hayawi hayawi, yamekuwa. hatimaye nimekutana uso kwa uso na selebriti wa globu hii ya jamii na mdau numero uno toka cesena, italy, baraka wa chibiriti, ambaye yupo bongo kwa mapunziko mafupi. baada ya kuwa tunawasiliana kwa mtandao kwa takriban miaka mitatu hatimaye tumeonana na hiyo furhara tuliyokuwa nayo si ya kusimulia. karibu bongo mzee mzima wa cesena. mai waifu wako wa kitasha nasikia anakuja wiki ijayo. poa tunamsubiria...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2008

    This is good.Haya ndo mambo ya mtandao na faida zake. Najua kuna watakajifanya kuuliza huyu ni nani na ana nafasi gani katika jamii.Tembelea hii tovuti mara kwa mara utayajua yanayojiri kila siku.Huyu ndo mtu wa watu Mr.CHIBI. Hats off

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2008

    mmmh huyo Chibiriti mwenyewe mbona kachoka hivyo....inavyoonesha hana "mapesa" zinazokunjika vizuri....hayo "manywele kichwani" tu mimi nipo hoi....hamna vinyozi huko alipotoka au ndo kama nilivyosema ni expensive kukata nywele...kama michu...toa uchafu wa huyu jamaa...TUMECHOKA....anatia aibu watu tunaokaa majuu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2008

    mmmh huyo Chibiriti mwenyewe mbona kachoka hivyo....inavyoonesha hana "mapesa" zinazokunjika vizuri....hayo "manywele kichwani" tu mimi nipo hoi....hamna vinyozi huko alipotoka au ndo kama nilivyosema ni expensive kukata nywele...kama michu...toa uchafu wa huyu jamaa...TUMECHOKA....anatia aibu watu tunaokaa majuu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2008

    swaaaafi sana na hivi ndivyo watanzania tulivyo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2008

    karibu Chibiriti, happy to see you.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2008

    NAFURAHA KUONA WATU WANAOWASILIANA KWENYE MTANDAO KWA MUDA MREFU WANAPOKUTANA NI JAMBO LA KUSHUKURU MUNGU NA KUTIA MOYO.UWE MFANO KWA WANAJAMII WA BLOG HII YA JAMII.HONGERA CHIBIRITI NA WADAU WOTE WA BLOG YA JAMII.TUENDELEZE LIBENEKE LA JAMII

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2008

    BIG UP CHIBI,KWA KWERI INAFURAHISHA SANA PALE WANAKIJIJI WANAPOKUTANA LIVE HUYU CHIBI.KWA KWELI NI MOJA YA WATU WALIOPATA COMENTS NYINGI NDANI YA KIJIJ HIKI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2008

    Michuzi ,

    Tafadhali mwonyeshe sehemu wanazouza fenicha nzuri mheshimiwa Chibiriti ikiwezekana arudi nazo Cesna.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2008

    Anony N02 naona umekula vumbi saana, eti anatutia aibu tulio majuu,,,nyoooo kama kweli vile..we uatafia hapo hapo Tandale kwa mkaanga maini.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 24, 2008

    doctor chibiritiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
    wadau hapo juu wengine mna wivu mpaka kwa celebrity wa globu ya jamii hio kali.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2008

    Kuna maannon wengine kazi yao ni kuchafua tu hali ya hewa. sasa wewe mwenyewe ndo unaona umenyoa nywele? hembu tulizana wewee. Chibi tunakufagilia we endeleza libeneke bwana!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2008

    Anon wa tarehe July 24, 2008 5:08 PM,Mbona huna adabu na heshima kwa binadamu wenzako kama wewe!? Nina wasiwasi kuwa huenda ukawa unaishi kwa taabu sana huko ughaibuni uliko hata kurudi tz huwezi,unabakia kumchambua wenzako waliokwenda kuona ndugu zao.Nyie ndo wale hata mkipata misiba nyumbani tanz ya ndugu zenu wa karibu hamuwezi kurudi kisa MAKARATASI....Shame on you!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2008

    Michu! ukisema Chibiriti ndio mdau numero uno unaferisha...kila mtu anajua mchango wake huyo jamaa lkn kumpa rank kwasababu alikupa hifadhi ulipoenda cesna umenikata stim....mimi mwenye mdau wa glob hii tangu Michu hujanunua digital camera ulikuwa unatumia stil pix, computer ulikuwa unatumia ya ofisini pale printpark eheheheeee, longtime tunanunua vitumbua pale kwa bi issa karibu na mawenzi hotel kudadek.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2008

    wewe anony wa july 24, 2008 5:07 pm naona hata darasa la 4 hukumaliza yaani akili zako finyu kabisaa wewe mtu awe na kitambi ndio ujue ana manoti? nyambafu kabisa nadhani wewe utakuwa baa medi ambae wmenye kuagizia bia nyingi ndio unaona mwenye hela!!!! kama huna la kukomenti wee uchune tu sio kutoa maneno ya kudhalilisha kwa binadamu mwenzio bila hata kosa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2008

    nyumbani ni nyumbani hata kuwe kichakani au vipi chibi!!!!
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 25, 2008

    kha...anon wa 2 kaniacha hoi. Kukaa majuu ndo kuchana nywele na kuvaa pamba? Mimi ndo maana hata company za wabongo sizipendi...mawazoni kwao muda wote ni competition...sijui kavaa cheni ya dollar ngapi na kiatu hichi au kile...duh...mpk mnaboa. Just be simple and humble. Its a blessing...dont turn it into a curse to others...

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 25, 2008

    Huyo anony wa pili hayuko majuu wala nini..yupo somewhere mitaa ya bunju au mbagala kwake ni majuu maana alidondoka toka Nachingwea majuzi tu...

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 29, 2008

    Hakuna kinachopatikana kwa urahisi Ughaibuni,bills & tax, bills & tax, bills ndo maisha yenyewe...Hivyo mtu kuweza kukata tiketi ya kuja nyumbani japo kidogo ni jambo la kushukuru.Tusiwe wepesi kuchambua mavazi na mambo yanayoonekana nje!!Kuna watu wengi wanavaa dhahabu kibao,nguo nzuri halafu ukienda kuangalia maisha yao ya kila siku ni michosho tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...