Mkuu wa nanihii ya nanihii,

Mie bwana naunga mkono na kupigania kwa nguvu hoja ya kukuza utalii kwa watanzaniakutembelea vivutio vya utalii haswa mbuga zetu za wanyama.

Swala la gharama ni tatizo kubwa lakini kukiwa na mipango mizuri kama vile kwenda kikundi gharama zinapungua sana.

Inasikitisha unapokwenda sehemu hizo unapishana na wazungu tu. Na inasikitisha zaidi wazungu hao wanapokushangaa. Wanafahamu Watanzania hatutembelei mbuga zetu.
NB: Pichani nikiwa na mai-waifu wangu kando ya bwawa la viboko,
Ngorongoro crater hivi majuzi.
Wakatabahu
ndimi Mdau Relex

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2008

    Jamani huyu si Uncle Othman, kamkumbatia nani jamani, mbona simjui huyu aliye kumbatiwa ?

    Komeni kabisa msije dhani ni Uncle kuparata , huyu ni Uncle wangu jamani tume toka mbali mweeh!

    Namzimia huyu Uncle sana ni Kiboko ya Mafisadi, utaparty naye ,utacheka naye, utadhani ni yakhe mwenzio , kumbe yeye ni yuko kazini, na hana mchezo, amerudisha heshima ya Nchi,EPA na mauchafu mengine yote yatamwaga hadhaani na amerusisha hadhi ya sisi wananchi kuwa wananchi na sio wawepo wachache Wenyenchi,

    Hongera kwa hilo, songa mbele , hapa kazi, funua mafisadi wote, JK,Othamn Oye,

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2008

    Jamani Kwa mbali kama ni Othman kumbe sio au? maana kwa mabli nilidhani ni Othman

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2008

    mimi nawaambieni mtakuja kuliwa na simba bure shauri yenu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2008

    Sawa nampongeza kwa kutalii lakini mimi nalia na wanawake wa Bongo hawajui kuringa wana wapenzi wao mwangalie huyo dada kama amekamatwa vile yaani hayuko tayari kushikwa, hawajui kujiachia kwa maneno mengine sitaki nataka jamani acheni hizo. Kama jamaa amekutunu jiachie huyo ni wako hadi ameamua kukuweka kwenye Blog si mchezo bibie kuwa Freeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2008

    Kuna mwandishi mmoja wa habari huko Moshi anaitwa Daniel Mjema wa gazeti la Mwananchi amefanana sana na huyo jamaa hapo kwenye picha.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2008

    Namuona mtu kama dada Ndina wa Tigo, nimepatia? Kama ndivyo nikupe hongera kwa mapumziko hivi ndio maisha nakumbuka kitabu cha Agoro Anduru (this is living) kwa hapa tuchukue ile maina yake ya juu (literal meaning)kwamba haya ndio maisha.

    Mdau Kiwoso

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2008

    mmh mdau hapo juu umenena,wanawake tujifunze kidogo kwenda na wakati ,wakina bibi zetu ndio wangeweza kufanya hiyo staili, ushakua my waifu wake jiamini basi kidogo. yaani unamfanya mwenzio awe ka mkabaji vile. othewise hongereni,mdumishe upendo wa wazi hivo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2008

    Othman mnayemzungumzia hapa, ni yule Rashid Othman, bosi wa Usalama wa Taifa au? Maana na yeye anavaa miwani lakini siijui sura yake vizuri!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2008

    e bwana anony wa 11:45 umenikumbusha hicho kitabu cha ''this is living'', huyo mzee Agoro Anduru mi namfahamu personally, mdogo wake alikuwa anafanya kazi na mdingi wangu mitaa ya kati pale Ngudu city, Mwanza. ni wajaluo hao akina Anduru....sijui kama vitabu kama hivyo bado vinapatikana, pamoja na vitabu vya Prince Kagwema..married life is a plant, na kingine nimesahau title yake ila ndani ya story kulikuwa na dogo mmoja alizaliwa hakumjua baba yake,baada ya kukua akaanza kumtafuta baba yake,alipompata jamaa akamkataa,alikuwa kingunge fulani hivi,so dogo alikasirika sana,akaona kama society yote imemkataa,akaanzisha libeneke moja la kufanya uhalifu mmbaya,ilikuwa mechi kali unaambiwa,akawa anajiita NOFANOSO= NO FATHER NO SOCIETY,...aisee kama kuna mtu anakumbuka jina la kile kitabu tafadhali sana andika hapa chini,nakitafuta sana, sijui kwa nini wabongo hawatumii vitabu kama hivi kutengeneza movie....tupo pamoja mkuu....
    EmergencyPoisoN.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2008

    Hongereni sana kwa kutalii.. maisha ni mafupi. Pia sina lengo la kumkandia dada huyo kwenye picha. Ila tu niungane na waliotoa hoja kwamba akina dada wa kitanzania bado sana sijui hamjiamini.. kuna wanawake wengine hawajui kupendwa..matokeo yake wakiachwa wanaenda kujibambika kwingine na wanakuta tofauti kubwa.. kurudi hawawezi.. maana it is too late.. Hivyo basi ukipendwa penda kweli kweli..pesa sio kila kitu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 29, 2008

    Naungana na Mdau aliyepost hiyo picha. Kwakeli inakera na kutia aibu mtu unapoenda mbuga za wanyama na kujikuta mweusi ni peke yako.Halafu wafanyakazi wa kule wanakushangaa mpaka wanakuja kukuuliza umekuja honeymoon au umekuja tu kutembea? Inamaanisha sisi wazawa ni mara chache sana tunatembelea hifadhi hizi.
    Mimi kusema ukweli nilikereka maana wazungu walikuwa wanatushangaa utadhani tumepotea njia au tumezamia. But kwa upande wa madreva na wafanyakazi they were very happy kuona watanzania wenzao wako pale plus they gave us extra special treatment kuliko hao wageni.
    I had fun kuona wanya live instead ya kuona kwenye TV na vitabu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 29, 2008

    Huyo ni daniel Mjema (Shotiii) mwandishi wa habari Moshi

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 30, 2008

    Nyie hapo juu kuweni waangalifu kama hamna uhakika huyo ni nani muulizen Michuzi mwenyewe. Lakini msitake kumchanganya rafiki yangu Othman Rashid na huyo mtu. Othman Rashid Njagu Mkuu hizo staili za kushika bibi hivyo kwenye mbuga za wanyama alikwisha stahafu miaka mingi sana. Kwanza angekuwa yeye pamoja na kuwa mtu wa watu unafikiri Misupu angekuwa na ubavu wa kumrusha hapo. Thubutu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 30, 2008

    mshkaji wa 5.21 ina maana uliwaona wanakunya live ikawa 'fun' ?

    natumaini hiyo ni typing error tu

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 30, 2008

    Usinikumbushe hizi abari, daah wale wafanyakazi wa huko mbugani hawajazoea kuona watalii wa kitanzania, ukifika hawakawii kukuambia kuna vyumba vya madereva apa bei rahisi! siwalaumu lakini wanajaribu kukufanya usevu na pia wanakuwa hawajazoea kuona mtalii mwenyeji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...