AS A UGANDAN WHO WORKED AND LIVED IN TANZANIA FOR CLOSE TO TEN YEARS IWOULD LIKE TO COMMENT ON THE ATTITUDE OF MOST TANZANIAN OFFICIALS WHENIT COMES TO MATTERS EASTAFRICAN.
TANZANIAN OFFICIALS SEEM NOT TO WANTANYTHING TO DO WITH SAY THE CUSTOMS UNION OR EVEN THE FREE MOVEMENT OFPEOPLE AND GOODS. AND USUALLY THEIR ARGUMENT IS THAT ANY SUCH A UNIONWILL BE A DISADVANTAGE TO TANZANIANS.

FOR INSTANCE IN THE GUARDIAN TODAY, OPPOSITION MP HAS AGAIN RETARATEDWHAT WE NON TANZANIANS HAVE HEARD OVER AND OVER AGAIN TO QUOTE HIM HE SAYS "Bakary added that Tanzania had enormous land resources, unlike its neighbours.
"He cautioned that the opening up of borders could lead the countryinto a land crisis. On employment, Bakary said with the common marketprotocol and free movement of labour, many Tanzanians risked losingjobs to highly educated and competitive Kenyans".

WELL, I WOULD LIKE TO COMMENT ON HIS STATEMENT BY SAYING THAT WHAT HEIS SAYING IS NOT WELL RESEARCHED AND THUS TO ME ITS NOT TRUE. THEIR IS NO WAY TANZANIA CAN LIVE IN ISOLATION FROM HER NEIGHBOURS JUST BECAUSEOF SUCH ISSUES.
FOR INSTANCE IN MY TOWN OF JINJA NYTIL A TEXTILE FACTORY HAS EMPLOYED A LOT OF TANZANIANS ON JOBS THAT WOULD HAVE OTHERWISE BEEN DONE BY UGANDANS. THOUSANDS OF TANZANIANS STUDY AND CONDUCT BUSINESS IN THE OTHER EAST AFRICAN NATIONS. THUS SUCH ALARMISTSTATEMENTS SHOULD BE DISCOURAGED AT ALL COSTS, UNLESS OF COURSETANZANIA PLANS TO BUILD A WALL AROUND ITSELF.
IN ADDITION OUR COUNTRIES HAVE BECOME STABLE AND THE WAGES HAVE IMPROVED THEREFORE FOR THE QUALIFIED, TANZANIA IS NOT REALLY AN OPTION WHEN SEEKING EMPLOYMENT.
I HOWEVER STAND TO BE CORRECTED ON THIS ISSUE AND I WOULD LOVE TO HEARFROM OTHER READERS ABOUT WHAT THEY THINK ON THIS PARTICULAR ISSUE.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI AFRICA MASHARIKI

Phillip Higenyi Kakuru
NewmanICT Resource/WebdesignICT MOVEMENT
Tel: +256775669099
P.O Box 5772
Kampala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2008

    TANZANIAN WE DON'T NEED EAST AFRICAN UNION, WE WILL LOOSE ALOT OF TAX, LAND AND JOBS GOING TO OUR NEXT DOOR'S. JAMANI TUKAENI NA NCHI YETU TUITUNZE IDUMU TUSIHARIBIWE MAZINGIRA (TUSIINGIZWE KWENYE MIZOZO HAWA WENZETU WANA HASIRA SANA) VITA EAST AFRICA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2008

    Michuzi nadhani hii article ya jamaa hapa inajitosheleza yenyewe kwani hakuna kitu ambacho amekisema kuhusu land na ajira kiufasaha. Amesema kunawatz kwao ambao wanafanya kazi kama manamba bila statistical comparison ya waganda na wakenya waliokwenye higher positions hapa kwetu.
    Pia nashukuru kwamba nipo naishi na waganda na wakenya hapa UK ambao wote wanajipanga kwamba wakimaliza shule sehemu kubwa ya ajira yao ni TZ kwani wanaamini kwamba kwao sio rahisi katika two ways: segregation based na ukabila , pia ajira zenyewe hamna. kitakwimu katika uganda 70-90% ya graduate hawana kazi na waliowengi wanafanya kazi za kujitolea.
    Kuhusu ardhi wote wanajuwa kwamba kupata ardhi kenya sio rahisi na wenyewe ndilo suala linalowagombanisha, uganda north wanajangwa. Therefore haihitaji professor kuexplain kwamba Tanzania will be suluhisho la matatizo yao.

    So jamani lazima tukubali kuwatunzia watoto wetu what we have now kwani watatulaumu baadae.

    Ni hayo tu.
    G7
    UK

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2008

    Ni kweli uliyoyasema...ndio tuna mawazo hayo...na mkitaka jumuia ya afrika mashariki kwanza fanyeni yafuatayo.
    1. Malizeni matatizo yenu ya ukabila;
    2. Malizeni matatizo yenu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe;
    3. Mjue kuwa Tz si pahala pa kuja na uzoa utajiri na kukimbia

    ciao

    Nyaningedere

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2008

    Pamoja na kulalamikia waganda na wakenya kuhusu ardhi ya Tanzania lakini mnajua kinachotokea siku hizi kuhusu ardhi Tanzanaia? Wananchi pamoja na viongozi wa vijiji na wilaya wanatapeliwa na Wageni kutoka nje (wazungu) kwa ahadi za kujengewa shule na visima vya maji. Sasa hivi kuna mgogoro huko Manyara kati ya wafugaji na muwekezaji ambaye anataka kulipa pango la ardhi la Tsh mil. 4.5 kwa mwaka kwa ekari 40 wakati wafugaji wanasema wanaweza kulipa hii pesa kwa serikali ili wabaki eneo hilo lakini serikali imekataa na kutaka kuwahamisha hawa wafugaji. Hawa wawekezaji ni matapeli kwani kila siku wanakuja na ahadi na misaada ili tuwapatie ardhi yetu na baadaye wanawaacha wananchi kwenye mataa. Kimsingi hawa jamaa wanatumia umasikisini wa wananchi pamoja na ufisadi wa viongozi ili kujipatia ardhi. Nawatahadharisha viongozi kwani kwani ardhi ndiyo suluhisho la ajira kwa nchi yenye watu wengi wasio na ajira kama Tanzania hivyo kitendo cha kuitoa hovyo kwa wageni inatufanya tukaribishe matatizo kama ya Zimbabwe. Hawa wazungu wakati tutakapowadai ardhi yetu watasema tunavunja haki za binadamu na kututangazia vikwazo. Viongozi msitupeleke huko kwani siyo muda mrefu hali kama ya Zimbabwe itatolea Tanzania kwani mnajua kuna kundi kubwa la vijana halina kazi mijini na siku wakiamua kurudi vijijini kwao na kutokuta ardhi yao hali itakuwa mbaya. Pia nawaasa baadhi ya watanzania wanaotumiwa na wageni katika kujipatia ardhi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2008

    Michuzi just tell him to read the history of East Africa and the reasons why it collapsed,hopefully he will come up with something good.
    Kwanza wameua sana ndugu zetu waliokua wakifanya kazi enzi za East African Community kwa sababu za wivu na chuki zao dhidi ya wageni,ni majuzi tu Mombasa kulikua na vurugu za madereva wa magari ya mizigo wakilalamikia suala la kuajiriwa kwa waganda kuendesha maroli na matajiri wa Mombasa huku wao wakitoswa.Hii ni picha ndogo inayoonesha ni kwa namna gani suala la shirikisho lilivyokua alikubaliki miongoni mwa wananchi wenyewe,bali ni kwa lengo la kutaka sifa tu kwa viongozi wetu.Uingereza tu wenyewe suala la wageni kutoka nchi wanachama wa EU bado linawaumiza kichwa namna wageni wanavyomiminika kwao hovyo.Tujifunze kutoka kwenye historia kwamba suala la shirikisho haliwezekani kivitendo,kwani wenzetu wakenya na waganda walishatuonesha tangu shirikisho la awali.Hasa Wakenya hawa wenzetu ni wanafiki na wanaojali maslahi yao tu,kamwe hawatokubali kuona unaendelea kiuchumi mbele ya macho yao,wenyewe kwa wenyewe hawapendani hadi kufikia hatua ya kuchomana moto sembuse wewe Mtanzania,au Mganda,acheni unafiki hapa hamna shirikisho fullstop!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2008

    kwa nini mnang'ang'ania sana hii jumuiya kuundwa? Mmeshaona watanzania wapole siku zote basi mnataka vyao tuu...thubutuuuu hampati kitu hapa.
    Sisi kama sisi tunajiweza wenyewe bila shirikisho ndio maana hatulihitaji kwa saana, tunaangalia mbele.
    Huko Uganda kila siku tunasikia majeshi yapo Congo huko wanaiba madini tuu, sasa mkija kwetu si mtatuua mchukue na ardhi Amin aliyosema yake?
    HATUTAKI JAMANIIIIIII TUACHENI NI TZ YETUUUUUUU!!

    eeeehh kerooooooooo!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2008

    Jumuia hii inaundwa kwa wachache tu.kwa WATANZANIA hakuna faida yoyote wadau.Kwanza tujue kuwa nchi zote tatu zinategemea misaada kuunda bajeti zao. Muungano gani utakao tegemea misaada???
    Nawaunga mkono wote mliojaribu kushambulia kuundwa EA

    malisa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 06, 2008

    kwanini tumejiunga kwenye jumuiya wakati tunafahamu matatizo yake.Viongozi wetu wa Tanzania na Akili zao wanazozijua wao..............? au ndio wakenya wanataka kuendeleza uongo wao kwamba Mlima Kilimanjaro upo Kenya, bado hawajaomba msamaha kwa hilo na wanataka kuzua lingine

    We are not suppose to join East Africa community on the first place.That is completely wrong!!!

    Kenge

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2008

    Jumuiya inaweza kuundwa na kufanya kazi kama vitu vitafanyika kiuwazi. Watu lazima tujue mikataba inayofanyika na vitu kama ivyo. Hii kusema Tz twajiweza wenyewe si kweli! East Africa Community ilipiga hatua sana kabla ya kuvunjika 1977 kutokana na political differences za viongizi. Madikteta, socialists na capitalists hata siku moja hawataweza kufanya kazi pamoja. Ni kweli...lazima hizi nchi nyingine zijitafutie masuluhisho ya matatizo yao lakini mimi sioni sababu ya kusema haiwezekani. EAC ya kwanza ilifanya kazi freshi sana mpaka tukawa na ndege zetu, na nini. Hadi hawa wa EU sasa waliipitia kujifunza jinsi ya kutengeneza communities. Enzi hizo wao walikuwa na EEC. Cheki sasa ivi wamefika wapi wao na sisi tumebaki kurudi nyuma. Kama ni tunaogopa kuhusu ardhi basi tueke sheria zitakazo tuhakikishia ardhi tunabaki nayo. Kama ni kuhusu employment...nayo ni hivyo hivyo. Matatizo tunayajua lakini tusiyafanye kuwa vikwazo vya maendeleo. Swali ni mtaendelea kujitenga hadi lini? Kuna mambo mengi ya kupitia na kuhakikisha yanakuwa sawa kabla ya muungano lakini sidhani kama ndo yawe sababu ya kuzuia maendeleo. Benefits za huu umoja ni kwanza sisi wenyewe Tz itabidi tupandishe kiwango chetu cha elimu kuweza kupambana na wenzetu. Pili tukijiunga uchumi na nguvu ya pesa yetu lazima itapanda. Tutaweza kuwa na control kubwa ya bei ya bidhaa zetu na kuzui magendo, nk.
    Lazima tuanze kwa hatua ndogo ndogo sio kukurupukia tu. Na lazima tuhakikishe viongozi wetu hawatuuzi kwa maslahi yao binafsi.
    Huyu bwana hapo aliyesema kuwa serikali inakataa kuwapa hao wafugaji hilo eneo (manyara) na wameweza ku-match bei atoayo mzungu(nmwekezaji)...basi inabidi waipeleke serikali mahakamani na itoe sababu zake. Katiba inafahamika ijapokuwa sijaona sehemu yeyote inapoongelea ardhi( very interesting) lakini yaongelea kuhusu haki za wananchi, nk. Kunyimwa haki ya Vitu kama hivi ndo inabidi tuvisimamie na kuhakikisha kuwa hatuuzwi.

    Mtoto aliyeenda shule
    P.S: Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2008

    Mimi nafurahi sana kuona watu wanasema ukweli. Mimi ni msomi wa kawaida sana na kweli kila nikiangalia "what is so special with the confederation..... and the like..." sioni labda watu wangesema "WITH BOLDED EXAMPLES" what are the expected outcome, what are the results ambazo zitakuwa REALLY TANGIBLE so that kila mtu ..... (acha mimi msomi wa kawaida...." ataziona???

    Kama kweli tupo sawa what are the results Tanzania is going to achive ..... tena should be in VERY SIMPLE terms and easily measurable even wit your naked eyes.....

    Hebu ninyi wasomi mliosoma na kuoan huko kujiunga na hiyo confedration tuasmbieni japo kupitia kwenye hata hizi BLOGS ili na sisi tuone

    Otherwise hebu tu-review our thoughts and see what are the ultimate results we plan to achieve from the confederation....

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2008

    Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
    Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
    BURIANI TANZANIA ... AU KILA LA HERI AFRIKA MASHARIKI?
    Na Mlenge Fanuel
    "Mtu akikushauri jambo la kijinga, huku anajua jambo hilo analokushauri ni la kijinga, na wewe ukakubali, basi atakuona, wewe zuzu!"
    -- Mwalimu Julius K. Nyerere, 1994/5
    Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafadhali isome barua hii ya wazi ya kukufikishia ujumbe kwamba Tanzania haiko tayari kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki (East African Federation, EAF) wala “Soko la Pamoja” la Afrika Mashariki, na kwamba Watanzania hatutaki Tanzania ijiunge na Shirikisho hilo.. Yatakuwa ni maafa makubwa kwa Tanzania na Watanzania iwapo Tanzania itajiunga na EAF hasa kwa mpangilio ulioko wa “fast track”. Ndiyo maana nimeanza na nukuu ya Mwalimu Nyerere, ambaye tayari baadhi ya watu, hasa wa nchi jirani za Kenya, Uganda na Rwanda, wameanza kumsingizia kwamba kwa kujiunga na EAF tutakuwa "tunamuenzi" Mwalimu Nyerere, huku wakijua fika ushauri wanaotupa wa kujiunga na Shirikisho na Soko la Pamoja la Afrika Mashariki hauna manufaa yoyote kwa Tanzania, wakidhania sisi Watanzania ni mazuzu tunaoendekeza wema wa mshumaa kuwaangazia wengine huku wenyewe unateketea, kwa minajil ya kupata misifa isiyo na tija.
    Ni kweli Mheshimiwa Rais umeunda Tume ya Kupokea Maoni kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini inatia mashaka iwapo huo siyo tu ni utaratibu uliouweka kuhalalisha maamuzi yaliyokwishafikiwa ya kuidumbukiza Tanzania kwenye EAF. Hii inatokana na muonekano kwamba Tanzania kujiunga na EAF kumeshaamuliwa tayari -- kutaka watu tujadili siyo kiinimacho tu? Mheshimiwa Rais, palikuwa na muswada uliopelekwa Bungeni wa Tanzania kujiunga na EAF, ambao Waheshimiwa Wabunge waliukataa, na serikali ikabidi iuondoe. Lakini mchakato wa Tanzania kujiunga na EAF ukaendelea tu, na kupuuza maoni ya Wabunge wetu tuliowachagua watuwakilishe. Ikiwa sikusikiliza vibaya, katika Bunge la Bajeti 2006/2007, Mheshimiwa Waziri wa Afrika Mashariki aliliambia Bunge kwamba patakuwa na KURA YA MAONI kuhusu Afrika Mashariki. Matokeo yake tumeletewa Tume badala ya kura ya maoni! Kana kwamba hiyo haitoshi, iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa wewe Mheshimiwa Rais wetu, ulimhakikishia Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwamba utafanya kila unaloweza kuhakikisha kufanikiwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki, kwenye mkutano wenu uliofanyika Mwanza. Je, maoni tunayotoa Watanzania kukataa kujiunga na shirikisho si "kilio cha samaki -- machozi yanakwenda na maji?" Wenyewe "wenye nchi" mshaamua mloamua?
    Pana maswali mengi mheshimiwa Rais ambayo ukitupatia majibu utakuwa umetuwezesha Watanzania tulio wengi kuelewa kuhusu mustakabala wa maisha yetu na Tanzania yetu:
    * Je, Ni sera ya CCM Tanzania kujiunga na EAF au Soko la Pamoja la Afrika Mashariki?
    * Je, Ilikuwa kwenye ilani ya Uchaguzi 2005 ya Chama Tawala CCM Tanzania kujiunga na EAF?
    * Je, Nani aliyependekeza Tanzania ijiunge na EAF? (Inabidi tumfahamu ili tuweze kumpamba maua iwapo Tanzania itafanya tunalodhani ni kosa la maisha la kujiunga EAF kumbe ikathibitika EAF ni manufaa tele kwa Tanzania ; vinginevyo inabidi tumfahamu ili tuweze kumzomea na kumuimbia nyimbo za kumsimanga pindi machungu ya EAF yatakapoanza kudhihirika muda si muda iwapo Tanzania itafanya kosa la maisha kujitumbukiza kwenye EAF. Vinginevyo itakuwa kama mikataba ya madini -- hatuelezwi nani aliwaalika na kuingia mikataba na 'wawekezaji' kwenye migodi.)
    * Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameshajitangaza kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki -- ikiwa na maana yote mengine yanayojitokeza sasa ni kuhalalisha na kusafisha njia ya Museveni kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki, hasa ukitilia maanani Rais wa Kenya na wewe Rais wetu mko kimya, ikielekea mmekubaliana na matamshi ya Museveni. Si hivyo?
    * Kutokana na maneno yanayosemwa na Wakenya na Waganda, Wanyarwanda na Warundi, inaonekana kama vile serikali ya Tanzania HAINA UBAVU wa kusema HAPANA kwa EAF -- kila mara Tanzania inazomewa inapohoji maslahi yake kwenye EAF -- au inapotaka kutumia uhuru wake ISIJIUNGE na EAF. Hivi karibuni Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania alisemwa kwenye vyombo vya habari kwamba hahudhurii vikao vya Afrika Mashariki -- na kumfanya Mheshimiwa Waziri Mkuu ajitokeze kumtetea -- na baadaye Waziri yule akaondoshwa toka Wizara ya Afrika Mashariki kwenye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri uliyoyafanya hivi karibuni Mheshimiwa Rais. Ina maana Tanzania ni kama mbwa anayeelekea kwenye mdomo wa chatu EAF -- amefyata mkia, anatoa kilio cha mwisho, na hana la kufanya zaidi ya kufanywa asusa na kumezwa -- au si hivyo?
    * Ni kwa nini Kiswahili SIYO lugha rasmi EAC, na badala yake ni kiingereza?
    * Kama shida ni ushirikiano, kwa nini Tanzania isijiunge na Msumbiji na Zambia , na kutengeneza shirikisho?
    * Kwa nini EAF inaharakishwa namna hii?
    * Ni nini Tanzania inahitaji kwenye EAF ambacho haiwezi kukipata bila kuwemo kwenye shirikisho hilo ? (Mbali na ngonjera za kisiasa, pengine na watu fulani kupata posho za vikao vya EAC na baadhi kuandikwa kwenye vitabu vya historia, vitu ambavyo havimsaidii Mtanzania mpiga kura wako anayesubiri neema tele na maisha bora...)
    * Pana bidhaa zipi za Tanzania hazifiki kwenye soko Kenya au Uganda , ambazo EAF itazifanya zifike sokoni?
    * Nani atakuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Afrika Mashariki, na ni upi mchango wa EAF kwenye uvamizi dhidi ya DRC?
    * Mheshimiwa Rais, hivi "Usalama wa Taifa" wa Tanzania una majukumu gani makubwa zaidi ya kulinda (uhuru) "Sovereignty" ya nchi yetu? Kwa nini "Usalama wa Taifa" haukupi picha kamili ambayo itakufanya usijisumbue hata kuja kutuuliza iwapo tunataka uhuru wa nchi yetu uondoke kupitia "soko la pamoja" na "Shirikisho la Afrika Mashariki", badala yake tukaendelea kulijenga taifa "letu changa" na kuulizana maswala ya maendeleo kama vile tutanufaikaje na maliasili tulizojaaliwa nchini mwetu?
    * Kwa kuitumbukiza Tanzania kwenye "Soko la Pamoja" la Afrika Mashariki, huoni kwamba utakuwa umekiuka kiapo ulichokula cha kuulinda uhuru wa, na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?
    * Kulikuwa na sababu gani ya kupambana na Idd Amin aliyetaka kipande "kidogo tu" cha nchi yetu, ikiwa leo tunaigawa sandakarawe nchi nzima kwa kisingizio cha soko la pamoja?
    * Tanzania itaondoka SADC? (Tayari nchi nyingine za Afrika Mashariki zimeanza kutuamuru tutoke SADC. SADC imeweka bayana kwamba wakati umefika wa kuchagua kati ya EAF au SADC.) Unadhani itakuwa ni busara kuondoka SADC? Kwa nini usitoe tamko kwamba Tanzania ya kesho ni ndani ya SADC?
    * Je sisi wananchi wa Watanzania tutaulizwa kuhusu kujiunga na "Soko la Pamoja la Afrika Mashariki" au ni uamuzi uliofikiwa tayari kwamba tutajiunga na soko la pamoja la Afrika Mashariki?
    * Huo Mkataba wa EAC/EAF uko wapi ili tuweze kuuona na kuusoma? Ni Watanzania gani waliousoma na kuuridhia kwamba SASA tunaanza kuwa kwenye mchakato wa kuelekea kwenye Shirikisho? (Inaripotiwa kwamba Tume yako ni sehemu tu ya taratibu ‘chovu’ za mchakato huo...)
    Watanzania tutafanyaje ili kuondoka kwenye EAF, iwapo Tanzania ijajikaanga yenyewe kwa kuingia kwenye EAF? Vipengele vya kujiondoa kwenye EAF viko wapi? Hautakuwa ni uhaini kuzungumzia kujitoa EAF, kama ambavyo si ruksa kuzungumza kujitoa kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ?
    Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, maswali hayo na mengine mengi yanaleta changamoto kwako binafsi kwamba zawadi kubwa kuliko zote unazoweza kutupa sisi Watanzania, ni kutukabidhi Tanzania yetu yenye "sovereignty" ileile au zaidi ya uliyokabidhiwa pale utakapoacha madaraka mwaka 2010 au 2015, panapo majaaliwa.
    Kwa taarifa yako Mheshimiwa Rais , Tanzania ndiye "Mbuzi wa Shughuli" kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki. Na mbuzi huyu amepangwa "kuchinjiwa kwenye maji" ili hata ukelele wake wa mwisho usisike. Hawatarudia makosa ya Jumuia ile iliyokufa 1977, kwa kutuacha bado tunafurukututa. Kujiunga kwa Tanzania EAF kwafanana na Punda wa kwenye hadithi moja iliyochapishwa Tanzania ambamo Simba baada ya kujeruhiwa, alishindwa kuwinda; na Sungura, Fisi na Punda wakaenda kumpa pole. Kumbe Fisi na Sungura walikuwa na lao jambo.
    "Simba kwa kuwa huwezi kuwinda naomba unile mimi", alianza kusema Sungura.
    " Asante sana kwa kunijali, siwezi kukula wewe rafiki yangu. Sasa nimefahamu wewe ni rafiki yangu wa kweli katika kipindi hiki kigumu cha dhiki!" alijibu Simba.
    Fisi naye akajitoa aliwe na Simba, ambaye pia alikataa kumla, akitoa sababu zilezile.
    Sasa Punda akawa njia panda: "Nikikaa kimya nitaonekana mbaya kwa Simba. Kwanza Simba mwenyewe kakataa kuwala wenzangu, na mimi atakataa... acha nijisemee tu kwamba najitolea anile..." aliwaza.
    Akaropoka, "Simba kwa kuwa huwezi kuwinda naomba unile mi..." Kabla hajamaliza maneno yake alirukiwa na kuraruliwa palepale.
    Kenya, Uganda , Rwanda na Burundi zina ajenda kadhaa kwenye EAF: mbali na zile "rasmi" zinazotangazwa hadharani. Ili ajenda zao zitimie, lazima "Punda" Tanzania awemo kwenye EAF ili aweze "kuliwa". Mheshimiwa Rais, ni wajibu na heshima kwako kuhakikisha Tanzania haijiungi na EAF kwa kuwa Tanzania haina ajenda mbali na ngonjera za kisiasa, pengine na posho za vikao kwa baadhi ya watu.
    Kwanza Tanzania siyo lazima ijiunge au ikubaliane na kila kitu kwenye ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wachache wanaounga mkono kujiunga na shirikisho la afrika mashariki, wanadai upo umuhimu wa kujiunga kwa vile "dunia nzima mwelekeo ni kujiunga pamoja, kama vile Jumuia ya Ulaya, EU". Kama sababu ni hiyo, kwa nini tusibakie SADC tuliko? Hivi tulipigania uhuru wa kusini mwa Afrika ili iweje? Watanzania tulitoa damu zetu, mali na uhai wetu, kukomboa Ndugu zetu walio Kusini mwa Afrika, sasa ukombozi umepatikana, pana wakati gani muafaka zaidi ya huu kuendeleza undugu wetu? Majirani zetu wa Afrika Mashariki tutaendelea kushiriana nao, kama tunavyoendelea kushirikiana na majirani zetu wengine. Kutojiunga kwenye shirikisho siyo maana yake tutakuwa maadui!
    Tanzania lazima ikae mbali na EAF, hata ikibidi kwa miongo kadhaa ijayo, ikiwa si moja kwa moja. Kwanza , Muungano wetu wenyewe una "mipasuko" ambayo haijasilibwa bado. Kabla ya kuulizwa kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki, tuulizwe basi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar . Tanganyika na Zanzibar , mara baada ya kupata Uhuru, hazikutimiza miaka mitano, "zikaishia" na kuwa Taifa moja Tanzania . Sasa jamani, Tanzania hata miaka hamsini haijafikia, nayo "iishie", tena kusikoeleweka? Tanzania ina manufaa tele SADC, kuliko kwenye shirikisho la Afrika Mashariki. Hivi, wakati tulipokuwa "Mstari wa Mbele wa Ukombozi Kusini mwa Afrika", majirani zetu wa Kenya na Uganda walikuwa wapi? Leo hii tukiwakubalia kuondoka SADC, watatuona timamu kweli?
    Mheshimiwa Rais Kikwete, kiasi inaeleweka ikiwa unaona pana ugumu wa wewe kuonekana unakwenda tofauti na Watawala wetu waliotutangulia, ambao huenda wanapendelea kuona EAF ikizinduliwa, Tanzania ikiwemo. Lakini mheshimiwa Rais, ndiyo maana kukawa na kikomo cha utawala cha vipindi viwiliviwili! Kwa kuwa umechaguliwa kwa ushindi "wa kishindo", imani yetu Watanzania imekuwa kwako kwamba utaweza kuipeleka Tanzania kule tunakotaka. Na tunakotaka sisi Watanzania siyo kwenye "soko la pamoja la afrika mashariki" wala EAF. Huo Muungano tu wa Forodha wa Afrika Mashariki unatekelezwaje? Matatizo na mizengwe iliyoko panaashiria nini pindi tukiwagaia nchi hii yote kwenye Shirikisho au "soko la pamoja"? Siyo maafa, Mheshimiwa Rais?
    Mheshimiwa Rais Kikwete, kwenye Jumuia ya Ulaya --EU, Uingereza na Jamhuri ya Ireland SIYO mataifa yaliyoko kwenye "Mkataba wa Schengen" wa Jumuia ya Ulaya, mkataba unaoondoa mipaka na vizuizi baina ya nchi za Jumuia ya Ulaya kwenye masuala ya Uhamiaji, japo Uingereza na Jamhuri ya Ireland ni wanachama kamili wa Jumuia ya Ulaya. Hii haikuzuia Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji, Ujerumani na nchi nyinginezo za EU zilizokubali kusaini kuendelea na "Makubaliano ya Schengen". Kadhalika , Iceland , Norway na Uswisi zimesaini "Mkataba wa Schengen" japo nchi hizo SI zanachama Jumuia ya Ulaya. Kila taifa linaangalia maslahi yake kama taifa. . Ulipoanzishwa umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki takriban karne moja iliyopita, Tanganyika haikujiunga mpaka ilipoona vema kwamba itakuwa ni kwa maslahi yake kujiunga. Hii haikuzizuia Kenya na Uganda kuanzisha Umoja wao wa Forodha. Tanganyika ilijiunga baadaye! Hata ile Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika, ilianzishwa baada ya kupita MIAKA HAMSINI tangu kuanzishwa ule Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki, japo nchi hizi zote tatu zilikuwa zinatawaliwa na Mkoloni mmoja takriban muda wote huo. Haraka ya sasa hivi ya nini? Wanajua wakituachia muda, tukienda hatua kwa hatua, hawataweza tena kuigeuza Tanzania koloni lao. Tanzania iendelee kuwa mwanachama wa SADC, na kuendelea kuwa imesaini kwa muda makubaliano ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki mpaka pale SADC itakapoanzisha Umoja wa Forodha wa SADC, ambapo Tanzania itajitoa kwenye Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki. Au busara zaidi, ni vyema Tanzania ikajitoa SASA HIVI toka Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki, na kuelekeza nguvu zake kwenye SADC. Kenya , Uganda , Rwanda na Burundi zinaweza kuendelea na Umoja wao wa Forodha, Soko la Pamoja na Shirikisho (waliite vyovyote wapendavyo), bila Tanzania kuwemo.
    Mheshimiwa Rais, ukubwa wa eneo la ardhi ya Tanzania ni zaidi ya Jumla ya eneo lote la ardhi ya Kenya , Uganda , Rwanda na Burundi ukizichanganya pamoja -- bila kuzungumzia rasilmali zilizoko. Halafu wanasema tuchanganye ardhi yetu na zao, halafu tugawane sawasawa kwa jina la "Soko la Pamoja la Afrika Mashariki". Hivi tukikubali ujuha huo, ni kwa nini wasituone sisi mazuzu?
    Swali kuu tunaloulizwa Watanzania na Tume yako mheshimiwa Rais ni iwapo Watanzania tunaona bado kuna sababu za Tanzania kuendelea kuwa nchi huru ambayo ni "dola", wakati ambapo kuna shinikizo nchi yetu igawe uhuru wake kwa kisingizio cha "soko la pamoja" na "shirikisho la Afrika Mashariki". Tuchukulie kwa mfano, tume itawahoji na kupokea maoni toka kwa watu laki mbili. Kati yao 80% wakasema Tanzania ijiunge kwenye "Soko la Pamoja" na "Shirikisho la Afrika Mashariki", 20% wakasema tusijiunge. Je, Mheshimiwa Rais, hiyo itakuwa na maana uamuzi utakuwa umesilibwa wa Tanzania kufikia mwisho wake, kwa kujiunga na Soko la Pamoja na Shirikisho la Afrika Mashariki? Je, hutatumia busara kama ilivyotumika kwenye Tume ya Nyalali ya Vyama Vingi pale Tanzania ilipoangalia maslahi ya taifa, na kuruhusu mfumo wa vyama vingi, bila kuangalia asilimia zilizotokana na tume? Ikiwa kweli kabisa umedhamiria kuipeleka Tanzania kwenye mwisho wake machinjioni Afrika Mashariki, kwa nini usiweke KURA YA MAONI kwa kila Mtanzania kupiga kura yake, badala ya kutumia Tume, angalau basi kuchelewesha kwa muda mauti ya Taifa Tanzania? "Soko la Pamoja" na pacha wake "Shirikisho la Afrika Mashariki" maana yake ni mwisho wa uhai wa Taifa la Tanzania . Ikiwa Tanzania itajinyonga (Mungu apishie mbali!) kwa kusaini mkataba wa "Soko la Pamoja la Afrika Mashariki" au ule wa "Shirikisho la Afrika Mashariki", basi Watanzania tutasahau "maisha bora kwa kila Mtanzania" na itabidi tujiandae kwa "Bora Maisha kwa kila Mtanzania", na kwamba wewe Rais wetu, Jakaya Kikwete, utakuwa umefeli vibaya kabisa jukumu lako la msingi tulilokupa -- kulinda uhuru na umoja wa Taifa la Tanzania na kubakisha Taifa la Tanzania kuwa dola huru kwa manufaa ya Watanzania mpaka pale utakapomkabidhi madaraka ya Urais wa dola la Tanzania huru Mtanzania mwingine.
    Kwa kuandika barua hii, imani yetu Watanzania kwako Rais wetu kwamba utaweza kuhimili mashinikizo yote ya nje, na kutusikiliza sisi raia zako, tunaotaka tubakie na taifa letu huru la dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
    Mwenyezi Mungu akujalie. Amin.
    Ndimi,
    Mlenge Fanuel
    Raia na Mwananchi wa Tanzania,
    Simu: +255 75 4372902,
    Email: mlenge@yahoo.com,
    Dar es Salaam, Tanzania.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2008

    WAPUNGUZE USHAMBA KWANZA NA KULALANA DAMU KWA DAMU, KWANZA HATA HIYO HABARI YENYEWE ILIVYOANDIKWA IMECHEMSHWA, THEY HAVE ALOOOOOOONG WAY TO GO TO ATLEAST TALK TO TANZANIANS, KWANZA KWA LUGHA GANI? WATAELEWANA NA WAHAYA TU SANASANA.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 06, 2008

    we dont need EAC coz now we are the member of sadc,we have only one membership and its satisfy for us we dont want EAC.kenya and uganda are member of ecowas that different.SADC allow his member to be in 1 membership only otherwise u must removed from sadc.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2008

    osusotyano nyabo/sebbo.
    sikiliza we mganda(shem wa michuzi) na wenzio wa kenya,rwanda,burundi na rwanda.hii biashara ya muungano HATUTAKI,na mkome kutulazimisha.kila kukicha kwenu ni mapanga shaaaa,ya nini? kaeni na shari yenu,tuacheni na umasikini wetu,umesikia?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 07, 2008

    Mtoto waliyeenda shule

    Umeongea mengi ya msingi sana...shule yako inajionyesha kwenye hayo uliyoyaandika.

    Watanzania wenzangu, suala la EAC halisa choice kama ambavyo wengi humu mnajidanganya. Dunia inaungana kuanzia Australia mpaka North America, East Russia mpaka ukingo wa visiwa vya Japan. Tanzania haiwezi kujitenga milele; sio kiuchumi, kijamii, kisiasa wala kiulinzi.

    Faida za kuwa na wageni kwenye nchi yetu (ili mradi wanafuata sheria zetu "MADHUBUTI") ni nyingi, nchi kubwa duniani zimenufaika ikiwamo UK na USA. Mimi naomba tu niwape ushauri huu; "Kama tunaogopa kuoga kwa sababu maji ni ya baridi, sharti tuyachemche yawe vuguvugu...lakini suluhisho sio kuacha kuoga moja kwa moja." Tutachemsha

    Mtoto wa Rombo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 08, 2008

    HUYO HAPO ANAYESEMA DUNIA INAUNGANA ANA AKILI KWELI?

    Wewe Mtoto wa Rombo,

    Yugoslavia ilikuwa federation (shirikisho) na ikafa, tena violently mpaka waBosnia kuchinjwa na kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja. WaCroatia nao walichinjwa na waSerbia na wakarevenge kwa kuua waserbia waliokuwa ndani ya Croatia. Baba wa taifa wa Yugoslavia mzee Tito (swahiba wake Nyerere) alisema waSlav ni dugu moya hivyo wadumishe huo udugu(na sisi tunadanganyana kuwa wa-East Africa ni dugu moya. Tokea lini mTZ akawa ndugu wa banyamulenge?). Matokeo yake kumbe watu walikuwa wanalazimishwa kuwa kwenye shirikisho. Vita ikaja na hadi leo tunajua nini matunda ya kulazimisha watu.

    Soviet Union ilivunjika vipande vingapi????

    EU yenyewe ingawa ina wanachama wapya hivi sasa, hivi majuzi tu Ireland imepinga treaty mpya!! Hawataki kuona EU inapelekwa huko watu wachache wanasema iende. Na hapo hawajawa shirikisho bado!

    East Timor imejitoa chini ya Indonesia tena kwa vita na watu wengi wamekufa.

    Kosovo wanataka kujitoa chini ya Serbia (ambalo nalo ni moja ya vipande sita vya yugoslavia iliyovunjika).

    MUUNGANO GANI UNAOONGELEA??????

    Mtoto wa Rombo,

    wewe unachanganyisha shirikisho na jumuiya. Tayari TZ iko kwenye jumuiya tena siyo moja, hata SADC nayo ni jumuiya. Dunia nzima kuna jumuiya zimejaa lakini hatujasikia Japan inataka kuwa nchi moja na Korea na China!

    Kwa hiyo ni UONGO kusema kuwa duniani nchi zinaungana. Kama unaongelea jumuiya, sawa ntakubaliana na wewe jumuiya zimejaa kede kede. Shirikisho, hapana!

    Niambie kama kuna nchi hata moja duniani ambayo katika miongo miwili iliyopita imetupa sovereignty yake ili ijiingize kwenye SHIRIKISHO!!!???

    Mungu ibariki TANZANIA!

    Mtoto wa Same Mashariki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...