Habari zilizoingia punde kwenye globu jii ya jamii zinasema timu ya F.C.BONGO ya Helsinki leo hii katika mechi yao ya kwanza ya Prevention Cup Helsinki imeweza kuwabwaga mabingwa watetezi wa kombe hilo SIERA LEONE bao 2-1 na kujipa matumaini makubwa ya kuendelea vizuri katika michuano hiyo ambayo yanashirikishwa na timu za mataifa mbali mbali.
Habari zinaendelea kudatisha kwamba vijana hao wa F.C.BONGO watajitupa tena uwanjani siku ya jumapili kwa kuchuana na CONGO na jumanne watakumbana na NIGERIA Kabla kukutana na GREECE alhamisi na kumalizia na ALGERIA jumatatu.

Mabao ya F.C.BONGO yalifungwa na John Ndembo na Ali Apepe.

Ujumbe wa FC Bongo kwa wana kilimanjaro Stockholm, mnaambiwa kaeni mkao wa nanihii. Chinja chinja wanakuja huko mwezi ujao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...