FC BONGO YA HELSINKI, FINLAND

Timu ya F.C.BONGO ya Helsinki leo hii katika mechi yao ya kwanza ya Prevention Cup Helsinki imeweza kuwabwaga mabingwa watetezi wa kombe hilo SIERA LEONE bao 2-1 na kujipa matumaini makubwa ya kuendelea vizuri katika michuano hiyo ambayo yanashirikishwa na timu za mataifa mbali mbali.
Vijana hao wa F.C.BONGO watajitupa tena uwanjani siku ya jumapili kwa kuchuana na CONGO na jumanne watakumbana na NIGERIA Kabla kukutana na GREECE alhamisi na kumalizia na ALGERIA jumatatu.

Mabao ya F.C.BONGO yalifungwa na John Ndembo na Ali Apepe.

Ujumbe kwa wana kilimanjaro Stockholm, mnaambiwa kaeni mkao wa nanihii. Chinja chinja wanakuja huko mwezi ujao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2008

    Hongera Vijana wetu, mwaka huu kweli kombe letu, manake squadi inatisha. vijana naona wako serious sio mchezo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2008

    nyinyi fc bongo si ndio mlitundikwa mabao na wana tampere kama mmesimama?
    au mmeazima wachezaji wao?
    haya lakini kila la kheri.....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2008

    Michuzi mi naona hizi ndio Jezi nzuri na zina mvuto wake kama ingekuwa ni maamuzi yangu ningeamua Timu yetu ya TAIFA ivae jezi kama hizi sio zile zisizo na mvuto sijui design wao ni nani...., kesema kweli Jezi za timu yetu ya TAIFA mbaya na hazina mvuto wowote ..., na sidhani hata kama wajezaji wanaonanaje uwanjani maana rangi zake zimelala..... hebu wadau mnisaidie labda mimi macho yangu yananidanganya !!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...