yanga leo imeichapa vital'o toka burundi bao 2-0 na kutinga nusu fainali ya kombe la kagame cup kiulaini. mabao yalifungwa na shamte ali dakika 13 na la pili alifunga amani dakika ya 19.
sasa yanga watakutana na tusker ambayo iliitoa rayon ya rwanda kwa mabao 8-7 kwa saba. hiyo ni bada ya dakika 90 kwisha na kupigiana matuta
sasa yanga watapambana na tusker toka kwa watani wetu wa jadi katika nusu fainali ya kwanza, na nusu fainali ingine simba itacheza na uganda revenue authority (ura) kesho hapo hapo neshno
Wacha unazi wa kukokoteza.Kama ni matokeo robo fainali zilianza jana.Au tangaza rasmi kwamba hii ni blogu ya Yanga kila mtu ajue.Ushabiki wa mgongo wazi huo.
ReplyDeletenaam, hapa ndio penye. Mwali lazima arudi Jangwani mwaka huu. It's been a while!!
ReplyDeleteHujui hata waliofunga mabao wacha ushabiki wa kuokOteza.Kiggi Makasi na Boniface Ambani ndio wafungaji.
ReplyDeleteYaani umeandika kinyongee kama vile ulikuwa unataka Dar Young Africans washinde haya wee omba mpite na nyie maana badala haya ya kutupa heshima yetu ya njano au kijani kwenye words zako naona unaweka yenu siongee kuhusu kuanza kiheshima with capital Y
ReplyDeleteLondoner
Ama kweli fedha za ufisadi zinatisha. Maana waandishi wa habari wengi siku hizi ni kufuatilia yanga wamefanya nini basi, na sio timu zingine. robo fainali hawakuanza kucheza yanga, lakini matokeo ya timu zingine 'hayakustahili' kuwekwa katika blog hii. Michuzi na wenzako, acheni unazi usiokuwa na msingi, kama mnalipwa na Manji semeni!! kushinda mpaka washinde yanga ndo muje kuandika hapa!! kila gazeti ukipitia ni kuipamba yanga!! yanga!! yanga!! oneni aibu nyie watu! huo mshahara mnaolipwa na Manji utawarudia puani, subirini tuingie msituni kukomesha ufisadi!!
ReplyDeleteAno.July 23, 2008 9:57 PM Pls jifnze kiswahili kwanza kabla ya kuja huku sio (Muje) ni (mje) ndo neno sahihi acha kuandika kiswahili kama una samaki njanga mdomoni. Ukiambiwa uandike kikristo je si itakuwa tabu!
ReplyDeleteNI MTANZAMO TU
Nakubaliana na waliochangia hapo juu, michuzi una ubaguzi mbona SIMBA hubandiki matokeo yake wakishinda, wakishindwa ndio unatangaza kwa makeke tuambie kama hii ni blog ya yanga tuanze kuipiga vita.
ReplyDeleteTunajua kila mtu ana ushabiki/mapenzi kwa timu yake lakini kama wewe mwenyewe unasema hii ni BLOG YA JAMII what that means?
Umemkosoa mwenzamo kwa kuandika muje na wewe ni mtazamo.Hakuna neno mtanzamo kwenye kiswahili.
ReplyDeleteNadhani humu ndani kunamtu hajuwi kiswahili vizuri.
ReplyDeletemara kadhaa anawalaumu watu wanaotumia neno. MU-***. Nadhani nenda kamuombe mamayo akufunze kiswahili vizuri.
hilo neno ni la uwingi wa neno U-**. Namshangaa pale watu wanapolitumia kwenye maeneo mengine kama... Munataarifiwa, Mu-naalikwa, Mu-natakiwa, nk haone tatizo. najuwa tatizo lake anachanganya kati ya utamkwaji wa neno na uandikwaji wake.
Najuwa tunatamka as if hakuna U, but haliandikwi hivyo tafadhali.
Ni hayo tu,
G7
UK