Michuzi,
Mimi sijawahi kutoa maoni yangu kwa blog yetu ya jamii lakini huyu kakuru kanipa hamasa maana hata sijajua anategemea kupata nafasi gani kwenye muungano wa africa mashariki, maana nashangaa au tunashangaa kimetokea nini mpaka wenzetu hawa leo wawe wamejua umuhimu wa muungano.
Wakati sisi Tanzania tuliliona hilo mapema zaidi na tukawa tayari kwa lolote na kakuru pia hawezi kukataa juu ya hilo, ni kweli Africa hatuwezi kwenda kila mmoja kivyake lakini kwa roho zetu za ubinafsi hatuwezi kwa sasa kuungana na hapa sio Tanzania tuu, mfano hao watani wetu wa jadi kakuru atuambia nini kinatokea katika kisiwa cha Misali kaskazini mwa Pemba, aseme nini kinatokea kwa Mlima wa Kilimanjaro, pia haitoshi atuambie nini kinatokea kwenye ziwa Nitron na mambo mangapi tunatofautiana kimawasiliano ya kiserikali.
Ikitokea kwa Tanzania kupata japo mafanikio madogo wenzetu hawa wanaumia, sasa hapo kweli jamani ndio pana ushirikiano kweli. Kama kupata mazuri iwe ni Kenya tuu au Uganda kwa sisi wamatumbi iwe hola, haiwezekani bwana Kakuru huo muungano wa kipumbavu.Kwanza mnatudharau kwa sababu hatujasoma kama nyinyi, halafu tuna matatizo kibao ambayo yanahitajika kurekebishwa bwana Kakuru.
Hata wewe mwenyewe waona sio kama huoni. Watanzania tuko macho sana kwa sasa, maana wasiseme kua hatujui umuhimu wa muungano wala tulikotoka ni wapi.
Hayo makao makuu kama wanataka wahamishe tuu, wakipeleka Mbale, Kampala au Ginja ni sawa tuu hata Nairobi, Kisumu au Mombasa ni sawa pia hakuna kitakacho haribika. Kwani kwa sasa muungano wa Africa mashariki wamatumbi hatuutaki labda baadae tena ikiwa wenzetu nyie mmebadilika na tayari tumeweka mambo yetu sawa kwa kizazi cha baadae.
Mdau Makambako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2008

    hili halina ubishi kwani nchi za afrika mashariki bado kila moja ina matatizo yake makubwa.Ambayo kimsingi lazima yawekwe sawa kabla ya kuungana.
    Tunajua Uganda bado nchi ya ki-dikteta,
    Kenya nayo ni ya kikabila
    Rwanda usiseme..ndio kwanza donda ndugu limeanza kupona,
    Burundi haswa..kuna Perepehutu hawashauriki....
    Tanzania,ndoa ya Zenj na Tanganyika inamshikeri!!

    Hivyo basi pamoja na nchi hizi kuwa na mafanikio katika nyanja tofauti bado matatizo niliyojatajaa yanafaa kuwekwa sawa.

    Vinginevyo, ndoa ya shirikisho la East Africa litakuwa la kutatua matatizo hayo badala ya kusonga mbele.eeeeeeeeeee!!

    ANYWAY...
    Bro Misupu Tunaomba updates za Bunge kwani LEO NI LEO!!
    "Mining sector reforms might be known today"

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2008

    Mimi ningependa kuwaswali wale walikuwa wanasema UK sio part ya EU. Hiyo information wametoa wapi? Juzi juzi Blair hakuwa President of the EU Council? Kama unaongelea kuwa haitumii Euro...kuwa specific...lakini UK ni a longterm member wa EU!

    mtoto

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2008

    safi sana mdau hapo wamatumbi hatutaki muungano,,point zako nzuri sana ila mie naongezea hawa majirani zetu wanarohombaya sana then wataturetea matatizo kenya kuna mungiki,uganda kuna L.R.A huko burundi na rwanda hali zao si shwali akina FNL,,cha msingi kila mmoja akomae kivyake,,we ona kama kuna umuhimu wa muungano kwa tanzania mbona majirani ndio wanaforce then watz wenyewe hawataki,,kifupi hakuna ishu katika muungano hapo,,kama muungano deal ombeni na muungano na somalia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2008

    Jambo moja dogo lakini muhimu katika hili ni hii dhana kuwa watu wa Uganda na Kenya wamesoma sana kuliko Watanzania. Dhana hii imejitokeza toka mwanzo wa majadiliano haya lakini pengine tungejiuliza imetoka wapi na kama ina ukweli ndani yake. Naona mimi imechomekwa na sisi tumeendelea kujadili hoja bila kuiangalia kwa umakini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2008

    This emphasis on the problems inherent in the Kenyan and Ugandan systems has been taken too far. The fact that there are problems in these two countries does not justify the bloggers' stance on the federation matters. Tanzania too has multiple social/political/economic problems. The bloggers would make you think that Tanzania is the promised land.

    Most Kenyans innocently believe that Tanzania is a land of very hospitable people. I now know better after working there for just half an year.

    My Swahili is very good, in TZ nobody would think I am a foreigner. Very often Kenyans are described as thieves, nyang'au etc, this is very worrying, I witnessed it on the streets of Arusha, in a boat from Bukoba to Mwanza and in several other places.

    In one instance an FFU guy stopped me at the entrance to KIA and demanded to check my bags with the explanation that he could not take chances since Kenyans come to the promised land only to steal. To me this is utter crap.

    When I came back home i tried to find out if Tanzanians face the same attitude in Kenya, i am yet to register any such complaint.

    This is precisely why I don't want this federation thing, we may form it and then things go the South African way. Kenya is not paradise but there is no hostility to foreigners.

    The long and short of it is that you need to clean up your act also, rid yourselves of xenophobia before you consider your country as the havens that we want to inhabit.

    Tell me, between Tribalism (so Kenyan) and Xenophobia, which is better?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...