tafadahali michuzi,
sio wote tuko Darsasa kiswahili chako kinachanganya kwani ni kiswahili cha bongo mitaani. sasa jitahidi uwe unatumia kiswahili kinachoeleweka kwenye blog yetu ya jamii kwa Mfano LIBENEKE; nimetafuta kamusi zote hakuna
mimi binafsi naipenda kwani ni zaidi ya TV zetu hapa
ahasante
Mdau Barnabas
fungua blog yako uweke kiswahili fasaha wengine hatuoni tatizo
ReplyDeleteNi kweli ndugu barnabas. Hata mimi nilikua napata shida na neno libeneke lakini nimelizoea sasa. Nakumbuka enzi zile niko tanzania na hasa Dar ukisema mtu anaendekeza libeneke ilikua unamaanisha anaendekeza ngono...ila najua kiswahili kinabadilika kwani hiyo ilikua miaka ya 80s na 90s...
ReplyDeleteMdau Barnabas utatafuta maneno mengi katika kamusi ya kiswahili na bado usipate maana yake. Mkuu wa wilaya ya nanii anafanya hivo kwa kuwa hii blog na ya wanajamii na ndo inayovutia kwa hicho kiswahili cha bongo mtaani. Panapo bidi kutumia ufasaha huwa inatumika ila hiki kiswahili ndo raha ya wengi kuingia katika blog hii. naomba kuwasilisha
ReplyDeleteSidhani eti kama neno hulioni kwenye kamusi yako/nyinginezo itamaanisha hilo neno halipo au si fasaha.Maneno mengine yaweka uzuri ndani ya blog kama hii.
ReplyDeleteSasa ndugu Barnabas kama lugha hii tu ya globu inakupa shida, ukienda bongo kwenyewe si ndo utazimia? Hebu nikuulize... hivi una miaka mingapi hujarudi nyumbani kwenu Tanzania? Manake huko nadhani kiswahili fasaha kilishasahaulika!!!
ReplyDeleteNi kweli bwana Michuzi,
ReplyDeleteunafanya kazi nzuri ila lugha ndiyo inakuangusha.
Jitahidi kuandika lugha fasaha na majina sahihi ya nchi kaka Ukerewe n.k
Tunaitegemea sana blog yako hasa sisi tulio huku ughaibuni.
tdduebAnon wa pili umenichekesha hapa hadi nimetafuta tissue paper kujifutia machozi, kwani umenikumbusha kipindi fulani tukiwa ofisini mtu kama hesabu haziko sawa na kusababisha nawe usibalance unashout na kusema "jamaa kanitimbanyia hapa" neno kutimbanya liliendelea mpaka siku moja alikuja jamaa mmoja toka musoma akasema jamani mnanitatiza hapo mnapotumia neno kutimbanya, kwetu ni kutweza nguvu, kwa maana ya rape, kwa maana ya siku hizi kubaka, ambapo zamani kubaka ni kitendo kilichotumiwa na watoto katika michezo yao ya kukamata/kubaka panzi. siku hizi kiswahili kimekuwa na kuongezeka tafsiri kwa kunyumbua na kutohowa baadhi ya maneno ambayo yanatumiwa kwa kitendo kibaya ila yanatamkwa kwa lugha muruwa.
ReplyDeleteSina hakika sana ila hiyo lugha au neno la libeneke watu wa kusini nikiwasikia sikia zamani sana wakilitumia kwenye ngoma zao kwa maana ya kuendeleza mapambano au kitendo cha kukazana na kusukuma jambo kwa ujasiri na bidii.Pole kwa kutatizika ila maneno ya mtaani yamekuwa mengi na inabidi wakati mwingine uyatumie ili ueleweke vema na jamii, hasa ya sasa, mara utaambiwa uko songombingo hueleweki bure hivyo lugha za kijiweni humu uzistahamilie na ujichanganye tu ili ufurahie uwepo wako humu kijiweni.
karibu kijiweni hata kama umri umeenda na shavu limeanza kuchuma kunde inabidi ujichanganye tuu ili uelewe ulimwengu unaendaje la sivyo utaliwa chekundu humuhumu kijiweni kwa maana utaachwa kwenye mataa au utaachwa solembaaaaaa barnabas, by the way asante kunikumbusha Mage wa ughaibuni.
ndugu Barnabas nitajaribu kukusaidia kidogo hilo neno lilitokana na nyimbo moja ya zamani kama sikosei ni ya moro jazz ambapo kwa wakati huo mtindo wao ulikuwa libeneke ndio katika nyimbo hiyo wanasema "waache waseme watachoka wao kijana saidi endeleza libeneke" wanataja majina ya wanamuziki wake basi ndio tena ikawa usemi
ReplyDeleteHapa zatakiwa hikma za Suleiman
ReplyDeleteWatu wengi wasomao blogu hii si vijana wa mitaani, ni watu watumizi wa lugha ijulikanavyo kwenye kizizi chake,maneno mengi jamaa wanatumia huwa ni uigo wa lugha nyingine kama kingereza na kifaransa,kama kumwita msichana staa au selebriti,hou ni uchafuzi wa lugha. I cant stop them you cant stop them from that type of degradation and pollution BUT make sure if you can allowance for some of us by providing a glossary of terms somewhere. I met someone who complained that he cant understand swahili anymore, for he learnt the language in 1975 after a years course in a university.unless we want to exclude those who learnt the language with the noble belief that it could become a mother language of the Afroamerican and Africans
Libeneke si ngono. Libeneke ina chimbuko lake wakati wa malumbano ya Cuban marimba na Masika Zole zole. Kuendeleza libeneke manake halisi ni kuendeleza kazi kwa moyo mnyofu, pasi shaka wala mashaka na kuwatumikia watuj kwa kile wanachokipenda bila kujali uhchovui wako wewe. Michu Dc wananii hii hii endeleza libeneke bwana watu lazima wajue lugha huwezi kuipata katika sijui kamusi manake tunaweza kubaki mayatima wa lugha kama dizaini ya akina barnabas ikiendelea kuwasha moto wa lazima kamusi. Michuu makamuzi kwa sana aende akatafute maana ya makamuzi
ReplyDeleteOya, wewe kama unataka kiswahili fasaha nenda zako darasani usilete mambo yako ya mwalimu Nyerere hapa, nenda TUKI pale UD utaelekezwa ....
ReplyDeleteSisi tupo hapa kufurahi na kupashana habari ,
Mdau East Coast
Mdau Barnabas, huna haja ya kutafuta maneno yanayotumika kwenye blog yetu ya jamii kwenye kamusi. Ukipata utata wa neno nenda kwenye sehemu ya maoni na uulize, la sivyo utaendele kubaki nyuma na kiswahili cha miaka ya ukilipotoka bongo. Lugha inakua na kubadilika na siyo vibaya kujifunza maneno mapya. Maneno ya mitaani yana radha yake bwana. Mfano kama kubonyeza kizenji na mengineyo...
ReplyDeletewewe acha hizo hata kingereza kinaengezeka kila siku.
ReplyDeleteTatizo si la michuzi hilo ni tatizo la baraza la kiswahili lisilo uptodate kamuzi yake often.
Jiulize why Merriam-Webster dictionary wameadd more than 100 words kwenye dictionary yao mwaka huu....Je ulijua mouce potato miaka mitano iliyopita ni nini?....Go figure....
Mwacheni kaka yetu aendeleze libene lake kwa nguvu bila kumkatisha tamaa.
Nyie wakimbizi mkirudi bongo mtashangaa na roho zenu mtashindwa kuongea kabisa kiswahili.
Go michuzi, go michuzi , go michuzi
Sasa jamani wewe kama hupendezwi na lugha inayotumika humu si usiingie tena basi maneno mengine yalitumika zamani kabla hamjaenda kubeba maboksi halafu saa hizi mtu anasema eti atumie majina fasaha.
ReplyDeletekama hujui kucheza na lugha mpaka upate tafsiri sisisi utashangaa,tumia hii blogu kwa kuwa current na kiswahili kinachokua sio unajivunia kujua lugha ya kubebea boksi ya mtaani
Dah Mmemshambulia kupita kiasi cha msingi ilikuwa apewe maana ya LIBENEKE halafu ambiwe Kausha, mdau hapa neno LIBENEKE linatumika kama SHANGWE au jambo la furaha,,hii kwa mauwezo yangu katika kiswaz. pa1
ReplyDeletehayawani hajifichi yani, wewe aliekuambia kuwa watu wanazungumza kiswahili cha kwenye kamusi nani,kiswahili kinakuwa kila siku na ndiyo maana watu wengi walio nje ya tanzania wanapenda kutembelea hii blog sio tu kupata habari mbalimbali pia na kungalia maneno mapya,sina uhakika wewe uko wapi, kama uko bongo na huyajui haya maneno basi nakushauri umeze wembe ukafilie mbali, na kama uko nje ya bongo na unaona kiswahili kinakuacha basi inabidi ufanye moja ya yafuatayo, rudisha u r ass bongo au ubaki uliko ubakie kutoa macho. tena ushike adabu yako kama unaona huna cha kuuliza ukae kimya, mwana mtoka pabaya wewe
ReplyDeleteMbega
Raha ya mgongo ni kuongea lugha ambayo mwenzie haelewi habari ndo hiyooooooo ndugu yangu. Vumlia tu wewe si boni hiya hiya braza au vipi?. Ndio zetu hizo
ReplyDelete