baadhi ya waombolezaji kwenye mazishi ya kepteni george mazula
marubani na wafanyakazi wa ndege toka makampuni na mashirika mbalimbali walikuwepo kumzika mwenzao
mkuu wa majeshi jenerali davies mamunyange akiwap pole mwenyekiti wa bodi ya atc alhja mustapha nyang'amyi na mkurugenzi mkuu david mataka kwa kifo cha kepteni mazula
balozi daudi mwakawago akiongea na makwaia wa kuhenga (kati) na dr. warid kaborou baada ya mazishi ya kepteni mazula

ndugu wa karibu wa kepteni mazula wakiweka mashada ya maua kaburini
mtoto wa marehemu george junior akiwa kwenye mazishi. nyuma yake ni kaburi la kaka yake walter aliyefariki mwaka 2006 na kwa bahati nafasi ya baba yake kuzikwa karibu hapo ilipatikana

mjane wa kepeteni george mazula na mwanae george n afande mstaafu mzee mbwile wakiweka shada la maua kaburini




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Brian, Junior, mama Mazula na ndugu na jamaa wote; Mungu mwenyezi awaimarishe katika kipindi hiki kigumu. "Sisi tulimpenda na mungu mwenyezi aliyemuumba amempenda zaidi na hivyo kumwita mahala pema mbinguni". Mwanga wa milele umwangazie ee bwana.........

    ReplyDelete
  2. RIP uncle....

    mheshimiwa Zitto hilo shati vipi?

    ReplyDelete
  3. Jamani na tusome alama za nyakati. Najua vazi la kanga ukizungumza ukweli kwamba limeshapigwa bao mashosti tutamaind.....ila si mmejionea wenyewe mlivyojisikia. Kwa hapo utakitafuta kiti cha nyuma mwenyewe...ukiulizwa kulikoni utadai unapenda fresh air...haloooo!!!!

    ReplyDelete
  4. Mungu amrahamu, huyu baba alikuwa mwema na wakujivunia kwa familia na jamii pia. Nakumbuka miaka ya 90' nilikwama airport mza nilikuwa naenda kuhudhuria semina kesho yake dar, sikuwa na ok, abiria wote walipanda nami nikaachwa pale, alipita akielekea ndani kurusha ndege akauliza mbona abiria wangu mmoja bado yuko hapa? akaambiwa ndege imejaa, akasema mruhusu atakaa na sisi kule mbele na nilikwenda kwa amani na salama na kuona jinsi marubani wanavyoendesha ndege zao, bila yeye kujua alinisaidia mara ya pili nilichelewa kufika airport kwa sababu ya foleni ya magari, nilipofika watu wote wameshakaguliwa na wameingia ndani ya dege na ngazi imepandishwa, nikaambiwa umechelewa, ngoja tumtaarifu rubani, walipomtaarifu nikasikia kwenye kipazasauti pale kwa checking officer anasema mruhusu aingie nateremsha ngazi, na nikasafiri nao. Sitasahau wema wake huo aliniokoa kwani nilikuwa nimeruka weekend kuhudhuria harusi ya ndugu nikijua j'3 asubuhi nitawahi kurudi ofisini. Nilijifunza vingi kwa wema wake huo bila yeye mwenyewe kujua. Namuombea rehma , Mungu amuangazie nuru ndani ya kaburi lake ampunguzie adhabu ya kabri, na mungu ailinde na kuifariji familia yake Amin.

    ReplyDelete
  5. Bwana wee kweli kama mdau wa 08:18am alivyosema hawa jama nafikiri walitoa dressing code kwa wahudhuriaji maana hiyo ni very western style, wenye khanga wako out of place. Jamaa walijiandaa vizuri sana wamempa send off nzuri sana. Naona wakerewe kweli wameendelea siku hizi maana hata huyo mjane huamini kama kafiwa jinsi walivyompamba, Naamini hata Marehemu amepumzika kwa amani. Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani, Amina.

    ReplyDelete
  6. wajameni, vazi la kanga sio kama limepitwa na wakakti, inategemea ni jinsi gani wewe mfiwa au nyie wafiwa mmeamua kumuenzi mpendwa wenu aliewatoka.. ingawa ktk kila misiba mashangingi yapo mfano hai ni mdada mmoja anaeitwa miriam chingwile, cabin crew ATC.. yeye naona alikuja pale kutafuta bwana, na sio kumzika capt wake.. lol. best subiria laurence masha akifa ndio uende ukafanye ukahaba kwa wasukuma.. uone watakavyokutoa baruti.. umezidi dada punguza..

    ReplyDelete
  7. Buriani kaka George!Nimejifunza kitu kikubwa katika maziko ya mpendwa kaka yetu. Kuishi na watu vizuri.Hakubagua watu kabisa.
    Ila nilivutiwa na shati la mh. Zito kabwe. Sijui aliambiwa na fundi awe analivaa kila kwenye tukio ili nyota yake ing'ae. Kifulana cha mbunge wa nanihii hakifui dafu!Kaka Zito,vipi bwana?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...