Salum saw this story on the BBC Sport website and thought youshould see it.

** Message **Aibu tupu iliyojaa hapa ulaya kutokana na scandal la TFF,mimi niliifumbia macho hii kama siioni lakini majarida mengi ya ulaya kila siku yanatupakaza ile mbaya yenyewe yaani, we acha tu...

** Jersey reprieve for Tanzania star **
Pardon for player who swapped jerseys with Samuel Eto'o. Click below to read the story..
/hi/football/africa/7487937.stm

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2008

    Ohhhhhhhh ona sasa kuna haja gani ya kuwa mbongo?si bora niwe mrundi,mrwanda au msomali kabisa!au bora nikichukua uraia wao huku niondokane na aibu,ufisadi,ufisadi kweli ni ugonjwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2008

    Bw. Michuzi huyu jamaa aliyetuma hii topic, kasema ulaya wanatumbona???.
    1. Kweli wbesite ya bbc ni ya UK kwenye link ya bbc africa. Nadir haroub lazima wamrudishie jezi ila sijui kama mchezaji kama alikuwa anajuwa hizo sheria kama angekuwa anajuwa hakutakiwa kufanya. Tanzania tubadilishe hizo sheria labda kama jezi ndio hizo hizo wanatumia kuchezea tena.

    2. Kuhusu jamaa yangu anayeponda ni mtanzania mwenzetu hapondi anasema ukweli wa mambo ulivyokuwa jamaa wenye jina hapo juu utaona kwenye link ni Emmanuel Muga
    BBC Sport, Dar es Salaam Story inaonesha ni kutoka Dar-es-salaam ni mwandishi wacha aandike wakati wake wakujulikana kama mwandishi.

    Chama cha mipira wawekeni wachezaji wenu darasani na nyie wenyewe pia kabla hamjajiabisha. From Pan African Oyeeeeeee Swahili Street. Mandazi road.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2008

    bro hii haipendezi hata kidogo. fikiria hata huyo Etoo mwenyewe anajisikiaje. kwenye bango kubwa BBC picha ya huyo mchezaji na bendera ya Tanzania kifuani. dhuuuu, hii noma. TFF kama jezi zinapungua basi anzisha harambee. tutawachangia ili mununue jezi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2008

    Wabongo kwa kulalamika!
    Huyo mwandishi kaandika kilichotokea, sasa tatizo liko wapi?
    Viongozi ndo baado wana mawazo ya mwaka 47 - yaani kubadilishana jezi wanaona kitu cha ajabu? Hiyo jezi thamani yake ni shilingi ngapi? TFF amkeni, kumekucha vinginevyo mtapigwa bao la kisigino!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2008

    Mbona tunalalamika kwamba ni aibu mara Bongo akufai....Swali hili sio Bongo pekee yake kila nchi au club kuna taratibu zao kunabaazi ya jezi hata manchester au Chelsea wachezaji wote wanafahamu kama ukibadilishana na mtu unabidi uilipie bila kujali ni star wa timu au la .

    Hii ni kutokana na baazi ya jezi kuwa gharama zake ni za juu kwenye utengenezaji.

    Sasa hapo tujiulize kwanza kabla hatujalalamika, je wachezaji walikuwa wanafahamu kwamba ukibadilishana jezi walikuwa wanatakiwa kulipia hizo jezi kabla ya mechi,? kama jibu ni ndio basi TFF sio wa kuwalaumu lakini kama jibu hapana hapa ndio tunaweza kuwalaumu kwani Mchezaji husika alikuwa hafahamu hilo

    Kenge

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2008

    Ingawa ni aibu lakini mambo mengine tunajitakia wenyewe hi habari tumeandika wenyewe watanzania sasa haina haja ya kusema wazungu ni mwandishi wetu wa kibongo ndio aliepeleka umbea huko bbc nae ni

    By Emmanuel Muga
    BBC Sport, Dar es Salaam

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2008

    ...Kama hiyo issue iliishapata solution, huyo muandishi alikuwa na haja gani ya kuipeleka huko BBC?? ama ndio mambo ya mradi kapata chake, basi? afterall, there
    is something called 'National Intereset'.....!?

    ReplyDelete
  8. Ok, mimi nimesoma hiyo story, kwlei inaonyesha umasikini wetu na kutuaibisha japo ni mzembe mmoja asiye na uzalendo ametuuza. Hata hivyo its not a very big deal, imeshatokea, dunia nzima nje ya Afrika hizo ndio habari wanazopenda kusikia kuhusu Afrika hivyo najua hazikuwa za kuwashangaza.

    Mimi sidhani kama ni busara mtu kusema anajuta kuzaliwa Tanzania au bora abadili uraia..hapo nadhani ni kupungukiwa na busara kidogo. Tunachopaswa kufanya ni kuangalia namna ya kutatua tatizo hili miongoni mwetu lisitokee tena.

    Funzo kubwa kwa viongozi wa vyombo vya jamii kama TFF ni kujifunza kutokuropoka kwani wao ni wawakilishi wa Taifa. Ona jinsi kauli ya kiongozi ilivyochafua sifa ya Taifa kwa kiwango kikubwa!! Mambo kama haya yangemalizwa kimya kimya ofisini.

    Hata hivyo yamekwisha sasa, yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Funzo tu ni kujifunza kufikiri kabla ya kutenda.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 07, 2008

    Kwa kweli mwakalebela hatufai tena kuwa katibu wa TFF kwa alishupapalia sana upumbavu ule kama ni maazimiao kikao ya kikao jee walipokuwa wanjadili hicho kitu waluwa wamelewa ?
    Mwakalebela aombe radhi kwa hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...