SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI A.K.A TFF LEO IMEIFUNGIA TIMU YA YANGA KUTOSHIRIKI MICHEZO YOYOTE YA KIRAFIKI NA KIMASHINDANO YA KIMATAIFA NDANI NA NJE YA NCHI KWA KIPINDI CHA MIAKA 2 KUANZIA LEO.
KATIBU MKUU WA TFF FREDERICK MWAKALEBELA AMESEMA MCHANA HUU KWAMBA KAMATI YA UTENDAJI, IKITUMIA MAMLAKA YA KIKATIBA YALIYOMO KATIKA IBARA YA 34 (1Q) INAYOELEZEA MAENEO YA MAMLAKA YA KAMATI YA UTENDAJI, IMEAMUA KUTOA ADHABU KALI KWA YANGA ILI IWE FUNDISHO KWA YANGA YENYEWE NA TIMU ZINGINE ZENYE MAWAZO YA KUGOMEA MICHEZO.
KWA MUJIBU WA KAMATI HIYO YA UTENDAJI, YANGA WALIFANYA MAKOSA YAFUATAYO:
1. KUAIBISHA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU, TFF NA NCHI KWA JUMLA
2. KWENDA KINYUME NA TABIA YA UANAMICHEZO
3. KUHUJHUMU KWA KUSABABISHA MAPATO YA MCHEZO KUPUNGUA
4. KUSABABISHA TFF KUKOROFISHANA NA WADHAMINI WALIOWEKEZA PESA NYINGI KUDHAMINI MASHINDANO
5. KUIDHALILISHA TFF KAMA CHAMA MWENYEJI WA MASHINDANO YA UKANDA WOTE WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI NA WAANDAJI CECAFA
6. KUHATARISHA USALAMA WA WATU NA MALI ZAO
7. KURUDISHA NYUMA HATUA NA HARAKATI ZA KULETA MAENDELEO YA KWELI KATIKA SOKA
AIDHA, PAMOJA NA ADHABU HIYO, MWENYEKITI WA YANGA MH. IMNI MADEGA NA KATIBU MWENEZI WA KLABU HICHO FRANCIS LUCAS WAMEPEWA SIKU SABA KUANZIA LEO WATOE MAELEZO NA KUTHIBITISHA MADAI YA KUWEPO KWA MAKUBALIANO YA KULIPWA SH. MILIONI 50 KABLA YA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA.
Safi sana, huu uamuzi ni sahihi kabisa. Nadhani sasa shirikisho la soka (TFF) kweli wameichoka Yanga, maana mpaka kufikia hatua kama hiyo sio kitu cha mchezo hata kidogo, hilo litakuwa pia ni fundisho kwa timu zetu, kwani hii tabia ikiachwa hivi hivi itaota mizizi. Na hao akina Madega wakishindwa kuthibitisha wachukuliwe hatua kali kama ilivyokuwa kwa brother Kaduguda aka Simba wa Yuda. Nadhani pia umefika wakati sasa wanachama wa yanga aka kandambili na wao waangalie jinsi ya kubadilisha viongozi, maana waliopo wameleta aibu kubwa sana. Du, sipati picha miaka miwili mechi za majaribio na Lipuli, ndo kusema hakuna safari za mechi za kujipima nguvu wala nini, du, mtakimbiwa na wachezaji muhimu.
ReplyDeleteSawa sawa TFF japo naona kama miaka miwili haitoshi ingekuwa miaka mitano hivi ili liwe fundisho la kweli, Imani Madege na mwenzie francis Lucas hawana haja ya kutoa maelezo ni kwamba wanatakiwa kufungiwa moja kwa moja kujishughulisha na masuala ya michezo ili kama kuna viongozi wengine wenye tabia kama yao wapate somo, jinsi walivyofanya hawa jamaa hakuna njia yoyote ya kusamehewa hata kidogo.
ReplyDeleteNaona TFF sasa wanafanya kazi tunayoitegemea.Hata hiyo adhabu haitoshi kwa mtazamo wangu kwani Yanga wanataka kuu-udhalilisha mchezo wa kandanda,ambao ni moja ya michezo yenye heshima kubwa duniani.Tusikubali kamwe tukaliwe vichwani na maauzi ya watu kama Madega ambae usomi wake sidhani kama unamsaidia!
ReplyDeletePamoja na kuafiki adhabu hiyo nashauri kanuni zibadilishwe ili adhabu wapewe viongozi waliofanya maamuzi mabovu kwa kuwa hapakuwa na kikao cha wana yanga kuamua kutopeleka timu. Pia wana yanga hata simba inabidi kuwa waangalifu wakati wa kuchangua viongozi bila hivyo wanaoumia ni wengi kwa maamuzi mabovu ya viongozi kujiangalia wenyewe.
ReplyDeleteNafiriki tatizo ni Uongozi uliopo madarakani Yanga na si Yanga kama asasi.Pamoja na kuringia taaluma na usomi wao imethibitika kupitia viongozi waliopo madarakani kuwa kusoma sio kuelimika!
ReplyDeleteTFF walitakiwa kwenda mbali zaidi na kuwafungia MAISHA kushiriki shughuli za kiungozi viongozi watakaobainika kukosa sifa na kututia aibu Wana-Yanga. Suppose kungetokea vurugu watu wakaumia ama hata kufa na uharibifu wa mali?
Sportsmanship ni ukubwa wa moyo na akili. Hata kama kulikuwa na makubaliano yasiyo rasmi hiyo isingetosha kuwa sababu ya kuvuruga mashindano kwa kiasi hiki.
Kwanza Yanga tumeshozoea kufungwa na Simba katika miaka ya karibuni, kwahiyo kama ni woga wala haukuwa na msingi, tumevulia hata vipigo vya Stars, ingekuwa hiki cha juzi?!
YANGA TUNATAKA MAGEUZI YA KWELI, UONGOZI ULIOPO UONDOKE KULINDA HADHI YA YANGA KLABU YENYE ZAIDI YA MIAKA 70. HII NDIO NJIA PEKEE TUTAKAYOPATA MSAMAHA WA TFF NA CECAFA, NA SIJUI CAF WATAKUJA NA RUNGU GANI.
HII NI RICHMOND YA YANGA, LAZIMA IONDOKE NA WATU.
HII AJALI YA KIMICHEZO KWA VIONGOZI WALIOPO YANGA HAIKWEPEKI!!
MADEGA UWE "KILONGOLA" YAANI UONESHE NJIA KUJIUZULU VIONGOZI WENZAKO WAFUATE.
MMEFANYA MAKOSA, LABDA KWA NIA NJEMA, ILI KULINDA HESHIMA ZENU NI KUKAA KANDO.
kwa maana hiyo Yanga waliokuwa mabingwa wa Vodacom nafasi yao ya kutuwakilisha ktk kombe la Afrika itachukuliwa na timu ingine?
ReplyDeleteHuo ni uamuzi ulichangiwa na chuki ya hali ya juu. TFF haina mamlaka ya kutoa adhabu kama hiyo kwa Club kwa kosa lililotokea kwenye mashindano ambayo hawana mamlaka nayo. Adhabu halali ni ile ya CECAFA tuu. Yanga pelekeni appeal haraka kwa kamati husika vinginevyo mnaweza kupinga hata mahakamani. Sheria yoyote inayomzuia mtu kwenda mahakamani inapingana na katiba ya nchi. Asiwadanganye mtu
ReplyDeleteSIJAONA UPUUZI KAMA HII ADHABU YA TFF KWA YANGA KAMA TIMU. HAYA MAKOSA YA AIBU YALISABABISHWA NA VIONGOZI WABOVU NA SIO WACHEZAJI NA WANACHAMA. HIVYO BASI KUIFUNGIA YANGA KWA MIAKA MIWILI TENA KWA MASHINDANO YA KIMATAIFA( AJABU YA NDANI WAMEWAACHIA) NI UONEVU MKUBWA AMBAO SIJAPATA KUONA! KUMBUKA KUWA YANGA NDIO INAFANYA KARIBU NUSU YA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA, SASA WACHEZAJI HAO AMBAO HAWANA MAKOSA YEYOTE NA MAAMUZI HAYO WANAKOSA INTERNATIONAL EXPOSURE UNATEGEMEA TIMU YA TAIFA ITAFANYA VIZURI KWELI?
ReplyDeleteADAHABU NI SAWA INATAKIWA IWEPO, ILA INATAKIWA WAADHIBIWE WAHUSIKA HALISI AMBAO NI VIONGOZI AKINA MADEGA NA WENZAKE. WACHEZAJI KWA KWELI WAMEONEWA KABISA! HAPO SASA NAONA TFF HAIKO KWA AJILI YA MAENDELEO YA SOKA ILA NI KUKOMOANA NA MAAMUZI YA KUKURUPUKA TUU.
MZOZAJI
me ndo maana nimestaafu kushabikia kandanda ya vilabu vya bongo.si mpenzi wa soka la TZ kwa kupitia clubs kutokana na mambo kama hayo walofanya Yanga.Timu pekee ninayoishabikia bongo ni STAZ.na hawa TFF nao wanafuata upepo tu kama bendera lkn wala hawajui wanachokifanya.sijui kama hiyo kanuni yao ni kweli inasema hivyo lkn kwa kuangalia ktk soka la kimataifa(Ulaya), kama timu ilikuwa ikishiriki Champions League ama Uefa Cup then wakafanya kosa flani basi adhabu inapotolewa na UEFA kamwe chama cha soka cha nchi inapotoka hiyo timu haina mamlaka ya kuongeza adhabu nyingine yeyote.
ReplyDeleteMfano kama ilivyotokea kwa BWAWA LA MAINI(Liverpool F.C. VS Juve) May 29 1985.Vurugu za mashabiki wa LFC zilisababisha vifo vya raia 39 wa Kitaliano. na hiyo ikafanya Vilabu vya England kwa Ujumla vikafungiwa kushiriki European Competitions kwa miaka kadhaa.Lakini chama cha soka cha Uingereza hakikuifungia Liverpool kushiriki mashindano yeyote yaliyo chini yao.
Pia Inter Milan, Roma na timu kadhaa zimeshapewa adhabu mara kadhaa kutokana na furugu za mashabiki ktk Champions League lakini vyama vyao vya soka havikutoa adhabu yeyote. Na hiyo ni sababu HAWAHUSIKI directly na mashindano yale .
Pointi yangu hapa ni kwamba walichofanya CECAFA ni sahihi na nadhani adhabu hiyo wala haitoshi isipokuwa hawa TFF wanajishebedua tu.hawajui wanachokifanya. Leo hii kiongozi mmojawapo atasema hili ktk media,kesho kiongozi mwingine atakuja na kuanza kumpinga mwenzie(Mfano Sakata la Cannavaro juu ya Jezi).
Hawa viongozi wa soka wa TZ kuanzia ktk clubs hadi TFF need to grow up. Vitendo vingi vya viongozi hawa vimekuwa na matokeo ya aibu. Hawajali kuwa tunaoumia ROHO ni sisi tunaotaka kuona soka la TZ likisonga mbele.
TFF inabidi ibadili uamuzi wake kwani hauna sababu za kimsingi kwao.ngoja tuone na CAF kama wataifungia YANGA.
ukiwaadhibu viongozi sasa adhabu itakuwa ime wafunza nini timu? timu inaundwa na watu wote hao kwahio ndio hivyo.ac milan na juventus walishushwa daraja timu sio viongozi nyie vipi.kwani yanga ikishinda mechi wanakuwa viongozi wameshinda au yanga timu yote?
ReplyDeleteMdau wa 6:13 kweli we Yanga. Una macho lakini Huoni. Punguza kupenda, khaakhaa!
ReplyDeletewewe anon wa July 29, 2008 6:13 PM huna hoja, hujui unachokiongea, nadhani umeweka ushabiki mbele kuliko kujua taratibu na kanuni. Kama chuki wanaochukiwa na TFF ni Simba na sio yanga kama unavyosema. Aliyetangaza adhabu ametolea na kifungu kilichotumika kutoa hiyo adhabu halafu wewe unasema kwamba hawana ubavu, hivi unafikiri sawa sawa wewe? sasa kama unabisha, washauri hao wajinga viongozi wako wakakate rufani uone kitakachofuata. Mimi nitakupa mfano mmoja, kuna mwaka Manchester United walikuwa wanashiriki mashindano ya Amsterdam Cup, na huko Wayne Rooney alifanya upuuzi wake, akapewa kadi nyekundu, FA ya Uingereza walichokifanya ni kuangalia kosa lake na walipoona kwamba kwa kosa kama lile katika kanuni zao anastahili adhabu, walimpa adhabu ya kukosa mechi tatu kulingana na kanuni zao japokuwa kosa lilifanyika katika mashindao ambayo hayakuandaliwa na FA ya Uingereza. Nimekupa mfano huo ili kujaribu kukufunua macho na kukusaidia ili ujue kanuni zinazotumika katika haya mashirikisho ya michezo zilivyo, na kama bado hujaelewa basi pole sana, ila habari ndo hiyo hakuna mashindano ya kimataifa wala mechi za kirafiki kwa miaka miwili na mimi naona adhabu ni ndogo kabisa.
ReplyDeleteHuu ni unyama!!
ReplyDeleteadhabu kwanza then maelezo baadaye?
Mimi nawaonea huruma wachezaji na wala si viongozi. Je wachezaji walikubaliana na uongozi juu ya kususia hiyo mechi?
Je TFF iliwahoji wachezaji na viongozi kuhusu chanzo cha kususia mechi na je, kulikuwa na makubaliano kati ya wadhamini na klabu kuhusu malipo kabla ya mechi?
Mithupu naomba ujaribu kutupa dondoo ya hichi kizaa zaa!! Maana kuna mchanganyiko wa vitu hapa, kuanzia kanuni za mpira, udhamini na adhabu.
Ninavyoelewa mimi adhabu ya kutoingia uwanjani ni kupoteza mechi, yaani pt. 3 na bao 3. Hayo mengine ntaomba wajuzi wa kanuni watuhabarishe kama hizi ni hasira hasara au kweli Yanga kama timu wanastahili adhabu (kama wachezaji waliafiki kususia pia).
Mdau NY.
Aacha upuuzi wewe uwe na akili ya kutosha............timu zote zipo chini ya TFF na CECAFA..........uwe unasoma hata katiba kabla ya kukurupuka..........bwege wewe......
ReplyDeleteHawa TFF ni wazushi, but anyway tumeizoea bongo ambayo politiki ipo hadi ktk soka. Hivi wadau naomba mnikumbushe adhabu waliyopewa Mtibwa Sugar na TFF baada ya kuingia mitini ktk mechi ya marudiano ya kombe la CAF na kufungiwa na CAF!! Mbona TFF walikaa kimya?? ina maana Mtibwa hawakuiabisha TFF A.K.A FAT? au ndio ili hadithi ya `` KUNYATA ANYATE KINYONGA, AKINYATA KICHECHE ANAVIZIA KUKU??`` kama kweli hawa TFF hawabeep, basi wainyang`anye Yanga ubingwa na kuishusha daraja (Maana inaonekana wana hasira). Hawan lolote wanachojali wao ni mshiko tuu na wala sio soka la bongo. Hadi leo hawajatangaza walipata sh ngapi mechi ya Camoon!! yaani ufisadi kila maahali?? Ni hayo tuu , naomba kuwasilisha!!
ReplyDeleteMdau Sao Paulo.
Waungwana wala msiumize vichwa hii ni mikwala ya kuku tu, Unazani wakiwafungia YANGA miaka hiyo miwili TFF watakula wapi? Wakati wao huwa hawalali kusubiria wanapokutana watani wa Jadi wapate vya milangoni ili wakavimbishe matumbo familia zao. Soka la bongo ni YANGA na SIMBA asikwambie mtu angalieni hata timu ya Taifa inaundwa na wachezaji wa timu zipi?
ReplyDeleteLigi yenyewe itakuwa imepooza bila kelele za wafuasi wa Msimbazi na Jangwani. Yote machungu ya TFF hawakupata kilicho bora kutoka milangoni jumapili ndiyo maana wamenuna
Mimi si Yanga wala Simba lakni naomba tu kujua ni vifungu vya sheria gani vinavyowabana? Jana nimesoma kuhusu yule mheshimiwa wa CECAFA na kwa ufahamu wangu ilionekana kama sheria ilimtoka mdomoni baada ya tukio la Yanga kuingia mitini. Sasa mimi ningekuwa Yanga ninge wataka wote CECAFA na TFF wanisomee mashtaka yangu na vifungu vya kunihukumu.
ReplyDeleteNina wasiwasi mimi hapana sheria kuhusu hatua gani achukuliwe mtu aliyeingia mitini. Miaka ya nyuma mheshimiwa mmoja akiitwa McTwist alitunga kisheria kiduchu kuhusiana na haohao Yanga (sijui nao wana mkosi gani) lakini - we, usicheze na Saigon, alijikuta yuko Kibera kwao. Sjui safari hii...
ndugu zangu hapo mi naunga mkono adhabu ya CECAFA na TFF... manake kitendo walichofanya hawa ndugu zetu si cha kiungwana kabisa.. sa jamani we umeona wapi timu inatambaa mitini kwenye uproffesional wa diz years? na kama ni suala la national team ligi inatimu nyingi wanaweza kuhama waje tuu.... tena yanga mkikaa vibaya hata manji atawakimbia.......
ReplyDeleteWEWE ANON WA July 29, 2008 10:31 PM
ReplyDeleteUNAMKANDA MWENZAKO WAKATI WAKATI WEWE MWENYEWE UNACHOKIONGEA HUKIJUI. UNAZANI FA WALIKULUPUKA TU KUMFUNGIA ROONEY HIYO INATEGEMEA NA MAELEZO YA REFA ALIYETOA ADHABU. KAMA ATAAMUA KUPELEKA MAELEZO YA MCHEZO KWA CHAMA CHA SOKA AMBACHO YULE MCHEZAJI ANACHEZEA BASI NI JUKUMU LA CHAMA HICHO KIMTOLEE ADHABU AMA LA KAMA ALIVYOFANYIWA ROONEY MBONA SCHOLES ALIPEWA KADI NYEKUNDU KWENYE MASHINDANO HAYOHAYO LKN HAKUFUNGIWA UNAJUA SABABU NI NINI? SABABU REFA WA MCHEZO ULE ALIAMUA ASIPELEKE MAELEZO YA FA NDIYO MAANA HAKUFUNGIWA. SASA SWALI LINAKUJA JE CECAFA WALIPELEKA RIPOTI YA MCHEZO ULE KWA TFF AU WAO WAMEKULUPUKA TU NA KUCHUKUA MAAMUZI YASIYO NA MSINGI? NASEMA HIVYO SABABU SOKA LA BONGO NI TIMU MBILI TU YANGA NA SIMBA, KAMA YANGA ITAFUNGIWA TIMU YA TAIFA ITAATHIRIKA VIPI NA MAAMUZI HAYO? MAANA KAMA YANGA IMEFUNGIWA MAANA HAKUNA MCHEZAJI WA YANGA ATAYEKUBALIA KUCHEZA TIMU YA TAIFA NA SI VINGENEVYO. SASA UKO NI KUENDELEZA SOKA AU KUDIDIMIZA SOKA KWANINI WASITOE ADHABU YA PUNGUZO LA POINTI KWA TIMU YA YANGA, TUWENAIGA MIFANO YA INCHI ZILIZOENDELEA WANAFANYA VIPI? MIFANO:- RUSHWA KATIKA LIGI YA ITALI, YANGA WANGESHUSHWA HATA DARAJA BASI LKN WALE WACHEZAJI WAWEZE KUTOA MCHANGO KATIKA TIMU YA TAIFA. AMKENI JAMANI TFF WAKO PALE WAO KUANGALIA KINACHOPATIKANA MILANGONI NA SI VINGINE
NATOA WITO KWA WANA-YANGA WOOTE KUSUSIA KWENDA KUANGALIA MECHI ZINAZOCHEZWA UWANJA WA TAIFA NA KWINGINEKO KAMA 'PROTEST' YA KUPINGA HIZI ADHABU HII LAZIMA ITAWAUMA MAFISADI WA TFF KWANI WATAKOSA SANA PESA ZA KUFISADI WAFE NA NJAA. MPIRA NI SIMBA NA YANGA BWANA HAPA TANZANIA. WAKIKOSA HELA ZETU WATASHINDWA HATA KUJIENDESHA...
ReplyDeleteLoooh nimesoma comments zote toka juu hadi jasho linanitoka.Nakubaliana na mawazo ya walio wengi.Lakini wanaoongelea wachezaji wengi kuwa national team-No.Kama walivyosema bahadhi ya wanablog,maana ya adhabu ni 'kuumiza'.Kama 'haiumuzi' siyo adhabu.Ili siku nyingine wachezaji wakipewa uamuzi wa kij*nga na hasa kapteni wao waukatae!Adhabu ni kwa yanga nzima ndiyo maana inaitwa timu(From English word TEAM).
ReplyDeleteMimi Yanga damu lakini hili sikubali,mtanisamehe wana Yanga wenzangu
"*****KUMBUKENI KWAMBA WATANZANIA HATUKO TAYARI KUWA NA "..EAST AFRICAN COMMUNITY****" HAWA WENZETU WATAANZIA "..MABALI SANA.." KWA JUHUDI NA MAARIFA KUHAKIKISHA TUNAJIONA HOVYO NA TUNAKULA "MATAPISHI YETU" HII NI "..HATUA YA KWANZA SUBIRINI MUONE YA PILI.." (MOJA YA SEHEMU YA MICHEZO NI AMANI PAMOJA NA KUUNGANISHA JAMII NA KUINUA UCHUMI)
ReplyDelete__USIBWABWAJE TU CHUNGUZA KWA MAKINI/UNDANI ZAIDI__