Ronald Mtawali a.k.a Ronnie Mtawali, jumanne ya wiki ijayo atajiunga rasmi na GTV kama Meneja Mkuu wa kampuni hiyo kwa hapa bongo.

Taarifa toka GTV inasema uzoefu wake mkubwa wa kufanya kazi hapa nchini pamoja na mafunzo mbalimbali aliyopitia vinamfanya Mtawali kuwa mtu anayefaa zaidi katika nafasi hii.
Ronnie anaungana na timu ya uongozi wa juu ya GTV akitokea Momentum Tanzania, kampuni inayoshughulika na uangalizi wa mipango ya afya na bima ambako pia alikuwa Meneja Mkuu. Huko majukumu yake yalijumuisha uangalizi wa kampuni kwa ujumla, mauzo, mipango ya ukuaji wa kampuni pamoja na utekelezaji wake.

Ronnie anatinga GTV akiwa na uzoefu mkubwa katika masuala ya masoko, mauzo, utendaji na uendelezaji wa biashara na watendaji kazi. Alianza maisha yake ya kazi kwenye sekta ya mahoteli, kisha akafanya kazi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambapo alishika nyadhifa mbalimbali nyeti. Baadaye alihamia MIC Tanzania (Tigo) ambapo alikuwa mmoja wa wakurugenzi.

Uzoefu wake kazini unakaribia jumla ya miaka ishirini.
Mkurugenzi wa Biashara wa GTV, Rhys Torrington ambaye alikuwa hapa bongo kutangaza uteuzi huu alisema, “ Tuna furaha kubwa kuwa na Ronald kama mwenzetu kwenye timu ya uongozi. Uteuzi wake unaonyesha azma ya GTV kuendeleza uboreshaji wa viwango vya huduma zake.

“Ronald anaungana nasi akiwa na uzoefu mkubwa wa utendaji pamoja na msukumo wa dhati katika nafasi hii vitu ambavyo vitaiwezesha GTV kuendelea kuongoza katika utoaji wa huduma za luninga ya kulipia hapa Tanzania”.

Wakati uteuzi wa Ronnie Mtawali unatangazwa, Charles Waituika ambaye amefanya kazi kubwa na nzuri akishikilia nafasi ya Meneja Mkuu kwa muda, anakwenda kuwa Meneja Mkuu wa GTV Kenya.

Tangu GTV Tanzania mwezi Agosti 2007, kumekuwa na hitaji kubwa la huduma zake, hili limekuzwa na ongezeko la ubora wa viwango vya idhaa zake pamoja na mteja kuwa na uwezo wa kuchagua kifurushi cha vipindi anavyotaka kuangalia.

Katika kuhakikisha kuwa kila mtu anapata nafasi ya kuwa na GTV nyumbani mwake, GTV imeenda mbele zaidi na kupunguza gharama ya kufungiwa mitambo yake kwa zaidi ya nusu katika promosheni ya katikati ya mwaka inayomalizika Julai 15.
Kwa mawasiliano zaidi:
Mabhe Matinyi,
Media Relations,
Silver Bullet PR,
+255 712 785695,
Ash Myers,
GTV Marketing Manager,
+ 44 7810 425622,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2008

    Hongera.
    Ulishamaliza ile MBA yako ya OPEN UNIVERSITY pale NBAA?
    Walishawapa digrii yenu au bado wanawazungusha?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2008

    Aisee huyu ni Forrest Whitaker nini? (mzee wa The last King of Scotland)

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2008

    Congratulations Ronny. U made it and I am sooo proud of u. Michuzi nilivyoona hii picha hapa kabba sijasoma kichwa cha habari nikadhani Ronny kadedi....tehetehtehetehetehetehe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...