Wans ageni, Chinja chinja F.C.BONGO ya Helsinki wamewabamiza Nigeria goli 3-2 na kujiongezea matumaini ya kuingia katika nusu fainali za Mashindano ya Kimataifa ya HELSINKI PREVENTION CUP.
Mechi ya leo ilikua ni ile ya Mbwa kala Mbwa, kwani Hao Wanigeria ndio tishio la timu zote katika mashindano hayo, Lakini wabongo wamepania mwaka huu kuwa kombe hilo lazima walifikishe Ubalozini Stockholm wakati watakapozuru huko tarehe 16 august mwaka huu na kuchuana na kilimanjaro fc ya Stockholm.

Fc Bongo mpaka sasa inaongoza katika Kundi A wakiwa na pointi 9, wakifuatiwa na Nigeria na Ageria wakiwa na pointi sita wote na mwisho wakishika mkia Congo na Greece wakiwa na pointi 3 kila mmoja.

Magoli ya Fc Bongo yalifungwa na Ubaldino, Kevin na Zakaria.
Alhamisi Wabongo wanajimwaga tena uwanjani kuchuana na Wagiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2008

    Wanaigeria wamefunga mdomo, kiboko ile.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2008

    na mazungu yanini hapo? ina maana hakuna wabongo wakutosha hapo? au ndio ma supervisor wa viwandani!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2008

    Jamani, mchezo wa jana mlicheza kwa ustadi na nidhamu ya hali ya juu. Nidhamu ya wachezaji inaonekana hata katika hiyo picha mliyopiga. Mnastahili pongezi nyingi sana. Endeleeni hivyo hivyo kombe mtalitwaa na kutupa sifa Watanzania wote.

    Watanzania wenzangu nawaombeni tujitokeze kwa wingi zaidi siku ya Alhamisi ili kuongeza ushangiliaji hivyo kuinua ari ya wachezaji uwanjani.

    Pia michango ya kifedha ni muhimu hata kama ni Euro 5. Mnaona kila siku jezi zinakuja zimefuliwa, madawa, maji ya wachezaji na gharama za kuleta vifaa uwanjani vyote vinalipiwa toka mfuko wa timu ambao haupati ruzuku toka mahali popote bali kwa kujitolea au kwa michango au mauzo ya vinywaji. Tunajivuna tunaposifiwa kila siku kwamba Tanzania ndiyo timu pekee yenye jezi safi na tofauti tofauti. Sifa hizi zinahitaji michango yetu sote.

    Viva Tanzania! Aluta Continua! Ushindi ni wetu!

    Asanteni.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2008

    It's all gud...get it done guyz.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...