mkurugenzi mkuu wa kampuni ya shivacom tanil somaiya (pili shoto) pamoja na bosi mkuu wa vodacom tanzania (kulia) wakimkabidhi funguo za grand vitara jipya ambalo shivacom wametoa kwa malkia wa miss tz 2008 nasreem karim usiku huu. shoto ni mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji mh. emmanuel ole naiko
miss tz 2008 nasreem karim akijidai na gari lake jipya baadha ya kukabidhiwa usiku huu kwenye fainali za vodacom miss tz 2008 viwanja vya klabu ya leaders dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. nadhani mwaka huu watz wameridhika kwanza si mhindi,pili hakutoke DSM,hapo mtu akileta nongono huyu ana lake jambo. CHA MSINGI AFUNDISHE JINSI YA KUJIANGUSHA JUKWAANI miss WORLD na sisi tunaweza tukasikika duniani.ajipige mweleka kama miss usa ktk miss universal,
    WAZO LA MSINGI HILI MZEE WA NANII WAFIKISHIE KAMATI YA MISS TZ

    ReplyDelete
  2. Haya mama hongera kwa kujinyakulia gari kazi kwako kama hujui kuendesha tafuta dereva mwenye leseni kuokoa ajali za barabarani.Kweli we ni mrembo lakini mi mnaniuzi mkiongeza hizo nywele za bandia? mnakuwa soo artificial. Naamini majudge walikuwa fair, hongera sana wa kukaya.

    ReplyDelete
  3. Hivi mnajuwa hizo nywele za bandia zinatoka wapi? ni INDIA, jana tu nilikuwa naangali BBC THREE hapa LONDON, JAMILIA, huyu ni mwanadada mwanamusiki toka BIRMINGHAM - UK alitaka kujuwa wapi nywele bandia zinatoka ambazo celebrities na akina dada wanafanya extension, basi akafanya safari kwenda India akafika sehemu inaitwa CHANNAI, anyway sijuwi kama nimepatia spelling ya huo mji!! akakuta kuna utaratibu wa kitumwa/slavery wa watu wote kukata nywele zao kila mwaka mara moja kataika majumba yao ya kuabudu mungu kama sadaka/ritual, na malipo yao ni kula pilau tu hapo kwenye Temple, na Temple uuza nywele hizo kwenye viwanda vinavyotengeneza hizi human hair kama tuzijuavyo sisi wanunuzi, akaende mji mwingine akakuta watu wanachakurachakura nywele kwenye majalala watu wamenyoa na kuzitupa wao wanaokota na kwenda kuziuza kiwandani, ni biashara kubwa sana India, watoto wengine maskini ya mungu ni miaka mitatu hawajuwi kinachoendelea walikuwa wananyolewa kwa nguvu pale Temple wakilia vibara vikitoa damu kwa kukata na visu vya kianyeji vya kunyolea hadi JAMILA alitoa mchozi. Should we think it twice, nahisi zingine i za maiti toka hospitali. Then the issue of human rights should come into this?

    ReplyDelete
  4. WE MDAU WA TATU ACHA KUPOTOSHA WATU,NYWELE BANDIA ZINATENGENEZWA KUPITIA PLASTIC,WANAYEYUSHA NA KUWEKA CHEMICAL FULAN.USIPOTOSHE UMMA

    ReplyDelete
  5. wewe anon. wa saa 3:46, hebu ongea point iliyokufanya uandike acha habari za kutueleza nywele zinatoka wapi, siyo mada ya miss Tz aliyeshinda, au unataka kutambulisha umma uko UK? ambao hawakuona hiyo prgm ya Jamelia watakua ni wachache sana, kwa hiyo wote tuanze kuandika kuhusu ile prgm?

    ReplyDelete
  6. hata mimi nimefurahi finally mwanza tumetoa the true queen. that what we call miss tanzania wa ukweli.

    ReplyDelete
  7. Acheni ushabiki washikaji, huyu demu hamna kitu, angalieni vema. Sijui kwa nini hawakuchagua Mhindi? Hashim, umekosa kabisa hata Mwarabu?

    ReplyDelete
  8. HAYA TENA MWAKA HUU KIDOGO TUPO KARIBU NA UKWELI LAKINI HUYU MISS TANZANIA WA MWAKA HUU MSOMALI HUYU JAMANI..........MISS MSOMALI

    ReplyDelete
  9. Mchangiaji wa pili alieleza kuhusu nywele za huyu dada mshindi na akasema yeye anaudhika na hii hali ya akina dada kufa-extension ya nywele zao ndipo hapo nikakumbuka jana tu niliona hii documentary katika BBC THREE Jamila akifanya research juu ya wapi hizi nywele zinatoka, ndipo nikaona bora nichangia hisia za huyu mchangiaji hapo juu wala sikuwa na maana ya kuonyesha kuwa niko LONDON kwani kwangu hiyo si big deal kama wewe unavyohisi kwani LONDON ni sawa na sehemu ingine yoyote hapa duniani, kwa taarifa yako tu maisha ya watu hata wa Dar es salaam baadhi yao ni mazuri kuliko hata ya baadhi ya watu hapa LONDON, mwisho kuna mtu mmoja anabisha kuwa nywele hazitokani na nywele za watu, zama hizi za utandawazi hili unaweza kulidhibitisha hata kwa ku-browse kwenye internet, BBC wana hii kitu inaitwa I-PLAYER program unaweza kuona vipindi vilivyopita kwenye internet tumia hiyo uone hiyo documentary I am talking about, nywele zinatokana na nywele za watu hilo halina ubishi na ndo the best kuliko zitokanazo na source ingine yoyote kama zipo, anasema nywele zinatokana na plastic, plastic gani hiyo huo ni uzushi kwani plastic yenyewe pia ni product from another raw materials (mabaki katika process ya kusafisha mafuta), pia zijamlazimisha mtu andike mimi nilichoandika na wala hakukuwa na condition yoyote katika picha humun kwa Michuzi whom I respect the legend, the photogapher maestro kuwa tuandike juu ya nini kuhusiana na picha hizo, ebu achani hasira zisizo na base be constructive tujaribu kuwa wastaraabu, lakini pia nashukuru kwa vile huu uwanja unaonyesha tukoja na tunajifunza communication muafaka katika jamii. Ni uwanja wa kuelimishana na wala sijasema dada aliyeshinda amefanya vibaya kuvaa nywele bandia, nahisi wewe ndo ulitaka kuonyesha kuwa upo UK, hata hivyo hakuna sababu ya kufanya hivyo kwa vile sikuacha profile yangu hapo sasa itanisaidia nini mimi kuonyesha kuwa nipo UK bila profile yangu hapo, wala haingii akili mwa hata mtu mwenye akili za kawaida ambaye si genius, I mean it does not click into even the inside of an ordinary person as it does not need a rocket science to disgree with your arguement. You know what? these kind of arguemenst utlimately will make some people not contributing in here even if they have some great ideas.

    MCHANGIAJI WA TATU HAPO JUU.

    ReplyDelete
  10. ok, sitaki kutoka kwenye main topic ambayo ni Miss TZ. Ila nataka tu kusema kuwa Anony wa 3:46 hayuko totally off. Hair extension zipo za aina 2; artificial na zipo zilizotokana na nywele za watu. Hizi za nywele za watu actually ni gharama zaidi na ni biahara kubwa nchi nyingi za Asia, sio India peke yake. Matajiri wenye hela kama mastaa wa muziki, movie na mamodel wanaoweka extensions huwa wanachagua hizi za kutokana na watu zaidi. Wengi wao huwa wanajua kuwa zinatokana na watu na inasemekana quality ni bora zaidi

    ReplyDelete
  11. nyinyi watu washamba sana,mimi nilikiona kipindi cha Jamelia kwenye BBC3 tena kilikua kinaitwa jamelia:whose hair is it anyways!

    kama alivosema anon 3:46 na anon 1:55.. kuna two weaves - synthetic na human hair. synthetic ndio haya ma plasticki kama african queen,rasta(braids) na dream girl. Human hair ndio kama milky way,sensations. hizi 100% human hair ni nywele za binadamu na ni za asili ya asia. they come from chennai,india some from indonesia.it is TRUE FACT acheni kukandia vitu hamko 100% sure. nyingine ni 70% human hair 30% synthetic. do your homework before you contradict

    ReplyDelete
  12. is this area for Miss TZ comments or hair jamani?

    ReplyDelete
  13. miss ameshinda kiuhalali, ila sitegemei ushindi wowote kutoka miss world.
    nywele za hyu dada ni plastiki, mtanzania anayeweza kununua nywele za kweli atakuwa tajiri sana. Sidhani kama yupo hapa, wala si msichana kama huyu. Hana hizi hela.
    Hata mastaa wengine wakubwa wanavaa plastiki tu kama sisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...