Lile chama linaloinukia katika medani hii ya soka wana-Tanzanite FC wana Mdobwedo, WanaTupwisa Lindanda, WanaZembwela, WanaBayankata, WanaAwamu ya Pili, Wanangu Wenyewe Wameibuka mabingwa katika Mashindano ya kusherehekea uhuru wa Marekani (July 4th) yaliyofanyika katika jiji la Birmingham Alabama jumamosi iliyopita.
Mashindano hayo yalizishirikisha timu za soka mbali mbli kutoka Atlanta, Ga. na Alabama. Ushindi huo ulikuja baada ya kufanikiwa kuifunga timu ngumu ya Mashada Fc ya Alabama kwa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali.
Mabao ya mchezo yalifungwa na Malik kwa kichwa na lile la ushindi liliwekwa kimyani na Muzi Mswazi baada ya kuipangua ngome ngumu ya Mashada FC. Hadi mwisho wa mchezo Tanzanite FC 2, FC Mashada 1.
Mchezo wa fainali uliwakutanisha mahasimu wawili wote kutoka Atlanta, Tanzanite Fc na Jamhuri FC. Jamhuri ilifanikiwa kuingia fainali baada ya kuisamabaratisha Togo kwa mabao 6-1. Mchezo ulikuwa wa kuvutia hadi half time si Mdobwedo wala Jamhuri waliokuwa wameona nyavu za mwenzie.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na iliwachukua dakika sita tu kabla FC Tanzanite hawajapachika bao kimyani, bao lililo fungwa na kocha mchezaji, former Taifa Stars na Ushirika ya Moshi player, Michael John.
Hadi mwisho wa mchezo Tanzanite Fc 1, Jamhuri Fc 0.
Weekend ijayo machampions wanategemea kuangusha BBQ la nguvu kusherehekea ushindi huo.
Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Tanznite FC.
Eureka!! Eureka!!
Kwa picha zaidi za mchezo usikose kutembelea
ebwana eeh ile safari ya bongo mlishaifanya ama ni domo kaya tu.Nifahamisheni
ReplyDeleteMnyamuru jirani yangu huyo, aka GAZA! amekuja bongo aliendeleze mkabana poa ona sasa anang'aaa Aminia Doto!!!!
ReplyDeleteAminia wakubwa japo sipendi mpira ila napenda mnavyowakilisha! Aminia
ReplyDeleteWewe uliyepost hii sijui kama unajua maana ya mdebwedo, kwajinsi ninavyojua hii timu SI mdebwedo.Na pia umetumia umetumia maneno mengi ya kuchanganya sana.
ReplyDeletemwandishi mbwembwe nyingi utadhani umekunywa maji ya chooni.timu yenu iko poa ila mwambieni kijana wenu Haji aache mapepe.ameshapata kadi nyekundu ktk game mbili mfurulizo.jamaa kichwa yake mbooofuu mboofuuu kinomi aiseeeee.alafu nasikia anasema anataka kupiga PRO,kwa akili yake ile hata ZIMANIMOTO wasingemchukua kwa free transfer. he needs to grow mentally.
ReplyDeleteMwandishi na Mchezaji mmwenzetu Mr Hambiliki Tunashukuru kwa mchango wako katika media.Lakini, tunaomba uboreshe uandishi wako.Ifahamu na kuielewa lugha unayotumia na tumia elimu yako ya uandishi vizuri.Sentesi ziwe na kiima na kiarifu,bila kusahau alama kama vil; koma na mkato bila kuweka maana maneno yasiyo eleweka.
ReplyDeletekutokana na picha zenu na matokeo yenu,inaonyesha timu yenu ni nzuri.ila tafuteni mtu mwingine awe anaandika habari za timu yenu.huyo aliye post habari hii inaonekana hata somo la kiswahili alikuwa analikimbia.kwanza hiyo paragraph ya kwanza kaianza kitaahira tupu.pili hajui maana ya baadhi ya misamihati aliyotumia."Mdebwedo"??????? sasa kama timu yenu inaweza kushinda na kuchukua ubingwa,utaiitaje Mdebwedo?kama kiswahili ndo hivyo,sasa hiyo lugha ya kigeni huko majuu ndo niaje?
ReplyDeleteAnon wa kwanza Safari ya Bongo bado ipo ikishakamilika mtafahamishwa. Mipango bado inafanywa na maongezi bado yanafanyika na makampuni yatakayo dhamini ujio huo. Pia timu wazamini bado zinanafasi ya kudhamini ujio. ahasanteni
ReplyDelete