mtendaji mkuu wa taasisi ya moyo (thi), dk. ferdinand masau, akiongea na waandishi leo hospitalini kwake. chini ni moja ya ambulensi zilizofika tayari kuwahamisha wagonjwa kuwapeleka hospitali ingine.
hadi globu hii ya jamii ilipokuwa inaondoka hospitalini hapo kiasi cha nusu saa iliyopita, hakuna mngonjwa hata mmoja kati ya 11 waliobakia aliyehamishwa na wala hakukuwa na dalili za kutimuliwa kwa wafanyakazi wa thi na vifaa vyao.
asubuhi daktari wa nssf alifika na kuangalia wagonjwa wote ambao inasemekana ni mmoja tu aliyekutwa mahututi. habari zinasema nssf wameshaandaa jopo la madaktari bingwa kadhaa. katika hospitali ya taifa ya muhimbili tayari kuwapokea wagonjwa hao wakati wowote.
akiongea asubuhi dk. masau alisisitiza msimamo wake wa kuiomba serikali kubariki maombi yake ya kuhakikishiwa kupata wagonjwa wa moyo kabla wafadhili wake hawajakubali kumpa pesa za uendeshaji ikiwa ni pamoja na za pango.
amedai kwamba baraka hizo za serikali zimekuwa zikipigwa danadana tokea enzi za mh. anna abdallah alipokuwa waziri wa afya. na kwamba endapo kama angepata baraka hizo mgogoro wake na nssf haikuwa na haja ya kuwepo kwani pesa angekuwa ameshapata.
alisema pia kwamba mwenye nyumba wake hajakamilisha ujenzi wa baadhi ya sehemu za taasisi hiyo kama ilivyoanishwa kwenye mkataba wao, jambo ambalo pia amesema linachangia wafadhili kusita kutoa mkwanja.
nssf wako tayari kuchukua jengo lao wakati wowote kuanzia sasa na kwamba hiyo haikuwa amri yao bali ni ya mahakama baada ya kufuata taratibu zote kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo.
kasema bila baraka hizo wafadhili wake toka marekani na ujerumani wanasita kutoa misaada zaidi kwani uhakika wa kupata wagonjwa wa moyo unakuwa haupo. wadau wengi wameiomba serikali iangalie namna itavyoweza kutatua tatizo hilo bila kuumiza kila upande - nssf, wagonjwa na dk. masau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2008

    CCM mnatuua, Bado Rais akija nje anasema rudini mkajenge nchi !!! nani atarudi na mambo kama ndiyo haya?? nina uhakika Dr. huyu na uzoefu wake na vyeti vyake akija huku analipwa hata dola 2000 kwa siku, lakini kwa moyo wake kajitolea kurudi nyumbani. Tuache ubinafsi jamani, na leo naenda kuomba uraia wa hapa. Na wewe Mwakyusa unaabisha watu wa Mbeya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2008

    Ama kweli aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.Leo viongozi wakuu wanamkwamisha huyu Dr. mzalendo ambaye anatufaa sisi tusio na uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya nchi.Hata hivyo kwani wana shida ya kutibiwa naye?Wao hospitali zao ziko Ulaya Bwana!
    Huyu Dr wala hahitaji mtaji toka serikalini TZ,je wewe waziri wa Afya kuna ugumu gani hapo?Hata kama mnaona atafaidi,mbona nanyi mnafaidi kwa wakati wenu,tena wala hamtukumbuki.Si afadhali hata huyu angalau anatukumbuka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2008

    Ukisema serekari utazeeka wewe muandikie barua mtukufu rais jk kama kweli ni mtu wa watu anapaswa kukusikia.

    kama hakusikii rudi zako ugaibuni waachie nchi waikongolowe wanavyotaka.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2008

    wacha ujinga wewe hapo juu. huyu dokta anacharge watu akiwatibu, hiyo siyo charity, it runs as the business. he is oblidged to pay for tenure no excuse for that.
    Acheni ujinga mnataka rais aingilie nini? amlipie kodi ya pango NSSF?
    narowminded people!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2008

    wewe anonymous wa 6:44 pm
    nazani hukuelewa poiti badala yake umekurupuka. hayo ndiyo maoni yangu nawewe weka yako usikimbilie kujibu maoni ya wengine ng'ombe mkubwa!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2008

    Kweli kabisa anonymous 6:44PM, kwanza vifaa vingine alipewa bure pale Houston (sio vipya) na hakulipa ushuru pale bandarini ingawa walimsumbua kuvitoa,huyu Dk anawa-charge wale wangonjwa sasa mnataka hata pango asilipe? Kuweni wakweli wajemeni!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 26, 2008

    ikiwa harusi,kitchen party,sijui maulidi,b-day tunachanga kwa nguvu zote.Sasa kama sababu zinaeleweka za huyu dr kushindwa kulipa pango,TUCHANGE.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2008

    Huyu jamaa anatakiwa kulipa kodi sisi tunaochangia NSSF yeye hakuwepo sasa anakuja kwa gia ya kuhudumia watu ili atunyonye musaidieni kwa michango ka ma mnataka kusaidia watz sio kusamehewa kodi, kwanza halipi TRA wakati anacharge gharama kubwa halafu anataka asaidiwe nini. nyie wa nje kaeni huko kama mnadhani huku hakuwafai ila sio kuja kwa kutuona sie wajinga na sisi tumesoma huko tukarudi. HE HAS TO PAY THE BILL OR GO

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2008

    Kwani anadaiwa bei gani.

    Ni mimi Zungu la unga - Ughaibuni

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2008

    Hapa wala hakuna mabishano sana ni kutofautisha vitu viwili tu:
    biashara na huduma ,
    NSSF wanafanya biashara wanapokodisha jengo na vilevile Dr. anafanya biashara kwa kuwatibu watu moyo hatoi huduma bure.
    Kwa hiyo lazima ALIPE kodi simple and clear.Aache ubabaishaji mapato anapata anapeleka wapi?lazima afanye mchanganuo kwenye biashara sio kuweka ishu kisiasa hapa.Halafu wajinga wajinga wanasema Rais aingilie,Kwa lipi??Rais ana mambo mengi muhimu ya kudeal nayo sio hili ambalo kuna vyombo kibao vinatakiwa kushughulikia.Sio kila kitu rais.
    cha chandu - uk

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 26, 2008

    Nadhani Dr. Masau aelewe kuwa kila jambo linaendeshwa kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo katika nchi husika.
    Alipoingia mkataba na NSSF alijua kabisa kuwa wajibu wake nini na haki zake ni zipi. Ni aibu kwa taasisi inayohudumia watu hasa wagonjwa ikionesha udhaifu wa kutimiza wajibu wake wa kulipa kodi ya pango.
    Dr. Masau kuwa muungwa wahamisheni hao wagonjwa katika hospitali nyingine na kuacha taasisi yako ikiendelea kutafuta njia nyingine za kuendesha shughuli zake.
    Hata hapa ninapoishi USA, kuna hospitali imepewa notice na wagonjwa wanatakiwa wawe wameondoka muda wa notice ukimalizika.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 26, 2008

    Nawale ambao baba wenye nyumba wao wanawafukuza kwapango nao waende kwa kikwete??? pumbavu!!
    wanapata pesa wananunulia viburudisho usafiri wanasahau wajibu wao. kwanza huyu jamaa inaonesha huu mchezo wa kumuomba anaupenda sana. Just run that thing as a business. hakuna mtu atapeleka mgonjwa india kama anaona wewe unafanya kazi bora. hakuna kubebwa kudaaddaaaaadeki...

    G7
    UK

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 26, 2008

    Mbona mnakurupuka jamani au nyie mnaweza kuamsha maiti jamani. Hivi hao madaktari bingwa wa muhimbili mnawajua ulizeni muambiwe afadhali mtu akumbie lipa kiasi fulani akusaidie kuliko kukuzunguusha. Mimi ya muhimbili yalinishinda na mpaka sasa familia yangu kama ikipata tatizo naenda Moshi au Nairobi. Hapo aliyekwama sio mtaalam ni jamii. Katika nji zote serikali inaweza dhamini taasisi kama hizi lakini kwetu mpaka jelemani au malekani

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 26, 2008

    alipe deni, kukimbilia kuwaita wana maombi si solution kwani kuna mapepo hapo hospitalini?
    mie naona kabisa huyu jamaa ni mbabaishaji, huwezi kuwa umeishi ulaya au marekani hujui umuhimu wa kulipa pango.
    arudi marekani akabebe mabox yake tu,
    kwani mimi nikitaka kurudi na kigari changu toka hapa UK,nikifika nisilipe ushuru? nitasema kuwa kigari hiki nitakuwa nikiwapa lifti jirani zangu hivyo JK aingilie.
    masawe acha utapeli

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 26, 2008

    Labda Dr. amesahau ule msemo wa "To whom you know not what you know" kama siri ya mafanikio. Jaribu kujifunza kutoka kwenye hii changamoto na ujenge network yako vizuri, si kwa upande wa wafadhili tu bali pia upande wa serikali na wadau wote kwenye biashara yako. Trust me hii kitu ipo pande zote za dunia na haitabadilika......

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 26, 2008

    i hate this dude, he bring shame to diaspora, when we go out of our mothercountry to learn and come back to practice complete unproffessional is shame. that institute isnot charity organisation and should self sustained itself from revenues collected rather than crying fawl to the media.
    The issue was imminent, if you dont pay rent you could evicted! whats difficult to understand about it?
    I hate "wasanii" especialy in sensitive sector as such.

    dogo

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 26, 2008

    Kweli anatoa huduma adimu , lakini lazima tujifunze kufuata sheria. Kama unadaiwa kodi ya pango ulaya au marekani utatolewa mbio kabla ya kufikia Bilioni 2.3. Hili limbikizo ni kubwa sana na inawezekana kabisa kujenga jengo lengine kwa bei hii.

    Anasema jengo lilikuwa lina kasoro ndiyo maana halipi kodi, mbona analitumia na kuwalipisha na kuwalaza wagonjwa ?

    Pili, uogozi wake hauna kitu kinachitwa "Business Continuity Plan" . Wakati NSSF ipo mahakani alitakiwa ameishajua wapi atahamishia wagonjwa mahututi ambao wapo chini ya majukumu yake na siyo kuita magazeti tu. Yeye ni daktari na siyo mtu wa PR.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 26, 2008

    nyie mlio changia mkimponda dr.masau inaelekea hamjui mnacho kichangia ila mnarukia gari kwa mbele! wahindi pamoja na viongozi wenu waserikali mngejua dau wanalo kula kwa kupeleka wagonjwa india mngepiga kimya kabisaa,na kwa taarifa yenu hisasa wanaandaa mpango wa kuanzishwa kwa tawi la hospitali ya APLO ya india ili iwe inatibu moyo hapo tz kisha muone wahindi watavyo kukamueni.
    kwanza kwa taarifa yenu kuanzia mfagiaji hadi mkurugenzi watakuwa wahindi[ajira kwa wabantu zitaota mbawa].kisha pesa mbele kama tai ndio matibabu baadaye hakuna cha kujililia ukasikilizwa hapa.
    NSSF sawa wote wanafanya biashara lakini angalau uzalendo huwa unakuwepo pale dr.huyu amtizamapo mtu asiye jiweza kuliko kina nanihii watakavyofanya.
    pia mkummbuke ndani ya fani kunakupigana vita ilimraditu wasione wengine wanainuka,ukitaka kujuwa madaktari wa muhimbii pia ambao wengi wao ndio walio sheheni pale wizarani wanavyokuwa na chuki binafsi dhidi ya madaktari waliotoka nje nenda ufungue hata ktk entry requirement za kuingia kufanya masters degree muhimbili,utakuta ahilia mbali kuwa huyu daktari aliyesomea chuokikuu tofauti na chao amefaulu nakuthibitishwa na watalaam tena wengine zaidi kuliko hata wao[maana humimbili kuna maprofesor tu,vyuo vingine duniani kuna hadi academic ambao ni zaidi ya prof],pia hawa ma dr wamefuzu internship tena wengine hata ktk hospitali za ulaya na wamekuwa wakitibu kwa kutumia technolojia za kisasa zaidi,kwa watu wenye bima zao na sheria kali,lakini kuingia muhimbili kufanya masters anatakiwa awe na minimum entry requarements za kuingia kufanya bachelor degree,SASA HAPA UHUSIANO WA CHETI CHA FORM SIX NA MASTERS UKOWAPI kama sio ukiritimba wa kuendelea kuhodhi fani hii kwa wao tu?hapa ndipo utakapo tizama ujuwe hatuta kaa tuendelee maana ukiritimba umejaa kila mahali,hata alikuwa na moyo wa kufanya chochote angalau kwa ajil ya uzalendo moyo huo hukatishwa na wachache wenye nia zao binafsi.
    cha msingi tu we chukuwa chako anza mbele,tafuta life lako uki win kula na wanao,waache wakubwa wakajitibu nje,maskini wajifie makwao noboby loses nothing ok?kama ndivyo sivyo acheni kumsumbua dr.masau ,heart surgery is not ajoke to pursue in the university,ni ndefu na ngumu,hata ningekuwa mimi ningeisha tambaa zamani sana kwenda wanako ithamini taaluma yangu wanipe mapene nile na wanangu hakuna haja ya kulumbana na wabongo,maana kitu kidogo tu cha kufanya dakika 10 wabongo wanaweza KULUMBANA WIKI NZIMA bila suluhu na kisifanyike pia.maana hii ndiyo hutufanya tuitwe waswahili.haya mzimeni dr.masau muwalete wahindi ili mle nao pesa za lion club,ndio maana hawataki kuishi kwingine zaidi ya city center na kariakoo.bro michuzi usibane hii.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 26, 2008

    jamaa anaomba wagonjwa zaidi apelekewa na serikali.serikali inachukua wagonjwa inawapeleka india kutibiwa.india inaingiza hela kibao nchini kwao huku daktari wa kitanzania hapewi wagonjwa alafu mnataka vijana warudi kuja kufanya kazi nyumbani.wewe unafikiri zile hospital za india bila wagonjwa zingeweza kumudu kodi?
    jamaa cha kufanya sasa auze vifaa hivyo aende kutafuta kazi nchi nyingine na hawaachie watu dili lao la kupeleka watu india au hawaachie wahindi waje kufungua hospitali ya moyo hapa nchini.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 26, 2008

    Dr Masau lipa kodi usitafute visingizio hapo,na haya ni matunda ya ubishi wako,uliombwa ujiunge na serikali ili upate msaada wa kuendesha shughuli zako ukawaona ni wapumbavu,sasa unakimbilia huko huko kuomba msaada!uliwaona watu waliokushauri ni wajinga kwasababu hawakuishi marekani kama vile kuishi marekani ndio unakuwa na akili kupita watu wengine.Lipa hela yetu ya NSSF tumeitolea jasho wakati wewe ulikuwa unakula kuku marekani

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 27, 2008

    wewe unaejiita G7 U.K
    kama huna cha kuchangia bora kaa kimya. wewe ndiye mpumbavu wa mwisho na unaonyesha wazi kwa maoni yako nyumba ya kupanga utalinganisha na sehemu inayookoa uhai wa watu?? au wewe ni chizi? hudhamini watu? au huna family inayoweza kupatwa matatizo? au hujuwi kuwa hostal za serikari hazijari wagonjwa? au ukiwa uk unaona uko peponi? acha ulimbukeni na penda kuchangia maoni kama binadamu mwenye kujari watu hujafa hujaumbika wakikupeleka wewe huko muhimbili utatoka? au hujuwi yanayo endelea? umeniudhi sana ila nimekuzarau kwani unaweza bishana na mwendawazimu bila juwa

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 27, 2008

    kwa wenyemacho tulisha liona hilichezo tangu zamani zile THI ilpo pigwa vita kisa tu eti imejitangaza kutoa huduma.lakini ukweli nikuwa kuna mkono wa wahindi na vijifisadi fulani visivyo jali afya za watu,ilimradi tu vinataka kunenepesha vijitumbo vyao na visharubu kwa pesa na deal za kupeleka watu india kupitia lion club. punde tu mtasikia hao wahindi wanajenga hospitali ya kutibu moyo tanzania maana wao kukupeni rushwa sio taabu,lakini mkae mkijuwa hiyo rushwa watakayo itoa,utailipa wewe au ndugu yako wakati utakapo hitaji matibabu hayo.
    kilakitu kinahita quality yake,hata hamfahamu kuwa hospitali nyingihapo nchini hazi meet engeneering standards za ujenzi wa hospitali,na matokeo yake kunaishia kuwepo hospital aquired infections kwa sababu mbalimbali zikiwemo poor ventilation,mwanga hafifu,poor location kati ya wodi moja na nyingine,separation kati ya entry ya medical personels na ndugu za wagonjwa,directions za madirisha,magnetic earth n.k hivi vitu vyote nyie hamfahamu mnadhani ilimradi tu jengo limesimama basi linaweza kuwa hospitali,wagonjwa wanakufa hata vyanzo vingine hamjui ni nini ilmradi tu matibabu yako sahihi!masau kasema waadhili wake wanahitaji NSSF warekebishe kasoro za jengo wao pesa za kulipa kodi kwao sio shida.Hata mimi nisinge somea nchi za watu huwenda haya yote nisinge ya juwa labda namimi ninge muona dr.masau tapeli lakini kwa sababu najuwa anacho kizungumzia siwashangai wapingaji na viongozi ambao wao wakiugua tu mbio kwenda nje!nyie si mmezoea kutibiwa ktk vibanda vya humo mitaani ambapo hata namna ya kufanya sterilization kiusahihi kwa kujali concentration tofautiza dawa za kuulia viini tofauti vya magonjwa na muda unao paswa kutumika hawafuati!wengine si ajabu hata HIV mnaipatia huko bila kujuwa,ilimradi tu mkiwaona hata matapeli wengine wamevaa koti jeupe na kipimio shingoni tayari mnajuwa dokta!kumbe wengine vihiyo tu hata umande hawakukanyaga kujuwa hicho chuo kikowapi wanakuuweni nyie bila kujuwa.
    kweli ujinga ni taabu na nibaba wa umaskini.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 27, 2008

    Jamani mbona wabongo mnapenda kuongea sana!!!!Ebooo! suala hapa sio kupelekewa wagonjwa au India inapata faida, noo hapa ni kodi haijalipwa mpaka deni limefika 2billion!!!SOLN: Deni lilipwe hayo mengine tutayaweka kwenye Mengineo.
    JK kasema tusichanganye siasa na biashara inabidi uchague moja,Siasa or biashara thats it.kukaa Ulaya au Amerika hakuhalalishi wewe kukwepa kulipa pango?Na kuna muda unapewa,sasa mpaka imefika hivyo i can say "la kuvunda halina ubani".NSSF hawatoi huduma wanafanya biashara na hizo pesa ni za walipa kodi.
    Kukwepa kulipa kodi nao pia ni ufisadi/usanii pure.Fisadi sio wale wa EPA or RICHMOND pekeyao.2 Billion ???Dr. lipa no way out.
    cha chandu - UK

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 27, 2008

    mimi kilichosalia naanzisha kampeni ya kuwapeleka madaktari wazawa nje,siolazima iwe ulaya,amerika,au asia,hata hukohuko afrika ilimradi tu ifikie wakati watanzania wajue umuhimu wa daktari mzawa. maana ukiwa nacho unakiona hakifai,kikitowekaunakijutia!
    sasa naandaa mkakati kabambe kuhakikisha naipafundisho serikali na watanzania ili wazinduke,kaeni mkao w kwenda kupanga foleni kwa wahindi,na serikali safari hii iwaite hao madaktari wa kigeni kama ilivyotishia kipindi kile cha ben tuone watawalipa kiasi gani kwa muda gani. maana hii taaluma nyeti naona inakosewa heshima yake sasa nchini.kisha sitotaka kusikia neno la UZALENDO HAPA maana watanzania na mashirika yao sio wazalendo pia! pia mamboya wito hapa yasiingie maana wito upo pale tu madaktari wetu wanapo kwenda kuisomea fani hiyo ambayo sio kilamtu anaweza kwenda kuisomea.
    litanichukua muda kidogo lakini sio zaidi ya mwaka,madaktari kaeni mkao wa kula kama wimbo wa siasa za kizalendo hauja wachosha!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 27, 2008

    Huyo g7 wa uk sidhani kama yuko educated manake huwa naonaga sana comments zake sehemu tofauti humu ndani na anaupungufu flani wa elimu.
    Jamaa kagoma kulipa kodi kutokana na nssf kushindwa kufanya matengenezo kutokana na mahitaji ya hospital kitu ambacho hata nyie mnayojifanya mko u.k na marekani kwa mbwembwe zote mnajua kwamba mpangaji ana haki zake pia.huko mlipo kama nyumba mlizopanga zina ubovu basi mara moja una ripoti kwa landlord wako wanafanya matengezo akishindwa unampeleka mahakamani.
    Dr.masau cha kufanya yeye alitakiwa kuwa shitaki pia hao nssf kwa kutotimiza makubaliano ya matengezo kwenye mkataba kama ni kweli malalamiko yake yalikuwepo kwa njia ya maandishi kwenye mkataba wao.haya mambo yote ya mawakili sema ndio hivyo kuna watu wako juu ya sheria na mambo mengi yanaendeshwa kienyeji.
    Umaskini wetu unasababishwa na wivu na ujinga.
    Watu wengine wanaropoka tu wanaona huyu daktari anafaidi au anaringa kwa vile ni daktari wa moyo.wivu wenu kwake hautamuangusha elimu alionayo kwani anauwezo wa kufanya kazi popote pale duniani na atapokelewa kwa mikono miwili na kwa unyenyekevu mno.
    Tuacheni kuhukumu watu kwa wivu jamani hatutaendelea popote.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 27, 2008

    Pumbafuuuuuu!!!
    wewe ambaye unasema mimi nimekurupuka kusema kuhusu hili suala ni chizi. kila kitu kipo wazi, kama ni hospitali or biashara lazima viende kibiashara na kama ukifuatilia maoni ya wengi humu wapo pamoja nami( so hatuwezi wote kuwa machizi zaidi yako).
    Kama hiyo hospitali inafanya kazi vizuri wahenga wasema chema chajiuza.. mbona watu tunatibiwa hospitali kadhaa bila kupelekwa na serikali?
    kwani hiyo yake yeye ndio pekee iliyopo ya binafsi? wangapi wanaenda regency, aghakhan na nyingine??

    Hakuna kuchanganya uzembe na kazi, halafu kwanini atumie michango yawatu wengine kuendesha biashara?? yaani wewe ukae huko sisi tuchange then ujikopesh usilipe!!!
    kweli wendawazimu wapo wa aina nyingi...

    G7
    UK

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 27, 2008

    Kwa Wale Ambao Mnataka Dondoo.....in Brief Sakata Lenyewe Liko Hivi..zaidi njooni JAMBOFORUMS.COM...kisha tazama thread hii kwenye SIASA



    [COLOR="Blue"]TAREHE 16/9/2003 [/COLOR]DR Masau alisign Memorandum of Understanding na NSSF
    Ambayo kama mmeisoma vizuri ilisema wazi kuwa NSSF wafanye renovation yale majengo ili yakidhi mahitaji ya THI na vile vile Dr Masau kwa niaba ya THI alikubali kuwa gharama za ile renovation zitachukuliwa na THI



    ([COLOR="Red"]Evidence soma MOU IPO KWENYE POST 55[/COLOR])





    [COLOR="Blue"]TAREHE 31/1/2006[/COLOR] DR Masau alisign Lease Ageement na NSSF



    katika agreement hiyo THI walikubali tearms and conditions ambazo wao wamechukulia lile jengo na pia walikubali kuwa NSSF watafanya matengenezo mengine as long as THI hawato default kwenye kufanya rent payments



    kwenye tenancy agreement Dr Masau alikubali angeingia kwenye majengo tarehe [COLOR="Blue"]1/3/2006[/COLOR] na agreement inasema angekaa [COLOR="Blue"]mpaka 28/2/2011[/COLOR]



    NSSF kwa kuona umuhimu wa kazi anayoifanya Dr Masau na THI walikubali kuwa Rent ya mwaka wa kwanza alipe Mwisho wa mwaka yaani [COLOR="Blue"]28/2/2007 [/COLOR]lakini baada ya hapo THI ilitakiwa ilipe rent ya mwaka in advance



    Vile vile Dr Masau alikubali na akasign kuwa service charge atalipa US 3 per square metre in advance



    [COLOR="Red"]LAKINI RECORDS TOKA HUKO HUKO THI ZINAONYESHA KUWA:[/COLOR]


    Dr Masau hajalipa Rent na service charge kuanzia [COLOR="Blue"]1/3/2006 [/COLOR]mpaka [COLOR="Blue"]29/2/2008[/COLOR]


    na katika kipindi hiki chote deni lake kama mtu anafanya mahesabu ya haraka haraka according to Lease agreement ni kiasi cha [COLOR="Red"]USD 837,696[/COLOR] na [COLOR="Red"]USD 314,136
    [/COLOR]

    ambayo ukiongeza 20% VAT utapata [COLOR="Red"]USD 167,539 [/COLOR]


    Na kutokana na records za THI kuna [U][COLOR="Blue"]invoice namba 08658 [/COLOR][/U] ilitumwa kwao tarehe [COLOR="Red"]22/4/2007[/COLOR] kama Mashabiki wa Dr Masau wanabisha waje kuleta vielelezo tofauti



    [COLOR="Red"][U]REACTION YA DR MASAU[/U]:[/COLOR]


    huyu mheshimiwa aliandika baruatarehe [COLOR="RoyalBlue"]2/5/2007 [/COLOR] kwenda kwa Waziri Kapuya, na copy kwa Waziri Mkuu na Rais kulalamika kuwa NSSF have been too hard on him na hawakuwa na haja ya kufanya hiyo...lakini hakutoa sababu ya kutokulipa deni na cha ajabu kama kawaida yetu wana JF mtaona katika [COLOR="Red"][U]CLAUSE no 5 ya Memorandum of Understanding[/U][/COLOR] ambayo huyu huyu Dr Masau alisign na NSSF inasema kuwa NSSF haitofanya matengenezo zaidi ya ile Hospitali endpo THI itadefault kulipa deni




    [U][COLOR="Red"][U]MWENYE MACHO HAAMBIWI ONA[/U][/COLOR][/U]


    Dr Masau ambaye ana PHD alikubali kusign hii contract na kisha akaamua kudefault kulipa kama alivyofanya TMJ na kwingineko analalamika kwenye hoja ya utetezi wake kuwa hawezi kulipa hilo deni kwani NSSF hawajafanya matengenezo yale majengo lakini huu ni uwongo wa hali ya juu kwani NSSF wako entitled lao pamoja na costs za renovation kama alivyokubali huyu Dr Masau



    Zaidi ya hayo NSSF walimpa notice ya siku 7 for non payment ya [COLOR="Blue"]USD 1,319,371[/COLOR]


    Baadae wakampa notice ya siku 30 kwa ajili ya kulipa renovation costs kiasi cha SHILINGI [COLOR="Blue"]1928,435,670[/COLOR]

    sasa jamani semeni integrity ya huyu mtu iko wapi?

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 28, 2008

    Mi nahisi hapa kuna tatizo la vijana wa ki-Masaki Masaki (walio na uwezo wa kutibiwa kokote) and ordinary class. Nikiangalia kwa ukaribu nagundua kuwa kuna shida ya kuangalia swala katika utaalamu wa kifedha na uchumi. Kwa waliomsikiliza Dr. Masau na ambao ni waelewa wa maswala ya Project Management watanipata vema. Huyu jamaa ndio anafanya biashara, but hata Muhimbili inafanya biashara.

    Na pia tukumbuke kodi ya jumba kama lile (tena lililo Mikocheni) si sawa na kodi ya kajumba ka Sinza huko. Huyu mheshimiwa anategemea zaidi income toka kwa wafadhili ili pia aweze kuwacharge wananchi wa kiTz kiasi kidogo cha fedha. Otherwise, akose misaada then atumie visenti vya watanzania kulipia kodi ya mjumba mkubwa kama ule. Pia tukumbuke ana wafanyakazi wanaohitaji mishahara na hali kadhalika kuna gharama nyingine za uendeshaji. Na mimi sijawahi kusikia wafanyakazi wake wakidai hawajalipwa mishahara.

    Sasa kama kakosa funds toka kwa wafadhili, nyie mnategemea afanyaje..!..?? Auze vitu vyake binafsi au...?? Kama mdau mmoja alivyosema, huyu jamaa akienda kujificha ughaibuni, atakula senti za maana.

    Tuwe na hekima na hali ya kufikiria kabla ya kukurupuka kuwa "he must pay" then yeye anaweza amua kuachana na taasisi aende zake kuajiriwa ughaibuni, then wewe unayeropoka ushuhudie watanzania wenzako wasio na uwezo wa kwenda India wakifa kama kuku..!! Msiropoke bila kufikiria, la sivyo mtaonyesha hamna hekima. Hapa swala ni kumshauri cha kufanya and not kumtolea maneno ya kashfa.

    Hekima ni chanzo cha maendeleo..!!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 28, 2008

    Maisha bora kwa kila mtanzania????????

    Wengi waliochangia wana mtazamo kuwa eti Dr. hataki kulipa pango! La hasha. Kama wamefuatilia sakata hili vizuri, kuna night grity za mkataba baina ya NSSF na THI ambazo zimetoa specification ya namna jengo linavyotakiwa kujengwa ili mpangangaji aweze kulitumia kwa malengo ya shughuli zake. Ki msingi Dr hajakataa kulipa, na akekiri anadaiwa. Lakini anachosema NSSF warekebishe jengo kulingana na makuliano ya kwenye mkataba ndo wapewe pango lao.

    Mathalani mtu unataka nyumba yenye uzio na geti, na unasaini mkataba na mwenye nyumba unaosema anakupangisha nyumba yenye uzio na geti. Lakini unaishia kukaa kwenye nyumba ambayo haina hivyo vitu. Je utakubali kulipa pango? au utamwambia mwenye nyumba aweke kwanza hivyo vitu ndo mlipe?

    Pia nawashangaa sana wanaomshambulia Dr.Masau eti ananyemelea vya bure. Jamani uzalendo uko wapi hapo. Infact Dr. anahitaji Goverment commetment katika kutoa hiyo huduma. Ni huduma hadimu, anaface challange kubwa sana toka kwa wahindi wanaokula hizo dili. Je tuache nchi yetu iliwe na wahindi au ijengwe na kina Dr. Masau?

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 29, 2008

    Mambo yanayoendelea kule JAMBO FORUMS.COM /SIASA ndio haya....


    MADAI YA DRMASAU/MWANAKIJIJI

    1) tarehe 22 Julai 2008, Dr Masau/ THI /Mwanakijiji walianza kampeni ya kushawishi na kupotosha umma juu ya ukweli halisi ya deni la pango linalomkabili.

    Huyu bwana aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kudai kuwa muda aliopea kuhama ni mfupi na kwamba kuna “mkono wa mtu” katika kadhia ya kuhamishwa Taasisi yake katika majengo yale. Aidha Mkurugenzi huyo alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akidai kuwa eti anataka kuhamishwa kwa nguvu ili majengo yale apewe Bwana Yusuf Manji na hospitali ya Appolo ya India.


    2) Na kutokana na mgogoro uliopo baina ya NSSF na THI, swahiba wake Mwanakijiji bwana MASAU tarehe 24 Julai 2008[/COLOR], pande zote mbili ziliitwa Ikulu kwenye kikao kilichokuwa chini ya wa Philemon Luhanjo, Katibu Mkuu Kiongozi, kutaka kupata ufumbuzi mzuri wa namna ya kuwahamisha wagonjwa ili wasiendelee kuathirika kutokana na mvutano uliopo baina Mpangaji na Mwenye nyumba.



    Na katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na wafuatao:

    -Katibu Mkuu Wizara ya Afya

    -Katibu Mkuu Wizara ya Kazi

    -Mtendaji Mkuu wa Muhimbili Profesa Lema

    -Mganga Mkuu wa Serikali

    - Bwana Emmanuel Ole Naiko Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Investment Center (TIC),


    na wajumbe walikubaliana kuweka utaratibu mzuri wa kuhamisha wagonjwa na kwamba Dr Masau atatoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo.




    Sasa kinyume na na makubaliano yaliyofikiwa tarehe 24 Julai 2008, Dr Masau alikataa kutoa ushirikiano kwa madai kuwa hakuwa na taarifa ya kutakiwa kuhamisha wagonjwa na kwamba NSSF hawakuwa na Amri ya Mahakama ambayo inadaiwa na cheerleader wake humu bwana MWANAKIJIJI


    UKWELI KUHUSU MADAI YA DR MASAU/MWANAKIJI NI HIVI:

    1)MAJENGO KUPEWA MANJI na HOSPITALI YA APOLLO

    Hapa hakuna ukweli hata kidogo kwani katika mjadala huu nimeweza kuwasilisha vielelezo vyote toka huko huko THI pamoja na Mahakama. Sasa ingekuwa bora kama Mwanakijiji naye akaleta docs toka kwa swahiba wake Bwana Masau ili wana JF tukacompare notes


    Nimeconfirm toka kwenye sources kuwa NSSF na MANJI hawajazungumza kitu kuhusu majengo yale.

    NSSF imefanya mazungumzo na hospitali ya Apollo kuhusu kuanzisha hospitali Dar es Salaam na HAYAHUSISHI kabisa majengo hayo kama anvyodai MWANAKIJIJI/DR MASAU

    Hospitali ya Apollo ilishatamka wazi kuwa inahitaji eneo lisilopongua eka 10 kwa ajili ya huduma hiyo na hiyo siyo siri.

    NSSF imekubaliana kimsingi na Chuo Kikuu DSM kuwa hospitali hiyo ijengwe Chuo Kikuu na bila kusahau kuwa kuna habari kuwa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili nacho kimeanza mazungumzo na NSSF kuangalia uwezekano wa kujenga hospitali hiyo Kibaha kwenye Makao Makuu mapya ya Chuo hicho.

    sasa Mwanakijiji tunakuomba utuletee vielelezo kuwa NSSF imeongea na Yusuf Manji au hospitali ya Appolo ili tucompare notes...surely su=idhani kama kwa mtu ambaye uko connected kama wewe hii itakuwa ni tatizo kwako



    2) THI HAWAKUPEWA MUDA

    Jamani wana JF mwenye macho haambiwi ona. Tuneona docs humu kuonyesha jinsi gani hili suala lilivyokuwa linashughulikiwa

    kwa kuwakumbusha wana JF ni kuwa suala la THI kuhamishwa liliamriwa na Mahakama Kuu mwezi Septemba 2007. Uamuzi na Amri hiyo ya Mahakama haikupingwa na THI. (ejea post no 55 kwenye hii thread)

    Ukwlei mwingine ni kuwa Wakili ya THI aliiomba Mahakama impe muda ili mteja wake ahame. Na mwezi Septemba 2007, Mahakama Kuu iliitambua notisi iliyotolewa na NSSF na hivyo basi kukazia hukumu yake ya awali kuwa muda wa notisi ukiisha THI wahame kwenye majengo ya NSSF.

    Jamani wana JAMBO FORUMS leo ni zaidi ya miezi 10 imepita tokea Amri hiyo ilipotolewa lakini THI bado haijahama.


    Je miezi 10 si muda wa kutosha?


    3) MKONO WA MTU
    Ajabu mwanakijiji sasa hivi anafanya kampeni za kupinga uchawi wa kila namna na kulalamika jinsi gani serikali ilivyowatelekeza MAALBINO. Lakini wakati huo huo anashabikia mambo ya kichawi kama "mkono wa mtu"

    haikatazwi mtu kuamini uchawi kwani hata mimi naamini upo na ndio maana ile mbuyu wetu kule Oysterbay upo mpaka leo achilia mbali mambo ya kuvunja nazi.

    Lakini kwa mtu ambaye yuko thousands of miles huko Detroit kulalamika eti kuna mkono wa mtu namshangaa sana. Unless kama alikuwa anazungumzia mkono wa mtu kuwa kuna kigogo serikalini hataki THI ifanikiwe...na kama ukweli ndio huo basi MWANAKIJIJI pamoja na DR MASAU tunaomba mtue ushahidi wa hilo.

    na hiyo haiondoi ukweli kuwa NSSF inaidai THI zaidi ya shs 2.3 bilioni deni ambalo THI hawajakataa kuwepo kwake.



    COURT ORDER au kutokwepo kwa AMRI YA MAHAKAMA:
    Mwanakijiji na na cheerleaders wako including Dr Masau mnaonekana nyinyi ni wavivu wa kusoma na kuchanganua mambo. Kila kukicha mnajidai mikataba ipitiwe upya, mara ohhh hatuna wasoma Mikataba etc

    sasa hapa hakuna cha zaidi ya mbinu za kutaka kuichelewesha NSSF kupata haki yake ambayo sidhani kama mnekuwa nyinyi mngekubali hilo.

    Kama mmesoma vizuri hiyo doc mtaona kuwa uamuzi wa Mahakama Kuu ulitolewa na Jaji M.H.C.S Longway tarehe 9 Septemba 2007.Amri ya kukazia hukumu hiyo ilitolewa tarehe 11 Septemba 2007.Amri hiyo ya Mahakama haijapingwa na THI hadi hii leo.



    In short huyu MASAU ni FISADI namba wani na tofauti yake na JACK PEMBA,KAJUMULO na akina GREY MGONJA ni kuwa huyu yeye ana PHD wenzake hawana. kwa definition ya UFISADI si kuiba tuu bali ni kuikosesha serikali mapato delieberately na sioni kwa nini mnataka kumtetea huyu mtu


    source: http://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=16067&page=71

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 29, 2008

    Mwanakijiji huna tofauti na Mtikila umenunuliwa na mbowe kiasi hata ukweli unapindisha, wewe kazi yako kuifitini serikali na hili la nssf una lako jambo.

    ndio maana kule kwenye raiamwema unatumia jina la Lula MWANANZELA na Tanzania Daima unatumia Nziku KUIKASHIFU SERIKALI KWA KILA JAMBO. mara ulianzisha mjadala wa kuwa wachagga wanaonewa.michuzi umeweka wapi ule mjadala wa kizushi wa huyu msemaji wa wachagga?sasa Masau hataki kulipa kodi jee wachagga ndio wanaonewa?
    mwanakijiji kama maisha ya kuwasafisha wazungu miili yao yamekushinda rudi nyumbani hukuiba kuliko kuishi wa majungu na fitna kiasi hiki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...