NBC yaendeleza mipango yake ya kusaidia jamii
• yatoa msaada wa vifaa vya elimu
• kuendelea kusaidia nyanja ya elimu nchini
• yatoa msaada wa vifaa vya elimu
• kuendelea kusaidia nyanja ya elimu nchini
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa msaada wa vifaa vya elimu kwa shule mbili jijini Dar es Salaam katika mpango wake unaoendelea wa kusaidia shughuli za maendeleo katika jamii (CSR) ambao unalenga elimu.
Jana wafanyakazi kutoka Idara ya Hazina ya benki hiyo walitoa vifaa vya maabara vyenye thamani ya Sh. milioni 2 kwa Shule ya Sekondari Mbagala Kuu, wakati wenzao wa Tawi la Samora jijini Dar es Salaam walitoa madawati yenye thamani ya Sh. milioni 2 kwa Shule ya Msingi Buguruni.
Akiongea jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa NBC, Bw. William Kallaghe alisema, “NBC ilipoanza mpango huu, ulikuwa ni mwanzo wa azma yetu ya muda mrefu ya kuhakikisha kwamba elimu nchini inatolewa katika mazingira bora. Tunatambua thamani na umuhimu wa kuwa na mazingira yenye vifaa vyote muhimu kwa ajili ya elimu na misaada hii inalenga moja kwa moja katika hilo.”
Mpango huo, ambao ulianzishwa mwaka 2007 wakati NBC ikisherehekea miaka 40 tangu kuanzishwa kwake, unalenga kuwashirikisha wafanyakazi wake katika miradi inayokusudia kuboresha maisha katika jamii wanazoishi.
Msaada huu ni sehemu ya mpango wa miezi mitano wenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 120 ambao utawashirikisha wafanyakazi katika kusaidia nyanja ya elimu nchi nzima. Kusudi la miradi hii ni kurudisha faida ambayo benki hiyo inapata ili isaidie jamii zilezile ambazo NBC inazihudumia.
Mipango ya maendeleo ya benki hiyo kwa mwaka 2008 inatoa kipaumbele kwa elimu, ambapo wafanyakazi wa benki hiyo watashiriki katika miradi 70 ya jamii inayolenga elimu.
jamani, kwa ushauri mzuri, huyu baba aliyevaa shati la kitenge anatakiwa kufanya mazoezi na aangalie anachokula. Ili kukwepa magojwa ya moyo na kisukari pia blood pressure
ReplyDeleteThanks to NBC
ReplyDeleteNaunga mkono juhudi za sekta binafsi kusaidia maendeleo hasa ya elimu nchini.
ReplyDeleteIla kwa idara nzima ya benki kubwa kama nbc kutoa msaada wa Shs Mil 2 ni dhihaka kwa wale wote wenye nia au ambao wametoa misaada kama hii.
jitu la miraba minne..
ReplyDeleteKutoa ni moyo. Wangetoa watu hata laki 5 basi tungefika mbali. Kila mtu atoe na makampuni yatoe kusaidia mambo yetu.
ReplyDeleteThanx NBC
Ni Kweli mdau. Benki ya NBC hivi majuzi tu ilitoa gawio la mabilioni kwa serikali wakati serikali inamiliki 30%. That is to say imekuwa ikitengeneza faida kubwa sana. Iweje eti tumilioni tuwili ndo tugawiwe.
ReplyDeleteCha kujiuliza hapa hiyo gharama ya Publicity, pamoja na event budget ni zaidi ya Millioni 2. Jamani nyie NBC hebu acheni kuigiza, millini mbili kitu gani.
hawa wabubge wetu mbona wanajiachia hivyo??? Hivi huwa hawajui matokeo ya kulaa kulaa ovyo?????
ReplyDeletekwa taarifa yenu yaani hicho ni kitengo tu kimeiwakilisha NBC sasa piga mahesabu kuna vitengo vingapi na branch ziko ngapi then zidisha kwa 2M utapata jibu jumla ni kiasi gani....
ReplyDeleteNBC tusonge mbele mnajitahidi hata japo kwa hichi kidogo....
Yes ni nakubaliana nawe kuwa hilo ni tawi na kitengo tu. Sasa kama wewe ni muelewa mzuri wa mambo ya uchumi, utaona kuwa kila tawi likitumia event budget yake peke yake, kwa shuhuli hiyo hiyo moja. Sasa kama kweli wanaijali jamii, kwanini wasingeconsolidate ili watoe katika awamu chache, na ile budget ambayo wangeitumia kama event management wangeongezea katika budget ya misaada ili shule nyingi zaidi zifaidike au vifaa vingi zaidi vinunuliewe. NBC wana hela asikwambie mtu.
ReplyDeleteNaskia sasa hivi wana matawi yasiopungua 50 (sina hakika) zidisha mara milioni mbili unapata millioni 100. Lakini hapo hapo hatuna uhakika kama kweli kila tawi litakwa na nafasi ya kushiriki kwa kuwa na shuhuli yake yenyewe. Unaweza ukashangaa chezo likaishia hapo. Kila mtu kwao, mbunge nae kashapata pa kufanyia kampeni.