MKUTANO WA NENO LA MUNGU NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE KUTOKA TANZANIA: READING UK 08-10 /08/ 2008.


Jumuiya ya wakristo katika Uingereza na Ulaya inawakaribisha katika mkutano wa neno la Mungu utakokuwa ukiendeshwa na mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege kutoka Tanzania.

Mwlm Mwakasege ni Mchumi na Mwalimu wa neno la Mungu ambaye mafundisho yake hayana mlengo wa aina moja tu. Njoo ufaidike katika maeneo yote ya maisha.

MATARAJIO
Wenye shida za kiroho, nafsi, mwili mnakaribishwa mpate majibu ya maswali yenu.
Mafundisho ya namna ya kujikomboa kiuchumi kwa mujibu wa neno la Mungu yatafundishwa.

Nyimbo za Injili kutoka Mwanamziki wa Injili Fanuel Sedekia kutoka Arusha
Timu ya Injili na uimbaji kutoka Norway inatarajiwa kuwepo.

Huu utakuwa wakati wa baraka sana jitahidi usikose nafasi hii ya pekee na Mungu atakubariki.
ANWANI YA UKUMBI
Rivermead Complex Leisure Centre,
Richfield Avenue, reading
Berkshire, RG1 8EQ
Mikutano itakuwa inaanza asubuhi saa nne paka saa moja jioni kwa siku zote tatu.

MAELEZO ZAIDI: Wasiliana na /Reading Lillian 07846700927,
Birmingham-07776358464 Jackson Kapama,
London 07817479845 Elias Mwema,
Milton Keynes, 07787357618, Jane maneno,
Brighton,07950324330 Joyce Jacob.
Southampton 07717435287 Sekela Komba

07944632826./ Rev, Emmanuel Chatawe-Mwenyekiti
07983615387 /Timothy Kyara- Katibu mkuu.

KARIBUNI WOTE.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2008

    ALELUHYA PASTA...Duh mambo kweli yamegeuka...enzi za ukoloni na kabla tulikuwa hatuvai hizo nguo yaani wakati ule tukitunza hadhi na migomba,hao mamisionary yaani waeneza dini hiyo ya kikiristu walikuja Afrika kutustaarabisha sisi washenzi...na sasa jamani Mnyakyusa anakwenda kule hingilandi kueneza dini hiyo hiyo...ati kweli ukiristu kule ulaya umedidimia kiasi kwamba makanisa yao yamegeuzwa kuwa shoprite na mahekalu ya kibaniani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2008

    Mwakasege,habari za Tukuyu...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2008

    huyu baba kwakweli anaupako wa hatari Mungu azidi kumpa nguvu.
    sweet
    Arusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...