Michuzi,
Samahani because i seem to be dominating your blog today. lakini i need to clarify and probably answer some of the comments that i received from my earlier post.
To Issa Kabengo i would like to clarify kwamba tuna ardhi ya kutosha Uganda and we dont really need any from Tanzania.
I dont know where you have been in Uganda but i believe wherever you went sidhani kama uliona squatters.
To anonymous who questioned the luck of clear criteria in implementing the federationi would suggest you contact the Eastafrican community offices in arusha, I believe they will be in a position to help you out.
Tu mdau wa USA tawi No 1 i would suggest you come back to Tanzania and use your education in developing you country. To the SADC or East Africa. ( Jaamani Tanzanians SADC does not need you-you need them, whereas with Eastafrica you are needed (Thus use your God given wisdom to find out where you would be at an advantage)
I didnt want to get to comment on The Museveni issue lakini sisi Wanganda tunaamini Museveni ana akili ya kutosha kustafu muda wake ukifika.
Lakini kingine ni labda kwa wapinga muungano, what do you think about moving the headquarters of the EA community say to Nairobi or Kampala, now that Tanzania hawatutaki.

ICT Resource/Webdesign
ICT MOVEMENT
Tel: +256775669099P.O
Box 5772
Kampala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2008

    Lakini sisi waganda tunaamini Museveni ana akili ya kutosha kustafu(kwa kiswahili fasaha "atastaafu") muda wake ukifika.
    Translation
    Yeye ni mavumbi atarudi kuwa mavumbi....
    ....Na mwanga wa milele umwangazie..Apumzike kwa Amani.
    haya tumeshayaona kwa marais wengi ambao waliondolewa madarakani kwa staili hiyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2008

    Kakuru,

    Sijui kama Kato pia anakuunga mkongo kwa maoni yako haya. Ukweli ni kuwa Muungano wa nchi ni kitu kizuri sana kwani sote tunajua kuwa mataifa makubwa kama USA ni matokeo ya muungano wa nchi nyingi. Nyerere alipenda sana Muungano wa Federation ya East Africa hata akajitolea kuwa Tanganyika isipiate uhuru wake mwaka 1961 ili izisubiri nchi za Kenya na Uganda kusudi zote zipate uhuru siku moja na kuunda Federation mara moja tungali wabichi. Kenya na Uganda hawakukubaliana na mpango huo wa Nyerere, hivyo sisi Tanganyika tukaendelea na kujipatia uhuru wetu kabla ya ndugu zetu wa Kenya na Uganda. Wakati ule ndipo mazingira yalikuwa mazuri sana ya kuunda muungano. Tangu baada ya uhuru, Uganda imekubwa na migogoro mengi sana ya wenyewe kwa wenyewe, Kenya nayo imekubwa na migogoro sana ya ukabila, wakati Tanzania iliyoundwa kutokana muungano wa Tanganyika na Zanzibar nayo ina migogoro mingi ya muungano na sasa ufisadi.

    Kwa Uganda na Kenya ambazo hazijawahi kuwa kwenye muungano wowote, mnadhani kuwa swala hilo ni jepesi sana, na wengi mnachukulia kuwa muungano utasidia kupunguza migogoro ya wenyewe kwa wenyewe iliyoko nchini mwenu. Sisi Tanzania ambao tumekuwa chini ya Muungano kwa zaidi ya miaka 40 tunajua matatizo yake, ndiyo maana tunaliangalia swala hilo kwa makini sana. Hatutaki kufanya pupa kama ilivyokuwa miaka hiyo ya sitini.

    Binafsi ningazishauri nchi za Kenya na Uganda kuisikiliza sana Tanzania kuhusu swala hili kwa vile ina uzoefu na mambo ya muungano. Acheni kukimbilia Muungani na kuiashambulia Tanzania huku mnasahahu kuwa mnayo matatizo ya ndani kwa ndani yanayohitaji kuondolewa kabisa kabla ya kuingia kwenye muungano.

    Kumbuka Experience ya EAC ambayo ndiyo viongozi wetu wakati huo (Nyerere, Kenyatta, na Obote) waliafikiana kuwa tuunde kama alternative ya federation. Hii haikudumu hata miaka kumi kutokana na sababu ndogo sana za kibinafsi. As long as kuna ukabila, ufisadi, na kudharauliana katika jamii zetu, muundo wa federation utatufanya tusakamane sana. Ni afadhali kabisa tuendelee na muundo wa sasa wa EAC at least for another twenty years kabla hatujaanza kuzungumzia federation ya east africa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2008

    WEWE MGANDA KAMA UNASEMA MDAU WA USA ARUDI TANZANIA KUENDELEZA NCHI YAKE KWA NINI WEWE USIENDELEZE UGANDA ? "UNALAZIMISHA" TANZANIA, NA SISI TANAKWAMBIA RUDI UGANDA UKAENDELEZE NCHI YAKO ACHANA NA MAWAZO YA KIBAGUZI.HUO MUUNGANO NI "WAKIBAGUZI".

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2008

    WEWE MGANDA USITAFUTE WATU WA KUINGIA KWENYE BLOG YAKO KWA KUTUMIA MGONGO WA "EAST AFRICA COMMUNITY".

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2008

    Kakuru,tumekusikia na tunakusikiliza na tutakusikiliza.
    Umetoa mchango amabao ni kwa manufaa yako wewe uliyefaidika na kazi uliyoifanya Tanzania ukitokea Uganda tunashukuru, na asante sana.
    Hili la kusema kwamba watanzania hawataki muungano sio sahihi kabisa. Wengi wa watanzania wanataka sana muungano wa E/A, lakini kwa aina au njia moja uwe na manufaa kwetu waTZ, au kwa njia yetu wala sio kwa mfano au njia yako wewe, kwa ajili ya mafanikio yako wewe au baadhi ya wanajumuiya wengine.
    Muungano wa E/A tunaoutaka sisi ni ule wa wewe kuja kufanya kazi kwa mwaka na nusu na kuondoka pale wataalamu wa kitanzania watakapokuwa na ujuzi au elimu sawa na uliyonayo wewe au watakaporudi/ watakapofika kutoka nje.
    Na wala sio muungano wa wewe na wengine wageni kukaa humu TZ,huku WATZ wasomi wakilalamika kwamba umechukua kazi yao. Nchi zote zilizo kwenye muungano zina sheria za wenye nchi katika kazi za nchi. Wewe unataka kufanya kazi katika kazi za wenye nchi na katika makampuni ya wenye nchi.
    waTZ wengi wanapenda sana muungano lakini ule unaowafanya waganda,warwanda, warundi na wakenya kufanya kazi tu- katika mashirika, makampuni au idara za muungano wa afrika mashariki na sio katika makampuni yasio ndani ya muungano na hasa yale ya kigeni ambayo yanatakiwa kutoa ajira asilimia 99 kwa wazawa.
    Hivyo elewa tunataka muungano ila kwa aina yetu sisi. Umekaa TZ , na kuona kwamba wapo wageni wengi kutoka Kenya,UG, Rwanda na Burundi wanafanya kazi kubwa kubwa TZ bila kinyongo, ila hakuna WATZ wengi Uganda au Kenya au Rwanda wameshika nafasi kubwa kubwa katika makampuni ya huko.Ukielewa hili basi utajua muungano tunaoutaka sisi.
    Kama swala ni lugha ya kiingereza au kusoma basi uelewe kuna waTZ sasa zaidi au karibu 15,000 wamesoma nje ya nchi, kama USA, UK(pamoja na Ulaya yote), Australia,NK na kumaliza masomo yao kwa lugha ya kiingereza kisafi na kizuri zaidi ya kiingereza cha lafudhi ya "kiganda" au "kikuyu". Na hawa ni work-force kubwa kabisa ambayo muda wowote watarudi nyumbani na elimu, uzoefu na ujuzi kamilifu kusaidiana nguvu na wasomi wa nyumbani kuweka mambo sawa kama mistari ya maelewano itawekwa. wanasubiri "Dual citizen ship law" ipite na waje rasmi nyumbani na kuiendeleza nchi kwa namna wanavyoona kimaendeleo.
    kama unaona muungano na TZ sio lazima basi unaweza anzisha wako(Uganda) na Congo(zaire),Rwanda, Burundi, Sudan na kenya ambao bado ni jirani zako na ukaenda moja ya nchi kufanya kazi tena.
    By the way wewe ni web designer hivyo ishi na ujanja ujanja wako wa hapa na pale na achia mambo ya Muungano halali na wenye haki kwa WATZ kwa waTZ wenyewe. Ukitaka oa MTZ na uwe raia wa TZ na njoo uone ni kwa nini hatupendi muungano wa design yako wewe.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2008

    Mhh,
    Sasa naona umeacha kuandika jambo la maana tunalolizungumzia hapa la muungano. Haya ya kujibu kwamba squatters ziko wapi Uganda hayako katika mjadala wetu kabisa. Maana umeanza kutoka katika mstari.
    Ni sawa na MTZ aseme sisi ndio tulimuondoa IDD AMIN Uganda na kufanya wewe KAKURU sasa kufaidi matunda hayo na kutufanya sisi TZ kuishi na shida toka 1977 hadi leo hii.Au ni sawa na kusema AIDS ililetwa TZ na waganda miaka ya 1983. Hivyo wao ndio sababu ya matatizo yaliyopo TZ.
    "Kwa kifupi hizo ni BS"
    Cha msingi federation ya East Africa haisaidii kwa sana TZ, ila ipe miaka mitano ijayo na TZ itakuwa ready kwa lolote.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2008

    we kakuruku ebu acha kutupotezea muda wetu.Shame on you to say "waganda tunaamini museveni ana akili ya kutosha kustaafu kwa wakati wake".It seems you dont think beyond your nose.

    Watu walitoa argument za msingi kabisa.Kama hakuna demokrasia uganda,kuna maana gani ya kuwa na muungano.Naomba usirudi tena kwenye hii blog ya jamii na upuuzi wako.Kwanza umetudharau watanzania,umesema hatujasoma,hatuna mwelekea na ujinga mwingi tu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2008

    Ndugu yangu Kakuru pamoja na usomi wako inashangaza kuona bado una fikira mgando kwamba ili uweze kujenga nchi yako ni lazima ukae katika nchi hiyo hiyo. katika dunia hii ya utandawazi 9ambayo nina uhakika unaijua vizuri sana) unaweza kujenga nchi yako vizuri sana hata ukiwa maili milioni moja kutoka ulikozaliwa. Kwa kifupi, watu wanajenga nchi zao vizuri tu na kwa namna tofauti wakiwa wanaishi sehemu mbalimbali, nyumbani na ughaibuni. Usitupotoshe. Ninajua mamilioni ya waganda walio Marekani ambao wanachangia asilimia kubwa ya uchumi wa uganda.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2008

    Kakuru uliyoyasema yote ni sawa kimantiki. Lakini kwa swala la SADC you are kind of disingenious. Mbona Kenya na Uganda mko COMESA? who has raised an eye brow? nadhani to be in SADC or COMESA its a choice.I wonder why should you make it an issue with TZ being in SADC and yet quite with Uganda being in COMESA, IGAD among many other blocks.

    Kakuru, Iam a pro East African Tanzanian, who believes that, for Africa to move forward we need each other, but I can assure you, TZ fears are very founded. in Kenya and Uganda, bado mna ukabila sana.

    juzi tumeona jinsi uraisi wa Kenya ulivyokuwa between wakikuyu na waluo..as if hakuna makabila mengine. We see it in Uganda how if you are not a Munyankole you are like a second class citizen! Museven changed a constitution to be a life time president-Iam not saying TZ is more democratic, no, but we expected a courtesy of decency for Uganda to respect the basics of democracy like term limit! Folks I guess you ought to clean your house first and not clamour for this federation, because I see my fellow TZ have a point.

    Burundi, Kenya, Uganda and Rwanda..are our neighbours and we appreciate them, but they cant take us for the ride. We know what is good for us. even if we wanted unity with Zambia, Malawi or Zimbabwe..its our choice. Honestly, personally Kenya and Uganda make me scary with their POLITICS of divide and rule.

    Ohh about taking your headquarter..and you think TZ have something to lose?...just take it.

    I wish ungeuliza kwa nini mpaka leo EU haitaki Turkey iingie kwenye European Union....Kenya and Uganda..try first to practice responsible politics and ofcourse TZ we arent perfect! I know, but Uganda na KENYA mnatuogopesha ati..mnapenda vita sana.we cant afford the endless Nothern conflict in Uganda, we cant afford wizi wa kina Kibaki..leting thousands die simply because you think your tribe is a God chosen heir to the presidency!

    TZ might have their own probs in their closet, but I think their have a valid point and you should sit down and adress their concern instead of name calling that hawajasoma au ni wapole...we had this so called federation and we know what we gained and lost in the process.

    Infact I think Burundi and Rwanda will make a very good partners in Tanzania, because like Kagame is entriching democracy and fighting economic battle. Nimeishi Uganda Kenya, but ukweli ni kwamba nyinyi ndugu zetu mko very different sana! mnapenda violence and I can assure you Kibaki cant stand and tell us anything to do with the federation with blood in his hands...

    Mdau wa Msewe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2008

    kakuru,

    I respect your opinions as they are yours.
    ILA, acha kuweka mambo jumla jumla (generalization), kwamba watanzania hatujasoma?
    HATUTAKI KUBURUZWA: when we see it fit we will accept the federation thing.
    ILA not in a near future, till the generations of the likes of MSEVENI and KIBAKI are gone. Unadhani MSEVENI au KIBAKI akipewa urais wa EA ataachia????!!!!!!
    EU imeanza mchakato zamani sanaaaaa na mpaka leo hakijaeleweka, UK still using pound, FRANCE n AUSTRIA recently refused via vote constitutional reforms,etc,etc, sasa itakuwa Tanzania.
    I will come back to you soon ngoja niendeleze kuchangia maendeleo ya nchi yetu TANZANIA !!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2008

    mh chakwanza hawa wa kenya ni walafi wa kila kitu hata mkila nao lazima wakombe mboga yote na kusema eti tumezubaa

    wanatuona si hatujui kizungu lakini wao ndo hawajui kabisa angalia lafudhi yao ya kizungu utafikiri wanaongea kilunga eti kumbe kizungu

    wanganda nao ndo wale wali babu ana uchu wa madaraka utadhani sijui nini ? halafu tukiungana huyo jose wa porini tutamwambia nini jamani?

    hatutaki kuolewa na mafisadi sisi tuacheni hivi hivi na ujinga wetu mbona kama wajinga na maskini mnatutamani ?

    nchi yetu bado ni bikira kabisa haitaki uchafuzi inapenda amani mkija nyie tutashindwa hata kula ugali wa muhogo hapo break point na ndovu barid mwe

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2008

    we kakuru sijui kakuku nendaga uko.

    unachouzi unadhalau unatuambia sisi hatuna elimu sitaki hata habari zako nenda huko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...