Bila shaka Mkuu wa Wilaya ya nanihii unaliendeleza libeneke kama kawa.
Baada ya salaam hii hapa naomba utoe habari hii kwa wadau wenzangu ili kujionea ni kwa namna gani watu hufanya vituko vya aina yake hapa Duniani.Ni matumaini yangu kuwa hautanibania.

Ndoa siku hizi zimeanza kuonekana ni kitu kilichopitwa na wakati hasa kwa wenzetu wa nchi za Ulaya, na hata wanasubutu kusema inabidi kwa sasa waachane na maswala ya kuoa/kufunga ndoa. Hapa kuna stori mpya inayopingana na nadharia hiyo.

Tarehe 06 Bibi harusi BRIDE KATIE 23 na Bwana harusi Darren McWalter 24 walifunga harusi ya aina yake huko maeneo ya bara ya Gloucestershire nchini Uingereza.
Ndoa hii ilipangwa kufanyika juu ya ndege tatu moja ya mchungaji, na mbili zikiwa kwa bwana na bibi harusi kila mmoja na ndege yake.
Hili lilishindikana kwani Askofu mkuu wa Canterbury alidai kuwa ndoa hii haitatambulika ndipo walipoamua kufunga ndoa kwanza kabla hawajaingia kwenye ndege kwa kusimama juu ya mbawa za ndege hizo zikiwa zinaruka na kutoa moshi hivyo kuleta mandhari mzuri na ya kupendeza.
Sauti kutoka kwa maharusi hao zilikuwa zikisikika kwa ndugu , jamaa na marafiki waliokuwa ardhini kwa kutumia vifaa maalumu vya kudaka sauti na kukuza sauti hizo kwa vipaza sauti, huku nderemo na vifijo vikitawala ardhini.

Ndoa za aina hii zimefungwa sana kwa haraka haraka tunaweza kukumbuka ndoa kati ya Tabu Ley wa Orchestre Afrisa International na
M'bilia Bel,

Unaweza kuangalia mwenyewe kupitia tovuti hii.

http://www.dancetracksdigital.com/
search/release.php?release_id=23554

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...