HABARI TOKA DODOMA ZINASEMA MBUNGE WA TARIME KUPITIA CHADEMA MH. CHACHA WANGWE (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA USIKU HUU SHEHEMU ZA KONGWA, MKOANI DODOMA.
KWA MUJIBU WA HABARI HIZO MAREHEMU WANGWE, AMBAYE ALIKUWA AMETOKEA BUNGENI DODOMA AMBAKO ALIHUDHURIA KIKAO CHA ASUBUHI, ALIKUWA NJIANI KUELEKEA DAR KWENYE MAZISHI YA HAYATI MZEE BHOKE MUNANKA AMBAYE AMEFARIKI DUNIA JUMAMOSI HII, AMBAPO LEO ANATARAJIWA KUZIKWA KWENYE MAKABURI YA KINONDONI, DAR.
CHANZO CHA AJALI HAKIJAJULIKANA NA POLISI HUKO KONGWA WAKITHIBITISHA HABARI HIYO IMESEMA MAITI YA MAREHEMU IKO KATIKA DISPENSARI YA KIJIJI CHA KIBAIGWA IKISUBIRI KUPELEKWA HOSPITALI KUU DODOMA KWA HIFADHI NA HUDUMA ZINGINE.
HABARI ZINASEMA MWENYEKITI WA CHADEMA MH. FREEMAN MBOWE LEO ANATARAJIWA KUTOA TAARIFA RASMI YA KIFO HICHO PAMOJA NA MIPANGO YA MAZISHI.
GLOBU HII YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA WAFIWA KWA NIABA YA WADAU WOTE. ITAENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MSIBA HUU MZITO KWA KADRI ZINAVYOINGIA. HIYO NI PAMOJA NA CHANZO CHA AJALI NA ENDAPO KAMA MAREHEMU ALIKUWA NA WATU WENGINE KWENYE HILO GARI, NA HALI ZAO ZIKOJE.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MH. CHACHA WANGWE MAHALI PEMA PEPONI
AMINA
Mungu amlaze mahali pema peponi Amen.
ReplyDeleteRIP Chacha Wangwe
ReplyDeleteMay Lord rest his soul in peace.
ReplyDeleteMbona ajali ni nyingi sana Tanzania?
Serious ajali zinaweza kuua watu wengi sana kwa mwaka kuliko hata malaria
Poleni sana wafiwa
REST IN PEACE.
ReplyDeletewewe ni mwanaume hadi MBOWE ANAKUOGOPA.
UNGEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA, KWANI USINGEKUWA NA MPINZANI KWENYE UCHAGUZI MKUU CHADEMA DECEMBER.
Mungu aliyemuumba Chacha Wangwe hatimaye amemchukua. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen (Ayubu 1:21)
ReplyDeletePoleni sana wafiwa Mungu awape faraja wakati huu wa Majonzi.
Sisi tulikupenda lakini bwana amekupenda zaidi. Roho ya Marehemu Chacha Wangwe ipate rehema kwa Mungu na ipumzike kwa amani.. AMEN.
ReplyDeleteNalo Pumziko la milele uwape ee bwana... na mwanga wa milele uwaangazie ..Marehemu wote waliotutangulia wapumzike kwa amani...Amen.
Namwomba Mwenyezi Mungu Ailaze Pahali Pema Peponi Roho Ya Marehemu Wangwe. Amina.
ReplyDeleteNawapatia Pole Za Dhati Wanafamilia na Marafiki Wa Marehemu.
SteveD.
bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
ReplyDeleteHakuna mtu mwenye upendo mwingi, kama afae kwa ajili ya mwenzake.Chacha, tutakukosa sana bungeni ulikua changamoto kubwa watanzania wenzako, na utakumbukwa na wapenda haki na maendeleo wote.
ReplyDeleteInna-lilah wainna Illah rajyun.
Du! unaweza kukufuru coz ukilinganisha ugomvi wa juzijuzi na jama zake wa chadema na ajali hii...anyway...rip Chacha Wangwe
ReplyDeletepoleni waheshimiwa wabunge hasa mh Sitta ambaye ameshindwa kujizuia kutoa machozi leo asubuhi wakati akiahirisha kikao cha bunge...wapiga kura wa tarime,wanachama wa chadema.n.k.
ReplyDeleteMungu alimpenda zaidi Chacha...
Jamani Chacha
ReplyDeleteWameku... wameona mwaka 2010 unaimaliza CHADEMA kwa kusema ukweli.
RIP poleni wanafamilia
My God!
ReplyDeleteMkombozi wa Wana-CHADEMA wasiotoka mkoa wa kule naniiiliii ...Poleni sana sasa changamkeni muendeleze changamoto ya kugombania haki zenu.
Ulale mahali pema peponi Chacha
Ngoja nifungue Jamii Forum nione mawazo yao maana wazuri sana kusema maovu akifa mhe wa upande wa chama tawala
ReplyDeleteInna-lilah wainna Illah rajyun.
ReplyDeleteSo sad jamani, RIP CHACHA WANGWE!!MAY ALMIGHT GOD REST HIS SOUL IN ETERNAL PLACE AMEN!
ReplyDeleteIt is really shocking but no way other than accepting what has happened.My sincere condolences to the family and all Tanzanians.
ReplyDeleteMay God rests the soul of Chacha Wangwe in Eternal Peace. Amen
Mungu aiweke roho ya Chacha Wangwe mahali pema peponi. Amina.
ReplyDeleteWEeee Michuzi acha kutumix mzee wa roiko mchuzi mix wewe tangu lini hii ikawa Globu hebu sema sawasawa Bwana tutakushtaki kwa Ndesanjo Ngasanjika kapisa.
ReplyDeleteMdau
Makini Makini Sana.
RIP Mh. Chacha Wangwe.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa kwa msiba huu mzito sana.
RIP Chaha wangwe.
ReplyDeleteInna Lillah Wainna Ilaih Raajiun
ReplyDeleteKuntakinte.
POLE KWA WAFIWA NA WOTE WA KARIBU NA WALIOGUSWA NA MSIBA HUU.
ReplyDeleteHili wazo la Mungu alimpenda zaidi linatoka wapi, wanaoishi Mungu hawapendi? !!!
Tuwe hai au tumekufa MUNGU anatupenda.
RIP Mheshimiwa !!!
Tutakukumbuka sana, Mola akulaze pema Amina.
ReplyDelete