Harambee tukusanye signature 100,000 za majina na ujumbe mfupi kwa ajili ya kuziwakilisha kwa vyombo husika kusaidia kampeni ya kupinga na kuachisha kabisa mauaji ya Albino.
Kila kukicha hii habari imekuwa ikiongelewa na kutunyima raha tulioko nje kwani tunashindwa kujibu tuhuma na kejeli hizi ambazo zinatupaka matope.
Kwa kutumia blog hii ya jamii shime wananchi andika jina na maoni mafupi hata kama ni sentesi mbili tupate signature 100,000 tuwakilishe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Kwa wanachama wa FaceBook group hii ipo na inakwenda vizuri pia ukiingia kwenye facebook (www.facebook.com) serch kwenye albino utaipata.

Ref: Angalia hii Video ya Al Jazeera

Na hii ya The New York Times
Sikiliza ya BBC Hapa
/tx/swahili_1530?size=au&bgc=003399&lang=
sw&nbram=1&nbwm=1

Mdau Pius Pius
Human Activist

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2008

    Mdau Pius asante sana,lakini naomba nipingane na wewe kidogo unaposema'kejeli na tuhuma'ukiwa unamaanisha tuhuma na kejeli kutoka kwenye hizo media ulizozitaja.Hili suala la mauaji ya albinos lipo.Ndiyo tufanye hiyo harambee lakini na serikali iendelee kuelimisha wananchi,kwa sababu mauaji ya albinos ni elimu duni inayosababisha jamii kuendelea kufikiria masuala na imani za kishirikina kila siku.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2008

    brother michuzi watu wengi hatukubali na mauaji au kuwatenga maalbino,lakini kuna link moja ya youtube uliyoiweka sikubaliani nayo kwamba white people ni albinos waliokuwa africa miaka ya zamani.

    ReplyDelete
  3. Papa Pius,

    Naungana na wewe kabisa kulaani kwa nguvu zote ukatili wanaofanyiwa hawa maalibino popote pale walipo Tanzania.

    Vyombo vya dola vifanye kazi ya ziada katika kukamata kuwafikisha mbele ya sheria watendaji wa vitendo hivi vya kinyama.

    Mashirika ya Kijamii yaweke msisitizo kwenye kuelimisha jamii nzima katika maeneo yote yanakotokea matendo haya yasiyo ya kibinadamu.

    Naomba Kuwakilisha,

    Soames, UK.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2008

    Huu ni ushenzi na ukatili kwa jamii ya Watanzania wenzetu ni uhayawani na haufai kuigwa.
    Asante mdau

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2008

    Waziri wa Mambo ya ndani anawajibika na hili lazima atuonyeshe kuna sheria amechukua, Miaka ile Mwinyi alionyesha uwajibikaji kwa kujiuzulu ikiwa ni kuwajibika na mauaji ya vikongwe huko Maswa Shinyanga leo hii tangu mwaka jana dec wameshakufa Albino 22 Tanzania nzima je kuna hatua gani ameshachukua tangu kipindi hicho?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2008

    Inaudhi inauma na hata sielewei jinsi gani nianze kuelezea machungu yangu juu ya suala hili. Roho za binadamu wasio na makosa zinapotezwa bila mtu yoyote kuchukua hatua. Jee ni serikali gani inayoshindwa kushughughulikia suala kama hili?. Hii haitakiwi kutokea katika jamii yetu jamani. Haya ni mauaji ya kinyama kama mauaji yoyote yale kwani hizi roho za albino zinatofauti gani na zetu Anduka jina langu hapo Hassan mnasi. Nipo Denmark

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 26, 2008

    Ndugu Pius, mi nimeingia facebook lkn nimeshindwa kujiandikisha kama mpinya unyama huu. Je ni lazima niwe member wa facebook? Plz nijibu maana mimi na familia yangu tunapinga vikali.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2008

    mauaji ya albino yanaendelea kwa sababu serikali inajifanya haina uwezo wa kuwafatilia na kuwakamata wale wanao chochea/kuwapa vijihirizi wauaji. mimi siamini kwamba serikali ni dhaifu kiasi hicho,au NAO WAMEPIGWA JUJU LA KUWAZUBAISHA NINI?
    huwezi kuniambia kuwa kuna wachawi au sijui waganga zaidi ya milioni nchini wanao chochea ujinga huu,sasa serikali kama itashindwa kuvunja mtandao huu ili waogope je wakiingia watu naofanya crime kwa kutumia teknolojia za kisasa serikali itafua dafu?tuache kuendekeza vitu vinavyoweza kumalizwa mara moja.sambamba na elimu inabidi wawekwe ma detectives wa kuwanasa wauaji ili waonyeshe walio watuma kisha mtandao uvujwe waadhibiwe jamii ijifunze kuacha ujinga huu hauna maana kabisa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2008

    Shime wadau tufanye hili litufanye tuonekane kweli Blog ya Jamii,
    Hii itatupa nafasi ya kuonyesha nguvu ya Blog na ile kampeni ya Michuzi yz kuifanya Blog itambulike kama kipasha habari kwa hili itafanikiwa.
    Na we Kaka Michuzi unatakiwa uweke msisitizo kwa ule wino wako mwekundu na uifanye hii topic iwe juu ya zingine. Nakushukuru we mdau Pius kwa kuliletga hili Mezani kwetu.
    Dismas Lyakuu - Texas

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2008

    SAMAHANI NDUGU MPINGA
    KWENYE FACEBOOK INATAKA UWE MWANACHAMA NA KWA WASIO WANACHAMA WA FACEBOOK WANAWEZA KUSIGN HAPA NA TUTAZIKUSANYA PAMOJA HIZI NA ZILE ZA FACEBOOK.
    PIUS

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 26, 2008

    Inachoshangaza zaidi kwenye Swala la Maalibino ni kwamba bwana Hassan ambaye aliojiwa na mwandishi wa habari amesema wazi kwamba rafiki yake alishiriki kuua albino,sasa serikali na polisi wake wapo wapi kuchukua hatua kwa huyo mtu ambaye ametajwa na bwana Hassan au ndio serikali ipo pale kuiba na kuchukua rushwa.je Tanzania ni nchi ya Sheria kweli au Sheria ipo kwa wachache na wengi wanaweza kufanya watakalo na hatua isichukuliwe.


    Waganga wote watakaokamatwa na nywele za Albino au Kiungo chochote washitakiwa kwani ni wauaji, watakuwa wamevipata wapi.


    Shame on you Tanzania Government.

    POPO

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2008

    yote haya yanatokana na kudai uhuru wakati wananchi hawana shule,mi nawalaani wote waliodai uhuru ndio wamesababisha haya,,pili vigogo ndio wanaotumia ndumba hizi za maalbino kwahiyo wasivunje,,inaniuma sana,,tatizo masikini na shule,,
    hiii hii hii

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2008

    ni jambo la kulaani na inabidi serikali iingilie kati kabla mambo hayajawa mazuri.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2008

    I am very much against this awful killing of innocent human beings. However, I was really appalled by the ignorance of the New York Times reporter. How on earth can you associate the discrimination of albinos to racial discrimination. Albinism is not a race but a biological condition and it is beyond me what he means when he says Africans were the first to discriminate...bla bla bla...and worse, that African albinos were pushed out of Africa into Europe. What a silly claim. Did he go to any school at all? If he did, he needs to go back there.

    I would like him to see this message and come clear out of his world of ignorance...

    Having said that, I appreciate that the video was not uploaded by the New York Times. It seems to have been edited with the silly claims inserted at paused intervals and it may well be that it was uploaded by a despicable individual with no knowledge of anything other than clicking, dragging and dropping...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2008

    #

    Tarehe July 27, 2008 3:57 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Al Musoma

    Nafikiri la awali ni serikali iifanyie kazi mara moja ripoti ya mwanahabari Vicky Ntetema. Waganga wa kienyeji waliomo ndani ya ripoti yake hiyo ni wauaji sawa na wauaji wenyewe kwani ndio wanaowahimiza wafanye hivyo. Vicky kafanya kitu kikubwa na hakika angestahili tuzo ya taifa.

    #

    Tarehe July 27, 2008 5:39 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Inasikitisha sana na inaonekana hakuna juhudi madhubuti zilizochukuliwa na serikali kudhibiti hali hiyo zaidi ya viongozi kusimama na kusema "tunalaani vikali vitendo hivyo" lakini hakuna kinachofuata baada ya hapo.

    #

    Tarehe July 27, 2008 6:42 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Kaka Michuzi unganisha hii na ile ya mdau Pius, Ukiweza ipigie Debe na wewe watu wasign tupo wengi na tunaweza kufikisha kama tunakupeleka ukapata visitor milion kwa mwezi mmoja iweje hii 100,000 ishindikane? Kama alivyosema mdau mmoja pale tufanikishe hili kwa kuifanya iwe Blog ya Jamii kweli.
    Ni mtazamo Tuu
    Bi Nsipitwe.

    #

    Tarehe July 27, 2008 6:52 AM, Mtoa Maoni: Anonymous katinko.usa

    kwa mtazamo wangu nashangaa serikali inasubiri nini kuwatafuta na kuwahukumu wahusika hii ni aibu siyo tu kwa taifa hata kwa muumba.

    #

    Tarehe July 27, 2008 9:15 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    NI JANA TU KUNA MDAU ALITOA MADA YA KULAAN MAUAJ YA ALBINO,LEO NIMEPATA HABARI KUNA MTU KAUAWA NIMESHTUKA SANA,YA NI AIBU KULIKO WALIYOIPATA SOUTH AFRICA KUUWA WAGAN,SIS TUNAUWA WENYEJ NA AFRICA IMEKUWA MSTARI WA MBELE KULALAMIKA KUHUSU UBAGUZ WAKAT SIS WENYEWE BADO TUNABAGUANA.NAONA HIZ NI DALIL ZA SIKU YA MWISHO POLEN SANA WAFIWA TUKO PAMOJA

    #

    Tarehe July 27, 2008 9:55 AM, Mtoa Maoni: Anonymous David Villa

    Kwanza natoa pole sana kwa ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu.Ni jana tu nilisema haya mauaji yapo tusilaumu Al-jazeera,CNN,BBC n.k.Wanablog tunaendelea kulaani hivi vitendo na kuitupia lawama moja moja serikali hasa waziri anayehusika kwa kushindwa kudhibiti hii hali.Kama hali itaendelea itabidi wananchi tufanye maandamano nchi nzima.Wanaharakati wa haki za binadamu mko wapi???

    #

    Tarehe July 27, 2008 11:55 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    It is a shame to all tanzanian's......shame on you........it is gonna get ugly very soon..the government needs to take actions...i am pissed...Now i see why white people calls us animals,i wont blame them considering wat is happening to tanzania....very sad.......

    #

    Tarehe July 27, 2008 2:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Mauaji ya albino ni jambo la kusikitisha, kikatili, na ni ukiukwaji mkubwa wa hahi za binadamu. Wanaofanya mauaji haya si waungwana hata kidogo, hawana hata chembe ya ubindamu hivyo hawa si watu wa kuwavumilia hata kidogo katika jamii ya Watanzania ambayo kwa muda mrefu imeaminika kuwa ni jamii ya wastaarabu. Hizo imani za kishirikina zilipita utu wa binadamu hazistahmilik hata kidogo. Serikali ishirikiane na kila raia mwema kutokomeza kadhia hii katika jamii yetu ambayo imewaweka ndugu zetu albino katika hali ya wasi wasi ndani ya nci yao wenyewe. Ni aibu kubwa kwa Taifa letu kwa mauaji haya ninawasilisha kwa wahusika kuwa wale wote waliokamatwa wachukuliwe hatua kali za kisheria. Mauaji ya albino ni kitendo kisichokubalika kabisa hasa katika jamii yetu ya Kistaarabu ya Tanzania. Ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi inayotambulika kikatiba nchini kwetu na pia katika jamii ya Kimataifa haukubaliki hata kidogo. Natumia fursa hii kuwapa pole wale wote walioathirika na vitendo hivi, wale waliopoteza maisha yao kwa kuuawa kikatili Mwenyezi Mungu awape pumziko la amani. Changamoto kwetu sote tunaoitakia mema Tanzania na kuwajali wenzetu albino Tushiriki kwa hali na mali kulaania vitendo hivi. Wale mliopo huko nyumbani Tanzania muwafichue wale wote wanaochochea mauji haya. Sote pamoja tuifanye Tanzania mahali salama pa kuishi kwa raia wake wote na wageni bila kujali rangi,dini, kabila, jinsi. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE. AMEN

    #

    Tarehe July 27, 2008 2:07 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Huu ni uzembe wa viongozi wa serikari yaani mimi naona hata wao hawadhamini maisha ya hawa watu.

    polisi mkuu wa mkoa wowote kwanzia sasa tukisikia mauaji hana kazi na atafikishwa mahakamani.

    kwani polisi kazi yao nini??
    au kama hawawezi wapeni ulinzi hawa watu kila sehemu walipo kuwe na dolia

    sio mnakaa tu mahofisini bila kazi na kusubili mishahara

    hawa watu wanahitaji kuishi kama wewe rais wa nchi unavyoitaji kuishi weka ulinzi

    yaani imeniuma kweli ila huu wote ni uzembe wa viongozi hawana wanaloliweza iwe rusha mmeshindwa kuizibiti na mauaji sasa mnafanyanini??? si mjiuzuru kama hamuwezi kazi sio kuuwisha watu kwa uzembe wenu

    hivi mumepewa madalaka jina au mlinde watu??? hao waganga wa kienyeji wako wangapi na seikari kushindwa kuwazibiti???

    watu wenyewe hawakuenda shule wanawashinda vipi??

    sasa kesho kwa mola mtajibu nini kama aliwapa nafasi za uongozi mukasababisha mauaji??

    naomba mpeane majukumu kamanda wa polisi wa mkoa wowote aweke ulizi hawezi ajiuzuru la sivyo yakitokea mauaji yeye ndiye atakekuwa mshitakiwa no moja!!!

    #

    Tarehe July 27, 2008 2:12 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    HALAFU WATANZANIA TUNASEMA TUNA SERIKALI TENA KWA BWE BWE KABISA TUNASEMA NI SERIKALI YA AWAMU YA 4.!!!

    MTU MWENYE AKILI ANGEDHANI SERIKALI YA AWAMU YA NNE INGEKUWA IMEIFUNZA MAMBO MENGI YA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO TOKA SERIKALI YA AWAMU YA 1, 2 NA YA 3..!!!

    BURE KABISA.

    #

    Tarehe July 27, 2008 2:58 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    KAMA SERIKALI ILIWEZA KUPELEKA WANAJESHI COMORO KWENYE VITA AMBAYO HAUTUSAIDII KITU CHOCHOTE,WANASHINDWA VIPI KUMALIZA HILI TATIZO ?

    SOURCE YA TATIZO LINAJULIKANA KWAMBA NI WAGANGA WA KIENYEJI,WATU WAMEFANYA INVESTIGATION,TATIZO LIKO WAPI ?

    WAPE KAZI WANAJESHI WAKAKAMATE WAGANGA WOTE NCHI NZIMA,WAPATE KIPIGO KIZURI KABISA THEN TUONE KAMA HUU UPUMBAZU UTAENDELEA....

    AMA SERIKALI IWAPE ULINZI,KILA MKUU WA MKOA APATE KUJUA KUNA ALBINO WANGAPI KWENYE MKOA WAKE NA HAKIKISHE HAKUNA HATA MMOJA ANAPATA MATATIZO.

    WATU WAMEKAA TUU MAOFISINI NA VITAMBI VIKUBWA,HAWAFANYI KAZI YOYOTE.

    SIJASIKIA WATU WAKISEMA IWEKWE KAMATI MAALUMU KUWEZA KUMALIZA HILI TATIZO,INAELEKEA FEDHA NI MUHIMU SANA KULIKO MAISHA YA BINADAMU,MAANA INGEKUWA ISSUE YA FEDHA WATU WANGEKUWA WAKALI KAMA NINI.

    ANYWAYS,MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.MAANA HII NI AIBU KUBWA SANA KWA TANZANIA...................

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 29, 2008

    Nalaani sana mauji hayo. Pia nasikitishwa kuwa serikali haikuweka makakati unaoonyesha dhamira ya kupambana na wimbi hili la mauji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...