JK akimkaribisha Ikulu Dar Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha-Rose Migiro. JK baadaye alifanya mazungumzo na Dr.Migiro. baada ya kurejea Dar leo baada ya kufanya ziara ya siku tisa mkoani Tanga ambapo alikagua na kufungua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2008

    Jamani kuuliza si Ujinga: Sasa kati ya hao wawili nani Bossi? Au kwa maana nyingine nani anatakiwa ku "kiss-ass"? Mmoja mkuu wa nchi na mwingine Umoja wa mataifa...Mhhh sielewi kabisaa...!! Ila hako kamama kwakweli kamesafisha jina...halafu hakazeeki...na huo ulaji wa UN? Lol....heri yako...!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2008

    Jamani twende turudi nyuma, mama huyu ana figure. Kuhusu nani mkubwa ni Rais kwa sababu ana madaraka wakati mtu wa UN hata kama ni Katibu Mkuu mwenyewe hana madaraka ila ana heshima. Mathalani, Rais wa nchi yoyote duniani ana uwezo wa kuamuru polisi wamweke ndani Katibu Mkuu wa UN ingawa atashutumiwa kwa kuvunja Mkataba wa Kimataifa unaolinda wanadiplomasia. Lakini kwa upande wake yeye Katibu wa UN, hawezi hata kumpiga mkwara tu Rais wa nchi hata kama nchi hiyo ni Zanzibar.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2008

    Mdau uliyeuliza.
    UNO ni 'NGO' tu ambayo wahusika ni nchi huru, na Tanzania ni sovereign state. Kwa hiyo boss hapo ni Raisi Kikwete.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2008

    Asha Rose is a very good woman, hana majivuno na cheo alichonacho, hana muheshimu kila mtu! hana upendo na ni mcheshi yote hayo ni very intellegent woman,ni mpenda kazi, hana makuu, yuko very simple!! tunakuombea dua mwenyezi Mungu akupe uwezo ufanye kazi yako kwa ufasaha na utoe maanuzi yenye busara be blessed sister!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2008

    i love that woman shes real and intelligent especially on zimbabwe's issue during AU Meeting...the rest snitchs

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2008

    uwazi umevuka mipaka.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2008

    kama hujui kiswahili lugha ya nchi yako hakika hata kizungu kitakutatiza. jaribu kujifunza au hata kwa kuuliza. Sijaelewa hana muheshimu au anamuheshimu? hana upendo au ana upendo? duh aibu kama sisi wenyewe hajui kiswahili jamani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2008

    Hellen nakushauri kabla hujatuma maoni yako ni vema yapitiwe na mtu mwenye uelewa kuliko kuandika Kisawhili kinachotia kichefuchefu.Ukikosea mara moja haidhuru.Lakini kosa moja linakuwa linarudiwa rudiwa-hana muheshimu!hana upendo nk.Rudi tena shuleni naamini hata Kiingereza itakuwa hivyo hivyo tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2008

    We Hellen Mhaya we! Hujui kiswahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...