kiongozi wa ngoma africa band ras makunja akikaanga mbuyu jukwaani na bendi yake

The Ngoma Africa band na Mziki wa dansi wa Tanzania watapanda jukwaani 9-08-2007 katika onyesho kubwa la Africa-Caribbean Festival, katika mji wa fedha za euro - Frankfurt,Ujerumani.


Ebrahim Makunja mtunzi na kiongozi mwimbaji wabendi hiyo ataiongoza jukwaani bendi hiyo maarufu yenye tabia za kupelekana mchaka mchaka na washabiki barani ulaya kwa kutumia mdundo wao wa dansi wa Tanzania.


Onyesho hilo ambalo linatazamiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki ambao wana mazoea ya kulisakata dansi hilo la bongo, dansi ambalo limefanikiwa kuteka nyara maelfu ya washabiki barani ulaya!
Siku ya tarehe 29-08-2008 Ngoma Africa watumbuiza katika onyesho lingine kubwa la mziki wa kiafrika litakalo fanyika katikati ya mji wa Hamburg,takika viwanja vya Altona, huko Ujerumani, ambako kadamnasi ya maelfu ya washabiki wanaisuburi bendi yao yenye kuwapa burudani ya muziki unaochezeka.
30-08- 2008 watakuwa katika mji wa Krefeld, NWR, huko huko Ujerumani.
The Ngoma Africa watakwea jukwaani na kuporomosha mziki moto moto wa pata shika na nguo kuchanika katika onyesho la AFRIKA FEST, onyesho ambalo limeandaliwa na shirikia lisilo la kiserikali la L.O.A (Light of Africa).
The Ngoma Africa na mdundo wao kutoka uswahilini utauhakikishia ulimwengu kwa mara nyingine kuwa muziki wa dansi wa bongo ni moto wa kuotea mbali na ni fyagio la kimataifa!
The Ngoma Africa ambao pia wamebandikwa jina la "Wazee wa Kukaanga mbuyu"pia wametajwa kuwa "The Golden Voice of East Africa" ndio bendi pekee inayoongoza kwa kuwanasa na kuwatia kiwewe washabiki kwa kutumia mdundo au mziki wa dansi wa tanzania ambao wenyewe wanauita "Bongo dansi"
Hebu cheki hapa uone shughuli...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2008

    hii!!! wadau wa Frankfurt !
    vichaa hao wanakuja!kazi kwenu,
    Si mnasema ibrisi wa mtu ni mtu?
    sasa hao wanakuja tena! wake za watu hakuna kukaa nyumbani

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2008

    haya ! wenye wanawake vijana! muwaziwie ! hao wakaanga mbuyu ngoma africa wanakuja!
    najua wakina mama hawakai nyumbani
    suku hiyo!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2008

    wachizani wetu Ngoma Africa! mpo tena katika mibuyu yenu !he kweli nawakubali,naona sasa Taraka nje nje huko ujiji

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2008

    kaka ras makunja kamatia hapo hapo!
    mpaka kieleweke,moto wenu unakubalika pamoja na madongo makubwa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2008

    haya vibwaya na vibwebwe juu,
    dansi alibakizi mtu si kwa vijana wala wazee !hizo ndio zao

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 30, 2008

    Hallo! ras makunja
    huko frankfurt usifikiri Kariakoo,usije ukaenda na manati njiwa wa huko wanapenda amani.kazi njema na bendi yako

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 31, 2008

    mziki wenu mzuri sana tena wa kiutu uzima,sio ngoma za kitoto,
    daima mbele

    ReplyDelete
  8. hivi nyinyi ngoma afrika,niwaulize kitu kimoja ule mzozo wenu na baba
    wa kambo ulimalizikaje.
    ni mimi dada Subira aka Sista.Subi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...