Je, unataka kumjua kiundani mgombea urais wa Marekani Barak Obama? Basi tafuta kitabu hiki ambacho mdau maggid mjengwa ametuandikia kwa faida ya wote wanaomhusudu Obama ambaye wengi wanampa nafasi kubwa kuingia Ikulu ya Marekani. Kimeandikwa kwa Kiswahili chepesi na kusheheni mapicha kibao ya mgombea huyu wa urais wa Marekani. Tayari kipo mitaani na bei yake ni poa kama inavyoonekana kwenye jalada lake la mbele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hongera sana kaka Mjengwa kwa kuandika kitabu kuhusu huyu "Dogo" aliyeshangaza dunia kwa kuweza kusambaratisha "The Mighty Clinton Empire". Kiu ya kutaka kujua zaidi ni kubwa na itapendeza sana kusoma ktk lugha ya nyumbani, kiswahili-nasikia nae anajifunza.
    "Dogo" huyu ambaye ni Genius anapeta kuelekea jumba jeupe,(halleluuuuuya!)tumkumbuke ktk sala zetu kwani McPori, aka McBabu, aka McChosho, aka McGrumpy, etc, ameanza mikakati michafu dhidi ya "Dogo". But in the end Dogo will prevail against all the odds!
    PS: as a lady i couldnt resist this- how about that smile ladies?! it gives me goosebumps! I'm just being honest...

    ReplyDelete
  2. Natumaini pia utatoa vitabu juu ya watanzania ambao ni mfano wa kuigwa katika uongozi.

    Wenye majina wangechangia ili Bwana Majjid ufuatilie.

    Hivi kuna Biography ya Mwalimu Nyerere?

    ReplyDelete
  3. Unapoandika habari kuhusu mtu ni lazima upate baraka zake kutokana na sheria za kiuandishi, je wewe umefanya hivyo? Na habari zake umezipata wapi kiutafiti, au kupitia magazeti, internet, televisions as some of them are pretty much wrong. I will agree with you if OBAMA himself read it before its publications as that is how should be.

    ReplyDelete
  4. Wow! bio ya huyu mtu sasa hivi ...?????

    Na mimi naunga mkono hapo bongo wapo watu wengi ambao wabongo wengine hata hawajui ni mashujaa kwa taifa letu na ndio tanganyika wenyewe .Kama unakipaji cha kuandika vitabu basi watafute watu mashuhuri ie....Huyu mmoja kafariki juzi kila mtu anajiuliza ni nani....Je miaka kumi kutoka leo kutakua na kitabu chake mahali popote cha kumbukumbu yake?

    Think about that tupalilie wakwetu kwanza tuachane na hawa wakwao ....

    Kwanza kwa sheria unaweza kujiingiza mkenge...I hope ni "friction book"

    ReplyDelete
  5. ...Looking for a fast buck, eh?

    ReplyDelete
  6. Anony wa August 03, 2008 8:29 PM, you mean FICTION?

    ReplyDelete
  7. I HOPU UNA "HAKI MILIKI" YA KUTOA HICHO KITABU. USIJE TIA WAHESHIMIWA MATATIZONI KWASABABU TUNAPENDA "KUKOPI KILA KUKICHA". MITAANI NA MADUKANI UJIONEE

    ReplyDelete
  8. what for?
    BARAKA OBAMA ?

    Goshh...!!!!!!
    May be the book about first Africal President who happened to be a woman and president of LIBERIA would have make sense.

    Anyway, market will tell if people are real interested or not.

    By the way, has somebody thought of asking for right to translate to swahili,"LONG WALK TO FREEDOM" of MANDELA?
    I think that will be much worth than about OBAMA !

    ReplyDelete
  9. I dont say the book is bad. Lakni kwa nini tupapukie watu wa hukooo na kuwaacha wa hapahapa kwetu. This is killing our own history kidogo. Kuna watu kama Dr.Asha Rose, 1st female in the world to hold such a post. Kuna watu kama Dr.S.Ahmed Salim, mwanadiplomasia wa kiatanzania anaesifika Africa, ana alieshika wadhifa wa ubalozi katika umri mdogo sana. Kuna watu kama Jk na wengine wengi tu. Huko ukoenda blaza mbali sana. Na ninashangaa umewezeje kupata detailed ( and precise) information za huyu mtu wa hukooo mbali. Wakati hapa kwetu ziro distance the information za hao wa-Tz zipo plent. YOU HAVE DONE A GOOD JOB, BUT THINK TWICE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...