Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mh. Samwel Sitta (shoto) akizungumza na Mbunge wa Rombo, Mh. Basil Mramba (kulia) na Mbunge wa Bukoba Vjijini, Mh. Nazir Karamagi, nje ya ukumbi wa Bunge mjini dodoma leo ambako kikao cha bunge kinaendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2008

    Kool and the Gang!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2008

    Hawa jamaa hawajakamatwa tu? JK jitahidi ndugu yangu, unaadhirika.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2008

    Spika Sitta, hawa jamaa wanakuambia nini?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2008

    Mover and shakers still in the game.Tanzania ina wasomi hawa tu wakifungwa tutaishije?These jamaaz will always be hapa hapa mtasema mtachoka

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2008

    Huenda hapo hao jamaa wanampiga Spika wetu mkwara!

    Karamagi ''..Aisee we Sitta achana na TICTS bwana! hujui kwamba mheshimiwa mstaafu ana chake humo?''

    Mramba ''...aise wee Sitta achana na mambo ya ndege ya Rais na Rada bwana! utamuumbua Mstaafu ebo!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2008

    ona raia kule nyuma wanavyotabasamu kumuona karamagi na pesambili,nadhani mawazoni mwao kinachoendelea ni hiki, BORA BABA ANGU NAE ANGEKUWA TU FISADI KWANI FISADI ANAHESHIMIKA KULIKO MTENDA HAKI PILI HASHTAKIWI WALA NINI ,kweli pesa sabuni ya roho ukiwa nazo mpaka supu ika aka 6anakusikiliza kwa makini japo anajua ulikula cha juu wakati wa kununua pipa la prezzo awamu ya muhishiwa aliyepita aka makaaa ya mawe ya kiwi la wira,wabongo sio wadanganyika ila ni waoga wa kuwawajibisha wenye pesa japo wao ndio wameporwa,uoga ukituisha ndio tuanze kupambana na ufisadi kwa sasa bado, tundika hii kapteni michuuuzi,ni vema mafisadi wakajua makaburi hayahitaji mbwembwe ndio maana hayana viyoyozi so wajifunze kuishi kwa haki,hala hala siku wabongo uoga ukiwatoka kazi ipo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2008

    ina maana wasomi wako wawili tu,hata kama ni wasomi lakini ni wezi sasa, wanaiba kisomi ama!?,hawa jamaa ni wabaya sana, waogopwe kama NGOMA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2008

    kwani Sitta mwenyewe si walewale tu. Halafu mbabe kama nini

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2008

    Sitta ndiye alikuwa mkuu wa kituo cha uwekezaji!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2008

    MAALIM ISSA TUNASHUKURU KWA "..FURSA.." ULIYOTUPATIA.VIONGOZI WETU WAKO HURU NA WANAENDELEA KUFAIDI "..MATUNDA.." YA KAZI YAO KATIKA "..BUNGE.."

    ".Bodi ya Ufisadi Na Gharama Endelevu."

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2008

    JK NA WABUNGA SAFI MUWE MWANGALIFU "..SANA NA HILI JAMBO.."

    WANAHARAKATI WA ARDHI NCHINI WAIONYA SEREKALI

    2008-07-22 17:37:25
    Na Devota Kabuta, Jijini


    Wanaharakati wa masuala ya ardhi wameitaka Serikali kusitisha zoezi linaloendelea sasa la wawekezaji kutwaa ardhi vijijini kwa ajili ya kuzalisha mazao yatakayotoa nishati hadi hapo sera na sheria kuhusu nishati uoto zitakapotunzwa na kujadiliwa vya kutosha.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Ardhi, Bw. Yefred Myenzi, ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akitoa muhtasari wa taarifa ya utafiti kuhusu nishati uoto Tanzania.

    Amesema hivi sasa, wawekezaji wanakwenda moja kwa moja vijijini na kuongea na wananchi wasio na uelewa wa masuala ya ardhi, hivyo uwezekano wa kuwarubuni ni mkubwa kwa kuwa hadi sasa hakuna sera wala sheria na kanuni zinazoelekeza namna ya kuendelea na mchakato huo.

    ``Uelewa wa jamii kwa masuala haya kwa ujumla bado uko chini. Wengi wanavutwa na ahadi za haraka bila kujali athari za muda mrefu,`` amesema Bw. Myenzi.

    Amesema hali hii inasababisha bei ya vyakula kuendelea kupanda huku taarifa ya benki ya dunia ikisema hadi asilimia 75 inatokana na chakula kutumika kwa nishati uoto.

    Amesema ni vizuri kama uwekezaji mkubwa ukaelekezwa katika nishati mbadala zinazotokana na jua, upepo na maporomoko ya maji bila kutumia mafuta yenye kemikali za kaboni.

    Aidha, amewataka wananchi wakatae kuondolewa kwa nguvu katika maeneo yao bila mjadala mrefu juu ya fidia kwa viwango vya soko badala ya kupangiwa viwango na mwekezaji.

    Amesema baadhi ya taarifa za kitafiti zinaielezea Tanzania kuwa ni nchi inayoweza kuzalisha nishati uoto hadi kiwango cha kutosheleza mahitaji yake kwa vile ina ardhi ya kutosha, maji na hali ya hewa nzuri.

    Amesema hivi sasa, nchi ina zaidi ya hekta milioni 88 zenye rutuba na kati ya hizo, ni asilimia sita tu ndizo zinalimwa.

    Amesema tafiti zinaonyesha pia kuwa hekta milioni 55.2 zinatumika kwa uzalishaji na kati ya hizo ni hekta milioni 10.8 hutumika wakati milioni 44.4 zimeachwa tupu, ingawa zinafaa mno kwa kilimo cha mazao ya chakula na mengineyo.

    Bw. Myenzi amesema utafiti umebaini kuwa takwimu hizo pamoja na mahitaji ya nishati na mazingira ya uwekezaji nchini, vimekuwa vichocheo vikubwa vya wawekezaji toka nje kutiririka kutafuta ardhi vijijini ili waitumie kuzalisha nishati uoto.

    Amesema hadi sasa, makampuni 37 ya ndani na nje ya nchi yameonyesha nia na mengine tayari yamepata ardhi sehemu mbalimbali nchini.

    Amefafanua kuwa, 13 kati yao ni ya nje, 6 ni ya wenyeji na manne ni mchanganyiko na 14 yaliyosalia hayajulikani kama ni ya kigeni au ya wenyeji.

    Hata hivyo, amesema mazingira yanaonyesha kuwa yapo makampuni ambayo yanaendesha shughuli za aina hiyo kimyakimya.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2008

    wE MICHUZI UNAOGOPA WASIJE WAKAKUBENEA NINI? acha kuminya mawazo ya watu nimekwambia spika anaongea na mafisadi kwani unabisha? au nawe ni kijifisadi kidogo? acha hizo

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2008

    Jk, "ACTIONS SPEAKS LOUDER THAN WORDS" please send these fake politicians to court of law to answer corruption charges

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2008

    watu mnaosema wamesoma...tafadhali fafanueni elimu zao hawa? Usikute ni ki-digrii au ki-masters tu! Alafu utakuta walisoma Urusi enzi za ukomunisti...tehehehe! Alafu kuna sehemu nimesoma Tanzania walipopata Uhuru kulikuwa na watu tisa tu wenye digrii...duh! Yani 9 tu jamani. Nadhani hao ni tisa babu aliowakubali katika serikali. Lakini bado aibu! Alafu watu wanashangaa mbona tupo nyuma leo...hehehe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...