Leo hii vijana wa FC BONGO ya helsinki imewabamiza Algeria goli 6-2 katika mchezo wa mwisho wa kundi B katika mashindano ya HELSINKI PREVENTION CUP.
Timu hii tishio tayari imeshajikusanyia ponti 15 swaaaafi kwa kushinda mechi zote tano na kukolifai kuingia semifainali siku ya jumatano watakapokutana na GUINEA.
Magoli ya FC BONGO yalifungwa na SAMI 2, FRANCIS 1, BOB 2 na EDO 1.
Mungu ibariki TANZANIA,
Mungu ibariki FC BONGO
Mungu Tubariki watanzania woote kwa jumla.
Habari zaidi za maendeleo ya FC BONGO katika mashindano hayo ya HELSINKI PREVENTION CUP utazipata hapa katika blogu yetu hii ya Jamii.
Hongera fc bongo, moto ule ule msirudi nyuma, mkishinda nyie ndio tumeshinda Watanzania wote. peperusheni bendera yetu juu huku nyumbani akina Maximo wameshindwa kufanya kweli.
ReplyDeletesiku wakifungwa kimyaa..! lakini hogereni..! ila mkirambwa muwe wa kwanza kutufahamisha!
ReplyDeleteNjooni mcheze na Yanga ndio saizi yenu.Nataraji siku hiyo hawataingia mitini.
ReplyDeleteNaona Bongo FC mambo mzuka sasa... endelezeni dozi katika Semi.. Tupo pamoja
ReplyDeleteWale madogo wawili mmoja mrefu na mmoja mfupi walizungusha kinoma pale kati, na yule mtoto jimmy kwanini siku zote anawekwa benchu tu, jana alikipiga vizuri sana.
ReplyDeletehuyo scolary aje kuchukua nafasi ya maximo, moto wake si mchezo tunawatakia ubingwa
ReplyDeletehongera fc bongo pamoja na kocha mr skorare. kwa kupeperesha bendera ya tz. ulaya.ceepit on ezze.
ReplyDeletemss benn. mariehamn