wanachofanya.
    Tunategemea hii idara na idara kama polisi, PCB na mahakama ndo ziwe mstari wa mbele kuwa angalau safi ,kufanya kazi zake sahihi na kufanya idara zingine kuogopa.Hii ita-send message ya nguvu kwa wezi na rushwa kupungua.
    Kama wasomi wapo kwa nini hizi idara zisiwe mfano wa mambo safi.
    Kutokana na kuoneana aibu ndo maana rushwa inabaki pale pale.
    Kumbuka enzi za nyerere hizi idara zilikuwa zinaaaminika sana na kufanya kila mtu kuziogopa na sisi tukasema huo ni udikteta. Kama udikteta utafanya watu kutikuiba basi ni mzuri kuliko uhuru wa kishenzi wa Rushwa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2008

    Anon wa mwisho kabisa...yani July 08, 2008 11:30 PM, nadhani hukunipata vizuri. Yani nimesema waamue kati ya dignity (kuwa wasafi na kukataa kukunja hesabu) au kuinua familia zao (nikiwa na maana kukunja hesaba na kupata mishahara yao kama kawaida kwa kusudi la kusaidia familia zao). Kwa iyo sijasema kuwa kula rushwa ni dignity. Nadhani kwa vingine tunakubaliana. Lakini ni sawa lazima wasimamie kazi yao kwa dignity. Ngojea nikupe mfano mwingine. A traffic officer pale bongo...mshahara wake wa mwezi ni kiasi gani? Tuseme ni kama laki moja (i sincerely hope its more) lakini twende na hiyo laki moja kwa mwezi. Yeye mwenyewe anajua kuwa akisimamisha magari matano...anaingizia serikali mshahara wake mzima. Na iyo ni kwa masaa tu! Alafu hapo hapo anajua hata hiyo pesa itaenda kulika huko juu. Hiyo haimpi motisha yoyote ya kufanya kazi yake kwa dhati! Same thing applies to these people. Kuna watu wanangojea hizo nafasi zao hapo. Yeye akijifanya msafi...kibarua nacho chakipa. Yeye (as an individual) hana nguvu yeyote katika kubadilisha system. Hata akifukuzwa kazi, kwenda magazetini kutangaza haitafika mbali. Kesi tunajua mahakamani nako ni kupigwa tarehe. Tatizo system nzima ya utawala Tanzania imejengwa ku-support serikali. Na serikali imeundwa na chama kimoja. Hivyo system nzima ina-support hicho chama kimoja tu! Sasa hapa utamsaidiaje mtu kama huyu katika hii tabu? Sababu kama hizi ndo zimefanya hadi kampuni ya nje (Enerst & Young) kuja kufanya hesabu. Wa ndani wote hawawezi maana wanajichunga.

    Hapo uliposema hicho nilicho-quote hapo hakipo ningependa kukuomba ukasome katiba ya nchi yako. Hasa hiyo ibara ya 7. Katiba utaweza kuipata hata kwenye site ya government. Mimi ndo huko nilipoishusha na kuisoma. Kusema kweli...inasikitisha. Kwa maneno mengine (in other words) Ibara hiyo inaosema Serikali haiwezi kushitakiwa wowote uvunjaji wowote wa sehemu hii ya katiba. Sehemu yenyewe yaongelea mamlaka ya serikali. Umenipata hapo?


    mtoto
    Jamani tuelimishane

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 09, 2008

    Ni mahesabu gani wanayoyachunguza ni kichekesho ya mafisadi?Sio umuhimu kwa ofisi ya ukaguzi wa hesabu za serikali kushiriki katika maoonyesho hayo kwani kazi yao haihitaji matangazo hivi kweli tunahitaji kua na banda la Ikulu,banda la makamu wa Rais,Banda la Waziri mkuu na n.k Hivi ni vichekesho.MUNGU IBARIKI ATANZANIA;.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...