Ndugu wa Paschal, Isaac Kasanga wa Easy Finance, kaiambia globu hii ya jamii sasa hivi kwamba mgonjwa alisafirishwa leo asubuhi kwa barabara baada ya kukosekana ndege.
Kasanga amesema Paschal anaongea vizuri tu ila analalamika kwamba ana maumivu makali kichwani na pia mkono wake wa kushoto umekufa ganzi.
picha ni kwa hisani ya


Upone haraka Paschal.
ReplyDeletePole sana Ndugu yangu lakini kweli hizi adventure kusafiri na pikipiki mpaka Dodoma jamani ai??
ReplyDeletepole sana kaka yangu mwenyezi mungu atakuondolea maumivu,ugua pole.
ReplyDeletePole sana "Mzee wa kiti moto", Ila jamaa ana pikipiki kubwa sana nadhani ni 3500cc, kwenda nayo Dodoma si ajabu ila cha muhimu ni je ilikuwa katika condition yake, yaani nzima, maana bongo mtu anaweza safiri na gari yenye tairi zenye kipara kuna kamsema ka kuagia mtu akianza safari "HAYA NGOJA NIOMBE MUNGU"
ReplyDeletepole sana kaka Mayalla,mungu akuponye na maumivu yote uliyonayo katika jna la bwana na mwokozi wetu yesu kristu."Hakika alichubuliwa kwa makosa yetu na kwa kupigwa kwake tumepona".
ReplyDeletePole sana Paschal, my prayers are with you for quick recovery.
ReplyDeleteMdau, USA
picha mbaya, inakatisha tamaa kwa wanaomtakia mayalla apone haraka.
ReplyDeletePole sana kaka nakuombea upone haraka.
ReplyDeleteMambo mengine mnataka tu kumjaribu Mungu, mtu unasafirije na pikipiki? Anyway, ndio imeshatokea. Ugua POLE
ReplyDeletePole sana! Wamuangalie kaka wa watu asijekua anainternal bleeding. Bongo saa nyingine mpaka upate scan inakua too late
ReplyDeleteJamani lakini pikipiki kutoka Dar - Dodoma naona mbali sana tu. Na mavumbi yale sio nzuri kwa afya acha ajali za barabarani
yaani kweli mtu aendeshe pikipiki from Dar to Dodoma, thats a little too much. Anyway, get well soon, lakini huo mchezo ulioufanya siyo wa busara kabisa.
ReplyDeletePOLE KAKA PASCAL KWANI HIYO BARABARA YA DODOMA KUNA NINI JAMANI?, MBONA ITATUMALIZIA WATU!, AU NDIO KAFARA YA MAFISADI HIYO KUMALIZA WATU INOCENT MHN!...
ReplyDeleteI pray for your quick recovery brother Pascal. May you get well soon.
ReplyDeleteHivi nani anashikilia rekodi ya kusafiri na pikipiki Tanzania?
ReplyDeletekaka mayalla na mapikipiki haukomi ndugu yangu? Umeshapiga chini mara nyingi, i thought ungeacha utumie hata corolla,
ReplyDeleteAnyway ugua pole, upone haraka na usirudi kwenye chombo cha miguu miwili na body yake ni mwili wako.
Jirani yako, Sinza
Ni kumjaribu Mungu vibaya. Nashangaa wale simba wa Mikumi kwanini walimuachia apite.
ReplyDeletePole Kaka
kweli kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake ila sijui wengine utafikiri hawaishi tanzania ooh mara simba wa mikumi kwani nani kakuambia kwamba kwenda dodoma toka dar lazima upite mikumi?
ReplyDeleteAnyway mi kwa mtazamo wangu dar kwenda dodoma kwa pikipiki wala si mbali kama ambavyo watu wengi wamesema ila sema tu kwa sababu ajali imetokea kila mtu atasema lake.
Pole sana pascal kwani barabara za tz kila mtu anaendesha kwa sheria yake ndiyo maana utakuta hata mabasi wana-overtake hata sehemu ambazo haziruhusiwi au lori linaharibika njia na linapaki bila hata kuweka viashiria kwamba kuna gari mbovu. Kwani ajali nyingi zinazotokea tanazania ni zile ambazo zinaweza kuzuirika kabisa kama maaskali wa usalama barabarani wangekuwa wanajua hizo sheria kwa kuanzia pale wanapotoa leseni kwani madereva wengi tanazania hawajui sheria za barabarani hasa walio dar es laam wengi ni wale wa kulipeleka gari mbele tu
Pole kwa ajali,lakini ninachoshindwa kuelewa ni kwamba tunasikia bongo imekuwa tambarale je inakuwaje hata ndege ya kumsafirishia mjeruhi ikosekane tena kwa mtu anayefahamika kama huyo? anyway maybe that's just me.mdau T.O
ReplyDeleteKWA MAREKEBISHO TU
ReplyDelete1. BARABARA YA DAR-DODOMA HAINA MAVUMBI KAMA MMOJA WETU ALIVYOSEMA. NI MKEKA. MNAKAA SANA NG'AMBO, HAMJUI HATA YANAYOFANYIKA KWENU.
2. UNAPOENDA DODOMA KUTOKA DAR HUPITII MBUGA YA MIKUMI. UNACHEPUKIA MOROGORO MJINI (MSAMVU) NA MBUGA YA MIKUMI IPO NJIA YA KWENDA IRINGA.
CHA MSINGI.
TUSIMLAUMU NDUGU MAYALLA, USAFIRI WOWOTE ULE RUKSA, BAISIKELI,, PIKIPIKI, GARI N.K (KWANI BARABARA YA DAR-DOM NI SAFI NA SAFE.
CHA MUHIMU.
TUMWOMBEE NDUGU MAYALLA APATE MATIBABU MAZURI (KWANI KUMWOMBEA APONE NI KAMA MTOTO KUKIMBIA BILA KUPITIA STAGE YA KUTAMBAA KWA TZ). HAPA NINA MAANA KUWA MATATIZO MENGI YA HOSPITALI ZETU NI KUTOA TIBA NZURI. QUALITY QUESTION. HAPA NINA MAANA YA MGONJWA WA GOTI KUPASULIWA KICHWA (remember?).
HOPE YOU GET BETTER BROTHER!
pole sana kaka Mayalla-Robert Mujuni
ReplyDeletePole sana 'anko'Paschal mungu atakubariki.
ReplyDeleteTusimlaumu Paschal:Kuendesha pikipiki nadhani ni 'obby'kuna watu wanapenda sana usafiri wa pikipiki.
Huyu ni mwandishi wa habari:Mimi bado nadhani alikuwa haendi Dodoma tu,Paschal alikuwa ana 'program' ya kuingia na vijijini kwenye safari yake ambako barabara zetu ni mbovu kwa magari,usafiri wa pikipiki ni mzuri zaidi kupata habari za vijijini.
Maoni mengine mmmh:Yameshajibiwa
POLE TENA SANA
ReplyDeleteBy FOTU
Pole kaka Paschal. lakini jamani vitu vingine haviingii akirini kiurahisi kwamba paschal huyu tunayemfahamu.ndio kachukua uwamuzi wa kusafiri na pikipiki mpaka dom?
ReplyDeleteyaweza kuwa alikuwa anataka kuweka rekodi,ila ni kitu ambacho huwezi tegemea kwamba mtu kama paschal anaweza fanya vitu vya jinsi hiyo.
tunaamini kwamba kifo hupangwa na Mungu lkn vingine mmh.
Paschal kaka yangu usije rudia ujinga kama huo tena.
pole sana Pascal Mayala.
ReplyDeleteMungu akujalie upone haraka.
pole sana kaka mayalla duh hio kweli ni adventure!nakukumbuka kwenye white paper a.k.a kitimoto, mbuzi katoliki!!get well soon brother!
ReplyDeleteNdugu zangu ajali haina kinga ila kuna mambo mengi yanayoweza kupunguza au kuepusha ajali, Kaka Mayalla kutumia pikipiki kutoka Dar hadi Dodoma ni jambo la kawaida kabisa na wala si la kushangaa kwani hizo pikipiki huenda mbalizaidi ya hiyo distance ila pikipiki inapopata ajali mara nyingi huwa mbaya sana.
ReplyDeleteKaka Paschal pole sana.
MDAU ; TOKYO.
Pole sana Pascal, nakutakia uweze kurudia afya njema,ila napenda upone haraka ili nije kukuchapa vibao na ikiwezekana nikufunge jail kabisa kwa kosa la kutarisha masiha yako nakutupa sisi tabu ya kuanza kukuonea huruma na kutushtua roho, kwakweli kitendo unacho fanya sio haki kabisa na napenda nikushauri uachane nacho , kama ilikwua ni kusave nauli una save nini zaidi ya kuishia hospital ,tena Mungu mkubwa huja patwa na namadhara zaidi.
ReplyDeleteNachokuomba ukipona achana kabisa na Pikipiki ni chombo hatari sana ,please achana nacho tunakuomba!
Pole sana ndugu yetu Paschal, ninakuombea upate kupona haraka na bila ya kuendelea kuwa na maumivu mengi.
ReplyDeleteNinaunga mkono kwamba wana-Bongo walio mbali wawe wanafikiria kuitembelea nchi ya badala ya kuropoka bila kuijua hali halisi ilivyo huku.
Pia, naomba kufafanua kwamba pikipiki yenye engine ya 3500cc itakuwa na engine kubwa kuliko hata Land Cruiser Prado au Land Rover za Defender/Discovery. Hata Valentino Rossi na wenzake hawafanyi mashindano na engine kubwa hivyo, kwani wanatumia mashine ya 800cc tu.
Pole our dear friend pascal, wana wa udsm facult of law 2007 tunakuombea kwa mwenyezi mungu upone haraka.
ReplyDeleteAmen
Kaka Mayalla,pole sana.Ndugu zangu,imeishatokea.Huu siyo muda wa kumlaumu ila kumwombea apone haraka.Kwa uzoefu wangu,lolote laweza kutokea.Akipona,nendeni mkampe maoni yenu ana kwa ana maana hapo atakuwa anayahitaji sana.
ReplyDeleteFOTU
ReplyDeleteNi wewe uliyekuwa unakaa Masaki na kupiga picha?
jamani ndugu zangu watanzania hebu tuacheni hizi fikra za sisi wanyumbani na ninyi wa ng'ambo.kila mada ikija lazima watu wapigane vijembe,mara oh mnakaa sana huko ng'ambo bila kujua yanayotokea nyumbani,au nasikia bongo tambarare,mimi naona inazidi kuongeza uhasama.kwani sisi wote ni wamoja na kila mtu na sababu zake za kuwepo alipo, wote ni watu wazima.hakuna aliyetekwa nyara na kulazimishwa aishi alipo.kwa hiyo naona haina haja ya kukumbushana tulipo.asante sana,mungu ibariki nchi yetu na watu wetu wawe na upendo,pia bwana mayala apone haraka.
ReplyDeleteocd.