Ali Kiba na wadau wakiwa ukumbi wa JJ Whispers huko Orlando katika makaribisho yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. USA watu wanajua kupiga pamba lakini UK wanajivalia valia tu unakuta hakuna mpangilio

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi mimi siujui muziki wake na wala simjui huyu kijana, je iko sehemu yakusikiliza muziki wake?

    Muziki wake ni taarab?

    Mdau Iceland

    ReplyDelete
  3. Oyaa, Dogo, hiyo midala utakayovuna huko ukirejea home tafadhali kapige shule,miziki miziki hiyo huwa kuna kupanda chati na kuporomoka unabaki na misifa tu. Mambo sijui ukanunue pamba kama za hao wanaojua kuvaa, ulimbukeni huo. huo mtaji kabisa wa shule ndugu yangu, wapo walivuna na wakavuma mpaka visiwa gani sijui walionekana ka wafalme,milaga, sijui nini leo hata 300/=tshs ya daladala wanaomba. Shauri yako. Afu ujue sio mavazi tu kuna marazi pia. Ohoo, maake wabongo mkiwa mastaa basi tena wote wazuri ni wako. shauri yako.

    ReplyDelete
  4. Kwa Mdau wa kwanz auanye dai USA wana jua kupiga pamba, , nimeishi nchi zote hizo mbili,nime ishi zaidi USA na weza kukuelewa kwa mtizamo wako, ila kwa mimi ningependelea zaidi UK wanavyo piga pamba ,wako smart na kistarabu zaidi ya walio USA.

    ReplyDelete
  5. Ndugu yangu mdau wa Iceland kwa kukusaidia huyo sio mwana mipasho. Anaimba Bongo fleva. Kama unahamu ya mipasho ingia kwenye website ya google halafu nenda you tube, chagua Hadija Kopa, utamsikiliza unavyopenda, nasikia huyo ndo malkia wa mipasho.
    Ahasante

    ReplyDelete
  6. WALIOMLETA ALI KIBA USA NAWAPA USHAURI WA BURE,TANGAZENI SANA UJIO WA HUYU DOGO KWENYE MITANDAO YA WAKENYA,KWENYE CLUB ZAO MTAPATA WATU WENGI SABABU WANAMZIMIA KINOMA,WABONGO WA USA SIYO KAMA WA EUROPE AMBAO WAKO CONNECTED NA BONGO.

    ReplyDelete
  7. Halafu dogo ukirudi usijikwaze uwe mstaarabu mpenda watu, kwenye shari wewe epuka hata ukiitwa fala, majivuno na ubabe hauna maana mwenzio ananyea debe pale Segerea eti mipombe ilimgiribu akampiga mtu ,hata kama mtu ndiyo mgomvi fikiria kwanza status. Samahani kwa kukuvuta sikio ndugu yangu.
    Mdau < JAPAN>

    ReplyDelete
  8. Anony wa Tarehe August 23, 2008 10:10 PM, jamaa anapiga aina fulani hivi ya bongo fleva.

    Ukitaka kuisikiliza angalia hii web: MK MUSIC GALAXY na utaipata kuisikiliza. We angalia mziki mmoja mmoja upande wa bongo flava.

    Mi nasikiliza nyimbo za kabila langu hapa upande wa Bongo Dance.

    PeAcE.

    ReplyDelete
  9. wadau us mimi siku zote huwa najiuliza hivi kwanini wabongo wa hapa state huwa hawazimi,au hawajali bongo fleva ,machizi wangu wote nilikuwa nawauliza kama watashuka mitaa ya md kwenda kumwona dogo kiba naona nakuwa kama nawawangia hivi sijui imekaaje hii,unakuta wakenya wanawazimia bongo artist kwa huku us kuliko sisi wenyewe wabongo.tukampe dogo mkono washikaji.

    ReplyDelete
  10. me nimesikiliza nyimbo nying za ali kiba kama hawapendi na maria achilia mbali asinati,nimekubali huyu jamaa kipaji,ana nyimbo nyingi kali sio wasanii wengine unakuta m2 ana nyimbo 1 tu ndo inabeba albam,keep it up ali k safari bado ndefu..mdau-turkey

    ReplyDelete
  11. Hakuna kujua piga pamba wala pumbi hapa. Hao USA wanavaa kata K. Mtu mzima unamkuta amevaa kma mtoto wa umri wa miaka 12. Ukiulizwa eti unakwenda na wakati. Pllllllllllllz. Mtu mzma na hekima zao huvai suruali chini ya miguu hta siku moja na kusema eti unakwenda na wakati. Alafu ukivaa hivo mwenyewe ndo unajiona wewe kabisa. Kheri ya wabongo wa UK wanavaa suruali iendayo na kiuno chao. Ulimbukni. Naungana na Mdau w juu hapo. Kiba rudi ukasome. Kwani hata hao kina Lil'Wayne wapo University wana major kwenye business na wame sol million in first week. Elim muhimu.

    ReplyDelete
  12. Tarehe August 25, 2008 3:23 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    wadau us mimi siku zote huwa najiuliza hivi kwanini wabongo wa hapa state huwa hawazimi,au hawajali bongo fleva ,machizi wangu wote nilikuwa nawauliza kama watashuka mitaa ya md kwenda kumwona dogo kiba naona nakuwa kama nawawangia hivi sijui imekaaje hii,unakuta wakenya wanawazimia bongo artist kwa huku us kuliko sisi wenyewe wabongo.tukampe dogo mkono washikaji.
    >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
    Sababu wadau wa STATE wengi wao wanapenda ulimbukeni. Wanasahau walipotoka. Wanataka wamsikize fiddy cent 24/7. Hawajui kumbuka chi yao. Wengine wamekaa US 2 yrs wakwambia washasahauhta kiswahili. Kma si utumwa na ulimbukeni sijui tuiteje

    ReplyDelete
  13. 1.nyie msiuzi watu mmekalia dogo nenda shule nenda shule,nyie mmemuuliza kujua mipango yake au mnafungua midomo tu kwa sababu ni haki yenu.
    2. nyie wengine mnajifanya mmesahau kiswahili kwa kwenda US ni maskini wa mawazo,kwa kiingereza gani mnachoongea mpaka mjifanye hamjui kiswahili.wamarekani wenyewe original wanacheka na accent zenu mbovu hizo waone kwanzaaa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...