baraka chibiriti akisalimiana na mdau beda msimbe mdau wa http://lukwangule.blogspot.com/ ofisi za daily news na habari leo, leo mchana. chini ni salamu za selebriti huyu wa blogu hii ya jamii ambaye amedhihirisha kwamba dunia ni kijiji kimoja hata uwe wapi...
Michuzi,
Napenda sana kutoa shukrani zangu nyingi sanaaa za dhati, kwa mapokezi mazito uliyo yafanya kwangu mimi, kunipokea hapa Bongo kwa kishindo, baada ya kupokelewa na wadau na wana kijiji wa fotobaraza J2 iliyo pita huko Makumbusho, ambapo nilifurahi sana tena sana kukutana na wadau hao.
Tena leo furaha imezidi kipimo baada ya kukutana nawe Mkuu wa Wilaya ya nanihii tena wilaya yangu mashuhuri.
Kwa kweli nimefurahi sana kwa ukarimu wako wa kunitembeza ofisini kwako na hata Bongo hii. Ninapenda kukushukuru sana tena sanaaaa......!!!! Maana bila ya wewe nisinge weza kufahamiana na wadau wengi sana kwasasa hasa wale wa Fotobaraza, maana wewe ndo wa kwanza ulie nionyesha FOTOBARAZA.

Mimi nimepata furaha sana tena sana, na kuwaambia wadau wote furaha yangu, ya kukutana na wewe, tuzidi kupendana watanzania wote ni dungu kabisa mimi tripu hii nimeamini baada ya kukutana na watu wengi sana ambao sikuwafahamu sasa tunafahamiana utafikiri tulikuwa tunafahamiana toka siku nyingi.
Tudumishe upendo huu tulio nao watanzania.

Mwisho kabisa napenda kutoa salamu nyingi sana kwa wadau woteee tena woteee kabisa, wanipendao na wasio nipenda, mimi ninawapenda woteeee....!!!! Tena sanaaaa.
B.CHIBIRITI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2008

    sawa kaka, mungu tubariki waafrika.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2008

    Huyu anatafuta umaarufu kupitia mgongo wa blog hii. Anataka kugombea ubunge nini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2008

    Anon wa pili,hata kama anatumia strategy ya umaarufu humu ndani kwa nia ya kugombea ubunge,wewe inakuhusu nini?! Watanzania wengine ndo maana maendeleo huwa ni finyu siku zote.Fuateni mifano ya wenzenu especially ughaibuni mjue wanafanya nini kuendelea na si kurudisha au kukatisha watu tamaa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2008

    nasi tunakupenda sana tena sana, yani saaaaaaaaaaannnnnnnnaaaaaaa kakayetu chibirit, kama ni kuzaliwa, wewe ni first born wetu kwa baba michuzi na mama blog yetu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2008

    Mkuu wa wilaya na nanihii mbona hutuambii wadau wa dar utakuwepo kwenye mahojiano ya friday nite live EATV na AER tukuangalie bana na kutuma maswali yetu live. Unabana sana bana. hatahivyo nashukuru nimesoma kwa Guardian lazima nikuangalie. na kukubandika maswali. Hongera kwa kupaishwa Mkuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...