leo nimelizwa shilingi elfu moja mia tano kwa kununua chupa hii ndogo ya maji kwenye mgahawa mmoja mashuhuri viwanja vya sabasaba ambao hata soda wamepiga marufuku kulazimisha ule kilaji chao. yaani roho inaniuma kweli... 1500/- kwa kachupa haka!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2008

    Haya yalinikumba eapoti dar na wala hawakuniruhusu kuingia na maji yangu kwenye ndege nikaishia kuyatupa! Aaaaa!

    malisa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2008

    Wahenga wanasema "Town is school". Pole kwa yaliyokusibu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2008

    Pole mzee wa Libeneke!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2008

    tukusaidiaje?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 07, 2008

    Ulilazimishwa kununua ama ulinunua mwenyewe mkuu? Maana hata kama ulikua hujauliza bei, uliporudishiwa hiyo jelo hapo naamini ukabaini kuwa bei ni mzozo kwako, ungerudisha tu hayo maji, ukaenda kujisevia maji ya bomba!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2008

    Pole kwa hayo. Maoni yangu kwako ni kwamba ni time tuanze kufikiria na vichwa vyetu na sio na ustaarabu wa wengine.

    Mimi nashauri siku ingine chukua chemsha maji nyumbani, weka kwenye chupa yako na zunguka nayo uendapo. Weka kwenye begi la mgongoni na sio kukumbana na gharama zisizokua na sababu.

    Ni vizuri kama tutaanza kuachana na culture na kutumia vichwa vyetu kupunguza matumizi au kufanya maisha yetu yawe nafuu na sio kulalamika tu kutwa..maisha mabaya lakini ni sisi ndio hatutumii akili tunaiga.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2008

    Ndugu yangu Bongo tunadhulumiana vitu vingi tu,ingekua nchi za wenzetu hii hali wasingeivumilia hata! Ila kwa kua tulishajikatia tamaa basi,tunaacha mambo yaende kama yatakavyoenda.
    Leo hii hata kabaa uchwara tu ka uchochoroni kanauza soda ya 350ml kwa tsh 400 au 500,na wabongo kimya wala hatulalamiki wakati soda za ujazo wa ml350 zinauzwa kwa tsh 350.
    Mikate tunauziwa tsh 500 wala hatustuki.Nikikuorodheshea listi hapa ya mahitaji ya msingi na ufisadi wa bei nitajaza kurasa 20.
    Je hivi bongo hakuna chama cha kutetea walaji? kama kipo kina kazi gani sasa?
    Ila kwa hili lako hata kama ni price discimination hao jamaa wamezidisha yani 328.6%rise in price?

    ReplyDelete
  8. michu ulitegemea nini ulipoenda kwenye banda la "tingisha tuone kama imekwisha"

    wazee wa vipande..aaa aa pole sana

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2008

    pole sana ila mjini shule hujuagiiii
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2008

    Pole bro. Michuzi kwa uchungu ulioupata kutokana na bei ya maji ambayo ulihisi hukutendewa haki, ila naomaba unipe pole na mimi, kwa uchungu nilioupata kuona hizo noti umezikunjakunja hapo mezani zingali mpyaaa ile pyeee zimetoka kwenye ATM we ushazitia mikunjo naamini una wallet sidhani kana ni sawa kuwa ukishazitoa kwenye pochi unahaki ya kuzikunjakunja,

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2008

    mie mwenyewe nilikoma chpsi na mayai 2 buku mbili taslimu!!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 08, 2008

    bwa shem mh! huyo annoy wa mwisho kanochekesha kweli kweli! kwani mi niklikutana na chips kavu book mbili na soseji moja 500 kwahiyo jumla 2500 ! nilikuwa na watoto wangu wawili wameisha get tayari kwa food ilibidi niwanyanyue haraka na biashara ya saba saba ikaishia hapo tukageuza home nikawapeleka sehemu wakala kuku mzima kwa 5000 na chips za upendeleo na soda ya bei halali . sijui huwa tunafuata nini kule , vumbi , wezi na watoto wanachoka sana usafiri shida hata kama unagari yako kutoka ni kimbembe yaani nashindwa kuelewa labda tumelogwa.
    ukilalamika utasikia jitu linakuambia hii ni saba saba kama huwezi toka au anakwambia starehe gharma bwana basi inabidi unyamaze

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...