mambo ndo yanazidi kuiva ndani ya Houston, ile siku ya siku ndo hivyo tena inakaribia, na mambo ndo yanazidi kuiva, ni ndani ya East African Summer Nite, ambapo siku hiyo pia yule " Hendsam" au 'Mtanashati' zaidi kutoka nchi za Afrika Mashariki atapatikana.
Bila kusahau BBQ itachomwa usiku kucha! Mbuzi wa kutoka Kericho, Vingunguti na Nakivubo wamekwisha wasili kwa ajili ya kitoweo cha usiku huo.
Bila kusahau 'couple' ambayo itapendeza zaidi watajishindia zawadi nono kutoka kwa waandaaji(suprise).
dj kaycee ambaye kwa sasa yuko mafichoni kujifua maalumu kwa ajili ya tukio hilo, amesisitiza kwa njia ya simu, kwamba mitwango itaanza saa 3 kamili bila ya kuchelewa, hivyo usikose flashbacks na old skoolz zile za miaka ya 80 na 90,
amesisitiza kwamba nyimbo hazitarudiwa hivyo wahi kiti chako mapema!
Pia waandaaji bado wanakaribisha majina ya 'ma'handsome' ambao wangependa kushiriki katika kinyanganyiro cha mtanashati wa East African in Houston,
the # is 281 236 5204
&
7135187222
haya ma-oldSkool yanatosha sasa. itisheni mikusanyiko ya Maendeleo na kupeana business ideas.Upumbafu tu huu ,wazazi wenu bado wanateseka kwenye nyumba za matope na wadogo zenu hawana hata ada za shule nyie kazi ku-party kila leo.
ReplyDelete