oliver mutukudzi akifanya onesho lake ukumbi wa zanzibar washington DC
wadau wa dc wakiinjoi muziki wa uhakika wa oliver mutukudzi klabu ya zanzibar. na chini mzee mzima na vijana wake wakifanya kweli
Yule nguli wa Muziki toka barani Africa Oliver "Tuku" Mtukudzi, usiku wa kuamkia leo amefanya onesho moja kali katika ukumbi wa Zanzibar On The Waterfront hapa Washington DC, onesho linaloonwa na wengi kama moja ya maonesho bora kabisa kufanyika ukumbini hapo mwaka huu.


Akiwa na kundi lake la the Black Spirits, Mtukudzi aliweza kuwakonga washabiki waliofurika ukumbini hapo wengi wao kutoka nchini Zimbabwe si tu kwa uwezo wake mkubwa wa kucharaza gitaa, bali kuimba na kutawala jukwaa katika kucheza muziki.

Washabiki wengi (ambao walikuwa na uwiano mzuri wa mchanganyiko wa rangi na mataifa) walionekana kukunwa na nyimbo nyingi za mkongwe huyo hasa ule wa Ndakuvara ambao kabla yake alielezea historia yake kuioanisha na ya wengi waishio sasa ambao huenda shule bila kujua kile wafuatacho shuleni.

Ktk show hiyo, Oliver alitanguliwa na msanii mcheza ala Nana Frimpong toka Ghana na mwadada chipukizi Loide toka Guinea Bissau na Msumbiji ambao hata hivyo hawakuonekana kuzikonga vyema nyoyo za washabiki.
Mdau Bandio M.T

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2008

    Hii ni nzuri sana 'TUKU',siyo mambo ya kuburudisha kwenye kumbi za starehe kwa kutumia CD iliyorekodiwa kabla na kufuatisha maneno kama bahadhi ya wasanii wengine wanavyofanya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...