Chama cha wanajumuiya ya wa-Tanzania wa Washington DC na vitongoji vtake (A.T.C Washington DC Metro) inawakaribisha katika mfululizo wa sherehe za Labour Day Weekend zitakazoanza Ijumaa ya tarehe 29 mwezi huu (Aug. 29) katika ukumbi wa Mirage Hall uliopo Hyattsville Maryland.

. Siku ya Jumamosi ( Aug. 30) itakuwa ni Juste Lounge iliyopo Bethesda Maryland na kisha siku ya Jumapili (Aug.31) tutarejesha shughuli Mirage Hall kufunga week end.

Jioni za Jumamosi na Jumapili (Aug 30 & 31) kutakuwa na michezo ya soka na nyama choma katika viwanja vya michezo na mapumziko vya Middlebrooke Maryland.

List kamili ya nani atafanya nini na wapi na mengine mema yatayoonekana katika Bash hili kwa mara ya kwanza basi endelea kufuatilia hapahapa.

NB: Vijana wa Atlanta ambao mlitoa maoni ya kutaka mechi na wataalam wa DC mnakaribishwa sana kuoneshwa tofauti ya Soka na chandimu. Kama mna nia ya kushiriki basi wasiliana na Rais wa chama kwa namba 443-278-6119 ama kwa kutumia barua pepe
tanzaniadc@gmail.com

Nyote mnakaribishwa
Uongozi
A. T. C. Washington DC Metro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...