nimenahatika kugongana na braza smasher na mwanae wikiendi hii akiwa ndio mwanzo karejea bongo (kimoja) kuja kuendeleza libeneke baada ya kuishi ughaibuni kwa takriban miongo miwili. anasema wito wa uzalendo ndio uliomrejesha na kwamba yuko tayari kula nasi vumbi. karibu sana smasher. usihofu sana braza, siku hizi bongo tambarare, wewe tu na mahesabu yako....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2008

    kaka mlete mtoto aje kupata propa,kwaliti,oganaizd edukeshen... we endelea na uzalendo wako.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2008

    Dhana ya 'uzalendo'. mh michuzi na wengine mna mawazo potufu kuhusu uzalendo. katika zama hizi za utandawazi, kuwa mzalendo si lazima ukae ndani ya mipaka ya nchi mama, na kukaa bongo kula vumbi hakumfanyi mtu kuwa mzalendo zaidi ya yule aliye ughaibuni akibeba mabox (na ku-wire mipesa huku huku nyumbani inayochangia kujenga uchumi wa nchi). Ningependa kuongeza hapa kuwa hata wale wanaopiga vita pendekezo la uraia wa nchi mbili wanasahau kuwa mafisadi wote waliokubuhu hawajawahi kuchukua uraia wa nchi mbili. Kwa hiyo unaweza kumkuta mtanzania anayeishi ughaibuni awe ni raia wa tz au la (mambo ya makaratasi haya)ni mzalendo wa dhati kuliko waziri mfisadi. ninaomba tujadili hii dhana kwa kina!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2008

    Eti!! nao wakajaribu kuiga kafulanaz!! Tee hee!!! (dRU)

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2008

    Karudi nyumba kulisukuma gurudumu la maendeleo?, Michu atachana msamba jamaa yako huyo, mwambie arudi kubeba boxi huku.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2008

    Du huto tufulanaz mlitovaaa ni uniform za blog ya michu nini??????????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2008

    mtu maisha yakikushinda Ulaya unarudi bongo kingereza kiiingi huna kitu,umekabwa na njaa sana basi utaonekana mwenda wazima mazee.
    Wabongo naomba msikubali hiyo hali tafuta makaratasi kwa hali na mali hata ukienda bongo ikiwa ngumu unarudi kwenye box

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2008

    Hongera braza smasher. Huo ni uamuzi mkubwa na wa kishujaa ambao wabongo walio wengi huku tumebaki kupiga hadithi. Nyie mnaokandia kurudi kwake pamoja na kijana wake na ambao mmeshindwa vita kama mnaweza jaribu.

    Ushauri kidogo kwa tulio ughaibuni, box inalipa lakini tukijichanganya nayo mno tutaishia "care home", AMUA SASA!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2008

    Hiiiii!!!!!!!!!!!! the fulanazi!!!
    ya blog ya jamii !??tunpendeza!??
    mweh! mweh!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 09, 2008

    Hongera sana kwa uamuzi uliochukua.Siwaelewi baadhi ya watu wanaopenda kukandia mambo ya watu wakati yao yanawashinda.Hakuna sehemu iliyoandikwa nilazima utoe comment kama huna cha kusema tulia na kama hukubaliani na mada toa sababu zako na ushauri wa kujenga na sio kubomoa na kukandia.Sisi kama watanzania tunatakiwa tuelimishane na kusaidiana katika mawazo na sio kuumizana kwa maneno.Wewe kama umekaa nje ya nchi na umejifunza vitu vyamaendeleo jaribu kuelimisha wengine nasio kuwatukana,kumbuka ulitokea hukohuko unakokukandia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...